𝗝𝗜𝗡𝗔 𝗟𝗔 𝗥𝗜𝗪𝗔𝗬𝗔: 𝗠𝗨𝗡𝗚𝗨 𝗡𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗘
𝗠𝗧𝗨𝗡𝗭𝗜: 𝗝𝗨𝗦𝗧𝗜𝗡 𝗕𝗔𝗥𝗨𝗧𝗜
𝗠𝗪𝗔𝗞𝗔:2024/2025
𝗦𝗠𝗦 & 𝗪𝗛𝗔𝗧𝗦𝗔𝗣𝗣: +255 752 474 397
𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗬𝗔 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗭𝗔
Alikuwepo kijana mmoja mpole, mkarimu na mwenye huruma jina lake aliitwa Baruti
Alikuwa ni kijana fukara sana, akubahatika kupata kazi ya kueleweka tokana na tatizo lake la usikivu yaani alikuwa hasikii vizuri, kila alipokuwa anaenda kutafuta kazi aliambiwa utaratibu wa ofisi ni kupiga simu sio kuchat
Baruti aliishi maisha ya tabu sana na kujiona hana thamani yoyote katika maisha yake lakini ukiachana na hilo alikuwa na kipaji kikubwa sana, ni mwandishi na mtunzi wa riwaya zinazofundisha na kuelimisha jamii, yaani zinachochea mabadiliko chanya katika jamii
"Ee Mwenyezi Mungu nimekukosea nini jamani, kwanini umeniumba kuja kuteseka hapa duniani, mitihani uliyonipa ni migumu sana, kwanini ukuridhika kuchukua uhai wangu nilipokuwa mtoto mdogo wa miaka 6, ukaruhusu maisha yangu yaendelee, lakini sioni thamani yoyote ya kubaki hapa duniani, 𝗠𝗨𝗡𝗚𝗨 𝗡𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗘"
Alisema Baruti ambaye alikuwa amekaa chini akiwa na mawazo mazito sana
Baruti alizaliwa akiwa mzima kabisa, alipofikisha umri wa miaka 6 aliugua maralia kali, hali iliyopelekea wazazi wake kumnunulia dawa inayoitwa kwinini ambayo ilimtibu lakini kibaya zaidi iliharibu masikio yake na kumsababishia ulemavu yaani changamoto ya usikivu
Mtu anaweza akawa na changamoto ya usikivu lakini akawa na kipaji kikubwa ndani yake na akapitia changamoto fulani akaanza kukata tamaa
Mpendwa usikate tamaa, changamoto ni sehemu ya maisha yetu kikubwa ni kumtanguliza Mungu, huwezi jua ana makusudi gani katika maisha yako
Tatizo hili liligharimu maisha yake lakini alimtanguliza Mungu, akaingia rasmi katika biashara akawa anauza karanga za kutafuna barabarani
Watu walianza kumcheka na kudharau juhudi zake, maana si kawaida mtu mwenye akili anauza karanga lakini Baruti hakukata tamaa aliendelea na biashara yake
Siku moja alikuwa anauza karanga usiku, akapita binti mmoja mrembo jina lake anaitwa Rahma
Rahma alikuwa ni mweupe maji ya kunde, kila mtu alitamani kuwa nae lakini haikuwa rahisi, alikuwa na misimamo mikali sana hakutaka mazoea na mtu yoyote
Baruti alitokea kumuelewa sana Rahma na hakujua anawezaje kumpata binti huyo, alifanya kila jitihada lakini hakuweza kumpata kabisaaaa
Ikatokea siku Rahma akapita maeneo hayo Baruti anapouzia karanga, Baruti akatumia nafasi hiyo kuomba namba ya simu na alipewa hali iliyowashangaza watu wa pale wa karibu tokana na wanavyomjua Rahma sio rahisi kumuamini mtu yoyote
Rahma akarejea nyumbani, gafla.....
𝗧𝗨𝗧𝗔𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗞𝗘𝗦𝗛𝗢, 𝗠𝗧𝗨𝗡𝗭𝗜 𝗔𝗠𝗘𝗧𝗢𝗞𝗔 𝗞𝗜𝗗𝗢𝗚𝗢
Tags
simulizi
Imekaa poa
ReplyDelete