TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

MUNGU NIONGOZE

𝗥𝗜𝗪𝗔𝗬𝗔 𝗠𝗣𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗧𝗢𝗞𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗠𝗪𝗔𝗡𝗗𝗜𝗦𝗛𝗜 𝗖𝗛𝗜𝗣𝗨𝗞𝗜𝗭𝗜 𝗝𝗨𝗦𝗧𝗜𝗡 𝗕𝗔𝗥𝗨𝗧𝗜

𝗠𝗨𝗡𝗚𝗨 𝗡𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗘
Ni riwaya ya kubuni iliyotungwa na kuandikwa na Justin Baruti inayozungumzia kuhusu maisha ya kijana mmoja aliyeishi maisha ya tabu sana, alitokea kumpenda msichana mmoja tena kwa dhati ya moyo wake na alifanya chochote kilicho ndani ya uwezo wake kuhakikisha mpenzi wake anapata kile anachostahili

Lakini huyu dada alikuwa ni mrembo sana, hakuendana hata kidogo na huyu kaka japo huyu mvulana alionyesha kumpenda na kumjali na ana nia ya dhati ya kuwa nae katika maisha

Changamoto zikaanza sasa, huyu binti uvumilivu ukamshinda, akawa anafanya visa mbalimbali ili yule jamaa amuache japo yule jamaa alimsihi sana amvumilie aweke mambo sawa lakini jitihada zake ziligonga mwamba, badala ya kubomoa ukuta yeye anajenga

Mwanamke yule alipata bwana mwingine, historia yao ya mapenzi ikaishia hapo
 
Yule mwanaume alimwambia kwa mara ya mwisho alipomkuta na bwana wake mpya kuwa maamuzi aliyochagua aangalie yasije yakamuumiza baadae, akawatakia maisha mema

Huyu kijana kwa huzuni sana, akapiga magoti kumuomba Mungu akisema 𝗠𝗨𝗡𝗚𝗨 𝗡𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗘 katika safari ya maisha yangu

Baada ya mwaka kupita yule jamaa alijikwamua kiuchumi akawa na maisha mazuri sana, akabahatika kupata mwanamke mzuri aliyemtii na kujali, waliheshimiana sana na kusaidiana

Yule mwanamke wa nyuma aliyekuwa naye maisha yake yaliharibiwa, yule mwanaume hakuwa na malengo nae bali kumchezea tu, akawa anamtafuta yule aliyemuacha zamani akajikuta amepoteza kila kitu..!

Ni riwaya nzuri sana inayofundisha na kuelimisha jamii

𝗠𝗨𝗡𝗚𝗨 𝗡𝗜𝗢𝗡𝗚𝗢𝗭𝗘 inakupa majibu iwapo unapitia changamoto katika mahusiano

𝗞𝘂𝗽𝗶𝘁𝗶𝗮 𝗿𝗶𝘄𝗮𝘆𝗮 𝗵𝗶𝗶 𝗺𝘄𝗮𝗻𝗱𝗶𝘀𝗵𝗶 𝗮𝗻𝗮𝘀𝗲𝗺𝗮;

"𝗠𝘂𝗻𝗴𝘂 𝗻𝗱𝗶𝘆𝗲 𝗺𝘄𝗮𝗻𝘇𝗶𝗹𝗶𝘀𝗵𝗶 𝘄𝗮 𝗻𝗱𝗼𝗮, 𝘁𝘂𝗻𝗮𝗽𝗶𝘁𝗶𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗮𝗵𝘂𝘀𝗶𝗮𝗻𝗼, 𝗹𝗮𝗸𝗶𝗻𝗶 𝗠𝘂𝗻𝗴𝘂 𝗻𝗱𝗶𝘆𝗲 𝗮𝗻𝗮𝘁𝘂𝗼𝗻𝘆𝗲𝘀𝗵𝗮 𝗻𝗷𝗶𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗲 𝗻𝗶𝗻𝗶 𝗸𝗶𝗹𝗶𝗰𝗵𝗼 𝗯𝗼𝗿𝗮 𝗸𝘄𝗲𝘁𝘂"

𝗠𝘄𝗮𝗻𝗱𝗶𝘀𝗵𝗶 𝗮𝗺𝗲𝘁𝗼𝗮 𝘀𝘂𝗹𝘂𝗵𝗶𝘀𝗵𝗼 𝗹𝗮 𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗮𝗺𝗼𝘁𝗼 𝗵𝗶𝘇𝗼 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗷𝗮𝗺𝗶𝗶

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post