TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

NAVINI

NAVINI 🔥😍
Sehemu 01----------05

"Salim! Salim! Salim nakuita mara tatu mwanangu, single mother sio mwanamke wakuoa. Mimi mama yako nakwambia sasa kama haunielewi sawa" bi Sharifa alimwambia kijana wake.
"Lakini mama mbona Navin hana shida ni mwanamke sahihi kwangu pia nimeona anaakili sana"
"Hakuna mwanamke asiye na akili mwanangu, tatizo tayari anamtoto utaoaje mwanamke aliyezaa na mwanaume mwengine?"
"Lakini kuwa na mtoto sio tatizo kwasababu baba wa mtoto hawana mawasiliano yoyote"
"Hivi haujiulizi kwanini huyo baba wa mtoto alimuacha? Halafu wewe sasa unaenda kubeba gunia la misumari unataka kuishi nalo ndani kwasababu gani?"
"Mama hebu naomba unielewe nahitaji kumuona Navin mimi sijali lolote lile"
"Ooh sawa asiyesikia la mkuu huvunjila guu"
Alisema huyo mama na kuangalia pembeni.
"Baba nawewe pia upo upande wa mama?" Salim alimuuliza baba yake ambaye alikuwa amekaa kimya pembeni.
"Alichosema mama yako ni sawa! Tafuta mwanamke mdogo mzuri oa achana na hao masingo maza walioshindwa maisha ni washenzi tu"
"Baba unakosea sasa"
"Mtoto koma onhoo unamwambiaje baba yako amekosea? Salim huna adabu?" Mama yake alikuja juu na kufoka kwa nguvu.
"Naomba mnisamehe wazazi wangu nimeghafirika tu" Ilibidi Salim awe mpole.
"Angalia maneno yakuongea na baba yako sio unajifanya unaongea kama na wahuni wenzio"
"Mama nisameheni, naomba niende"
Salim aliinuka.
"Nenda salama ila huyo mwanamke singo maza kwangu simtaki"
"Daaah!" Alisikitika sana Salim.
Aliondoka akiwa mnyonge sana.
"Hivi inamaana mwanamke akiwa singo maza hafai kuolewa? Kwanini wanawake wenye watoto wanachukiwa sana? Naanzaje kumuacha Navin mimi? Ni mwanamke sahihi kwenye maisha yangu. Na wazazi wangu je? Daaah!" Alijiuliza maswali mengi sana na kukosa jibu.
***
"Mpenzi upo sawa kweli?"
Baada ya Salim kurudi nyumbani alikutana na mpenzi wake Navin. Ambaye alikuwa ameenda kumsalimia, ilikuwa kawaida yao mara kwa mara Navin alikuwa akienda kukaa kwa Salim iwe wiki moja au hata mwezi mmoja na mwisho huondoka na kurudi kwao. Alikuwa akiishi na mama yake mdogo.
"Ah kwema mke wangu, umeshindaje?" Alijikaza Salim na kumsalimia.
"Salama mpenzi wangu, vipi nyumbani hawajambo?"
"Wote wazima wife, ila daah nina mtihani mzito sana"
"Mh! Mtihani gani huo? Mbona unanitisha?" Aliuliza Navin akiwa na wasiwasi sana.
"Kuhusu wazazi wangu wamekataa nisikuoe"
"Jamani! Kwanini wamekataa sasa?"
"Kwasababu wewe singo maza"
"Uwiiiiii mimi jamani!" 
Naveen aliangua kilio kama amefiwa.

Itaendelea.
Mwalike na mwenzio aje kusoma mambo ndo yameanza.


NAVINI😍
NO: 02

"Sasa unalia nini Navin? Bora nisingekwambia tu" 
"Acha nilie Salim niache nilie mimi! Oooihiii kwanini? Kwani nilipenda nizae bila ndoa? Sikupenda kuwa singo maza mimi sikupenda jamani" Alisema kwa kilio Navin.
"Hebu nisikilize basi mimi ndio ninayekuoa sio ndugu zangu. Wao ni watu baki ndoa yetu sisi wawili sio mama yangu wala baba yangu, unanielewa?"
Alimuuliza Navin alikuwa akilia kwa kwikwi.
"Hebu nyamaza na unisikilize basi"
"Sawa nanyamaza ila naumia sana"
"Pole usijali mimi siwezi kukuacha"
"Muongo utawasikiliza wazazi wako utaniacha"
"Niamini Navin nakuoa"
"Kweli Salim?"
"Kweli mke wangu"
Hapo walikumbatiana na furaha ikarejea kwao.
"Sasa kesho itabidi urudi nyumbani na mimi nitaongea na shangazi yangu mmoja hivi anapesa sana shughuli yule atatafuta mshenga ataleta barua kwenu na mengine yafuate lazima nikuoe mke wangu"
"Sawa nafurahi sana kusikia hivyo"
"Usijali nakupenda sana siwezi kukuacha"
"Nashukuru mpenzi wangu"
Furaha na vicheko vilitawala kwao.
Navin alisahau yote na kufurahia mwanaume wake amekubali kumuoa, siku hiyo walishinda pamoja na kesho yake ilipofika Navin aliondoka na kurudi kwa mama yake mdogo.
"Mamdogo jiandae siku yoyote mkweo anatuma mshenga hapa walete barua ya uchumba" Navin alimwambia mamdogo akiwa na furaha tele.
"Wacha wee, usiniambie mbona nataka kupiga vigeregere kwa furaha"
Alisimama huyo mama na kufurahia sana.
"Naolewa mama mdogo yani ninaraha sana moyoni"
"Hongera mwanangu ndoa ni jambo la kheri hilo lazima ufurahie"
"Ndio nafurahi sana"
"Haya mimi nawasubiria kwa hamu sana"
"Sawa"
Furaha ilitawala kwao, akajulishwa hadi mama mzazi wa Navin aliyekuwa akiishi mkoani pamoja na ndugu wengine.
***
"Shangazi mimi nimekuja nia yangu nataka kuoa" Salim alimfuata shangazi yake aitwaye Latifa alikuwa mwanamke mcharuko sana kutwa shughuli kwenda ngomani kilasiku.
"Wacha wee mwanangu kidume umekua baba unataka kuoa? Aririririii..."
Alipiga vigeregere kwa furaha.
"Shida moja shangazi mwanamke ninayetaka kumuoa ni singo maza anamtoto mmoja na nyumbani Baba na mama wamekataa nisimuoe" Aliongea kwa huzuni Salim.
"Wanawazimu wale nakwambia Salim wazazi wako sio wazima! Singo maza ni ugonjwa kwani? Mwanamke angekuwa na ukimwi sawa shida anamtoto tena mmoja usimuoe? Wajinga kweli hao" Alisema shangazi Latifa.
"Ndio maana nimekuja kwako shangazi nataka kumuoa Navin nampenda sana"
"Kwanza nashukuru sana mwanangu umekuja kwangu unaakili sana wewe Salim. Mimi nakusaidia kilakitu tena ndoa itafanyika hapa kwangu unaoa kweupe mchana juakali wanga wote wakuone mwanangu umeoa, hao wazazi wako wakitaka waje waipotaka wasije au unasemaje?"
"Nipo pamoja nawewe shangazi yangu"
"Ewaaah piga tano mwanangu"
Waligongeshana mikono.

Itaendelea.
Usibonyeze hapa kama wewe ni mtoto

NAVINI 😍
NO: 03

"Sasa shangazi fanya mpango wa mshenga jumapili hii apeleke barua ya uchumba nyumbani kwao Navin"
"Hilo jambo dogo sana tena hela yakuweka kwenye barua natoa mimi lazima uoe mwanangu, singo maza na yeye ni mwanamke kama wanawake wengine anastahili kupendwa, kuolewa na kuheshimika kwenye jamii"
"Kweli kabisa shangazi"
"Unaona eeh? Mimi japokuwa wananiona mkorofi sijui mcharuko lakini nina akili zangu na hekima ninazo mwanangu. Nakwambia utaoa subiri"
"Sawa shangazi nashukuru sana"
"Usijali ukikwama lolote niambie shangazi yako narekebisha pesa sio shida zangu unanijua mwenyewe" Alisema akijitingisha, alikuwa amebandika kope ndefu, shingoni anacheni kubwa ya dhahabu. Hereni, Pete bangili zote alivaa dhahabu tupu. Alikuwa mwanamke mweupe sana alijichubua hadi mishipa ya kijani ilikuwa inaonekana. 
"Najua shangazi yangu"
"Sasa je? Wewe tulia utaoa mwanangu na utaishi na mkeo vizuri kabisa"
"Sawa nashukuru sana"
"Haya mwanangu"
"Basi acha mimi niende"
"Hamna shida nenda tutawasiliana"
"Sawa shangazi"
Salim aliondoka akiwa na furaha tele. Akatoa simu yake na kumpigia Navin.
"Mambo mpenzi"
"Safi baby kwema uko?"
"Kwema mama, sasa nilikuwa nakwambia nitakutumia pesa mfanye maandilizi na mkwe wangu, jumapili hii kuna ugeni posa inaletwa sawa?"
"Ooh jamani, nashukuru mpenzi wangu nitafanya hivyo"
"Sawa usijali ngoja nikutumie pesa"
"Sawa mpenzi"
Salim alihamisha kiasi cha pesa na kumtumia Navin ambaye alifurahia sana na kumjulisha mamdogo ambaye alimpigia simu mama yake kijijini na kumpa taarifa.
"Mdogo wangu nashukuru sana umeishi vizuri na Navin hadi amepata mume anaolewa? Nashukuru sana"
"Dada usijali jamani huyu ni mwanangu kikubwa tumshukuru Mungu"
"Ni kweli kabisa"
***
"Nishampata mshenga barua kaandika tayari nimeweka laki moja mwanangu, sasa umpeleke huko ukweni kwako" 
Siku ilifika na shangazi Latifa alimuita Salim kwake na kumkutanisha na huyo baba ambaye ni mshenga alikuwa na rafiki yake.
"Sawa shangazi nashukuru sana"
"Unashukuru nini sasa? Ni wajibu wangu wewe wala usijali"
"Sawa shangazi"
Salim aliondoka na wale washenga wawili na kuwapeleka hadi nyumbani kwao Navin ambapo kulikuwa na pirikapirika nyingi zakuwapokea wageni.
"Nyumba ndio hiyo hapo mimi naenda"
"Sawa hakuna tatizo"
Salim aliondoka hakuingia ndani. Wale wazee wawili waliingia na kupokelewa kwa furaha sana.
Barua ilitolewa na ikapokelewa vizuri.
Ndugu, jamaa na marafiki walikula na kunywa kwa furaha sana.
"Mama nimepeleka posa nyumbani kwao Navin na shangazi Latifa ndiye amenisaidia naomba basi kwenye ndoa yangu usikose mama yangu" Salim alimpigia simu mama yake na kumjulisha.
"Unasemaje wewe mtoto? Latifa ndiye alikuzaa? Hebu ngoja msinichezee" bi Sharifa alikata simu na kutafuta namba za shangazi Latifa na kumpigia huku kifua kikiwa kimejaa kwa hasira kali. 

Itaendelea.

NAVINI 😍
NO:04

"Hallo wifi" Simu ilipokelewa na shangazi Latifa.
"Wewe Latifa hivi kilichokufa umsaidie Salim kupeleka posa kwa huyo singo maza nini? Ulisikia nataka mwanangu aoe singo maza? Mbona kiherehere sana wewe mwanamke!" Alianza kuongea kwa kufoka bi Sharifa.
"Kwahiyo wewe mwanamke hujui kusalimia eeh? Bora huyo singo maza anaakili kuliko wewe mama Salim akili huna! Mwanamke mjinga sana yani badala yakutetea mwanamke mwenzio unamkandamiza. Singo maza si ugonjwa, na yeye anahaki yakuolewa kama wanawake wengine unanisikia wewe kifukutu?" Shangazi Latifa alimwambia wifi yake. Hapo alikuwa yupo zake saluni akibandika kucha. Alikuwa lishangazi la mjini, shangingi haswa. Hamna fasheni ilimpita hamna shughuli hakuarikwa, aliitwa rich aunty Latifa.
"Wifi ndio uniite mimi kifurukutu kweli?" Aliuliza bi Sharifa.
"Kwendraaaaa bibi wee kaka yangu alikustili tu mwanamke hujulikani mbele wala nyuma sijui ulianguka na mwali chooni, halooo!" Alicheka cha nguvu shangazi Latifa.
"Sawa nashukuru kwa matusi yako lakini sijapenda tabia ya wewe kumsaidia Salim amuoe huyo singo maza sijapenda kabisa na kwangu sitaki nikuone nitakumwagia hata maji ya moto mwanga mkubwa wewe"
"Mwanga mwenyewe, na hapo sio kwako kwa kaka yangu nakuja muda wowote nitakaotaka upo? Na kingine harusi tunayo na tunatamba nayo, singo maza ndani ya nyumba anaolewa kweupeeee Hahahaha!" Alicheka shangazi Latifa na kukata simu, alimuacha wifi yake akiwa na hasira sana.
"Imekuaje mbona nasikia habari za singo maza vipi?" Mdada wa saluni alimuuliza shangazi Latifa.
"Mwezangu nina kijana wangu mtoto wa kaka yangu anataka kumuoa mwanamke wake, sasa yule mwanamke anamtoto mmoja basi familia nzima hawamtaki amuoe, kijana akaja kwangu nimsaidie. Sijaona kosa la yule mwanamke leo wamepeleka posa uko mengine yaendelee na nitasimamia kilakitu lazima aolewe huyo binti kuwa na mtoto kwani kilema wamuache tu"
"Kweli kabisa mwanamke kuwa na mtoto sio sababu asiolewe"
"Ni kweli Latifa umefanya la maana sana kumsaidia huyo mwanao amuoe mpenzi wake"
"Ingekuwa mwanamke anaukimwi nisingekubali amuoe, shida ni mtoto tena mtoto mwenyewe yupo kijijini huko kwa bibi yake anasoma tatizo lipo wapi?"
"Hakuna tatizo mbona, fanya mpango wa sale tena"
"Hilo tena mnauliza?"
"Halooo harusi tunayo...
"Na tunatamba nayo"
"Hahahaha!"
Walisapotiana hapo.
***
"Baba Salim, kitendo alichofanya dada yako sijakipenda" bi Sharifa alimwambia mumewe ambaye siku hiyo hakwenda kazini.
"Kitu gani tena mama Salim mbona unanitisha?" Aliuliza huyo baba akiweka pembeni gazeti alilokuwa akisoma.
"Latifa amemtafutia wazee Salim na leo hii wamepeleka posa kwa huyo mwanamke wake singo maza"
Bi Sharifa alitamka singo maza kama kitu cha kuchefua alikuwa hapendi kabisa.
"Unasemaje?" Aliuliza baba Salim na kusimama wima.

NAVINI 😍
NO:05

"Ndo hivyo nakwambia, leo hii posa ishapelekwa huko kwao dada yako amenikera sana"
"Hivi imekuaje anaingilua familia yangu yeye kama nani? Ndiye mama wa Salim au?"
"Hata mimi sijui"
"Ngoja yule dawa yake ndogo"
Alitoa simu yake
"Unataka kufanyaje? Hee mpigie akuchambe unamjua Latifa hajapoa, mimi nimempigia kanichamba hadi kaniita kifurukutu"
"Hee kifurukutu ndio nini tena?"
"Hata najua basi anajua yeye aliyesema"
"Hahahah ila Latifa anamaneno"
"Kashindikana yule anamaneno mengi sana"
"Sasa tunafanyaje? Na swala akilishikiria Latifa ujue atalifanya kwa nguvu zote si unajua mama shughuli yule? Atasimamia kilakitu sisi wazazi tutaonekana hatuna akili"
"Mmh nakosa lakusema mume wangu"
"Kwa ilipofikia haina jinsi, Salim anamaanisha anataka kumuoa huyo mwanamke wake, sasa chakufanya mke wangu tushirikiane nao Salim amuoe"
"Mmh hapana kwakweli moyo wangu mzito hautaki kabisa mwanangu amuoe huyo mwanamke"
"Mke wangu kwani akimuoa unaishi nae wewe? Hebu tuwaache waowane, akiona ndoa chungu si wataachana kwani shida nini?"
"Sasa mwanangu akateseke kwenye ndoa kweli?"
"Ateseke na nini? Mwanaume anatesekaga kwani? Yule ni kidume acha amuoe. Mpigie simu Salim badae aje tuongee nae"
"Mmh haya"
Aliitikia kishingo upande bi Sharifa.
Akampigia simu Salim na kweli jioni yake alienda kwa wazazi wake.
"Tumekuita mwanangu, sisi tumekubali wewe umuoe huyo singo maza wako" bi Sharifa alianza kusema.
"Anaitwa Navin mama" Salim alimwambia mama yake hakupenda kuona akiitwa singo maza.
"Sawa haya Navin muoe na kilakitu tutakusaidia"
"Nashukuru sana wazazi wangu kuwa upande wangu"
"Usijali tusipokuwa upande wako nani tena atakuwa nawe"
"Kweli hakuna mwengine"
Ugomvi kuhus singo maza ukaishia hapo.
Mahari ilitolewa na mipango ya ndoa ilifanyika hatimaye ubani ukapita Salim na Navin wakawa wanandoa kamili.
Shangazi Latifa aliwafanyia sherehe kubwa ukumbini, hapo waliarikwa watu mbalimbali shughuli ilikuwa kubwa walikula na kunywa, wakatunzana hapo hadi kunakucha.
"Mwanangu nampa kiwanja kipo kigamboni, kina thamani na milioni 35" Shangazi Latifa alisema akirembua macho yake na mikope mirefu aliyoweka alikuwa kama katuni.
Bi Sharifa alikuwa anasonya pembeni.
"Anajifanya kumpenda mwanangu hana lolote mwanga yule" 

Soma mpaka mwisho wa story kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post