TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

KOKU 01-05

[8/30, 12:34 PM] Mr AB: KOKU 😋🫦♥️

NO: 01---------05
"Unashingo tamu" kwa sauti nzito, alininong'oneza sikioni,   akanipumulia pumzi yake ya moto. Nilisisimka sana! Nilitoa sauti bila kupenda. Kwa utaalamu mkubwa aliendelea kuinyonya shingo yangu na kuing'ata kimahaba. Nilizidi kupagawa, nililia bila kupenda.
Alishuka chini na kushika chuchu yangu moja akaanza kuipikicha kwa vidole yake vigumu kiasi. 
Ghafla akaivamia chuchu yangu ya upande wa kushoto na kuingiza mdomoni mwake.
"Oishhh.." nililalamika. Hakujali alizidi kunyonya ile chuchu na kuwa kama anaimung'unya.
"Jamaniii..aaah! Usini oooshsh" sijui nilitaka kusema nini maneno hayakueleweka.
"Tulia mke wangu" kwa sauti nzito aliniambia. Nilisisimka  sana, mwanaume alikuwa na sauti nzito nzuri iliyojaa mahaba mazito sana.
Aliendelea na zoezi lake la kunyonya chuchu na kuzipikicha hadi zikasimama na kuwa ngumu sana.
"Unachuchu tamu mpenzi" alizibusu na kuzidi kunivuruga.
Haikutosha akashuka chini kwenye tumbo langu kiukweli nimejaaliwa tumbo kubwa kutokana na unene nilionao. 
Kuna wakati hata nilikuwa naona aibu kuvua nguo mbele ya mwanaume kwa sababu ya tumbo langu ila huyu mwanaume hakujali.
"Unatumbo tamu sana mpenzi wangu" alisema akilinyonya kimahaba na kuning'ata ng'ata. Alinimaliza pale alipokuwa akizinyonya nyama za tumboni. Hadi mbavuni. Nilipiga kelele bila kupenda, 
"Kumbe hata tumbo kubwa lina raha yake" niliwaza nikiendelea kupokea raha hizo.
Kidume kiliendelea na kazi yake alishuka chini taratibu kwenye mgodi.
"Tanua mapaja mke wangu" nilikuwa mateka kwake naanzaje kukataa sasa? Nilitanua bila kupenda mguu mmoja magharibi mwengine kasikazini.
"Waooo" alichombeza akainamisha kichwa chake chini na ulimi wake ukazama mgodini na kuanza kudeki bahari.
Mwanaume alikuwa vizuri sana. Alikuwa mjuzi haswa sehemu hiyo nilijikuta nalia bila kupenda.
"Ooisshh taratibu jamanii...uuuuhh..nipe..nipeee oooh mama naaa..uuuh ashhhh" sauti yangu ni kama ilimzidishia wazimu alizidi kuzama chumvini.
Maji ya utamu yaliruka na kumchafua lakini hakuniachia aliendelea.
"Utaniua..inatosha..ni..a..cheee...ooooh"
Nguvu ziliniisha.
"Pole love..pole mke wangu.." aliniambia akaniacha. Akanikumbatia sikuwa na nguvu.
"Nimechoka" kwa sauti ya kichovu nilimwambia.
"Pole jamani ila mbona bado unachokaje mapema hivyo" aliniambia akicheka sijui aliniweka staili gani nikashtukia mchi upo ndani ya kinu akaanza kutwanga.
Utamu niliosikia hauna mfano. Sikuwahi kukutana na mwanaume mtamu kama yeye.
Nililia na kulia, niliongea hadi kizungu wakati niliishia darasa la saba hata English kozi sijawahi kusoma.
Mwisho sauti ilikauka. Mwanaume hakuniachia alinishughulikia haswa. Nilikojoa hadi nguvu ziliisha kabisa nikalala na kumuachia kila kitu.
"Pole sana mpenzi, nimekuchosha nisamehe nitakuja tena siku nyingine" aliinuka kifuani kwangu. Sikuweza hata kumuangalia macho hayakuwa na uwezo wa kuona vizuri. Nilimtizama kwa mbali alishuka kitandani nikamuona anavaa nguo ghafla akasogea mlangoni akafungua mlango na kutoka nje.
Sikujua kilichoendelea tena hadi niliposhtuka kumekucha asubuhi baada ya mlio wa simu yangu kuniamsha. Mwili mzima ulikuwa unauma kiunyonge nikainuka na kuchukua simu yangu shoga yangu Zulfa alikuwa amenipigia simu nikapokea.
"Wewe Koku upo wapi hadi sasa hujatokea dukani?" 
Kwanza nilishtuka. Akili yangu kama ilirudi nilipata nguvu na kukaa kitako simu nikaiweka pembeni bila kumjali rafiki yangu nilisikia akisema.
"Haloo..halooo Koku" aliita lakini sikujali akili yangu ilihama sikuelewa.
"Hivi nini kimenitokea jana usiku? Ile ni ndoto au? Yule mwanaume ni nani?" Nilijiuliza maswali mengi bila kupata majibu nikajaribu kuvuta sura ya yule mwanaume sikuweza kuikumbuka.
"Inaweza kuwa ndoto" nilijifariji ila ghafla nikakumbuka kitu. Nikashusha mkono wangu hadi kwenye sehemu zangu za siri. Ajabu nilikuwa nimetumika na mbegu za kiume zilijaa nyingi.
"Mungu wangu! Kumbe ni kweli sio ndoto oh masikini mimi!" Nilianza kulia.

Itaendelea.

KOKU 😋🫦♥️

NO: 02
Wakati naendelea kulia simu yangu iliingia meseji. Nikanyamaza na kuichukua. Nikaona meseji ya tigopesa nikaifungua na kusoma.
"Umepokea shilingi laki moja kutoka kwa wakala Kivuyo Athuman" muamala ulisomeka hivyo. Nikashangaa! Kwanza nikajifuta machozi na kurudia kusoma tena.
"Mh nani kanitumia hii pesa?" Nilijiuliza mwenyewe.
"Au wakala kakosea namba?" Bado nilizidi kujiuliza bila kupata jibu. Nilikaa nilifikiria bila kujua.
"Ah nikaoge kwanza maana nanuka jasho la mwanaume nisiye mjua" niliinuka kiuvivu na kusimama. Zile mbegu za kiume ukeni kwangu zilinikera sana.
"Mijini mingine sijui haijui kama kuna kondom unanifanya usingizini na mimbegu yako unaiacha tu si ungevaa kinga mxiuh shenzi zako uko ulipo" nilichukia kwa hasira nikatoa shuka ambalo lilikuwa limechafuka nikajifuta zile mbegu baada ya hapo nikalikunja kunja na kuliweka pembeni.
Nikachukua beseni na kujaza maji lile shuka nikaliweka ndani ya lile beseni na juu nikanyunyizia sabuni ya puff.
Baada ya hapo nikaifua haraka haraka maji machafu nikamimina kwenye ndoo ya chooni. Nikaweka maji masafi nikaisuuza na kuiweka pembeni.
Mwilini nilikuwa mtupu sijavaa nguo yeyote, ikabidi nichukue upande mmoja wa kitenge na kujifunga kuanzia kifuani nikabeba ndoo yenye maji machafu mkono wa kulia na mkono wa kushoto nikabeba ile shuka niloifua hadi nje.
Nyumba ninayoishi ya vyumba vya ndani vinne ambavyo wapangaji wote walikuwa wasela hakuna anayeshinda nyumbani kila mtu na mishe zake kurudi usiku au siku za wikiendi mara moja moja ndio tunaonana.
Nilipofika nje kwenye kamba nikaanika ile shuka na kumwaga yale maji. Nje ya nyumba kuna kisima nikaenda na kujaza ile ndoo nikapeleka bafuni. Nikarudi ndani nikabeba mswaki pamoja na sabuni nikarudi bafuni nikaoga na kujisafisha.
Nilipomaliza nikarudi ndani na kuchagua gauni nikavaa na kutoka.
Nikiwa njiani niliangalia simu yangu nikakuta Zulfa alinipigia na kutuma meseji za lawama sana na ile meseji ya pesa bado ilikuwepo.
"Sina hela halafu watu wanakosea kutuma pesa watajua wenyewe naenda kuitoa" nilisema peke yangu nikitembea. Nikaenda hadi kwenye kibanda cha tigopesa nikaitoa ile pesa yote. Moja kwa moja nikaongoza kwenye baa moja na kukaa hapo.
"Niletee supu ya mbuzi na chapati mbili" nilimwagiza mhudumu aliyefika kunihudumia.
Baada ya muda mfupi aliniletea. Nilikuwa na njaa sana nilikula yote.
"Niletee pepsi na maji lita moja ya baridi" niliagiza nikaletewa nikanywa pepsi yote. Yale maji nilikunywa nusu nikalipa pesa. Nilishiba mno nikapumzika kidogo mwisho nikatoka nje na kuchukua bodaboda.
"Nipeleke Kz Cosmetics" nilimwambia huyo mwendesha boda boda. Safari ikaanza hiyo haikuwa mbali sana tukafika nikamlipa na kuingia dukani.
"Hee Koku ndo nini umefanya leo?" Nilifika nikapokelewa na lawama za Zulfa.
"Niache nikae chini kwanza, tena unipe pole yani ungejua yalonikuta mwenzio ungekuja mbio nyumbani sio kusubiri nifike hapa utoe lawama" nilimwambia nikiwa nimekaa chini ndani ya duka letu kubwa la vipodozi.
Ni duka ambalo tulichanga msingi mimi na Zulfa na kuamua kufungua na kuuza pamoja. 
"Haya yamekukuta yapi tena?" Zulfa aliniuliza.
"Kwanza nipe pole shoga"
"Hee pole bila kujua kama ulikuwa na bwanako Kirungu miye nikupe pole ya nini?"
"Umeanza uchizi wako  bwanangu sio Kirungu bwana"
"Bibi wee Kirungu yule sura fii kama alolipukiwa na bomu simpendi nyoko yule"
"Zulfa sitaki muache mume wangu"
"Hehehee haloooo halo ya mume wee mume hiyo kwio mume anaye panya itakuwa wewe na Kirungu wako ha ha haaa"
"Mshenzi wewe na sikuadithii yalonikuta"
"Aah bibi wewe tuachane na Kirungu hebu nambie mpenzi wangu yamekukuta yapi mabebi?"
"Mh mazito ndugu! Sijui niseme nimebakwa sijui nimetoa mzigo mwenyewe..
Kabla hajaendelea Zulfa akadakia.
"Wee usinambie umepata bwana mpya"
"Bibi wee tuliza mshono hakuna bwana mpya wala wa zamani nimefanywa tena na jini"
"Mtumee huyo jini umempata wapi?"
Zulfa alishika tama mkono shavuni ikabidi nimueleze ule usiku ulivyokuwa.
Zulfa alibakia katoa macho anashangaa.
"Dunia hii inamambo sana"
"Shoga asubuhi nimefua shuka mbegu za kiume kibao baba yule kajua kunimwagia"
"Masikini nakuhurumia lakini jamaa yupoje mchezoni?"
"Si nimekwambia anayajua kaka mtamu yule uwiii hatarii sijaona mwanaume mtamu kama yule"
"Wee usiniambie shoga yangu umeukatikiaje na miuni yako ile uwiii shoo ilinogaje kwanini hamjaniita nipige chabo nile kwa macho ila nimefurahi kupata shemeji jini yule Kirungu uachane nae sasa"
"Zulfa maneno gani hayo sasa?"
"Bibi wee mpet pet mumeo jini achana na Kirungu simpendi yule na kichwa chake kama kitunda cha ubuyu"
"Ha ha haaaa Zulfa chizi wewe ujue"
"Chizi mwenyewe shemeji yangu jini nakupendaaa sanaaa" kwa sauti kubwa Zulfa alisema nilicheka sana.

Itaendelea.

KOKU 😋🫦♥️

NO: 03
"Tena sijakwambia Zulfa mwenzio leo sijui nani kakosea kutuma pesa imekuja kwangu" nilimwambia kuhusu ile pesa nilotumiwa na wakala.
"Bahati hiyo shoga umetumiwa bei gani?"
"Laki moja"
"Wee usiniambie! Kwahiyo ulimrudishia au imekuaje?"
"Nimrudishie nani na shida hizi nimeenda kwa wakala kutoa mtu mwenyewe simjui nani pesa imetumwa kwa wakala nimesubiri nipigiwe simu kimya nifanyaje sasa?"
"Achana nao maisha magumu wanajifanya kukosea namba nipe elfu ishirini mwaya"
Nilitoa ile pesa nikampa elfi thelathini Zulfa.
"Na lanchi mchana juu yangu" nilimwambia.
"Weweeee piga kelele kwa bosi lady akeee"
Zulfa alifurahia nilicheka.
Mara wateja wakaanza kuingia ikabidi tuwe bize kuwahudumia na maongezi yakaishia hapo. Tukaendelea na kazi yetu hadi mchana ulipofika tulifunga duka na kwenda sehemu ya chakula tuliagiza na kula pamoja tulipomaliza tukarudi dukani kazi ikaendelea.
Usiku saa tatu tulifunga duka kila mmoja akatoka na kwenda nyumbani kwake.
"Usiku mwema mpenzi kesho uwahi kufungua" Zulfa aliniaga.
"Sawa nitawahi kwaheri" 
Tuliagana.
Nilirudi nyumbani nikiwa nimechoka sana nikafikia kuoga na kupanda kitandani. Usingizi ulinipata haraka mno.
Ghafla nikaanza kuota yule mwanaume wa jana amefika.
"Pole na kazi kipenzi changu, umechoka sana ngoja nikukande mwili wako" alinitoa shuka nilojifunika na bahati mbaya nilikuwa nimezoea kulala bila nguo zaidi ya kujifunika shuka tu.
Mwili wangu ulikuwa mtupu bila chochote, alinigeuza kifudifudi akatoa mafuta na kunipaka taratibu akaanza kunikanda nilijisikia raha kiukweli, mikono yake iloyojaa misuli ilokomaa na yenye nguvu ilipokuwa ikinikanda mwili wangu nilihisi burudani sio kidogo na yote mpenzi wangu Hosea ambaye Zulfa alizoea kumuita Kirungu hakuwahi kunifanyia hivyo kwanza alikuwa bahiri sana, hakuwa romantic kabisa yeye mapenzi yake yalikuwa kitandani tu tukitoka hapo hana habari na mimi. Tabia yake ilikuwa inanikera sana ila sikuwa na la kufanya.
****
Mwanaume wangu wa usiku aliendelea kunifanyia masaji mwilini. Aliendelea hadi alipomaliza kuninyoosha viungo vyote akalala pembeni yangu.
"Napenda kukutizama ukiwa unafumba macho yako mazuri, unasura nzuri sana mpenzi huniishi hamu napenda mwili wako mlaini. Tumbo lako tamu hakika sijutii kukupenda" Aliongea kwa sauti nzito haswa iloyonisisimua.
Nilitamani kuongea kumuuliza yeye nani ila mdomo ulikuwa mzito maneno hayakuweza kutoka zaidi yaliishia akilini mwangu tu.
"Najua unamaswali mengi sana juu yangu. Usijali mama ipo siku utanijua ila tambua mimi ndio mumeo, lala salama mpenzi nitakuja kesho kukuona tena" Aliinama na kunibusu mdomoni na kwenye paji la uso. Nilifarijika kiukweli, akafungua mlango na kutoka nje nilitamani nisimame nimuone wapi alipoelekea lakini sikuwa na nguvu usingizi mzito ulinipitia nililala hoi.
Nilishtuka tayari kumekucha asubuhi nilikurupuka haraka nikabeba ndoo ya maji na kutoka hadi bafuni nikajimwagia fasta na kutoka nikavaa nguo na kuondoka. Nje nilichukua boda boda hadi dukani nikafungua na kuingia ndani.
Siku hiyo Zulfa alichelewa kufika nilimuwahi hadi saa nne ndio akafika.
"Shoga mambo, jana nilikuwa na shemejio basi kanichosha mjinga yule hadi nimechelewa kuja kazini" Alianza kulalamika.
"Pole mpenzi ndo mahaba hayo mwaya"
"Aah mahaba gani kuuana tu mtu kama katoka jela kifuani masaa matatu sijui alinipakia mkongo yule ujue Shabani anamambo ya kipuuzi sana siku hizi anaenda shoo muda mrefu nimemshtukia jana nikamchamba asinipakie mkongo mimi atafute kahaba uko amlipe ndo ampakie yani kanichefua sana" Zulfa alizidi kulalamika nilicheka mno.
"Pole ndugu yangu ila kaona akuridhishi ndo maana kaamua apake mkongo ufurahi"
"Hakuna kuridhishana sio hadi masaa kumi kifuani hata nusu saa muhimu ajue wapi anishike sio kupiga mihuri tu kama afisa wa nini nyoko yule kanikera"
Nilicheka mno.
"Kupiga mihuri ndo kufanyaje tena?"
"Heee hujui? Mwanaume anashindilia tu hakuna mauno hakuna kuchombeza hiyo ndo mihuri kang'ang'ania kati hapo hapo haendi kulia wala kushoto sijui alikatwa hospitali hakwenda jandoni yule aah simtaki tena bora nibaki mjane"
Nililala chini kwa kicheko Zulfa alikuwa muongeaji sana nilicheka mno hadi mbavu ziliuma.
"We cheka tu yatakukuta, na shem jini vipi usiku alikuja?"
"Mwezangu kaja anaachaje sasa kashapata mke"
Tuligongesheana mikono na kucheka.
"Enhee nipe ubuyu shoo ilikuaje?"

Itaendelea.

KOKU 😋🫦♥️

NO:04
"Mwenzangu nilirudi nimechoka nikajimwagia maji nikapanda kitandani kulala"
Nilianza kumuadithia Zulfa.
"Enhee ikawaje ndugu yangu?" Aliuliza akiinuka kwenye kiti na kukaa chini.
"Sasa mbona unakaa chini jamani?" Nilimuuliza.
"Aah uko juu sisikii vizuri naona nachelewa bora nikae hapa chini nikusikie kwa karibu" Maneno ya Zulfa yalifanya nicheke, nikaendelea kumuelezea sasa.
"Nakwambia ile usingizi umenipitia tu! Mwanaume wa usiku kaja ila anasauti tamu mashaallah sauti ya kiume bwana hadi nimepagawa"
"Weewee hapana chezea shem darling akee" 
Tulicheka na kugongeshana viganja vya mikono.
"Enhee nipe ubuyu shoga ikawaje?"
"Zulfa kwa kupenda umbea sasa!"
"Ha ha haaa umbea suna bibi wee endelea"
"Basi akaanza kunichombeza oh mke wangu pole na kazi umechoka sana ngoja nikukande mwili! Shoga yangu kama unavyonijua sipendi kulala na nguo nishazoea kulala mtupu"
"Tenaa kwa raha zako ungelala na nguo ungemtamanisha saa ngapi shem jini umejiachia hadi majini wamepegawa" nilicheka sana.
"Basi mwezangu nikaanza kufanyiwa masaji konk nililegea mwili wote, kaka anamikono yenye nguvu yule sijui ndo Samson wa Delila yule wa kwenye Biblia yani hatari tupu, masaji yaliyoenda chuo yenye digrii na vyeti vyake, Zulfa nilivurugwa"
"Unafaidi Koku hadi raha huyo shemeji hana mdogo wake aje kwangu na mimi?"
"Acha uchizi wako ha ha haaa!"
"Ushanitamanisha mwenzio huyo ndo mwanaume sasa sio hawa wanaume zetu wanatupakia mkongo nguvu za kiume hawana shida tupu aah mi washanichosha leo shem akija mwambie na mimi nataka mume anipe hata babu yake"
"Uwiii Zulfa huna akili wewe ha ha haaa"
"Ninazo bwana nishachoka kuchezewa na wanaume wasiojielewa hela hawatoi nguvu za kiume hawana sasa ya nini kuwa nao?"
Nilicheka sana.
Wakati tunaendelea kuongea ghafla aliingia dukani Hosea yule mpenzi wangu.
"Mh mauzauza mengine hayo watu tuna shem jini lenyewe sijui limetokea wapi mfyuu" Zulfa alisimama na kutoka nje. Walikuwa hawapatani yeye na Hosea mara nyingi Zulfa alikuwa akimchamba Hosea na kuishia kugombana.
"Karibu" nilimkaribisha Hosea.
"Asante, mambo"
Alinisalimia akikaa kwenye kiti kile alichokalia Zulfa mwanzoni.
"Safi tu"
"Upo kimya mpenzi hadi nakumisi"
"Hamna miye nipo bize tu mambo mengi"
"Oh pole mke wangu"
Niliguna nimeitwa mke sio bure kuna jambo.
"Asante"
"Sasa baby mwenzio nina shida najua utanisaidia mumeo nisiadhirike"
Alianza nilijua tu kuna bomu litaripuka.
"Shida gani?" Nilimuuliza.
"Nahitaji elfu hamsini nataka kwenda bagamoyo kuna ishu nafuatilia"
"Mmh sawa ila mi sina hela biashara yenyewe ngumu nipo nipo tu"
"Daah Koku usinifanyie hivyo please nipe pesa mwenzio dili likitiki tutaishi vizuri mpenzi unajua wewe ndo mke wangu nitakuoa tutaanza familia yetu" 
"Nimekusikia ila mimi hela sina kwahiyo nikaibe?"
Hosea alisimama kwa hasira na kunikunja.
"Naona nakubembeleza tu unanipa hiyo hela au unipi?"
"Heeee! Ndo unataka kunipiga?"
"Sio nataka nitakupiga toa pesa?"
"Sina pesa nikupe matako hebu niachie mimi"
"Sikuachii nakwambia"  akanipiga kibao usoni sikukubali nikajikakamua na na mimi nikamrudishia.
"Aah umekuwa jeuri unanirudishia sasa subiri"
Akaniachia akawahi droo yenye hela na kufungua. Kulikuwa na milioni tatu mauza ya siku mbili ambayo hatukupeleka bank kutokana na ubize wetu akaanza kukomba zile hela nikatoka mbio nje.
"Zulfaaaa.wee Zulfa weweee" nilimwita Zulfa ambaye alikuwa fremu za mbele anapiga umbea.
"Kimbia njoo"
Zulfa akajua kimenuka akatoka mbio na kuja dukani kwetu.
"Kuna nini?" Aliuliza.
"Hosea anachukua hela ndani kanivamia na kunipiga" Nilimwambia na ghafla nikamwona Hosea anatoka ndani mbio.
"Uwii kachukua hela anakimbia"
"Wee asinitanie mwiziiii huyo jamani mwiziiiii kaiba hela dukaniiiii mkamateniii mwiziiii" Zulfa alipiga kelele huku akimkimbiza Hosea. Watu wakajaa na kuanza kumkimbiza wakitilia mwizi na Zulfa akiongeza sauti juu zaidi.

Itaendelea.

KOKU 😋🫦♥️

NO: 05
Watu walijaa zaidi na wengine wakamkamata Hosea na kuanza kumpiga. Muda mfupi tu Hosea alitapakaa damu na uso wake ulivimba sana.
"Mpigeni mshenzi huyo anaacha kufanya kazi anategemea kuibia wanawake mbona sisi hatudangi tunajitafutia kwa jasho letu mmalizeni kabisa" Zulfa alikuwa akisema kwa sauti na watu walizidi kumpiga Hosea.
"Zulfa wanamuua jamani waambie wamuache" nilimuonea huruma kiukweli.
"Nini wewe? Hebu kelele uko acha wamfunze adabu akitoka hapo ajue kufanya kazi na kutafuta kwa jasho lake mjinga huyu! Muueni kabisa" Zulfa alisogea mbele akampokonya gongo kijana mmoja na kumtwanga nalo la kichwa Hosea. Roho iliniuma sikuweza kuendelea kuangalia niliondoka na kurudi dukani nikakaa chini.
Ghafla nikaona watu wakitawanyika na difenda la polisi likafunga breki pale alipokuwa akipigwa Hosea. Na Zulfa naye alikuja mbio dukani akakaa chini nilipokuwa mimi tukawa tunatizama kule lile difenda liliposimama, wakashuka maaskari wawili wakaubeba mwili wa Hosea ambaye alikuwa amepoteza fahamu wakampakia kwenye gari na kuondoka naye.
"Bora tumemkomesha!" Alisema Zulfa akinitizama.
"Hela hizi alizoiba milioni mbili yani mauzo yote alisomba mjinga yule kanikera" alisema Zulfa akiwa ameshika zile pesa.
"Zulfa sio sawa kumuitia mwizi ona alivyopigwa ameumia sana na sijui wale polisi wamempeleka kituo gani masikini"
"Mxiuuh nenda mfate bwanako tena koma kuongea ujinga mbele yangu" alisimama Zulfa na kuingia dukani. 
"Na siku imeharibika nafunga duka kama unakitu chako ndani beba tuondoke maana tusije kukosana hapa nishatibukwa" alisema akianza kufunga milango, nilisimama na kuingia ndani ya duka nikabeba mkoba wangu na kutoka, Zulfa akafunga duka na kuondoka. Sikuwa na budi na mimi nikatoka na kutafuta usafiri nirudi nyumbani ilikuwa jioni tayari.
****
Nilifika nyumbani nimechoka mwili na akili, nilifungua mlango na kuingia ndani, nikasimama nikitazama chumba changu kama ndio mara ya kwanza kukiona mawazo mengi yalinijaa akilini. Zaidi swala la Hosea lilinikosesha raha niliumia kiukweli.
Sikutegemea kama ingekuwa vile, kiuvivu nikasogea hadi kitandani na kukaa hapo mawazo yakizidi hadi kichwa kilianza kuniuma, nilivua nguo nikajifunga kanga na kujaza maji kwenye ndoo nikaenda bafuni nikaoga na kurudi ndani, nilitupa kanga pembeni nikiwa mtupu nilijilaza kitandani.
Sababu ya uchovu usingizi nao ulinipitia, 
"Amka Koku ule chakula najua umechoka" nilikuwa ndotoni ila akili na mawazo yangu yalikuwa wazi niliweza kujua yote yanayoendelea. Nilijiona nimeamka na yule mwanaume wa usiku alikuwa pembeni yangu alinipa sahani yenye chakula. Kilikuwa chips na kuku. Nilikuwa na njaa nilikumbuka hekaheka za kutwa sikuweza kula kabisa, njaa niliyonayo sikuweza kukataa nilikula kile chakila chote uku yule mwanaume akiwa pembeni yangu akitabasamu.
"Asante" nilijaribu kumwambia ila sauti haikutoka maneno yangu yaliishia kwenye hisia tu sikuwa na uwezo wa kuongea.
"Usijali Koku nipo kwaajili yako kuhakikisha unakula na kukaa vizuri, nitakulinda kila dakika hakuna lolote litakalokutokea wewe ni wangu nakuahidi nitakuoa" aliongea huyo mwanaume ambaye sikujua hata jina lake ni nani.
"Kwanini nashindwa kuongea natamani nikufahamu zaidi wewe ni nani?" Kwa vile alijua mawazo yangu niliongea nikijua atanisikia japokuwa sauti haitoki.
"Mimi ni binadamu kama wewe usiniogope mimi si jini, nakupenda Koku vumilia ipo siku utaweza kuongea na mimi kwasasa muda bado" alisema akinitizama. Alikuwa mwanaume wa kawaida hatishi si mwarabu mweusi mwenye haiba ya kiume ila alifanana na wale wamarekani weusi alikuwa mzuri. Nilimtizama sana usoni nikimchunguza na kuishika sura yake ya kuvutia.
"Nakupenda, usiku mwema mpenzi wangu" alinisogelea akanibusu mdomoni akasimama na kupiga hatua. Kiukweli sikutamani aondoke nilitamani kumuita sikuweza. Nilibakia naumia moyoni!
Alipofika mlangoni akageuka na kunitizama.
"Baby nitakuja kesho usijali nipo kwaajili yako" akanikonyeza akafungua mlango na kutoka. Nilipagawa! Sio siri nampenda huyu mwanaume wa usiku. Sikuweza kulala nilibakia na mawazo nikitazama mlangoni labda atarudi haikuwa hivyo! Oh masikini moyo wangu.

 KOKU 😋🫦♥️

NO:06
Sijui usingizi ulinipitia saa ngapi, nilishtuka kumekucha. Niliamka kiuvivu nikashika simu yangu na kukuta missed call nyingi Zulfa alinipigia. Nilipiga mihayo kiuchovu ilikuwa saa mbili asubuhi. Niliamka na kuvaa kanga nikabeba ndoo na kutoka hadi bafuni nikaoga na kusafisha kinywa nikarudi chumbani. Nilivaa na kujiandaa nikatoka na kufunga mlango vizuri.
"Mambo nakuja nipo njiani" nilimtumia meseji Zulfa. Nikatafuta bodaboda iliyonipeleka hadi dukani ambapo nilimkuta Zulfa amekaa chini anakunywa chai.
"Karibu mrs jini" alinikaribisha Zulfa akitabasamu. Nilijihisi kuchoka mno! Nikajibwaga chini na kukaa nikiegemea kiti kilichokuwa pembeni.
"Za tangu jana?" Nilimsalimu.
"Nzuri tu, kumekucha siku nyingine Mungu atuepushie mauzauza" alisema niliishia kucheka.
"Nimechoka sana" nilimwambia.
"Shem jini kakuchosha na leo"
"Hapana yale majanga ya jana yalinichosha sana mwili na akili havina kazi"
"Mh pole, mumeo nae hajambo?"
"Mume gani?"
"Mwanaume wa usiku"
"Mmmh hajambo"
"Mbona umeguna?"
"Jana amekuja tena"
"Wee nipe khabari ikawaje?"
"Nimebahatika kuiona sura yake ni mwanaume mzuri mno Zulfa"
"Eeh lazima awe mzuri majini ndo walivyo wapo kama waarabu wazuri ndevu nyingi nywele ndefu hadi raha na weupe wao mashaallah jamani!"
"Mh Zulfa yule sio mwarabu ni mweusi!"
"Wewe usiniambie sasa jini gani mweusi au mchawi?"
"Yule kaka ni mweusi mzuri kama mmarekani mweusi urefu wake kama wale wacheza basketball na jana ameniambia yeye si jini ni binadamu"
"Mh makubwa! Ukichelewa kufa unajionea mengi"
"Zulfa nimechoka sana na maneno yake kaniacha na mawazo sana"
"Pole shoga yangu, sasa utafanyaje au nikupeleke kwa mganga?"
"Hapana"
"Kwanini tena?"
"Sio siri nampenda tena nampenda mno jana ndo nimegundua ilo nampenda yule kaka mwenzio sitaki kwenda kwa mganga wala kanisani awe jini au mzimu namuhitaji sana nampenda kwakweli"
"Loooh! Kupatwa kwa kupenda uku watu wamependa majini halooo nicheke mie"
"Cheka tu omba yasikukute"
"Haya shoga ngoja nikuagizie chai unywe mrs mwanaume wa usiku maana ushasema sio jini atakuwa kibwengo"
Alisimama Zulfa na kutoka akaniacha nimekaa taswira ya yule mwanaume inanijia akilini nikajikuta natabasamu mwenyewe.
"Nakuahidi nitakuoa" nilikumbuka maneno yake nilitamani iwe leo. Kweli kupenda kubaya.
"Haya mwezangu mbona unatabasamu peke yako?" Zulfa aliingia na kunikuta natabasamu.
"Nimemkumbuka mpenzi wangu"
"Tusio na wapenzi mbona tutakoma mwaka huu" alisema akikaa chini, nikacheka.
Baada ya muda kidogo mdada anayeuza chai alifika na sinia akanitengea chai ya maziwa na maandazi mawili akaondoka.
"Toa shavu mama jini na akija tena mwambie akutajie jina lake ndo mapenzi gani simjui shemeji yangu jina lake nikimtunga usikasirike"
"Jishaue umtunge jina la ajabu sitaki"
"Basi muulize anaitwa nani"
"Sawa nitamuuliza"
Nilianza kula Zulfa alisimama na wateja wachache walifika akawa akiwahudumia.
***
Siku iliisha salama jioni ikafika, tukaanza kufunga duka letu.
"Koku najua unapenda bendi leo Malaika wanapiga Kona bar ujue?" Zulfa alinambia.
"Shoga yangu umenigusa kunako, wanaanza saa ngapi?" Nilimuuliza.
"Kwenye saa tatu hivi kunaanza kuchangamka"
"Sawa sasa turudi nyumbani tukajiandae mida hiyo tukutane au unaonaje?"
"Sawa mimi nawahi mapema na savanna zangu utanikuta"
"Unajishaua mi nitakunywa soda tu"
"Nyoo usijifanye mlokole ukai karibu yangu"
"Ha ha haa badae bwana" 
Tulifunga duka kila mmoja akaondoka na njia yake.
Nilifika nyumbani nikaenda kuoga, nikajiandaa na kusimama kutoka. 
Nikafunga mlango nje nikachukua usafiri hadi Kona baa, nikawasiliana na Zulfa tukakutana, mwezangu aliagiza Savanna mimi nilikuwa nakunywa Castle lite. 
Bendi ilianza nyimbo mbali mbali zikawa zinapigwa, pombe nazo zilikolea kichwani. Tukawa tunasimama na kwenda mbele tunacheza tunarudi tunaendelea kunywa.
Mara kwa mara tulikuwa tunaensa chooni kukojoa kutokana na pombe tunazokunywa, nilisimama nikaongoza hadi chooni, nikajisaidia na kutoka. Ghafla mkono wa kiume wenye nguvu ulinivuta na kunipeleka pembeni ya choo kwenye giza. Sikutarajia ili mapigo ya moyo yalienda mbio sana, Niliogopa na kuanza kutetemeka.
"Koku unafanya nini hapa nani amekuruhusu kunywa pombe?" Sauti ya kiume iliniuliza nilizidi kuogopa na mbaya zaidi sauti niliifahamu haikuwa ngeni.
"Wewe nani?" Niliuliza sauti yangu haikutoka. Nilizidi kuogopa nikakumbuka hii hali inanikuta wakati gani. Nilijaribu kumtizama usoni huyo mwanaume macho yangu yakagongana na macho ya mwanaume wa usiku. Moyo ulishtuka. Pombe zote ziliisha kichwani.

Itaendelea.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post