TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

DEREVA MUUAJI 2

HITMAN DRIVER-02
                                                      (Dereva Muuaji)

Muandishi…………………….AZARIA G.MSULWA
Wasiliana nami……………..0657072588/0742334453
Kurasa zangu za kijami zote zina tumi jina la @StoryZaEddy-tz 

ILIPOISHIA
“Mumemuona yule fala?”
Kijana mmoja mwenye asili ya kihindi akiwa amesimama kwenye chumba kimoja cha gorofa ya hoteli hiyo ya gorofa iliyo toa eneo lake kwa ajili ya kufanyika kwa shehere hiyo.
“Ndio mkuu”
“Nahitaji mumteka kimya kimya kwa sababu amemchukua demu wangu, nataka kumuonyesha ni namba gani mapenzi yana uma”
“Sawa mkuu andika kazi imeisha si yule boya anaye rusha rusha pesa”
Kijana huyo wa kihindi akatoa simu mfukoni na kuwaonyesha wanaume hao wanne picha ya Jol na wakatingisha vichwa wakimaanisha wameelewa na wakatawanyika na kuingia katika sherehe hiyo na kumfwatilia Jol hatua hadi hatua ili wakipata nafasi wamteke bila ya mtu yoyote kugundua chochote

ENDELEA
“Baby nina hamu bwana”
Jol alimgong’oneza Glory.
“Umechukua room”
“Hapana baby si unajua hoteli hii ni ya baba hivyo nikichukua room hapa ata zingua na hata kukodisha kwenye hapa nimemtumia rafiki yangu kufanya hivyo”
“Basi twende kwengine japo bby sherehe yangu haijaisha”
“Usijali tuna enda kisha tuna rudi”
“Sawa mimi sina la kusema mpenzi wangu”
Jol na Glory wakaondoka hotelini hapo na kuwafaya watekajaji walio pewa jukumu la kumteka kuanza kumfwatilia kwa ukaribu. Taratibu Jol akaanza kuyachezea maziwa ya Glory huku mkono mmoja akiendesha gari.
“Baby tupo barabarani”
“Kidogo”
“Angalia usije ukagonga mume wangu”
Glory alizungumza kwa sauti iliyo jaa mahaba na kumfanya Jol kupunguza mwendo wa gari na akalisimamisha pembezoni mwa barabara ambayo haina magari mengi.
“Nimeshindwa kustahimili baby”
Jol alizungumza huku akilaza siti ya Glory, kutokana sio mara yao ya kwanza kufanya  mapenzi ndani ya gari, Glory hakuwa na hiyana yoyote zaidi ya kukubaliana na kile anacho kihitaji Jol. 
“Wamesimama”
“Funikeni nyuso”
Kiongozi wa watekaji hao alizungumza huku wakipunguza mwendo wa gari yao na wakasimamisha gari nyuma ya gari la Joly, wakashuka wanne na umuacha dereva, wanne walio shuka kila mtu ameshika bastola mkononi mwake. Wawili wakazunguka upande wa Jol huku mmoja akizunguka upande alio kaa Glory. Kwa kutimia kitako cha bastola, wakavunja kioo cha upande wa Jol, kwa haraka wakafungua mlango na kumchomoa Jol ambaye tayari alisha vua suruali yake na kusalia na boksa. Kwa kutumia kitambaa chenye dawa maalumu ya usingizi wakampachika Jol kitambaa cha puani na kurupuka yake ya kuleta ubishi mbele ya watekaji hao ikaisha. Wakamuingiza Jol ndani ya gari waliyo nayo aina ya Toyota Alphad. Wakamuingiza Glory ndani ya gari huku naye akitulizwa na kwa kuwekawa kitambaa chenye dawa ya usingizi.
“Endesha gari yake tukaitelekeze”
Mmoja wa watekeji alimuambia mwezake mmoja na akakimbilia ndani ya gari ya Jol, akafunga Milango na wakaondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi. Wakafika kwenye moja ya situ mbezi Luis na wakaiteleleza gari ya Jol, na aliye iendesha gari hiyo akaingia ndani ya gari la wezao na safari ya kutoka ndani ya jiji la Dar es Salaam ikaanza huku gari hiyo ikiendeshwa kwa mwendo mkali.
                                                                                        ***
Mama Jol ashusha pumzi taratibu na kukiweka kando kitabu cha President’ Wife anacho kisoma kilicho andikwa na muandishi Azaria Msulwa. Akavua miwani yake na kutazama saa ya ukutani, ndani ya chumba chake hicho. Akashusha pumzi taratibu, akaichukua simu yake na kuipiga namba ya Jol, ikaita kwa mara kadhaa hadi ikakatika. Akarudia kupiga kwa mara mbili ila haikupokelewa. 
‘Saa tano…Mmmmm’
Alizungumza kimoyo moyo huku akinyanyua kitabu hicho na kuanza kusoma, ila hazikupita dakika mbili akakiweka tena pembeni na akasimama mara baada ya kusikia mnguruo wa gari. Akafungua dirisha la chumba chake kilichopo gorofani. Akatazama nje na kuona gari za mume wake tatu zikiingia. Akashusha pumzi huku akiwa na wasiwasi kidogo. Mlango wa chumbani kwake ukafunguliwa na mzee Mashushua akaingia.
“Hujalala hadi sasa hivi mke wangu?”
Mzee Mashushu alizungumza kwa sauti ya kilevi huku akimsogelea mke wake na kumbusu shavuni.
“Namsubiria Jol”
“Ameenda wapi usiku wote”
“Aliniaga ana kwenda kwenye birthday ya mpenzi wake”
“Hahahaa Jol na mawenge yake naye amepata mwanamke?”
“Kwani hata wewe si ulikuw ana mawenge kama yako na ukanipata”
“Hahaa ila yake yamazidi bwana”
“Napata wasiwasi kwa sababu ametoka bila walinzi”
“Kwa nini?”
“Amesema ni birthday ya mpenzi wake na hakuhitaji walinzi”
Mzee Mashushu akaka kwenye sofa na akatoa simu katika mfuko wa koti la suti aliyo vaa. Akaitafuta namba ya Jol akaipiga, ikaita hadi ikakata.
“Hapokei”
Mzee Mashusha alizungumza huku akiitazama simu yake.
“Hata mimi nimeipiga namba yake ila haipokelewi”
“Ata kuwa ana furahia maisha. Acha nioge mke wangu ikifika saa sita hajarudi uta niambia”
“Sawa”
Mzee Mashushu akavua nguo zake moja baada ya nyingine na akaingia bafuni kama alivyo zaliwa. Baada ya mdua akatoka bafuni akiwa amemaliza kuoga huku kiunoni mwake amejifunga taulo.
“Mke wangu nipe basi cha kulalia”
“Hapana baba Jol, mwanangu haja rudi hiyo hamu ya kufanya mapenzi naitolea wapi?”
“Khaa Jol amesha kuwa dume la mbegu, utakuta huko ana enjoy wewe umejawa na wasiwasi. Nipe bwana mke wangu”
Mzee Mashusha alizungumza huku akiyatomasa maziwa ya mke wake ambaye ana jua ndio yamejaa hisia nyingi.
“Niache bwana”
Mama Jol alilalama ila akazidiwa kwa hisia na kujikuta akilazwa kitandani na mzee Mashushu taratibu na wakaanza mtanange wa kiutu uzima wa mwendo wa taratibu.
                                                                                        ***
Gamba akafungua dirisha la chumbani kwake ambalo lina ona eneo yanapo simama magari ya nyumba hiyo. 
‘Mmmm hajarudi?’
Gamba alijiuliza huku akiwa na wasiwasi. Akaichukua simu yake ya kitochi akaitazama na ina oyesha ni saa sita usiku kasoro dakika tano. Akashuka kitandani na kuvaa tisheti yake, akatoka nje na kuwafwata walinzi wawili wa getini.
“Vipi kaka”
Walimsalimia Gamba.
“Salama aisee dogo hajarudi?”
“Ndio bado hajarudi”
“Mmmm”
“Vipi kwani?”
“Sio kawaida yake kuchelewa kurudi”
“Labda ata kuwa na amenogewa na sherehe si alisema hivyo”
Gamba akafungua geti dogo na akatoka nje na kutazama barabara ya lami iliyo nyooka na hapakuwa na gari lolote linalo pita katika barabara hiyo ya mtaa wenye majumba ya kifahari na majumba wanayo ishi watu wenye pesa nyingi.Gamba akarudi ndani huku moyo wake ukiwa na wasiwasi sana.
“Si una namba yake?”
“Ndio ila simu yangu haina salio”
“Mpigie kwenye yangu ina salio”
“Jol hapokei namba mpya. Kama una salio niunge japo mia tano”
“Sawa kaka”
Mlinzi mmoja akamuunga Gamba kifurushi cha kupiga na akaipiga namba ya Jol, ikaendelea kuita ila haikupokelewa.
“Hapokei”
“Tulia akirudi nita kustua”
“Sawa”
Gamba akarudi chumbani kwake ila kengele ya hatari ikaendelea kugonga kwa nguvu kichwani mwake, kila alipo jaribu kufumba macho kuutafuta usingizi ulio katika, ila hakuweza kabisa kulala zaidi ya kujikuta akijigeuza geuza kitandani hapo.
                                                                                       ***
“Mke wangu utamu wako huauishi kwa kweli”
Mzeee Mashushu alizungumza huku akihema mara baada ya kumaliza mtanange huo ulio chukua dakika ishirini na tano”
“Asante mume wangu”
Mama Jol akaingia bafuni na kuoga akarudi huku macho yake akiyatupia kwenye saa ya ukutani na ina onyesha ni saa sita na nusu usiku.
“Baba Jol nina wasiwasi. Hadi sasa hivi saa sita na nusu mtoto hajarudi”
Mzee Mashushu aliye anza kupitiwa na usingizi akajigeuza na kutazama saa ukutani.
“Hembu naomba simu yangu”
Mama Jol akaichukua simu ya mzee Mashushu mezani, akaipiga namba ya Jol na ikaendelea kuita ila haikupokelewa.
“Alikuambia ana kwenda wapi?”
“Aliniambia Mbezi Mwisho”
“Mbezi Mwisho kwa nani?”
“Aliniambia tu kwa rafiki zake ila sijajua ni kwa nani?”
Hali ya hatari ikaanza kupiga kichwani kwa mzee Mashushu ambaye japo wamempa mtoto wao uhuru wa misha ila sio mtu wa kuto kupokea simu kwa wakati mrefu.
“Nitolee nguo”
Mama Jol akafungua kabati na kutoa suruali na tisheti. Mzee Mashushu akavaa haraka haraka.
“Naenda kumuuliza Gamba ana weza kuambia ni wapi alipo”
“Sawa, au tuwapigie simu polisi?”
“Wafanye nini? Nina watu kila sehemu ya hii nchi polisi wa kazi gani kama nikihitaji kuwapigia simu polisi nitampigia mimi mwenyewe IGP sawa, wewe tulia acha wasiwasi”
“Sawa mume wangu”
Mzee Mashushu akatoka ndani ya chumba chake na akatoka nje na kumgongea Gamba ambaye kwa haraka aliitikia na akatoa nje.
“Hujalala tu?”
“Hapana mzee”
“Nani….Jol alikuaga?”
“Ndio alisema anakwenda kwenye sherehe ya rafiki yake?”
“Alitoka muda gani?”
“Kama saa moja kasoro hivi”
“Mimi na mama yake tuna mpigia ila hapatikani?”
“Hata mimi nimejeribu kufanya hivyo mzee ila hajapokea”
“Mmmm sasa ata kuwa ameicha simu wapi?”
“Sijajua mzee”
Mzee Mashushu akaitafuta namba ya kiongozi wa genge lake la siri linalo itwa Mamba Squard. Akapiga hatua kadhaa kutoka sehemu alipo simama Gamba.
“Ndio mkuu”
“Kijana wangu leo alikuwa maeneo ya huko kwenu hembu nifanyie uchunguzi unipe jibu kwa sababu alikuja kwenye sherehe ya birthday”
“Sawa mkuu dakika kadhaa”
“Nashukuru”
Mzee Mashushu akakata simu.
“Ngoja tusikilizie hii simu itatupatia muongozo wa kujua nini cha kufanya”
“Sawa mkuu”
Wakasubria na ndani ya dakika tano simu ya mzee Mashushu ikaanza kuita.
“Ndio”
“Ahaa vijana wangu wana sema wamemuona kwenye hoteli yako alikuwa na rafiki zake wakifanya sherehe hapo”
“Hiyo sherehe bado ipo?”
“Ndio ina endelea”
“Pumbuvu nina kuja hapo”
“Sawa mkuu”
Mzee Mashushu akakata simu.
“Walinzi wamesha kwenda kulala una weza kuendesha gari?”
“Ndio mzee”
“Kamuambie mama akupe funguo ya hiyo Range Nyeupe”
“Sawa”
Gamba akaingia ndani na kumgongea mama Jol
“Mama nimegizwa funguo ya Range Rover nyeupe”
Baada ya dakika Mbili mama Jol akatoa huku akiwa amevalia suruali na tisheti huku chini amevalia raba.
“Na mimi nina kwenda”
Mama Jol alizungumza huku akimpita Gamba na kuelekea nje. 
“Vipi na wewe?”
“Na mimi nina kwenda huko munapo kwenda”
“Kaa ndani, yupo hotelini kwetu na rafiki zake wana fanya sherehe hapo”
“Ila mum..”
“Ni usiku na ukitegemea walinzi wa barabarani wamesha kwenda majumbani kwao kujipumzisha. Nina toka na Gamba siwezi endesha kichwa kina pombe sasa hivi”
Mama Jol ikambidi kuwa mpole kwa maana ana elewa uhatari wa kutembe ana mume wake bila ya walinzi.
“Kuweni makini”
“Usijali mke wangu”
Mama Jol akambusu mumewe shavuni, wakaingia ndani ya gari, taratibu Gamba akaendesha gari hilo hadi getini.
“Sikilizeni hakikisheni ulinzi una imarika na kama kijana akirudi nipigieni simu”
“Sawa mkuu”
Mzee Mashushu akapandisha kioo na safari ikaanza huku ukimya ukiwa umetawala ndani ya gari.”
“Gamba?”
“Mmm”
“Umejifunzia wapi kuendesha gari?”
“Jol amenifundisha mzee”
“Ohoo imenibidi nishangae kwa sababu niliwahi kukuona mara moja una egesha gari ya Jol kwenye maegesho”
“Yaa kuna siku kadhaa tulikuwa tuna enda sehemu ana nifundisha na nina mshukuru Mungu kichwa changu ni chepesi kwenye kushika jambo”
“Sawa sawa. Una ijua ile hotel yetu”
“Ndio mzee”
“Sawa twende huko”
Gamba akaliendesha gari hilo la kifahari la boss wake hadi wakafika katika hoteli yake ya kifahari ya nyota tano iliyopo Mbezi mwisho.
“Karibu sana boss”
Wafanyakazi wake walimkaribisha kwa heshima.
“Shukrani. Mdogo wenu nasikia yupo hapa, wana fanyia wapi hiyo part?”
“Garden mkuu”
Wakaeleka hadi kwenye eneo la wazi lenye swimming pool na wakaowaona rafiki wa Jol wakiendela kufurahia maisha.
“Hizi kelele haziwasubui wateja wa mavyumbani?”
Mzee Mashushu alimuuliza meneja.
“Tumewaambia waweke mode ya sondrpoof kwenye vyumba vyao hivyo hawasikii chochote kinacho endelea nje”
“Musiniambie mumempa Jol hili eneo bure?”
“Hapana mkuu aliye kodisha sio yeye”
Mzee Mashushu akaendelea kuangaza macho yake kumtafuta mwanaye na hakumuona.
“Gamba hembu nenda kaangalie angalie maeneo yale yenye kiza”
Gamba akaelea maeneo yanye mwanga hafifu ila hakumuona Jol zaidi ya rafiki wa Jol wakiwa na wapenzi.
“John”
“Kaka Gamba”
Rafiki wa karibu wa Jol aliitika kwa kustuka huku akicha kumnyonya lips rafiki yake.
“Umemuona Jol?”
“Ahaa…Jol aliondoka kama masaa matatu hivi na Glory”
“Wameenda wapi?”
“Kwa kweli hawajaniambia”
“Sawa”
Gamba akarudi sehemu alipo simama mzee Mashushu na meneja wa hoteli yake hiyo.
“Mzee mmoja wa rafiki zake amesema aliondoka na Glory”
“Hawajachukua room hapa kwako?”
“Sidhani ila tuna weza kucheki kwenye list ya wateja”
Wakaelekea hadi mapokezi na wakatazama list ya wateja katika computer ila hapakuwa na jina la Jol.
“Mzee nina wazo”
“Zungumza tu”
“Una onaje tuka angalia cctv kamera ili kujua huyo Glory ana fananaje ili kama ni kupatafuta kwao basi iwe ni rahisi”
“Kweli Gamba wazo zuri”
Wakaelekea katika chumba kikubwa chenye tv kumi za inch stini na tano zenye kamera nyingi za hoteli hizo inazo rekodi kila tukio. Vijana wanne waliomo katika chumba hicho wakaanza kuonyesha video jinsi Jol alivyo ingia hotelini hapo akiwa na wezake. Mzee Mashushu akatazamana na Gamba walipo ona tukio la Jol kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo.
“Hembu simamisha kidogo”
Gamba alizungumza na kijana anaye onyesha video hizo akazisimamisha. Gamba akawatazama wanaume watatu ambao waliingia katika sherehe hiyo huku wote wakionyesha umakini wao kwa Jol.
“Play”
Gamba alizungumza huku macho yake yakifwatilia nyendo za watu hao. Wakawashuhudia wakitoka ndani ya hotel mara baada ya Jol na mpenzi wake kutoka dakika mbili. Gamba akatazama namba za gari waliyo ingia watu hao ambao walikuwa wamevalia kitanashati kiasi cha wote waliomo ndani ya chumba hicho hadi mzee Mashushu mwenyewe hakuwafikiria vibaya zaidi ya Gamba ambaye nafsi yake ina hisi wanaume hao watatu ni watu hatari sana na kuondoka dakika mbili baada ya Jol kuondoka hotelini hapo ni ishara tosha wana mfwatilia Jol.
                                                                            ITAENDELEA
Haya sasa, mambo yanazidi kuwa matamu. Jol na mpenzi wake Glory wametekwa na watu wasio julikana ni wapi wana pelekwa na itakuwaje? Gamba wasiwasi una mjaa na kuwatilia mashaka watu walio kuwa wana mfwatilia Jol je ni nini kitatokea. Usikose kufwatilia mtiririko wa hadithi hii sehemu ya 03.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post