TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

DEREVA MUUAJI 3

HITMAN DRIVER-03
                                                      (Dereva Muuaji)

Muandishi…………………….AZARIA G.MSULWA
Wasiliana nami……………..0657072588/0742334453
Kurasa zangu za kijami zote zina tumi jina la @StoryZaEddy-tz 

ILIPOISHIA
“Hembu simamisha kidogo”
Gamba alizungumza na kijana anaye onyesha video hizo akazisimamisha. Gamba akawatazama wanaume watatu ambao waliingia katika sherehe hiyo huku wote wakionyesha umakini wao kwa Jol.
“Play”
Gamba alizungumza huku macho yake yakifwatilia nyendo za watu hao. Wakawashuhudia wakitoka ndani ya hotel mara baada ya Jol na mpenzi wake kutoka dakika mbili. Gamba akatazama namba za gari waliyo ingia watu hao ambao walikuwa wamevalia kitanashati kiasi cha wote waliomo ndani ya chumba hicho hadi mzee Mashushu mwenyewe hakuwafikiria vibaya zaidi ya Gamba ambaye nafsi yake ina hisi wanaume hao watatu ni watu hatari sana na kuondoka dakika mbili baada ya Jol kuondoka hotelini hapo ni ishara tosha wana mfwatilia Jol.

ENDELEA
Mzee Mashuhu akapiga picha ya Jol na Glory wakiwa pamoja kisha wakatoa ndani ya chumba hicho.
“Nina watumia vijana wangu picha wata saidia kumtafuta na kujua ni hoteli gani ata kuwepo kwa maana walivyo toka wana onekana wana enda kulala”
Mzee Mashushu alizungumza huku akiwa ameongozana na meneja pamoja na Gamba.
“Mzee kama huto jali nina weza kwenda kumuuliza rafiki yake ana weza akatuelekeza nyumbani kwa wazazi wa Glory”
“Ni kweli hembu shuhulikia hilo”
“Sawa mzee”
Gamba akaelekea moja kwa moja eneo inapo endelea shuhuli ya siku ya kuzaliwa ya Glory japo wahusika hawapo ila waalikwa wana endelea kula, kunywa na kufurahi.
“John”
“Ndio kaka Gamba”
“Ahaa…unapafahamu nyumbani kwa kina Glory?”
“Ndio”
“Una weza kutupeleka kwa sababu Jol bado hapokei simu zake”
“Ahaa…”
“Nimekuja na baba yake Jol”
“Ohooo, sawa sawa”
John akakubali japo kishingo upande kwa maana ana achana na starehe anazo zipata hotelini hapo na kuamua kwenda kumsaidia Gamba. 
“Shikamoo”
John alimsalimia mzee Mashushu.
“Marahaba, sura yako si ngeni”
“Ni kweli, nina soma chuo kimoja na Jol”
“Sawa tupeleke nyumbani kwa huyo nani sijui”
“Glory”
“Ndio ana ishi wapi?”
“Kimara Suka”
“Twende”
Wakaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hilo huku mzee Mashushu kwa mara kadhaa akijaribu kupiga namba ya simu ya Jol ila aina ita bila ya kupokelewa.
“Jol na huyo msichana wana mahusiano ya muda gani?”
Mzee Mashushu aliuliza huku akimgeukia John aliye kaa siti ya nyuma.
“Ahaa kama mwaka na nusu”
“Kwa hiyo muna fichiana siri?”
John akapata kigugumizi cha kuzungumza.
“Tumefika tuna ingia wapi?”
Gamba aliuliza.
“Tuzunguke ni upande ule wa pili wa barabara?”
John alionyesha njia ya kupita an wakafwata maelekezo yake hadi wakafika nyumbani kwa wazazi wa Glory.
“Piga honi”
Mzee Mashushu alizungumza na Gamba akatii. Mlango wa nyumba hiyo ya kawaida ukafunguliwa na akatoka mzee.
“Yule ni baba yake”
John alizungumza na mzee Gamba akawa wa kwanza kushuka.
“Habari yako muheshimiwa”
Mzee Mashushu alianza kuzungumza huku akizunguka upande ulipo mlango wa nyumba hiyo.
“Salama habari”
“Nzuri, samahani kwa kukusumbua usiku huu. Mimi ni baba mzazi wa kijana mmoja ana itwa Jol”
“Ohoo Jol, karibu sana mkuu”
Baba Glory alizungumza huku akiw ana tabasamu.
“Nashukuru. Kijana wangu aliondoka na kijana wako je kuna mawasilino yoyote muliyafanya kati ya masaa kama matatu nyuma?”
“Nisiwe muongo sijafanya kwa kweli kwa sababu aliniaga kuwa leo ni sherehe yake hivyo atakuwa pamoja na Jol kwenye hiyo sherehe”
“Sawa sawa kwa maana nimejeribua kumpigia simu Jol na hapokei”
“Ngoja nimpigie Glory”
Baba Glory akaingia ndani na baada ya muda akatoka akiwa na simu mkononi. Akaipiga simu ya binti yake ila nayo haikupokelewa.
“Hapokei”
“Basi tubadilishane namba kama kutakuwa na chochote kitakacho tokea basi usisite kunifahamisha”
“Sawa mzazi mwenzangu”
Wakabadilishana namba na mzee Mashushu akarudi ndani ya gari na wakaondoka eneo hilo, wakamrudisha John kwenye sherehe walipo mtoa.
“Kijana”
“Ndio baba”
“Endapo huyo mpumbavu mwenzenu akikupigia simu muambie nime kasirika na…..”
Mzee Mashushua akaikatisha sentensi yake huku akimtazama John aliye shuka ndani ya gari.
“Gamba tuondoke”
Taratibu wakaondoka hotelini hapo huku Gamba akili yake ikifanya kazi kwa kasi kama computer,
“Mzee”
“Ndio”
“Nina mashaka kidogo”
“Mashaka gani?”
“Ile gari ambayo iliondoka hotelini dakika mbil kabla ya kuondoka kidogo imenipa mashaka kwa sababu wale watu walio kuwa ndnai ya lile gari walitoka ndani ya sherehe ya Jol na wezake hivyo walivyo ondoka nao wakaondoka wana onyesha ni watu ambao wana mfwatilia”
“Wale masharobaro uatakuna ni wajinga zake Jol. Una jua sijamfwatilia Jol kwa kipindi uta kuna naye ameanzisha vijivikundi vyake. Na…”
Mzee Mashushu akaikatisha sentensi yake na kuipokea simu ya mke wake.
“Vipi baba Jol umempata?”
Mzee Mashushu akashusha pumzi taratibu.
“Bado ameondoka na mchumba wake sijui wamelekea hoteli gani na mwanao amekua kidume hadi ana mavalisha mwanamke pete, bila ya kututambuisha au wewe amekutambulisha”
“Hajanitambulisha bwana kwa hiyo hamjuini wapi wameenda?”
“Ndio mke wangu. Dar es Salaam hapa kuna mhoteli mengi una hisi nita jua ni wapi alipo. Narudi kulala hadi asubuhi kama bado hajarudi tuta fwata utatibu mwengine. Uta kuta tuna hangaika usiku huu kumbe mwanao kashikilia kiuno huko alafu simu na huyo mpuuzi mwenzie wamezitoa sauti”
“Mume wangu nafsi yangu haina amani kabisa”
“Najua ni wasiwasi wako kwa sababu mwanao hajawahi kulala nje ya nyumba ila kama ungekuwa amesha wahi kulala basi usinge kuwa na wasiwasi. Tuna rudi nyumbani”
“Daa baba Jol mbona una chukulia hii ishu kirahisi namna hiyo”
“Sasa una taka mimi nifanyaje?”
“Si una watu wengi wewe kwa nini usiwape namba ya Jol waka itrace namba yake na wakajua ni wapi alipo mume wangu. Mbona una taka kuyafanya mambo kienyeji”
“Sawa sawa nimekuelewa”
Mzee Mashushu akakata simu.
“Wanawake bwana juu ya watoto wao wana kuwa wasumbufu sana”
Mzee Mashushu alizungumza huku akiazama namba katika kitabu cha kumbukumbu katika simu yake. Akaipita namba ya IGP, akairudia akaitazama kwa muda kidogo kisha akaitafuta namba ya RPC wa Dar e Salaam na akaipiga, ikaita kwa sekunde kadha kisha ikapokelewa.
“Mzee Shikamoo”
“Marahaba pole nimekuamsha?”
“Hapana mzee hujaniamsha nipo doria si unajua hatulal sisi”
“Ni kweli, sasa nina shida moja naomba unisaidie”
“Shida gani mzee wangu”
“Kijana wangu wa kiume hadi majira haya yajarudi nyumbani kwangu nimejaribu kufwatilia alikuwa kwenye serehe moja kwenye hoteli yangu ile ya Mbezi Mwisho, hivyo kama huto jali hembu wapatie vijana wako wa ifwatilie simu yake kwa sababu tuna piga na haipokelewi, najua ningelifanya mwenyewe ila nimeona ni vyema nika kushirikisha”
“Hakuna shaka mzee na umefanya vizuri sana kunishirikisha basi acha nilifwatilie kwa haraka kisha nitakupatia jibu”
“Nashukuru”
Mzee Mashushu akakata simu. Wakafika nyumbani kwake na geti likafunguliwa na kuingia ndani. Simu ya mzee Mashushu ikaanza kuita kabla hata hawajashuka ndani ya gari.
“Ndio RPC”
“Vijana wanu wameweza kufwatilia na kuikuta simu ya kijana wako ikiwa ndani ya gari lake maeneo ya Mbezi Luis kuna pori moja gari imetelekezwa na dalili zinavyo onyesha kuna uhalifu ulio tendeka kwani suruali ya kijana viatu na nguo zimeachwa itakuwa ni vyema kama ukija ukajionea kwani nami pia nina elekea huko”
“Sa….sa…wa”
Mzee Mashushu alizungumza kwa kigugumizi.
“Geuza twende Mbezi Luis haraka haraka haraka”
Gamba akalirudisha nyuma kwa kasi gari hiyo huku akikunja kona iliyo zifanya tairi ziserereke, kitando hichi kiliwashangaza walinzi wote. Gamba akapiga honi kuashiria geti lifunguliwe na walinzi wakafanya hivyo,
“A….emenitumia location hii hapa”
Mzee Mashushu alizungumza huku akimuonyesha Gamba ni wapi wanapo paswa kuelekea. Gamba akazidi kuonyesha ujuzi wa kuendesha gari hiyo. 
“Mzee funga mkanda”
Gamba alimuambia mzee Mashushua ambaye jasho lina mwagika kwa wasiwasi. Akafunga mkanda huku mikono ikimtetemeka kwa woga. Gamba akaongeza kiwango cha kiyoyozi ndani ya gari huku akizidi kuichochea gari hiyo inayo kwenda kwa kasi. Ndani ya muda mchache wakafika katika eneo ambalo gari ya Jol imetelekezwa na watekaji. Gamba akafunga breki na gari ikaserereka mita kadhaa na ikasimama huku askari walio wahi kufika eneo hili wakishangaa. Gamba akawa wa kwanza kushuka huku mzee Mashuhu akifwati. 
“Karibu sana mzee”
RPC alimkaribishi mzee Mashushu huku akimpa mkono.
“Asante nini kimetokea”
“Tumefanikiwa ku trace namba ya kijana na imetufikisha hapa. Kama unavyo jionea gari tumeikuta imetelekezwa huku porini na vitu tulivyo vikuta ni hivi hapa na kioo upande wa dereva kimevunjwa ikiashiria kwamba ni tukio la kiuhalifu ndio llilo tokea hapa”
“Huruhusiwi kupita”
Askari mmoja alimzuia Gamba kuingia kwenye uzio wa utepe wa njano walio uzungushia hapo.
“Kuna vitu natazama”
“Eneo bado lina fanyiwa uchunguzi”
Askari huyo akajikuta akishangaa kumuona mzee Mashushu akiifungua utepe huo na akapita na ikwa ni nafasi kwa Gamba naye kuingia huku wakifwatiwa wa RPC.
“Gari ndio yenyewe”
Mzee Mashushu alizungumza huku akitazama kadi ya gari ambayo imesajiliwa kwa jina la Jol.
“Inavyo onekana watekaji walikuwa wana muhitaji Jol mwenyewe na si mali zake kwa sababu kama ni wallet yake hii hapa na ina kiasi cha dola elfu moja na mia mbili. Nina weza kukuuliza swali mzee”
“Ehee……!”
Mzee Mashuhu aliitikia kwa mshangao huku akili yake ikiwaza ni adui gani ambaye ameigusa familia yake kwani katika biashara zake haramu anazo ziongoza wamejiwekea sheria ya kuto kuzigusa familia zao hata kama kutatokea uadui kati ya wafanya biashara ila mke na watoto hawapaswi kuguswa kabisa.
“Wewe ni mfanya biashara mkubwa, je una hisi kuna mtu au kikundi cha watu ambacho kina weza kufanya hili tukio”
“Sina wa kumuwazia”
“Hata wa kumhisi”
“Sina IGP, vitu vya kijana wangu mpatieni kijana wangu huyo”
Gamba akapatiwa vitu vya Jol.
“Naomba unisaidie kufanya upelelezi wa kumpata kijana wangu”
“Sawa nita jitahidi kadri ya uwezo wangu, nimesha wasiliana na wakuu wa polisi wamikoa ya jirani iliyo tuzunguka ili kuweka baadhi ya vizuiri kwenye barabara zetu na magari makuba na madogo yanayo tembea usiku huu yata kuwa yana kaguliwa”
“Nashukuru, ila nahitaji hili swala lisitangazwe kwenye vyombo vya habari bado ni mapema sana”
“Hakuna shaka”
Gamba akaingia ndani ya gari ya Jol. Kutokana gari hiyo ina tunza rekodi ya kamera za siri zilizo fungwa kuzunguka katika gari hiyo. Akarudisha matukio nyuma.
“Mzee”
“Ndio Gamba”
Gamba akahamia siti ya abiri na mzee Mashushu na RPC wakachungualia ndani ya gari hiyo kwa kupitia tv ndogo iliyomo ndani ya gari hiyo wakaona jinsi gari aina ya Toyota Alphad ilivyo kuwa ina wafwatilia Jol na mpenzi wake hadi wakafika sehemu na wakasimama. Wakawaona watu watutu walio funika nyuso zao wkaishuka huku wakiwa na bastola mikononi na wakatekeleza tukio la utekaji na mmoja wao akaendesha gari hiyo hadi walipo itelekeza porini.
“Tumepata namba ya gari ya watekaji”
RPC aliwaambia vijana wake na kwa kutumia simu ya Jol ambayo Gamba ana jua neno la siri akaipakua kipande cha video kinacho onyesha kutekwa kwake na gari ya watekaji hao, akaituma kwenye simu mzee Mashuhu ambaye kwa haraka akaituma kwa RPC.
“Hadi hapa tutakuwa tumepata muendelezo mzuri. Nikuhakikishie tu kwamba watekaji wote wata patikana”
“Nashukuru. Gamba tuondoke”
Wakaingia ndani ya gari. Mzee Mashuhu aliye fura hasira akaitafuta namba moja na akaipiga,
“Mkuu”
“Mwanangu ametekwa, nakutumia video nahitaji iwafikie vijana wako wote. Hadi jua lina chomoza nahitaji kijana wangu awe amepatikana kwa garama yoyote na walio husika kwenye huo utekaji nawahitaji wakiwa hai tumeleewana?”
Mzee Mashuhu alizungumza kwa kufoka huku macho yakimwa yametoka. 
“Haki ya Mungu nina apa nita waua nita waua wote washenzi wale nita wauaaaaaa”
Mzee Mashushu alizungumza kwa ukali ambao kwa kipindi chote ambacho Gamba ameishi na mzee huyo hakuwahi kumuona akiwa kwenye hali kama hiyo.
                                                                            ITAENDELEA
Haya sasa, mambo yanazidi kuwa matamu. Jeshi la polisi wamefanikiwa kugundua eneo lilipo telekezwa gari la Jol na wamepata video ya kutekwa kwa Jol na video hiyo imesambazwa kwa maskari wote na msako mkali una endelea je ni nini kita tokea je Jol na mpenzi wake wata toka salama kwenye mikono ya watekaji hao. Usikose kufwatilia mtiririko wa hadithi hii sehemu ya 04.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post