HITMAN DRIVER-01
(Dereva Muuaji)
Muandishi…………………….AZARIA G.MSULWA
Wasiliana nami……………..0657072588/0742334453
Kurasa zangu za kijami zote zina tumi jina la @StoryZaEddy-tz
“Habari yako Gamba?”
“Salama boss shikamoo”
“Marahaba, una jua toka kuja kwako kwenye hii nyumba yangu naona madhari yana pendeza sana, kusema kweli unajitahidi kwa kiwango kikubwa sana”
“Asante sana boss wangu”
“Ahaa nimekaa na mke wangu tumeona tukupandishie mshahara kutosha elfu themanini tuliyo kuwa tuna kulipa kwa kipindi chote cha mwaka mzima na sasa tuta kulipa laki na hamsini na kwenye kulidhibitisha hilo, nina kupatia mshahara wako mpya leo hii hii”
Gamba macho yakamtoka akapokea kiasi cha laki moja na nusu kutoka kwa bosi wake huyo.
“Ohoo Mungu asante kwa neema zako. Kweli wewe u mwema kila wakati”
Mzee Mashushu, akatabasamu kwani Gamba amekuwa ni kijana mchapaka kazi na mwenye kujituma. Japo jumba leke hilo la kifahari lina eneo kubwa ila Gamba ana jitahidi kuhakikisha ana fanya usafi na kutunza bustani zote ikiwemo bwawa kubwa la kuogelea lililomo ndani ya jumba hilo.
“Na kitu kingine nahitaji kusikia maoni yako”
“Bila shaka boss”
“Una onaje tukakuongezea japo vijana wawili ambao watakuwa wana kusaidia hizi kazi na nawaza kama huto jali nikupeleke Veta ukajifunze japo fani uipendayo kwa sababu kuna leo na kesho una weza kuanzisha maisha yako sehemu nyingine tena”
“Daa….!! Mungu akubariki sana baba”
“Usijali unajua kuishi na watu vizuri ni moja ya nguzo kubwa kwenye maisha yangu na ukiangalia nahitaji kuingia kwenye mbio za ubunge mwakani basi hapa katikati una weza soma chochote ukipendecho. Ila kwa sasa usinijibu ni nini unacho taka kwenda kusoma ila jaribu kutuliza akili fikiria kinacho weze kukusaidia hapo mbeleni nami nita jitolea kukusomesha kwa asilimia mia moja”
“Sawa boss nashukuru sana na mwenyezi Mungu apate kukubariki”
“Amen. Haya endelea na kazi”
“Asanye sana mkuu”
Mzee Mashushu akaondoka eneo hilo na kumuacha Gamba akiwa na tabasamu pana usoni mwake. Gamba aakaingia kwenye nyujmba ya pembeni wanayo kaa wafanyakazi wa kiume, moja kwa moja akaingia ndani ya chumba chake kati ya vyumba vitatu vilivyomo ndani ya nyumba hiyo ambayo ni nzuri japo wana ishi wafanyakazi. Akafungua tranka lake la kuhifadhia nguo, akafungua kufuli na kutoa kibubu cha mbao na akaweka kiasi cha laki moja na ishirini na akabakisha elfu thelathini ya matumizi. Akafunga vizuri tranka lake na akasimama. Akajitazama kwenye kioo cha dreasing table.Akatabasamu kisha akatoka nje.
“Ankoo Gambaaaa”
Jol mtoto wa kiume wa mwisho wa mzee Mshana mweye umri wa miaka kumi na tisa alimuita huku akimpa tano Gamba.
“Niambie Jol”
“Poa tu anko shikamoo”
“Marahaba, leo mbona umetoka mapema chuo?”
“Ahaa tulikuwa na mitihani hivyo nimemaliza mapema tu nikaona nirudi zangu nyumbani si una jua mzee ameniletea ps5”
“Ohoo”
“Halafu nilisahau kukuambia, ameniletea hiyo na games zote mpya”
“Vizuri”
“Umemaliza kazi nine nikufunge na timu yako ya vibonde”
“Hahahahaa”
“Kuna majani nataka kuyanyweshea kule bustani ya nyuma nikimaliza basi nita kuja”
“Sawa anko nakusubiria”
Jol akaondoka na kumfanya Gamba atabasamu kwani amekuwa akiishi na familia yam zee Mashushu vizuri na wamekuwa ni watu wanao mpenda kiasi cha kwanba hata mgeni akija kwa mara ya kwanza hawezi kugundua kwamba Gamba ni fanyakazi wa bustani. Gamba akafanya kazi zake haraka haraka ila kwa umakini mkubwa na akamaliza. Akarudi kwenye nyumba anayo ishi, akaoga na kubadili nguo za kazi na kuvaa nguo za kawaida kisha akaeleka katika chumba maalumu cha michezo ya video(Video Games) kilicho andaliwa kwa ajili ya Jol na marafiki zake pale wanapo kuja kumtembelea kwani Jol ni mtoto wa mwisho wa mzee Mashushu kati ya watoto watatu huku wawili wakiwa ni watoto wa kike huku wa kwanza akiishia Marekani akifanya kazi kwenye kampuni kubwa ya utengenezaji wa vifaa vya electronic vya Apple huku binti wa pili wa mzee Mashusha akifanya kazi kwenye shirika lake binafsi la kuhudumia wamama na watoto wasio jiweza linalo fanya kazi ndani nan je ya nchi ya Tanzania.
“Eheee tena nilikuwa nina panga kikosi chukua pad”
“Waooo pad zake ni nzuri”
“Yaa nimeicheza jana usiku nimeona kuna utofauti kati ya ps 4 pro na hii ps5. Wameboresha vitu vingi hususani graphics”
“Ohooo”
Jol akatoa kichupa kidogo mfukoni mwake na akatoa kidonge kimoja na akakimeza na kukirudisha mfukoni kichupa hicho chenye vidonge vingi. Gamba akamtazama Jol ambaye maisha yake yamekuwa ni maisha ya kula vidonge ili apate nguvu.
“Upo sawa lakini?
“Ndio ankoo”
Jol alizungumza huku akitabasamu.
“Nachukua the bluss”
“Mimi kama kawaida timu yangu ni Liverpool”
Wakaanza kucheza mchezo huo wa mpira huku kila mtu akijitahidi kuhakikisha ana mfunga mwenzake. Mama Jol akafungua mlango wa chumba hicho kimya kimya na kumtazama jinsi Jol alivyo jawa na furaha kwani Gamba amekuwa ni mmoja wa watu ambao toka amefika kwenye nyumba hiyo wamempa Jol furaha na kumtoa kabisa kwenye maisha ya upweke yanayo tegemea dawa zake ambazo endapo ata zikosa japo kwa siku mbili basi kuna uwezekano mkubwa wa kufariki dunia. Gamba amekuwa ni mtu ambaye ana cheza naye michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa kikapu ambapo katika jumba hilo kuna viwanja viwili kimoja kikiwa ni cha tenes huku kingine kikiwa ni kiwacha cha kikapu.
“Goooooooo”
Kelele za Jol zikamstua mama yake kutoka kwenye dimbwi la mawazo yaliyo changanyikana na furaha na huzuni kwani wamezunguka hospitali zote kubwa duniani kuutibu ugonjwa wa Jol ila wameshindwa zaidi ya kupewa dawa ambazo ana paswa kuzitumia hadi pale atakapo fikisha umri wa miaka ishirini na mbili na baada ya hapo kuna uwezekano ugonjwa wake kupona.
“Nilisema ankoo nita kufungaa ona Lukaku amesha kuweka hahahahaa”
Joll alizidi kusangilia.
“Sawa ngoja nianzishe”
Mama Jol akafunga mlango taratibu na kuelekea chumbani kwake.
“Hayo hayakuwa makubaliano ya biashara zetu umenielewa”
Mzee Mashushu alizungumza kwa kufoka huku simu ikiwa sikioni mwake.
“Hata kama una nijua vizuri umenielewa. Kwenye maswala ya pesa sihitaji upumbavu, umeletewa mzigo ukiwa umekamilika sasa hizo janja janja zako sitaki kuzisikia sawa”
Mzee Mashushu akakata simu hiyo huku akiwa amefura kwa hasira.
“Nini tena mume wangu”
“Si hawa wa Russia, wamepelekewa mzimgo na vijana. Halafu wana sema mzigo upo pungufu wasiniletee upuuzi mimi”
“Ila mume wangu jamani mi naona hii biashara ni bora ukaachana nayo isitoshe una ingia kwenye siasa, sasa hivi tuna kila kutu ambacho kina weza kutufanya kuishi tutakavyo mbona sasa una endelea kuing’ang’ania”
“Nisikilize mke wangu. Mali na kila kitu kimetokana na hii biashara. Na nimeirithi kutoka kwa wazazi wnagu hivyo siwezi kuiacha. Namuomba Mungu amsaidie Jol hali yake iwe sawa ili nimtambulishe kwenye hii biashara kwa sababu yeye ndio dume langu ana paswa kuanzia pale nitakapo ishia mimi”
Mke wa Mashushu akashusha pumzi taratibu.
“Ila kuwa makini mume wangu naamini na tambua kwamba wale wa Russia ni watu hatari sana”
“Usijali mke wangu. Nina toka kuna watu nina kwenda kukutana nao”
“Usichelewe basi kurudi”
“Usijali”
Mzee Mashushu akambusu mke wake mdomoni kisha akatoka chumbani kwake. Akafungulia mlango na gari yake ya kifahari aina ya BWM X7 na mlinzi wake kisha akaondoka nyumbani kwake hapo akiwa ameongozana na gari nyingie mbili lilizo beba walinzi wake binafsi kwani yeye na familia yake wana lindwa wa walinzi wenye mfunzo ya hali ya juu.
“Don Mashushu tuna elekea wapi?”
“Nyumbani kwa Don Rafael”
“Sawa mkuu”
“Mkuu nina weza kukuuliza”
Mlinzi binafsi wa Mashushu aliye kaa pembeni ya dereva alizungumza.
“Uliza”
“Yule kijana wako wa kazi ni wapi umemtoa?”
“Nani Gamba?”
“Ndio”
“Mke wangu alimtoa kijijini kwao huko ni mtendaji kazi mzuri sana”
“Je ana fahamu juu ya hizi biashara zetu?”
“Kamwe hatambui, kama wanangu wenyewe tu hawajui sembuse yeye kibaraka. Mke wangu pekee ndani ya ile nyumba ndio ana jua kwa sababu yeye ndio msiri wangu na nilikuwa naye toka tupo wadogo shule za msingi na aliweza kushuhudia panda na kushuka kwangu kweye hizibiashara. Mbona umeuliza?”
“Simuamini jamaa”
“Ondoa shaka naye kwa maana nimemfanyia upelelezi wa kina na hana shida yoyote”
“Sawa mkuu”
Wakafika katika jumba kubwa la kifahari la rafiki yake wa karibu ambaye toka utotoni wamekuwa katika biashara zao nyingi.
“Karibu sana kaka”
“Nashukuru”
“Uso wako una onekana kuwa na hasira”
“Hujakosea ndugu yangu. Nimepokea simu kutoka Russia, wana sema mzigo umefika pungufu jambo ambalo siku zote una tambua kazi zangu hazijawahi kufanyika chini ya kiwango”
“Mmmm ina bidi uanze kufwatilia mwenendo mzima, ina wezakana umepunguzwa wakati ulipo kuwa una safirishwa”
“Sasa pesa yangu wameishikilia wana hitaji mzigo mziga. Hivi wananioa mimi ni mpuuzi sana”
“Tuliza hasira kaka kuna njia nyingi za kuipata hiyo pesa, kwa usalama au kwa njia za kishetani hivyo tulia ndugu yangu hakuna kinacho shindikiana.”
“Nipatie wisky kidogo nishushe hasira”
Don Raphael akamimina kiasi hicho cha pombe kali katika glasi ngumu mbili na taratibu wakaanza kunywa.
“Mpango wako wa kisiasa bado upo?”
“Upo pale pale na najua unajua endapo nikiingia serikalini biashara zetu zita zidi kuwenda vizuri na hatuto kuwa na wafwatiliaji”
“Ila naona kama uta jiweka kwenye nafasi mbaya”
“Nafasi gani?”
“Nafasi ya kuandamwa na vyombo vya habari na kama unavyo jua vyombo vyetu vinavyo weza shikilia bango habari za udaku”
“Najua sheria yetu unaijua kila anaye ingia kwenye kumi na nane basi tuna muua. Mwnedo utakuwa ndio huo huo tuta hakikisha wote wana kufa”
Mzee Mashushu alizungumza kwa msisitizo kiasi cha kumfanya Don Raphael wagonganishe glasi zao ikiwa ishara ya kufurahia maisha na nguvu ya pesa waliyo nayo.
***
“Mamamaa nimealikwa bwana na rafiki zangu”
Jol alizungumza huku akiwa amemaliza kujiandaa.
“Sherehe ya huyo rafiki yako ina fanyikikia wapi?”
“Kwao ni Mbezi mwisho ndipo inapo fanyika”
“Basi ina bidi uende na walinzi wako”
“Khaa mama unajua mimi sipendi maisha ya kuandamana na hao walinzi wenu bwana”
“Jol hiyo jni kwa usalama wako”
“Mama tunaishi Tanzania nchi ya amani na upendo na isitoshe nipo kwenye gari nani ata nidhuru”
Jol akachukua funguo ya gari lake na kuaza kutembea kuelekea nje.
“Mama nahiaji uhuru, kwa sasa mimi ni mwanaume ambaye nina girlfriend wangu”
“Gilfriend?”
“Ndio mama, nipo chuo una hisi niyakosa kuwa na msichana. Muda mwengine tuna hitaji muda wa sisi kuwa wenyewe na si kuongozana na hao walinzi wenu”
“Haya urudi kabla ya saa sita usiku”
“Sawa mama nakupenda”
Jol akambusu mama yake shavuni.
“Nakupenda pia mwanangu”
Jol akaingia ndani ya gari yake aina ya Jeep Grand Cherokee. Akaliendesha kwa kasi hadi getini alipo mkuta Gamba akizungumza na walinzi wengine.
“Anko Gamba”
“Wapi tena mbona mbio mbio”
“Demu wangu leo birthday yake hivyo nina wahi saa moja sasa hivi sherehe ina anza saa mbili hivi”
“Ohoo kuwa makini kwa maana naona leo huna dereva”
“Usijali anko”
Jol akapandisha kioo cha gari lake na kuondoka.
“Umeweza vipi kuzoeana na huyu kijana”
Mlinzi mmoja wa getii aliuliza.
“Kwa nini?”
“Ana onekana ni mwenye dharau hajawahi kutusalimia yaani akiingia ni mahoni akitoka ni kama hivi”
“Labda nyota zimeendana”
“Kwa kweli aisee”
Jol akafika katika eneo alilo muandalia mpenzi wake sherehe ya kuzaliwa kwake, akaungana na marafiki zake ambao wamemsaidia kuandaa sherehe hiyo ya kifahari. Sherehe hiyo ikaanza baada ya mpenzi wake kufika eneo hilo akiwa ameongozana na rafiki zake wanne wa kike. Jol akamkaribisha mpenzi wake huyo na sherehe ikaanza huku vinywaji vikiwa ni vya kumgwa, chakula hususani nyama choma zikiwa zimezagaa kwenye kila kona ya eneo hilo lenye bwawa kubwa la kuogelea. Jol akasimamisha mziki na watu wote wakamsikiliza, akamsogelea mpenzi wake na akamvisha pete ya uchumba ya garama na kuwafanya walio alikwa kushangilia
“Asante baby nakupenda sana”
Glory alizungumza huku akimwagikw ana machozi ya furaha.
“Nakupenda pia mke wangu mtarajiwa. Party iendeleeeee”
Jol alizungumza kwa sauti na mziki ukaachiliwa na shangwe zikaendelea. Jol akatoa kibunda cha pesa na akaanza kumrushia Glory, noti moja moja na kuwafanya wapambe wa Glory kusaidia kuokota pesa hizo. “Mumemuona yule fala?”
Kijana mmoja mwenye asili ya kihindi akiwa amesimama kwenye chumba kimoja cha gorofa ya hoteli hiyo ya gorofa iliyo toa eneo lake kwa ajili ya kufanyika kwa shehere hiyo.
“Ndio mkuu”
“Nahitaji mumteka kimya kimya kwa sababu amemchukua demu wangu, nataka kumuonyesha ni namba gani mapenzi yana uma”
“Sawa mkuu andika kazi imeisha si yule boya anaye rusha rusha pesa”
JIUNGE LEO KWENYE GROUP LA HITMAN DRIVER KWA ADA YA SH 4000 TU KWA MWEZI. TIGOPESA 0657072588 AZARIA MSULWA
Tags
simulizi