TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

ANANIUMIZA NAOGOPA KUMWAMBIA 01

ANANIUMIZA NAOGOPA KUMWAMBIA NO 1

MTUNZI JOGOO POLL 

NO 0657 774735

naitwa maliyamu wengi upenda kuniita mamu naishi kwenye nyumba ya kupanga sasa mule kwenye nyumba tunaishi wengi wapangaji sasa kuna mkaka 1 nimetokea kumpenda sana sio kumpenda labla tuwe wapenzi nimempenda awe mume wangu 

sababu vigezo vyote ninavyovipenda mimi anavyo mpole ni mtu mwenye uluma si msemaji sana ni mtu wa kusikiliza nyimbo za dini akiwa amepumzika nyumbani japo ananichanganya simjui dini gani maana utasikia kaswida mala kwaya mala shehee anatoa mawaidha mala unasikia mwamposa anaunguluma kwenye TV yake 

maisha yake ni tofauti sana na vijana wengine yeye kila mtu anamwita dada na sisi wote tumezoea kumwita kaka na akuna anayejuwa jina lake zaidi ya kaka si muongeaji sana labla upate nafasi ya kumuuliza jina yeye mwenyewe japo anasikia mimi naitwa maliyamu au mamu lakini ajawai kuniita dada maliyamu au dada mamu

yeye uniita dada tu.

naisi asiyewai kupenda ataniona kama sina akili lakini mimi simaanishi namtamani namaanisha awe mume wangu na utamaduni wetu unanibana mimi kwenda kumwambia fikla zangu juu yake anaweza akaniisi mimi sijatulia au akanifikilia vibaya zaidi akanichukulia kama wale mguu ukutani chake mkononi 

nikawa nawaza nitafikishaje ujumbe kwake ajuwe mimi nampenda awe mume wangu nilitamani tungekuwa kwenye iyo nchi mwanamke anamtolea maali mwanaume ningemtolea mimi uyu anioe 

naamini wanawake wengi tunaweza kuwa ivi lakini tunashindwa kusema isia zetu kwa yule unatamani angekuwa wako na si wanawake tu ata baazi ya wanaume wanaweza kumpenda mwanamke lakini akashindwa kumwambia sababu ya mazingila aliyonayo yule mwanamke 

mfano mwanamke mbunge wewe unauza genge ata akija kununua kitunguu kwako utaishia kumwangalia tu alafu wana usemi wao  wakubwa wanafaidi 

wengine utasikia wanasema tutaishia kula kwa macho 

yote ni maneno ya kushindwa kupeleka isia zao kwa yule muusika sasa najiuliza mimi nitafanyaje ajuwe niliwaza nikalala siku ikapita 

siku 1 ilikuwa jumapili yule mkaka ninayempenda alikuwa anafua mimi nilikuwa nimefungua pazia ya dilisha langu mamwangalia tu natamani nimwambie nimsaidie kufua kulikuwa na ali ya hewa ya mvua basi nilikuwa nishapata wazo la kuanza nalo ili nifikishe ujumbe wangu kwake 

niliwaza akianika nguo zake zikikauka nikiona mvua inataka kunyesha naanua alafu namnyoshea mashati yake vizuri alafu nampa moyoni mwangu naomba amalize kufua aondoke akiludi akute nimemfanyia ivyo nimpe nianze kutengeneza ukalibu juu yake kiukweli nampenda sana nataka awe mume wangu.

sasa namwangalia tu jinsi anavyofua moyoni nasikia raha mala dada mmoja wale wasio na aibu akamfata akiwa amevaa kanga 1 naisi ndani akuvaa kitu akamwambia kaka naomba sabuni mwenzio nataka nifue sina sabuni wala pesa ya kununua sabuni.

yule kaka akasema usiwaze dada ingia ndani uchukue pesa apo mezani ukanunue sabuni yako ila samahani lakini kama nimekukosea kukukwambia kachukue pesa sababu mimi miguuni nina mapovu siwezi kuingia ndani.

yule dada akasema bila samahani kaka utakuwa umenisaidia sisi tusio na waume tunapata tabu kweli.

lile neno liliniuma sana alafu dada uyu kajitoa ufahamu kweli nikawa naumia roho kama vile yule kaka nishamwambia isia zangu alafu kakubali sasa naona wivu kwa kweli natamani kutoka kumwambia yule dada jieshimu ukome kufata wanaume za watu na kanga moja.

mala yule dada anamwita yule kaka kaka siiyoni pesa yenyewe apa mezani juu imeingia chini ya uvungu naomba uje uinue meza niiname niokote samahani alafu mpaka kadi yako ya benk imedumbukia chini ya uvungu.

kaka akanyanyuka akaingia ndani ili akanyanyue iyo meza.

alipoingia tu upepo wa mvua ulifunga mlango kwa nguvu puu mshindo wa mlango uliumiza roho yangu sana.

namsikia kaka anasema dah mlango utakuwa ushajiloki uu.

namsikia yule dada anasema mshindo wa mlango umeangusha kanga yangu.

dah yani niliumia mimi mpaka niliamua.........

ITAENDELEA 

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post