TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

NKURUMAH

Ndugu Nkurumah alipoingia Marekani kwaajili ya masomo katika chuo cha Lincolin mnamo 1935, alikuwa hana pesa zakutosha kukidhi gharama za kujikimu.

Kutokana na maswahibu hayo ndugu huyu alianza biashara ya kuuza samaki lakini biashara hii haikuwa na mafanikio alipata anguko la kiuchumi na kubaini hawezi kuwa salama katika utoshelevu wa nini ale kesho yake.

Akaacha biashara na kuishia kuwa mtu asiye na kazi hofu ikawa inamwandama katika nchi ya ugeni anatanga tanga akafika katika mitaa ya Harlem akihangaika nini litabadirika.

Kama ilivyo asili inavyowajali iliowaamulia hatma fulani ili kubadili kitu katika maisha, Nkuruma alikutana na mwanafunzi mwenza kutoka Lincolin ambaye katika asili alitoka Demarara huko Guinea akampasha kisa chake ndipo ndugu huyo katika asili akamjibu: "usijali kaka yangu, ninadhani naweza kutatua swala la makazi kama mwanzo" 

Alimweleza kile alichojua kuhusu familia ya kihindi ya magharibi waliokuwa waungwana na wakarimu haswa na kama akienda kuwaeleza jambo la Nkuruma alihisi wangeweza kumsaidia.

Hakika vyakutosha mara baada ya kusimulia kisa cha Nkuruma kwake macho yake yalitokwa na machozi alimpatia chumba cha ziada bwana Nkuruma na kumsihi kwamba asihofu kuhusu malipo ni mpaka atakapokuwa salama kiuchumi.

Msaada huu pekee ambao mwanafunzi na familia hii ulitoa kwa Nkuruma ulimsaidia kumaliza masomo yake na kurudi Afrika kuwasilisha funguo za uhuru wa kisiasa katika bara la Afrika. Ndiyo Ubuntu ndiyo njia yetu na ndiyo njia inayoweza kuileta Afrika tuitakayo.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post