—Ni mwafrika aliyeuzwa utumwani mnamo 1724 akiwa na umri wa miaka 14 kuna wakati alijulikana kama "Kalkuleta ya Vijinia" kutokana na uwezo wake mkubwa kupindukia wa kutatua hesabu ngumu kichwani mwake.
—Wengi wakihitimisha kuwa huenda alipata ujuzi wake huko barani Afrika alikotoka kwa kuwa alikouzwa watumwa walikuwa hawapewi elimu.
—Uwezo wake katika uchakataji wa hesabu ngumu ulitumiwa na wapigania haki ya kuondoshwa utumwa kama alama yakuonesha kwamba Wazungu si bora kuliko waafrika yeye akiwa mfano katika mazungumzo yao.
—Alipimwa kwa kuulizwa hivi kuna sekunde ngapi katika mwaka? alijibu kwa dakika 2' kwamba ni 47,304,000sek, na walipomuuliza ni sekunde ngapi mwanadamu wa miaka 70 siku 17 na masaa 12 alijibu kwa dakika moja na nusu. kwamba ni 2, 210,500,800.
—Moja ya waliokuwa wakichakata majibu katika karatasi alimjulisha Fuller kwamba alikuwa amekosa kwasababu jibu lilikuwa ni dogo sana ndipo akajibu kwaupokea kwamba: "Mkuu, umesahau miaka mifupi" ndipo miaka mifupi ilipoongezwa na jibu likawa sawa sawia.
—Unapokuwa haufahamu ulipotoka kwasababu unajifunza walipotoka wengine hauwezi kutambua utukufu ulionao.
Tags
Historia