KUTANA NA MTUKUTU JONAS SAVIMBI, MTUKUTU HASWAA ALIYEISUMBUA SERIKALI YA ANGOLA, HATIMAYE ALIULIWA KIFO CHA KUTISHA.
Jonas Malheiro Savimbi ni moja ya Wanasiasa na Wapigania Uhuru katika moja ya mataifa yaliyopo kusini mwa Afrika yaani Angola.
Jonas Savimbi ni nani ktk Ardhi ya Taifa la Angola na nje?. Jonas Savimbi alizaliwa mnamo Agosti 3,1934 ktk Eneo lijulikanalo kama Munhango Jimboni Bie Angola wakati wakoloni Wa Kireno wakilitawala Taifa hilo .Savimbi kwa miaka zaidi ya 30 alipigana Msituni hii inamfanya kuonekana Mpiganaji hodari wa vita vya Msituni .Aliuawa kinyama Karibu na Eneo lijulikanalo kama Lucusse ktk jimbo la Moxico Nchini Angola .
Jonas Savimbi Alikuwa ni mwanasiasa na kiongozi wa muda mrefu Wa Kikosi cha Askari wapigania Uhuru Wa Msituni .Angola ni moja ya mataifa yaliyojinyakulia Uhuru kwa mtutu Wa Bunduki ikisaidiwa na mataifa yaliyokuwa mstari Wa mbele (Frontline States) kama Tanzania ,Zimbabwe Nk . Jonas Savimbi Alipigania Uhuru kutoka kwa Wakoloni Wa Kireno na Baada ya Uhuru Wa Angola mwaka 1975 yeye aliendelea kupigana na Serikali ya Angola kwani ktk fikra zake aliamini bado watu Wa Angola hawajapata Uhuru kamili .
Kihistoria yeye ni mtoto Wa Mfanyakazi wa Reli ya Benguela ,baba yake alikuwa ni Mkuu wa kituo cha Reli .Kitaaluma ,Alisoma ktk shule za kidini za misheni ambazo kwa wakati huo zilikuwa ngumu sana Kuwapokea watu weusi kutokana na moja ya ndugu yake Savimbi kuwa moja ya machifu Wa kabila la Ovimbundu basi ikawa rahisi kufanya Urafiki na wamishionari Wa Roman katoriki na kufanikiwa kuhitimu masomo yake ya awali na baadaye alipata ufadhiri Wa kimasomo na kwenda ng'ambo (Ulaya) .
Savimbi Alisoma taaluma ya madawa(Udaktari) katika chuo kikuu cha Lisbon nchini Ureno mnamo mwaka 1958-1960 ,Chuo Kikuu cha Fribourg mwaka 1961- 1964 na baadaye alijiunga na chuo kikuu cha Lausanne nchini Uswizi huku akibobea ktk Sayansi ya Siasa (Political Science) mnamo mwaka 1964-1965. Huku akiwa masomoni huko Lisbon miaka ya 1950 alianza kuupinga utawala katili Wa Kireno nchini Angola .
Mnamo mwaka 1961 Savimbi alipata kiu kubwa sana kuamua kufanya harakati za kulikomboa Taifa la Angola kutoka ktk makucha ya wakoloni Wa Kireno hivyo akajiunga na moja ya kundi la wapigania Uhuru lijulikanalo kama Popular Union of Angola (UPA) ,Baadaye National Liberation Front Of Angola (FNLA) lililokuwa chini ya Uongozi Wa Holden Roberto .Alijiunga kama mpiganaji Wa kawaida asiye na ujuzi mkubwa ktk mapambano ya Msituni .Mnamo mwaka 1965 Alipata nafasi ya kwenda nchini China na kupata mafunzo makubwa ya kijeshi akibobea mapambano ya vita vya Msituni (Guerrilla war) .Mwaka huo alikutana na kiongozi Wa Taifa la Uchina Mao Tse Tun ,Viongozi Wa Kijeshi na wanasiasa Wa chama cha Kikoministi ambao wote kwa pamoja walimpa mbinu mbalimbali za kukabiliana ktk vita vya Msituni .
Savimbi aliwahi kaririwa na Gazeti la Reader's Digest akisema " Kutoka kwa Mao na Wakoministi nilijifunza namna ya kupigana na kushinda Vita vya Msituni .Lakini vilevile nilijifunza kuendesha Uchumi au Taifa ,Utajiri Wa Taifa hutengenezwa na hatua zinazochukuliwa na watu Binafsi ".
Baada ya mafunzo ya kijeshi huko China Savimbi alirejea nyumbani na kuendeleza harakati zake za ukombozi Wa Taifa la Angola .Aliporudi alianza taratibu kuwahamasisha watu Wa jamii ya Ovimbundu ambao ni robo tatu ya nchi hiyo kuanza kujitambua na kupigania Uhuru wao kutoka kwa Mkoloni Wa kireno.
Mnamo Machi 13, 1966 Baada ya kuona kundi la FNLA ni dhaifu sana halifikii malengo yake aliamua kujiengua au kujitoa na kuunda kundi la wapigania uhuru lijulikanalo kama National Union for the Total Independence of Angola (UNITA) na kuanza kuendeleza ndoto yake ya kuung'oa utawala Wa Kireno .Udhaifu Wa FNLA ulitokana na mapigano yake dhidi ya watawala Wa Kireno kuanzia nchini Zaire kwa sasa DRC .Kutokana na sababu FNLA walikuwa dhaifu sana na kiu yake Savimbi ilikuwa ni kuanzisha mapambano kutokea ktk Ardhi ya Angola Siyo Zaire (DRC).Savimbi alishirikiana na Antonio da Costa Fernandez waliunda UNITA ktk Eneo lijulikanalo kama Muangai kwenye jimbo la Moxico .Mnamo Disemba 25,1966 pambano la Kwanza La UNITA lilifanywa dhidi ya Wakoloni Wa Kireno .
Savimbi ndiye kiongozi Wa wapiganaji Wa Msituni aliyesalia nchini Angola huku akipigana na Wareno kwani alikuwa amejiamini vilivyo dhidi ya utawala katili na dhalimu Wa Wareno .Mnamo Novemba 10,1975 Taifa la Angola lilipata Uhuru wake kutoka kwa Wareno .Hatimaye Harakati za kutaka kuunda Serikali huru ya Angola zikaanza na chama cha MPLA kikiwa ni miongoni mwa vyama vilivyokuwa vikipigania Uhuru dhidi ya Wareno kiliunda Serikali mpya.
Savimbi kama miongoni mwa wapiganiaji Wa Uhuru Wa Angola hakuridhishwa na ugawanaji Wa madaraka na hatimaye kuapa kupambana kwa njia ya vita vya Msituni mpaka atakapotwaa madaraka na kuiangusha MPLA .Kilichomuudhi sana Savimbi kitendo cha.....................!!!!!.
ITAENDELEA.
*************
PIA,
UNAWEZA KUJIUNGA NA GROUP LETU LA SIMULIZI HUKO WHATSAPP KWA AJILI YA KUSOMA MAKALA NYINGI ZAIDI ZA KUSISIMUA KILA SIKU.
UNALIPIA KIASI CHA SHILINGI 1500 TU KWA MWEZI MZIMA.
HIVYO KAMA UKIPENDEZWA KUJUMUIKA NA MEMBERS WENGINE KULE KATIKA GROUP, MTUMIE MESEJI ADMIN KWA KUBOFYA LINK HAPO CHINI AMBAYO ITAKULETA KWA URAHISI MOJA KWA MOJA WHATSAPP KWA ADMIN KWA MAELEKEZO ZAIDI YA UTARATIBU WA KUJIUNGA.
KAMA BADO HAUJAJIUNGA NASI KATIKA GROUP MPAKA LEO HII, JUA KUWA UNAPITWA NA MENGI.
*******************
#PIA USISAHAU KUFOLLOW UKURASA HUU WA STORIES ZA KUSTAAJABISHA, PAMOJA NA KUSHEA ILI NA WENGINE NAO WAPATE KUELIMIKA🙏
Tags
Historia