TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

USIKATE TAMAA, JARIBU TENA

USIKATE TAMAA, JARIBU TENA..
Kuyafikia Mafanikio ya maisha yako sio kitu rahisi. Kuna wakati magumu na mabaya yatakuijia na utajisikia kukata tamaa na hutatamani kuendelea mbele tena.Utaachana na juhudi ya safari ya Mafanikio yako na utaona ni bora ukaishi maisha ya kawaida kama watu wengine.Utaona hamna haja ya kujisumbua bure, kwa sababu huoni matokeo yoyote ya kile unachokifanya.....
 
Watu wengi tunapokutana na magumu katika kile tunachokifanya ndio unakuwa mwisho wetu wa kuendelea mbele zaidi.Tunaachana na juhudi zetu kwa kike tulichokuwa tunakifanya tunaenda kuishi maisha ya kawaida. Tunabaki kwa kujisemea kuwa mafanikio ni kwa watu wachache na mafanikio ni bahati. Kitu amabacho sio kweli.....

Rafiki yangu najua kuna magumu katika kazi unayofanya, najua kuna changamoto unazopitia na zinakusumbua kweli. Najua Kuna saa unakutana na matatizo na unahisi kama dunia yote iko kinyume chako. Najua Kuna muda unaona kabisa hakuna mtu anayekupenda na Wala huoni msaada wowote kutoka kwa watu wako wa karibu zaidi hasa ndugu jamaa na marafiki, Kuna wakati unaona kila mtu ni msaliti katika maisha yako, hata MUNGU mwenyewe Kuna wakati unaona kama hakupendi vile na amekuacha kabisa......

Sio wewe peke yako, katika Kipindi hiki watu wengi hujiuliza maswali magumu sana kutokana na magumu wanayopitia katika maisha yao na huwa ni Maswali ambayo hayana majibu. Kipindi hiki watu wengi wanapata msongo wa mawazo na kuona kila kitu kama kimesimama kati maisha yao. Tumaini la maisha yao linakuwa halipo tena. Kifupi wanakuwa kama wamekufa ingawa wanaishi.

Inawezakana ndio mchumba wako kakuacha. Inawezekana ndio mme au mke kakukimbia na hakutaki tena. Inaweza kuna rafiki au mtu uliyemuamini kakusaliti. Inawezekana ndio biashara yako imekufa na hauoni matumaini tena ya kuiendeleza. Inawezekana umefukuzwa kazi na hauna sehemu nyingine ya kuanzia. Inawezekana ndio unaumwa sana na umekata tamaa ya kuishi tena. INAWEZEKANA NDIO…..

Rafiki yangu, Kuna kipindi kwenye maisha unapitia kiasi kwamba unahisi kama umewekewa gunia la misumari na unaona hakuna anayeangaika kukutua huo mzigo wa misumari unayohisi kuwekewa. Kuna kipindi kigumu katika maisha yako unaweza Kupitia kiasi kwamba Unaona kila mtu kakukimbia na huna msaada wowote, hata wale ambao hukawazania, wale ambao uliwaamini sana unawaona hawapo karibu yako tena. Na unaona kama misha yamefika mwisho na hauna tumani la kuishi tena..

Nini cha kufanya sasa unapopita katika kipindi kigumu......

Usikate tamaa rafiki yangu. Moja ya kanuni ya watu waliofanikiwa leo, ni watu ambao kukata tamaa kwao ni mwiko. Wako tayari kujaribu mara nyingi zaidi mpaka waone matokeo. Kufanya biashara umejaribu mara ngapi? Kutafuta kazi umejaribu mara ngapi? Kama haujafikisha mara mia(100) nenda kajaribu tena. Ndio rafiki yangu kajaribu tena.

Gumu linapokuijia katika maisha yako jifunze Kupitia gumu hilo na uendelee mbele. Najua sio rahisi, najua inauma sana. Kama ingekuwa rahisi kila mtu angefanya. Lakini najua unao uwezo ndani yako wa kutoka kwenye maumivu hayo uliyonayo ya kuachwa na mwenza wako, kusalitiwa na umpendaye, Kukataliwa na umtarajiaye. Najua unao uwezo mkubwa sana ndani yako wa kutoka kwenye changamoto hiyo inayokusumbua sasa. Upo uwezo mkubwa ndani yako rafiki yangu. kama yasemavyo Maandiko...

"Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na MUNGU ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu.
Mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili"
     ( 1 Wakoritho 10:13)

Siku zote Mafanikio yanatekwa na watu wenye nguvu. Watu ambao wako tayari kujitoa kwa kila hali ili wafanikiwe. Watu ambao wako tayari kujaribu mara nyingi zaidi kadiri wanavyoweza mpaka waone matokeo ya kile wanachofanya au kukitaka. Usikate tamaa rafiki, jaribu tena na Tena....

Unaweza kutoka katika maumivu unayopitia leo hii, Unaweza kuvuka katika magumu unayopitia leo. Unaweza rafiki yangu. Wewe ni wa thamani sana. Kuna nguvu kubwa ndani yako ya kukutoa hapo ulipo. Unapopitia katika kipindi kigumu kumbuka una nguvu hiyo ya kuamka tena na kuendelea na safari ya mafanikio ya maisha yako...
   Yawezekana huniamini nisemacho, basi amini haya MANENO ya Maandiko Matakatifu...

 " Je, si mimi niliyekuamuru? uwe hodari na moyo wa Ushujaa. Usiogope wala usifadhaike, Kwa maana BWANA MUNGU WAKO, Yu Pamoja nawe kila uendako"
      (( Yoshua 1:9 ))

  

TAFAKARI NJEMA RAFIKI YANGU.....
             🙏🙏🙏

       BWANA AKUBARIKI....
            
    TUZIDI KUJIFUNZA, NA 
   TUSICHOKE KUJIFUNZA..
         ✍️✍️✍️

Mwanasaikolojia & mshauri,
    Mwalimu Sunzu 🗯️
      0765900743

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post