TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

KUTANA NA ALIYEKUWA MSHAURI WA RAIS MOBUTU SESE SEKO, ANAYEISHI MAISHA YAKIFUKARA MNOO KWA SASA.

KUTANA NA ALIYEKUWA MSHAURI WA RAIS MOBUTU SESE SEKO, ANAYEISHI MAISHA YAKIFUKARA MNOO KWA SASA. 
Pichani ni aliyekuwa mshauri mkuu wa rais wa Zaire kwa sasa DRC MOBUTU SESESEKO.

Wakati wa Utawala wa Mobutu huyu mzee alikuwa mtu wake wa karibu sana na alikuwa na kazi ya kumpa ushauri ambapo aliweza kumshauri mambo mengi sana,

Alimshauri Mobutu ajilimbikizie mali, alimshauri Mobutu amuue kikatili Pierre Mulele eti kwa kuwa tu alikuwa ni rafiki wa Lumumba na pia kwa hofu ya kupatikana mtu wa kuwaletea Upinzani madarakani.

Aliishi maisha ya starehe yeye na Mobutu Seseseko huku wakila bata vilivyo kwenye makasri na kutembezwa kwenye meli yao ya mv KAMANYOLA
Walikula maisha huku wananchi wakiogelea kwenye umasikini wa kutupwa, Watu wengi sana waliuwawa kinyama chini ya Ushauri wa huyu mzee.

Sasa baada ya Mobutu kupinduliwa huyu mzee alikosa wenyewe alirudi mtaani na kwenda kuishi na zile familia alizokuwa akizionea wakati akiwa Ikulu na Mobutu, alikwenda kuishi na familia ambazo zilipoteza wapendwa wao kwa ushauri wake wa kidhalimu.

Hata hivyo bado yupo hai Mungu ameamua kumuadhibu kwa njia hii, anapatikana jijini kinshasa ambapo ni Masikini fukara na anaishi kwa maisha ya kuombaomba mitaani

Yaani Kutoka Ikulu alipokuwa anakula pweza na mivinyo ya Ufaransa hadi mitaani ambapo anaishi kwa taabu na kulishwa kwa masimango.

Tukio hili ni funzo sana kwa watu wenye Madaraka, wakumbuke kuishi vizuri na watu kwani ipo siku Mungu atakushusha kutoka huko ulipo hadi mitaani ambapo utaenda kuishi na Wale wanyonge uliokuwa unawaona siyo kitu mbele zako.

#TAFADHALI RAFIKI, USIACHE KUSHEA KWA WENGINE ILI NAO WAWEZE KUJIUNGA KATIKA GROUP HILI MAKINI KWA AJILI YA KUELIMIKA NA KUBURUDIKA.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post