SIKU OSAMA BIN LADEN ALIPOZILIPUA BALOZI ZA MAREKANI ZILIZIPO NCHINI TANZANIA NA KENYA, HAKIKA HAITOSAHAULIKA.
Na Mfaume Hassani Hamadi.
Mashambulizi hayo yaliyofanyika kwa tofauti ya dakika chache kati ya ubalozi ulioko Dar es Salaam na ule wa Nairobi, ndiyo yaliyomtambulisha kwa mara ya kwanza kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaida, Osama bin Laden.
Kabla ya tukio hilo ni watu wachache mno waliokuwa wakimjua Osama na washirika wake likiwamo kundi la kigaidi la Al Qaeda.
Osama Bin Laden, alitambulika rasmi kama mtu hatari katika uso wadunia hali iliyopelekea shirika la upelelezi la marekani FBI, kumuweka katika kitabu chake cha wahalifu 10 wakidunia waliohitajika zaidi.
Agosti 7, 1998 balozi mbili za marekani nchi za Afrika Mashariki, Tanzania na Kenya zililipuliwa kwa wakati mmoja katika shambulio la kigaidi lililo ratibiwa na kundi la kigaidi kutoka Misri ambalo ni katika mtandao wa Al Qaeda chini ya Osama Bin Laden.
Zaidi ya watu 213 walipoteza maisha, ikiwemo wafanyakazi na raia wa kawaida. Watu 44 walikua ni wafanyakazi na raia wamarekani (raia 12 wa marekani, na wafanyakazi 32)
Katika shambulio la Nairobi inakadiriwa kua raia 4000 walidhurika na shambulio.
Baada ya shambulio marekani ilikuja kutoa msaada wa kuokoa na pia kuwarudisha nyumbani raia wake walionusurika.
Jambo ambalo ni baya na lakuhuzunisha kabisa ni kwamba miongoni mwa magaidi waliotumika kutekeleza mashambulio haya walikua ni raia wa Tanzania na kenya, wakishirikiana na raia wengine kutoka nchi ya Somalia na nchi za uarabuni.
DAR ES SALAAM, TANZANIA.
Ilikua ni siku ya ijumaa tarehe 7 Agosti, 1998, ambapo gari aina ya lori lililokua limebeba vilipushi baruti, lilijaribu kuingia katika eneo la ubalozi lakini likazuiliwa na walinzi getini.
Dereva baada yakuona hivi aliamua kulipusha mabomu yake palepale alipokua. Ilikua mbali kidogo na jengo hali iliyosaidia kupunguza madhara.
Bahati nzuri, shambulio la Dar es salaam halikuleta madhara makubwa ukilinganisha na kule Nairobi. Hii ni kutokana na sababu kua ubalozi haukua katikati ya mji, na hapakua na makazi ya watu karibu na balozi. Balozi ilikua kando ya mtaa wa Bagamoyo. Watu 11 walikufa na Zaidi ya 80 walijeruhiwa.
NAIROBI, KENYA.
Shambulio la Kenya lilikua ni kubwa Zaidi na lilileta maafa makubwa ukilinganisha na la Dar es Salaam. Hii ni kutokana na location ya ubalozi uliokua Kenya.
Huku mbinu iliyotumika ikiwa ni ileile ya lori, majira ya saa nne na nusu asubuhi watu wawili walikua ndani ya lori lililokua likisogea karibu na ubalozi wa marekani njia panda ya barabara za Moi na Haile Selassie karibu na kituo cha reli. Lilikua Lori dogo lililobeba kilogramu 700 za baruti.
Jitihada zakuingia katika gereji iliyokua chini ya balozi zilishindikana kwa sababu yakukataliwa na mlinzi bwana Benson Okuku Bwaku.
Ndipo gaidi Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali alipoamua kutupa kombora lamkono ambalo lilimkosa mlinzi na kumpa nafasi ya kukimbia.
Gaidi mmoja (Al-Owhali) alikimbia na mwingine alieitwa Azzam alianza kufyatua risasi hovyo na baadae akajitoa muhanga kwa kujilipua ndani ya lori. Mlipuko ulikua mkubwa kiasi chakusikika umbali wa kilometa 16. Ndani ya balozi walikua watu 44.
Mbali na kwamba jengo la ubalozi halikuanguka lote kutokana na uimara wake, vifo vingi vilitokana na mshtuko ulioingia ndani kupitia madirisha na kuangusha baadhi ya kuta za ndani.
Jengo dogo jirani la ufundi lilibomolewa na vifo vingi vilitokea katika jengo hili lililoanguka kabisa. Raia wengi walikufa.
Hata baadhi ya magari na watu walikua barabarani waliathiriwa na mlipuko wa bomu hali iliyosababisha magari mengine kuchomwa kabisa na abiria wake waliokua ndani.
MAREKANI YAPANIA KULIPA KISASI KUPITIA
OPERATION INFINITE REACH.
Baada ya tukio la Agosti 7, marekani haikuridhika kuwaacha magaidi salama na ilitaka kuwapa donda watakalokua wakiliponya kama walivyofanyiwa raia wa marekani na balozi zake.
Mapema ya Agosti 20, 1998, siku ya 13 baada ya shambulio Afrika mashariki, Makombora ya marekani yalielekea huko Sudan kwa Al bashir na Afghanistan, katika operesheni iliyopewa jina la “Operation Infinite Reach”
Hii ilikua ni operesheni maalumu iliyolenga kumuua kiongozi wa Al-Qaeda Osama bin Laden na washirika wake kama Ayman Al-Zawahiri waliosadikika kuwepo katika kambi ya kundi hilo, katika mji wa Khost Afghanistan.
Operesheni hii pia ililenga kusambaratisha kiwanda cha madawa “Al-Shifa Plant” kilichokua Sudan ambacho kilisadikika kumtengenezea Osama Bin Laden kemikali aina ya “VX nerve” iliyotumika kutengeneza silaha zakikemikali na vilipushi.
Mmiliki wa kiwanda cha Al-Shifa alisemekana kua na ushirikiano na Bin Laden, kwa kumpa msaada wa kifedha.
Katika uchunguzi wa.............!!!!!.
INAENDELEA KATIKA GROUP.
*************
UNAWEZA KUJIUNGA NA GROUP LETU LA SIMULIZI HUKO WHATSAPP KWA AJILI YA KUSOMA MAKALA NYINGI ZAIDI ZA KUSISIMUA KILA SIKU.
UNALIPIA KIASI CHA SHILINGI 1500 TU KWA MWEZI MZIMA.
HIVYO KAMA UKIPENDEZWA KUJUMUIKA NA MEMBERS WENGINE KULE KATIKA GROUP, MTUMIE MESEJI ADMIN KWA KUBOFYA LINK HAPO CHINI AMBAYO ITAKULETA KWA URAHISI MOJA KWA MOJA WHATSAPP KWA ADMIN KWA MAELEKEZO ZAIDI YA UTARATIBU WA KUJIUNGA.
KAMA BADO HAUJAJIUNGA NASI KATIKA GROUP MPAKA LEO HII, JUA KUWA UNAPITWA NA MENGI.
*******************
#PIA USISAHAU KUFOLLOW UKURASA HUU WA HABARI FORUMS, PAMOJA NA KUSHEA ILI NA WENGINE NAO WAPATE KUELIMIKA🙏
Tags
Historia