WHATSAPP: 0785276697
SIMULIZI: UMUTWALI
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
“Ona hawa mweu wanakuja shule muda huu kama shule ya baba yao” mwalimu alisema kisha akahamuru walengwa wasonge mbele kupiga magoti, alifura akabadilika kawa Mbogo.
SONGA NAYO...
“Mwalimu, tu tusamehe” sauti ya kike iliongea kwa uwoga.
“Sihitaji msamaha.... Kenge nyinyi. Alex...” mwalimu aligoma kutoa msamaha kisha akamwita mwanafunzi aitwaye Alex kwa sauti kali.
“Naam!...” akaitika.
“Nenda ofisini kalete fimbo” akaagiza.
“Zipo sehemu gani?” akahoji.
“Chini ya meza yangu” mwalimu alijibu huku akitoa jicho tamanio kwa walengwa.
Mwanafunzi baada kusikiliza agizo akaongoza moja kwa moja zilipokuwa ofisi za walimu, alirejea amebeba fimbo ya mpera akakabidhi kwa mwalimu. Fatuma akaonekana dhahiri shahiri hofu ikimzonga baada kuona fimbo imeletwa, akionekana kutetemeka kwa uwoga kama kitoto cha Paka kinyesheacho mvua.
“Yes!...fimbo hii ndio nipendezwayo. Nyinyi Kenge leo nitawachapa viboko mpaka kiboko kikatike” mwalimu alitoa vitisho mara baada kupokea fimbo aliyokabidhiwa.
“Donald, kamata chini” mwalimu alifoka huku akimpiga fimbo za mgongo mlengwa.
Alikamata chini baada mwalimu kufoka akachapwa fimbo mpaka alihitaji kudondosha chozi, kwakuwa mwanaume akajikaza kikondoo akachapwa kisha akaruhusiwa akakae.
“Fatuma, nyoosha mkono” mwalimu aliamuru mara baada kumwadhibu mlengwa wa kwanza.
“Wewe, si’nimekuambia nyoosha mkono” mwalimu alisema mara baada kugundua mlengwa kifikra hayupo nae.
Alishtuka akaongoza kwa ghadhabu kumfuata mwalimu akanyoosha mkono akachapwa kisha alikwenda kukaa huku machozi yakitiririka, mwalimu baada kuwaadhibu wanafunzi akarejea kufundisha fasihi andishi linalotoka katika somo lake la kiswahili. Wanafunzi wakatulia tuli! wakawa makini kujifunza mpaka mwalimu alipomaliza kufundisha na kuwaaga, yalipita masaa kadhaa mara kengele ya mapumziko ikagongwa wanafunzi wakatoka nje walikwenda kupata poza tumbo. Donald alikwenda kununua mihogo ya kukaanga kisha akanunua juisi ya Embe mwishowe akaongoza kutulia chini katika mkorosho anakula, alipokuwa anakula ghafla akashtuka mara kuhisi ameshikwa bega alipogeuka ana kwa ana akamwona mlimbwende ameshika sahani iliyokuwa na chipsi na glasi iliyojaa juisi ya Embe.
“Naweza kujumuika na wewe?” Fatuma mlimbwende aliuliza huku akionyesha tabasamu bashasha.
“Unaweza” Donald alijibu huku akizidi kufakamia chakula.
“Asante...karibu kula” Fatuma alisema kimzaha mara baada kukaa chini ya mkorosho.
“Kula!...siwezi kuchanganya chakula naogopa kuvuruga tumbo” akagoma.
“Isitoshe nina chakula...wewe endelea kula chako” akakomea.
“Sikatai, una chakula lakini radha tofauti. Usijivunge karibu kula” Fatuma alibembeleza mpaka mlengwa uvumilivu ukamshinda akala chakula kwa kuonja.
“Aagh!...kitamu” Donald alisema kwa kumpaka mafuta mhusika alionekana kutabasamu kisha akandelea kula chakula chake mara baada kuonja chakula.
Baada kuhitimisha chakula kengele ya kurudi darasani ikagongwa wanafunzi wote wakarudi darasani, waliongoza pamoja walipofika wakatemana kila mmoja alikwenda kukaa katika kiti huku wakisubiri masomo yaendelee. Baada ya muda wanafunzi wakanyamaza baada kuingia kwa mwalimu anayefahamika Catheline Temba, alikuwa mwalimu wa darasa anayefundisha Historia alifundisha faida na hasara zitokanazo na utalii. Alipofundisha mara akaondoka akawaacha wanafunzi wakijisomea baada siku ndefu ghafla kengele ya kurudi nyumbani ikagongwa, hekaheka za wanafunzi kwenda kusikiliza matangazo zikaendelea maradufu wakiwa tuli mara mwalimu anayefahamika majina Ludovik Kalombo mwalimu wa taaluma akapanda katika jukwaa akaanza kutoa matangazo.
“Motto!...” akahamasisha.
“Elimu haina mwisho jilinde na zinaa” wakahamasika.
“Kesho mapumziko itakapofika Jumatatu zamu yangu nawakumbusha kuwahi maana atakayechelewa hama zake hama zangu” mwalimu Kalombo aliongea huku akitoa macho akiashiria kuhimiza.
Alipotangaza akawaruhusu wanafunzi kuondoka, Donald akiwa njiani akielekea nyumbani mara akahisi sauti nyororo ikimwita akageuka amwone amwitaye akatabasamu baada kugeuka na kuwona amwitaye.
“Hujataka kuongozana nasi?” alikuwa Fatuma akahoji mara baada kuwa pua na mdomo na mlengwa.
“Niliwatafuta sikuwaona” alijibu Donald kisha polepole wakatembea kwa kuongozana.
“Oooh, tulikwenda kusafisha ofisi ya walimu” shogaye Fatuma afahamikaye Amina Ndoro aliongeza mazungumzo huku akikwepesha macho kwa kutazama pembeni kwa aibu.
waliongozana walikwenda katika kituo cha daladala huku wakipiga soga, walipofika Chicago wakasubiri daladala za Mbezi hawakusubiri sana mara daladala ikawasili wakapanda hawakupata kiti wakaongoza kusimama nyuma. Daladala kwakuwa ilijaa na hakuna wakushuka daladala ilitembea mpaka Kimara mwisho Fatuma na Amina wakashuka wakalipa nauli kisha wakamwaga Donald, kondakta akapiga debe kisha akaamuru daladala ing'oke.
**********
Fatuma binti pekee wa mfanyabiashara mashuhuri aitwaye Kandir Magoa, amezaliwa kisiwani Zanzibar asili yake na lafudhi yake ya kiarabu. Anaishi na wazazi Dar es salaam katika nyumba walionunua wazazi Kimara mwisho, walihama visiwani wakaja bara baada kutokea baa la njaa Zanzibar.
*********
Amina binti kitinda mimba wa mwanajeshi mstaafu Ndoro Mapambano aliyefariki katika vita ya kwanza ya dunia na binti wa nesi mstaafu Rose Mkalange aliyefariki kwa ugonjwa wa kifua kikuu, Amina mwanamwali wa kitanga anaishi na bibi mzaa baba katika nyumba aliyoachiwa na wazazi Kimara mwisho akalelewa na bibi baada wazazi kupoteza maisha.
**********
Donald Mtalanze mzawa wa Dodoma, anaishi na wazazi Kimara suca katika nyumba ya familia baada wazazi kununua nyumba kutoka kwa wakili mstaafu. Masaa kadhaa yakayoyoma baada kutoka shule hatimaye akafanikiwa kufika nyumbani salama.
“Ngriiiiii!...” mlio wa kengele ulisikika ukilia mara baada mlengwa kuwasili katika lango kuu la nyumbani.
“Nani?...” Angel akiwa ndani akasikika akihoji huku akikimbia kwenda kufungua lango.
“Donald...” akapayuka.
“Unaongea kidebwedo...” Angel alichombeza utani mara baada kufungua lango na kuonana na mlengwa.
“Nimechoka sana...” Donald aliongea kisha wakaingia ndani mara baada mlango kufungwa.
“Pole sana...” Angel alisema huku akimpokea begi Donald kwa huruma.
“Asante...” akashukuru.
Walipofika sebuleni akampokea begi Angel akaongoza moja kwa moja chumbani, alimwacha Angel ameongoza jikoni kumwandalia msosi baada dakika kadhaa akarejea sebuleni akiwa amebadili vazi. Alimkuta Angel kashamwandalia chakula anatazama runinga alikwenda kula kisha akahoji huku akimeza fundo la Ugali kinywani.
“Angel, wazazi watawahi kurudi leo?.”
“Sijajua.”
Tags
simulizi