TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

DAWA ZINAZO CHANGIA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

DAWA AMBAZO ZINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME:-
Tafiti mbalimbali zimegundua dawa ambazo zina athari kubwa juu ya nguvu za kiume na hutumiwa mara kwa mara.

Hapa chini ni dawa zinazopaswa kuepukwa na wanaume, ili wasipoteze nguvu zao za kiume. 

Sababu mbalimbali zinaweza kusababisha vikwazo hivi, lakini baadhi ya sababu zinahusishwa na aina sita ya dawa kama ilivyotangazwa na Shirika la Habari la ANI, ambalo lilitayarisha taarifa maalum juu ya mada hii.

 *Dawa ya kutuliza maumivu* 
Watu wengi hawasiti kutumia dawa za kutuliza maumivu hata kwa maumivu wanayohisi ni madogo.

Lakini, je, unajua kwamba dawa zilezile za kutuliza maumivu zinaathiri uanaume wako na kuufanya usiwe na matokeo mazuri kitandani?

Dawa za kutuliza maumivu huzuia kuundwa kwa seli za uzazi na huvuruga homoni nyingi ambazo ni muhimu katika kufanya tendo la ndoa kati ya wanaume na wanawake.

 *Dawa ya kuzuia wasiwasi (anti-anxiety* )
Watu wengi wanaolalamika kuhusu matatizo ya akili na kuwa na wasiwasi hutumia dawa ili kukabiliana na hofu.

Walakini, dawa kama hizo hupunguza hamu ya tendo la ndoa.

Dawa hizi zinaweza kusababisha mtu kupoteza hamu ya kufanya mapenzi.

Wakati mwingine hata husababisha wanaume kupoteza fahamu zao kabisa.

 *Dawa ya kutibu kuganda kwa damu* 
Dawa zinazotumika kutibu kolesto, ambayo ni mgando wa damu, pia zina mchango mkubwa katika kupunguza nguvu za kiume.

Wataalamu wa matibabu wanasema kuwa dawa hizi huingilia utendaji wa seli za uzazi.

Utafiti: Dawa hii ilikuwa itibu tatizo la moyo 'bahati mbaya' ikageuka tiba ya upungufu wa nguvu za kiume

Tanzania: Dawa za kuongeza nguvu za kiume zatambuliwa na serikali

Utafiti unaonyesha kuwa dawa zinazotumika kutibu kuganda damu wakati mwingine husababisha matatizo kwa wanaume wanapolala kitandani na wake zao.

 *Dawa za msongo wa mawazo (Sonona)
Dawa hizi, zinazojulikana kama "benzodiazepines," mara nyingi hutumiwa kutibu magonjwa ya wasiwasi, kama vile wakati mtu anaogopa vitu ambavyo havipo na yuko peke yake.

Magonjwa mengine ambayo hutumia dawa hizi ni pamoja na kukosa usingizi na maumivu ya misuli.

Lakini, upande wa madhara ni kwamba huathiri utendaji wa seli za uzazi wa kiume na hisia.

Dawa ya Kuzuia Shinikizo la damu
Wagonjwa wanaotumia dawa za shinikizo la damu wanaweza pia kukumbana na changamoto nyingine ambayo ni kupungua kwa nguvu zao.

Dawa hizi zinaingiliana moja kwa moja na mishipa ya damu na pia hufanya kazi na mfumo wa neva.

Wataalamu wengine wameongeza kuwa yapo hata matatizo ambayo wanawake wenyewe wanakumbana nayo na dawa hizo ambazo zinahusiana na viungo vya uzazi.

 *Dawa za Kifua Kikuu
Dawa za dukani kama vile dawa za kupuliza katika pua zilizoziba na dawa za kwaida za kupunguza kuziba kwa pua zina athari zake.

zinaweza kusababisha matatizo katika tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.

🔸Ongea na daktari
Zungumza na daktari wako ikiwa unafikiri kuwa dawa ina athari mbaya kwenye utendaji wako wa tendo la ndoa. Usiache kutumia dawa yoyote bila kwanza kuzungumza na mtoa huduma wako.

✍️.... Ushauri wangu changamoto zote unazo ona zinakukabiri lazima Kuna visababishi hivyo Ukitumia virutubisho lishe vitakusaidia kurutubisha mwili wako na kuondoa kabisa visababishi vya changamoto yako na baada ya mda utaanza kuona afya yako inarejea kawaida.

Natambuwa Hali ningumu lakini usipo jiweka sawa kiafya Hali itakuwa ngumu zaidi kwasababu uwezo wako utapunguwa Kila siku zinavyo enda.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post