TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

MJUE OSCAR KAMBONA MPIGANIA UHURU ASIYEZUNGUMZWA, ALIYEISHIA KUWA NA UADUI MKUBWA NA MWALIMU NYERERE.

MJUE OSCAR KAMBONA MPIGANIA UHURU ASIYEZUNGUMZWA, ALIYEISHIA KUWA NA UADUI MKUBWA NA MWALIMU NYERERE. 
Jioni ya Ijumaa ya tarehe 13.8.1925, huku mvua kubwà na radi kali zikirindima kijijini Kwambe, wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma, alizaliwa mtoto wa kiume akiwa buheri wa afya. Wazazi wa mtoto huyo, Rev. DAVID KAMBONA na Bi. MARIAM KAMBONA, wakampa mtoto huyo jina la OSCAR SATHIEL DAVID KAMBONA. Mvua na radi hiyo, kwa mujibu wa mila za kijijini hapo, "nyumbi hii, bombi hii", ilikuwa ni baraka na ishara kuwa mtoto huyo atakujakuwa wa kipekee.

KAMBONA, tofauti na watoto wengine, hakusomea shuleni elimu ya awali bali alifundishwa na wazazi wake pamoja na mjomba wake ambao wote walikuwa walimu. Mafunzo hayo ya awali yalikuwa yakifanyika chini ya mwembe huku chai na mihogo vikiwa pembeni.

Baadae KAMBONA alipelekwa shule ya Kati ya Mt. Barnabas, Liuli. Akiwa shuleni hapo, KAMBONA alikuwa kipanga na "aliwatimulia vumbi" wanafunzi wote kwa miaka yote alipokuwa shuleni hapo.

KAMBONA alifaulu vizuri mitihani yake na akachaguliwa kujiunga na "Alliance Sec. School", Idodomia ambayo baadae ikajaitwa Mazengo Sec. School. Almanusra KAMBONA asiendelee na masomo kwani baba yake hakuwa na uwezo wa kulipa £ 30 kwa mwaka. Uwezo wa KAMBONA "kutema yai" ndio uliomponya kwani alifanikiwa kumshawishi Askofu kumlipia ada hiyo baada ya kusali Sala ya Baba Yetu kwa Kiingereza!.

KAMBONA alisoma shule hii pamoja na J. Lusinde, E. Mzena, B. Ngwilulupi, A. Nsekela, A. Nyirenda na K. Chiume. Ni akiwa shuleni hapo ndipo kwa mara ya kwanza, KAMBONA alionana na NYERERE aliyekuwa akifundisha St. Marys, Tabora.

Baadae, KAMBONA alienda kufundisha shule hii na akakutana na J. Lusinde na K. Chiume na baadae akawa "Schoolmaster".

KAMBONA alikutana na NYERERE kwa mara ya 2 kwenye Mkutano wa taifa wa waalimu mwaka 1954.

Mwaka 1955, KAMBONA alijiunga na TANU iliyozaliwa tarehe 7.7.1954 na akaonesha bidii kubwa huku akifanya kazi kwa kujitolea kwani TANU haikuwa na fedha. Bidii yake ilipelekea kuwa Katibu Mkuu wa TANU.

KAMBONA alitembea nchi nzima kwa miezi 6 akionana na Machifu na wanavijiji na kufanikiwa kuingiza wanachama 10,000. Baadae akiendelea na harakati hizo na baada ya miezi 12 akawa ameingiza wanachama 100,000. Viongozi wenzake wa TANU walimpongeza sana kwani TANU ikawa inaenea kwa kasi sana.

KAMBONA alikuwa na mawazo ya kimaendeleo kwani kutokana na michango ya wanachama aliweza kufungua akaunti ya kwanza ya TANU. Kwa hakika, hili lilikuwa ni jambo la kihistoria.

Mwaka 1957, KAMBONA alipata fursa ya kwenda UK kusomea LLB kwa miaka 3 na hivyo akaenda huko.

Tarehe 27.6.1957, KAMBONA aliweka historia kwa kutangaza Kiswahili BBC kwa mara ya 1 akisema-: "Hapa ni London, kwa mara ya kwanza BBC inawaletea habari kwa Kiswahili wananchi wa Afrika Mashariki. Asalaam Aleikhum".

Kutokana na talanta yake kubwa ya uongozi, KAMBONA alichaguliwa kuwa Kiongozi wa wanafunzi chuoni na Mwenyekiti wa Tawi la TANU, London.
Kati ya tarehe 26.6.1959 na 7.8.1959, NYERERE alikwenda UK kwa matayarisho ya uhuru wa Tanganyika na akalala chumba kimoja na KAMBONA ambaye walikuwa "wameshibana" sana. Katika "Press Conference" ya 1991 KAMBONA alisema- "TANU haikuwa na hela hivyo ili kubana matumizi, nikakaa na NYERERE room yangu chuoni na hii ilisaidia tuwe na muda mwingi wa majadiliano".

Tarehe 19.11.1960, KAMBONA alimuoa Miss Tanganyika mrembo, Bi. FLORA MORIYO toka Kilimanjaro. Harusi hiyo ya kukata na shoka ilifanyika St. Paul Cathedral, London na kuhudhuriwa na wageni waalikwa 400. NYERERE alikuwa ndiye msimamizi aliyemsindikiza Bi. FLORA altareni. Ilikuwa ni harusi ya kwanza ya watu weusi kanisani hapo na ilitoka kwenye magazeti mbalimbali ya Ulaya.

KAMBONA alirejea Bongo kuendelea na harakati za uhuru akihudumu kama Waziri wa Elimu na Katibu Mkuu wa TANU.

Katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Tanganyika, KAMBONA aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi.

KAMBONA alipendwa sana nchini kwani alikuwa msomi, mwanasiasa hodari, mtanashati na vijana wengi walimuiga staili yake ya nywele "KAMBONA Style". Kwa hakika, KAMBONA alipendwa sana.

Usiku wa tarehe 19.1.1964, askari wa kambi ya Colito(Lugalo) waliasi wakidai marupurupu na nafasi za juu za vyeo kwa Waafrika. Rais NYERERE na Mh. RASHID MFAUME KAWAWA walitoroshwa na mlinzi wao, PETER BWIMBWO usiku wa manane hadi Kigamboni na kufichwa kwenye nyumbaya Mzee KIZWEZWE.
Mawaziri wote walibanisha makwao baada ya kupigiwa simu na Mh. J. LUSINDE, Waziri wa Mambo ya Ndani, kuhofia usalama wao. KAMBONA ndiye pekee aliyeingia "fronti" kwani si tu raia waliokuwa wakimpenda bali pia askari. Waasi walionekana kutulia baada ya mambo yao kuwekwa sawa lakini baada ya Rais NYERERE kuibukia Ikulu toka mafichoni baada ya siku 3, waasi "wakalianzisha" tena hivyo ikabidi maasi hayo yazimwe kwa msaada wa Waingereza na baadae Wanaijeria.

 
KAMBONA alikuwa ni mmoja wa mawaziri wachache sana waliokuwa wakijua mchakato wote wa muungano kwa undani na pia alishuhudia utiaji saini hati za muungano huko Zenji, tarehe 22.4.1964 kati ya Rais NYERERE na Rais wa Zanzibar, Mh. ABEID AMAN KARUME.

 KAMBONA Atofautiana na NYERERE Mfumo wa Chama Kimoja
Baada ya ziara ya China 1965, NYERERE alivutiwa na "alikuwa ameoza" kwa siasa za China na mfumo wao wa siasa hivyo akaunda Tume tarehe 28.1.1964 ili ipendekeze mfumo gani unaifaa nchi yetu. Tume hiyo ilikuwa chini ya Mh. KAWAWA ikapendekeza mfumo wa chama kimoja. KAMBONA, ambaye daima alikuwa hapepesi macho wala hayumbishwi, aliweka kunji na kutosaini ripoti hiyo na badala yake akatayarisha ripoti yake ya kutaka mfumo wa vyama vingi na NYERERE akahuzunishwa sana na msimamo huo wa KAMBONA.

Kipindi hiki NYERERE aliishamuondoa KAMBONA kwenye wizara zile nyeti.

Tarehe 7.7.1966, NYERERE, akihutubia Taifa katika sherehe za 77, NYERERE alitumia mafumbo "kumpa za uso" KAMBONA ambapo alisema viongozi wanaonekana kujipatia mali nyingi kiajabu hawafai hata kidogo.

Tarehe 9.6.1967, KAMBONA alibwaga manyanga kwa kujiuzulu U-Katibu Mkuu wa TANU na Uwaziri wa Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini ambapo alitaja sababu za kiafya kuwa ndizo zilipelekea achukue uamuzi huo.

Kwakuwa KAMBONA alikuwa ni mtoto wa mjini, alitonywa kwamba kuna mpango wa kumkamata na kumsweka kizuizini.

Hivyo, usiku wa kuamkia tarehe 26.7.1967, KAMBONA, mkewe, watoto wake 2 na msaidizi wa kazi walifunga virago na ku-drive hadi Kenya kwa staili ya "James Bond"! Watu wengi walipigwa butwaa ni kwa vipi aliweza kutoroka bila kubambwa!.

Usiku wa siku hiyo jijini Nairobi, KAMBONA na familia yake walikwea "pipa" East African Airways Flight 720 kwenda "Kwa Mama, huku, huku nyuma ikadaiwa alitoroka na mamilioni ya fedha!.

Siku chache baada ya KAMBONA "kula kona", NYERERE, akiongea na viongozi wa TANU Morogoro, alisema : "Itachukua muda mrefu kufahamu sababu za Bw. KAMBONA kujiuzulu, lakini jambo moja ni dhahiri; KAMBONA amenidanganya mimi, TANU, TZ na Afrika".

Baada ya kusikia vijineno kwamba amesepa na mamilioni, tarehe 6.9.1967, KAMBONA alikanusha vikali na kuitaka serikali ya Tanzania iwasiliane na ya Kenya kupata uthibitisho kitu ambacho serikali ya TZ hakikufanyika.

OTTIN na MATTIYA KAMBONA, 
Hawa wadogo zake KAMBONA walionja "joto ya jiwe" kwani walinyakwa usiku tarehe 30.12.1967 na kuwekwa kizuizini, Ukonga.

Familia zao zikasambaratika vibaya sana kufuatia kukamatwa kwao. OTTIN alikuwa ni "Journalist" na MATTIYA alikuwa mfanyakazi Wizara ya Kilimo. OTTIN alikuwa amemuoa raia wa Martinique na walikuwa na watoto 2 wadogo na MATTIYA alikuwa amemuoa Mgambia wakiwa na mtoto wa miezi 3 tu. Wanawake hao walifukuziliwa mbali na kurudishwa makwao pamoja na watoto wao!.

Jumanne ya tarehe 23.1.1968, KAWAWA, 2nd VP, alilitaarifu Bunge:

"Wote mnajua kwamba Bw. KAMBONA aliikimbia nchi mwaka jana, 1967. Kabla hajaondoka, tarehe 6.12.1966, TZS 500.000/= ziliingizwa kwenye akaunti yake toka benki moja ya Uingereza. Uchunguzi wa BOT toka KAMBONA atoroke umeonesha kuwa tangu Juni 1965 na Desemba 1966, KAMBONA aliingiza katika akaunti yake jijini Dsm TZS 896,800/=. Kambona pia alikuwa anamiliki majumba mengi (Nyumba Magomeni-Plot No. 21,39 31), (Kunduchi bichi-Plot No.28), (Msasani bichi -Plot No. 92), (Morogoro-Plot No. 89) ns (Songea-Plot No.21)".

Baada ya TZ kuitambua Biafra, serikali ya Rais YAKUB GOWON ilikasirishwa sana hivyo ilimwalika KAMBONA aichafue TZ . Kwahakika, "jipu likawa limepata mkunaji" Hivyo, KAMBONA akaenda na kutoa muadhara Lagos tarehe 14.6.1968 ambapo "alimchana" vilivyo Rais NYERERE

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post