DijitoStore - Business software

JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI

JINSI YA KUPIKA NJEGERE ZA NAZI
MAHITAJI

1. Njegere nusu kilo
2. Nazi 2
3. Nyanya 2
4. Karoti 1
5. Pilipili hoho 1
6. Kitunguu maji 1
7. Thoum kiasi
8. Mafuta ya kupikia kiasi
9. Chumvi kiasi

JINSI YA KUPIKA NJEGERE
1. #Chambua njegere, zikoshe, kisha zitie kwenye sufuria na maji uzichemshe ziive kiasi lakini zisilainike sana.

2. #Safisha nyanya uzimenye na kuzikata. Pia katakata hoho, karoti na vitunguu. Twanga vitunguu thoum. kisha kuna nazi uchuje tui zito na jepesi.

3. #Bandika sufuria jikoni, weka mafuta ukaange vitunguu, vikishabadilika rangi tia hoho kaanga kidogo kisha utie thoum na nyanya pamoja na karoti, endelea kukaanga.

4. Mimina njegere, tia chumvi na umimine tui jepesi, wacha lichemke. kisha tia tui zito liache lichemke kiasi na uzito wa njegere ukiwa sawa, tayari epua......

.5. Chakula kiko Tayari kuliwa 
kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post