TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

WATU HATARI KATIKA MAHUSIANO

Huyu ni mtu ambaye huchukua nafasi ya mzazi kwa kila mtu wanayemjua. Anataka kukusimamia kwa kila kitu unachofanya kama vile wewe ni mtoto mdogo. 
Atakuhukumu sana, anasema ukweli lakini bila upendo na hana nafasi ya neema au msamaha. Yeye anafikiri maneno yakikuchoma ndio utabadilika. Kibaya zaidi ni kwamba haachi kukukosoa wala kukupa nafasi ya kutekeleza (practice) kukosolewa kwako mwisho unapata msongo wa mawazo (frustration).

Hari yako itakuwa mbaya sana kama utaonyesha udhaifu wako, ataushambulia ujasiri wako mpaka utajihisi dhaifu. Ukimkosea anakukunbusha zamani... unataka ufanye kama zamani...au ulivyonifanyia vile sikuamini tena kwamba unaweza kufanya vizuri.

Watu aina hii wanajali sana kushambulia makosa yako Kuliko kuunganishwa na wawe (make connection).

Hawajui tofauti ya udhaifu na dhambi kwa hiyo huwahukumu wengine kwa kila jambo. Huyu anakunyoshea kidole wewe tu, mpaka utahisi kujuta kuwa naye katika mahusiano.

Watu wa aina hii wanapenda ukweli na uadilifu. Wanafikiri vizuri (clear thinker) ukiwauliza kwa mambo ya maono sawa, ila kwa mambo ya mahusiano ukweli wao unagubikwa na sumu za kukosoa sana mwingine (mpenzi) mwisho unalemewa na hatia.

Mara nyingi utajihisi hatia na kulemewa na kujilaumu ukiwa nao unajikuta wewe ni mkosaji tu hakuna jema hata moja.

Wakati mwingine hukukosoa kama hivi....kama wewe ungekuwa ni mtu wa hi hivi...usingefanya hivi...

 Ni watu wazuri sana kama mambo kufikiri ukiwa nao utakuwa salama lakini kwa mahusiano ni mzigo. Wanasema ukweli lakini bila huruma_hawatumii kanuni ya kunywa vizuri inayosema; maneno yako yawe na neema(fikiri ukiambiwa wewe utajisikiaje), kuzungumza ukweli katika upendo na kuzungumza katika roho ya Imani.

Kwa hiyo hao ni watu wa kufanya nao kazi si watu wa kuwa nao kwenye mahusiano ya mahaba.

#malackbayaga

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post