TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

JINSI YA KUPIKA SAMBUSA ZA NYAMA

JINSI YA KUPIKA SAMBUSA ZA NYAMA 
MAHITAJI YAKE NI :- 

Nyama ya kusaga kg 1
Ajinamoto kjk 1 cha chai
Vitunguu kama 10
Karoti 5
Gligilani puch 1
Swaumu na tangawizi iliyosagwa 1/2 kkmbe
Chumvi kiasi upendacho
Unga wa ngano

  Jinsi ya kuandaa:-
Marinetti nyama na swaumu na tangawizi, kisha changanya vizuri kisha iache kidogo iingie viungo kama dk 10 au tano kisha injika jikoni iiive mpka ikauke kabisa kisha weka pembeni iPoe

Chop vitunguu maji na karoti na boga na daniq kisha changanya na nyama iliyokuwa tayari imesha iva vizuri kisha baada hapo tunaingia hatua ingine

Hatua inayofuata ni kutengeneza manda ya sambusa wengine hupenda kukunua manda ya bakresa ila mmi huwa napenda kutengeneza manda yangu mwenyewe

Hatua jinsi ya kutengeneza manda

Unga wa ngano 1/2 na 4
Chumvi kidogo sana
Changanya vizuri na unga kisha unaweza kutumia maziwa au maji we mwenyewe ukipenda uchaguzi wako

Baada ya hapo unaingia sasa kukanda unga wako wa manda ,hakikisha usiwe mlaini wala kuwa mgumu sana

Kata madonge yanayoendana yaani kulingana na ukubwa kisha sukuma dizaini ya chapati ila isiwe nyembambaa 

Pakaza mafuta upande mmoja kisha nyunyiza unga kwa mbali kisha weka donge uliosukuma weka juu yake tena endelea hivyo mpaka madonge yako yaishe kisha
Sukuma kwa pamoja mpaka iwe nyembamba upana wa chapati ya kawaida

Andaa moto wa kawaida kama umepalia wali kisha chombo cha kuchomea chapati kisha ziweke moto uwe kiasi kisha baada ya hapo bandua moja moja mpaka ziishe kisha kata kipimo unachotaka ili ufunge sambusa azako

Funga sambusa zako kisha zichome katika mafuta masafiii sana kisha choma sambusa zako baada ya hapo sambusa zipo tayari kwa kuliwa

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post