KUTANA NA MSITU HUU WA KUTISHA WENYE MAUZA UZA KEDE KEDE UPATIKANAO MKOANI NJOMBE.
Njombe ni mmoja wa mikoa 31 ya Tanzania, uliorasimishwa kuwa mkoa mwaka 2012 mara baada ya kutenganishwa na Iringa inayopatikana Nyanda za Juu kusini Kwa Tanzania. Hapo awali Njombe ilikuwa ni wilaya ndani ya mkoa wa Iringa ikiwa ina ukubwa wa eneo la mraba la Km 21,347. Sensa ya mwaka 2012 ilionesha kuwa Njombe ina wakazi wanaofikia kuwa 702,097. Mkoa wa Njombe ni maarufu kwa kilimo cha mahindi na viazi.
Makabila makubwa ya wenyeji mkoani Njombe ni Wabena, Wakinga na Wapangwa, na uwiano wao ni 37:11:3.
Kama ilivyo mikoa mingine, Njombe ina historia yake ya kipekee. Neno "Njombe" lenyewe limetokana na jina la mti unaoitwa "Mdzombe" ambao ulipatikana kwa wingi eneo la Mdandu yalikokuwa makao makuu ya Ngome ya Mjerumani wakati huo (Bomani). Mkoa wa Njombe Una vivutio vingi sana vya utalii, Nyumbanitu ni kimojawapo.
Neno "Nyumbanitu" ni muunganiko wa maneno mawili; nyumba na nitu. Neno "Nitu" manaake ni Giza au Nyeusi. Hivyo Nyumbanitu maana yake ni nyumba yenye Giza au nyumba nyeusi.
Nyumbanitu si nyumba kama lilivyo neno lenyewe, bali ni msitu mdogo wenye ukubwa wa hekta mbili na nusu (2.5) tu. Msitu huu mdogo wenye mambo ya kustaajabisha upo katika Kijiji cha Mlevela, Kata ya Mdandu Wilaya ya Wanging’ombe, ni Km 15 kutoka Njombe mjini.
Kwa sasa msitu huo unatunzwa na wanandugu , Julius Vangameli Msigwa na Alex Vangameli Msigwa, ambao kabla ya kutembeza wageni msituni huwa lazima waulize nia ya ujio wa wageni husika. Kuna ambao huenda nyumbanitu kuomba mizimu iwape baraka Katika mambo yao. Kuna ambao huenda kuchuma dawa, wengine huenda kujifunza Mila na desturi za mahali hapo nk.
Kabla ya kuingia ndani ya msitu huo mdogo ni lazima wenyeji (Familia ya Msigwa) ambao ndio wenye msitu wao wafanye maombi mafupi Kwa mizimu ili wapate ruhusa ya kuingia. Si kila mahali unaweza kutumia kuingia ndani ya msitu huo, kuna njia maalumu ambayo Si rahisi kuijua, labda wenyeji tu.
Iwapo utathubutu kuingia ndani ya msitu huo bila kibali cha familia iliyopewa jukumu la kuulinda, hakika yatakukumba makubwa ya kimiujiza ujiza,
Tags
Duniani