Dada mmoja aliyekuwa akifanya kazi kama msaidizi wa ndani katika jumba moja la kifahari, siku moja akiwa anajiandaa kwenda kazini alipigiwa simu na boss wake kuwa asiende kazini kwani wamempata mfanyakazi mpya.
Alilia sana kwa muda mrefu kwani alijua jinsi familia yake livyokuwa ikimtegemea kutokana na mshahara wake. Baada ya kulia kwa muda akakumbuka maneno ya kwenye maandiko matakatifu yasemayo, " Binadamu hupanga mipango yake, lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi-Mungu. Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa,
lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu. Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake"
baada ya kukumbuka maneno hayo akajisemesha taratibu, " Mungu akiufunga mlango mmoja, hufungua milango mingine mingi ya riziki kwa watu wake" Kisha akanyanyuka na kuendele na kazi za nyumbani.
Siku moja akiwa anapita nyumba kwa nyumba, ofisi kwa ofisi akitafuta kazi akakutana na kijana mmoja ambaye akamwambia, " Dada unaweza kunisaidia kitu tafadhali ofisnini kwangu? Mhasibu wangu hajaja ofisni kwa kuwa ameacha kazi bila kunipa taarifa na kwenda sehemu nyingine na pia sina wakunisaidi.
Binti akasema, " Lakini kaka mimi mfanyakazi wa ndani sijui lolote kuhusu masuala ya ofisini" Usijali nitakuelekeza kila kitu na kukupeleka shuleni pia mpaka uelewe.
Binti akaanza kutokwa na machozi ya furaha huku akimwambia Mungu wake asante kwa kuwa umenijibu sala zangu kwa kunizifanya ndoto zangu kuwa kamilifu.
Funzo la leo
Mungu anaweza kukuinua kutoka sifuri mpaka kuwa mwenye kuheshimika na kukubalika kama utamtegemea yeye.
AMEN
#Darasalamahusiano
Tags
sms