DijitoStore - Business software

ASILIA NA MAANA YA JINA MBOKA MANYEMA (Tabora)

Historia hii itakufungua na kuelewa kwanini Mkoa wa TABORA huitwa MBOKA MANYEMA
Wanyamwezi wengi wanapenda kupaita Tabora 'Mboka' au 'Mboka Manyema' wengine hupaita 'Empire Bakuba'
Wamanyema, Waha na Wanyamwezi ni kama "dugu mmoja" tu. Wamanyema na Waha wengi wanaishi Tabora. Hivyo, mchanganyiko huo wa binadamu huleta hadi mchanganyiko wa lugha na Maneno.

Hii ni Misemo ya utani tu 
Mboka=Nyumbani, 
Manyema=imechukuliwa kama mtu wetu. 
Na 'Empire bakuba' = Mpigania himaya' 

Kumbuka hili jina la 'Empire Babuka' limetumika kama kinogesho tu, pia lilipata umaarufu kutoka kwa Mwanamuziki Pepe Kalle katika bendi yake 'Empire Bakuba'. 

Kwa hivyo Wanyamwezi wakalichukua na kuanza kulitumia wanaposema 'Mboka Manyema' humaanisha Wamanyema ni watu wetu au Manyema ni nchi yetu'. | Na wanaposema 'Empire Bakuba'' humaanisha 'mapigano ya Himaya yetu'

Wanaosema hivo sio Wanyamwezi peke yao, hata Wamanyema waliolowea hapo Tabora, kwani ukizingatia hapo Tabora Wamanyema wamekaa miaka mingi sana na kuchanganyikana na Wanyamwezi original mpaka na wao wanaonekana Wanyamwezi.

Ilikuakua vipi Wamanyema na Wanyamwezi kuchanganyikana?

Wakati wa vita vya kwanza vya dunia baina ya Mjurumani na Mbelgiji, Jeshi la Mbelgiji kutoka kongo (Congo-Belegie) waliiteka Kigoma baadhi ya raia wa kimanyema na waha waliingizwa jeshini kwenda kupigana vita, miongoni mwao alikuwepo Mzee Bilali Mafumu Kalindula, mzee huyu alizaliwa mwaka 1886, ni mzee mmoja wapo alieshiriki katika ujenzi wa meli ya Graf von Gotzen au Liemba mwaka 1913 baada vita kuanza yeye na wenzie wote waliingizwa jeshini, baada ya kigoma mjini kutekwa na Congo-belegie, Wajerumani walijenga ngome Uvinza. 

Wanajeshi wa Congo-Belegie wakiwa katika kasi kubwa ndani ya uwanja wa vita walifanikiwa kufika maeneo ya Usinge wakielekea Kaliua hadi Tabora. 

Wanajeshi wa Congo-Belgie waliishambulia kwa mizinga mji wa Tabora mwaka 1916 wakati wa vita ya kwanza ya dunia. Wakazi wa mjini Tabora walionekana kuyalaki majeshi ya Congo-Belegie mwaka 1917. 

Kwa hivyo basi Wamanyema na Waha waliolowea Tabora baada ya vita hivyo, walikaa huko huko na wakachanganyikana na Wanyamwezi. Na ndipo maneno hayo yakawa yanazuka na jina hilo la 'Mboka Manyema' likadumu hadi sasa. Lakini kabla ya vita hivyo Wamanyema walikuwa wanaishi Kigoma na walikuwa wameshafika Tabora miaka mingi kipindi cha utumwa. Na walikua wakisafiri kwa mguu kutokea Ujiji hadi Tabora kupitia njia ya Rubuga miembeni (Kagera) hadi Tabora.

Kwa hivyo vita vya kwanza vya dunia iliongeza wamanyema kutoka Kigoma kuja Tabora, kwani baadhi yao walichukuliwa kama wanajeshi haswa katika jeshi la Mjerumani ambalo lilikuwa linatetea himaya yake ya Tanganyika dhidi ya mbelgiji.



kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post