TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

MJI WA QUSWAY (Tabora Ya Leo)

Tabora
Mji wa Qusway Mji huu kabla ya haujaitwa jina Tabora''ulifahamika kwa jina la Unyanyembe''tangu 1800-1837 Alipotawala Chifu wa Mwanzo aitwaye Chifu Swetu'' I mwaka 1800-1837 katika kipindi hicho ndio alifika Qusway kutoka Bagamoyo, Wanyamwezi hawakuweza kutamka Qusway'' basi wao walimuita Kiseh'' naye aliishi juu kidogo ya kilima kilichopo nje kidogo ya Tabora mjini katika njia ya kuelekea Itetemiya-
Mji wa tabora wakati huo ulienea kwihara na Itetemya sehemu ya mji waliokuwa wakikaa watu wengi uliitwa kwa Kisehi huyo kisehi alikuwa Mzee wa Mji labda ndiye aliyeuanzisha.'
Wazungu nao walipo fika walimuita kazeh' na hicho kilima walikiita kazeh hill yaani kilima cha kazeh' na hivi ndivyo wanahistoria wengi wamemuandika hivi kufika kweke huko kulibadilishs jina la mji huo baada ya kukaa hapo na kupata umaarufu hasa kutokana na biashara walizokuwa wanafanya na Wanyamwezi wa hapo''
huu ndio Mji Mkongwe wa Tabora ambao Liwali Thnei bin Amir akiishi hapo hata wafanyabiashara wakubwa wakubwa wa Kihindi kama vile Mussa Mzuri waliweka makazi yao hapo
watu wengi walikwenda hapo na Mji ukawa hapo pakaitwa kwa Kiseh na jina la Unyanyembe likaanza kupotea kidogo kidogo na umaarufu ukawa ni mji wa Qusway/''

Kuitwa tabora Mji huo wa Qusway haukudumu sana katika kulitumia jina hilo bali Shughuli za biashara zilizokuwa zikitendeka ziliubadili Jina Mji huo tena.'

Kulikuwa na biashara za kuuza viazi vilivyochemshwa na kuanikwa- ambavyo huitwa kwa Kinyamwezi Matobolwa'.biashara hizi zilikuwa maarufu hapo kwa Qusway ambazo ziliwafanya watu waswme twendeni kule kunakouzwa Matobolwa.'-
Kuna kauli mbili hapa kuhusu jina hilo kutoka kwa waarabu waliofika hapo wao wakashindwa kutamka Matobolwa wakatamka twendeni kunakouzwa tabora na hapo ndipo likasehelea jina Tabora''
na pia husemwa kwamba Waarabu waliofika hapo waliona hivyo viazi vinapendwa sana na wenyeji wakaviita Twa'amun boura''yaani Chakula kizuri''kimatamshi ya Kiarabu Ta'abora yaani Tabora'')

Dola ya Zanzibar chini ya Sayyid said iliendelea kuijenga miji mbali mbali ya tanganyika, ukiwa pamoja na Mji huu Sanjari na kutuma makungi mbali mbali ya wataalamu na walimu makadhi na maliwali tangu Utawala wa Swetu 1 Mpaka tawala za machifu wote takriban 
Mbali na ujio wa Qusway wakati huo Swetu( I ) hata utawala wa fundikila tayari mzee rajabu bin juma bin hemed al murjeeb kutoka Shangani Zanzibar alikwisha wasili na kuweka makao yake Ndavelwa Itetemiya
mwanzo harakati za wazanzibar ilikuwa hapo Itetemiya na baadae kujengwa ikulu ndogo kwihara''-

Lakini mwanzo Sayyid said aliujenga Mji wa kahama Shinyanga na Mwanza pakiitwa Nchi ya Wasumbwa katika mwaka 1830.Khalafu baadaye 1852 ndipo alipoujenga Mji huo wa Tabora''
Wazanzibar walipofika tanganyika ilikuwa desturi yao ni kujenga Miji au kambi walizo zita Bandari inasemwa ya kuwa bandari moja ilijegwa Msene katika Nchi ya Wasumbwa yaani kahama katika mwaka 1830'-na moja Ujiji katika mwaka 1845.'
Lakini Mji Mkuu wao uliitwa kazeh na baadaye uliitwa Tabora nao hudhaniwa haukujegwa mpaka (ilipofika) mwaka 1852''

Baada ya Swetu 1 Utawala wa tabora ukawa chini ya fundikila bin Swetu,Fundikila alifanya kazi na Mzee juma El Murjeb akiwa ni Mkwewe baada ya Mzee juma kumuoa Bint Fundi kila Aitwaye kalunde,lakini hata ilipofika mwaka 1830,-
Walipata Mtoto aitwaye Muhammed bin juma bin hemed EL murjeeb ambaye alizaliwa Stone Town Zanzibar.Sayyid said alimtuma Said salum Al Lemky kuwa liwali wa Dola ya Zanzibar-Tabora na Thnei bin harth akiwa ni kadhi mkuu wakishirikiana na Mzee juma murjeeb walifanya kazi kuu ya kuusomesha Wanyamwezi
hata hivyo katika mwaka 1876 baada ya kufariki fundikila Uchifu ulichukuliwa na Mkasiwa bin kiyungi katika mwaka huo sayyid said Majid akamleta Adallah bin Nasib el muttafy'

Sayyid said na utawala wa zanzibar ulikubalika vizuri katika tabora na maeneo mbalimbali ya tanganyika hivyo tabora ilikuwa ndio baba ya tanganyika kwa kuteuliwa kuwa ndio Ngome madhubuti na kuzikombawa nchi zilizokuwa kuwa na machifu makatili''Mpaka hapo kituo cha pili cha harakati za ujenzi zilihamia kwihara palipojengwa ikulu ndogo Na said salum El lemky wakishirikiana na Thenei bin Amir kazi hii ya kujenga Tembe zilizotumika kama ikulu ndogo ya Dola ya zanzibar ilifanyika takriban majimbo yote ya dola hii ya zanzibar
Lakini kwa bahati mbaya sana na masikitiko makubwa leo hii tembo hizi zote , ukianzia hii ya tabora ile ya muhammed khalfan Ujiji zimeitwa au zinaitwa Tembe za Dr Livingstone.Lol''
haya maajabu ya ulimwengu,tembe ya shekh Said salum El LEMKY NA THNEI BIN AMIRI EL HARITH chini ya Dola ya Zanzibar imekuwa ya Dr livingston ipo haja ya kuiangalia historia yetu mara mbili mbili vijana vijana wamesha tudanganya sana,'

Hakuna maelezo yoyote yanayohusu kazi halisi zilizofanywa na Waislamu hawa katika tembe hizo isipokuwa maelezo ya kupachika pachika na kumnasibisha Dr Livingston na harakati za kukombowa biashara ya Utumwa kisha kuwanasibisha Waarabu na Biashara hiyo basi hakuna kingine cha kuzungumzia,-

hakuna maelezo yeyote ya maana ya kihistoria zaidi ya maelezo hayo,basi tena maelezo hayo utayakuta takriban vituo vyote utafikiri hakuna jambo lolote la maendeleo lilokuwa likifanywa isipokuwa ni warabuu utumwa?? 
Mbali na hayo ukilitazama jengo lenyewe huo muundo na ujenzi wake haufanani hata kidogo na kazi ya Mzungu hata vifaa vilivyopo ndani ya jengo hilo havina nasaba na Wazungu mbaya zaidi vitabu vyote vya kale takriban havikulinasibisha jengo hilo na Ujenzi wa Dr LIVINGSTON bali vimeeleza wazi wazi kuwa wajenzi ni hawa tuliowataja/' 
lango kuu la tenbe hiyo lililotengenezwa na mafundi staidi kwa mtindo wa ki Zanzibar 

Mlango wa tembe ya kwihara iliyonakshiwa kwa nakshi za Kiarabu kutoka Zanzibar (Zanzibar Door) je Dr livingstone alikuwa Muarabu?
kuna na makubadhi ndani ya tembe ya kwihara Dr livingston alivaa makubadhi?.? Vipo vitu vingi vilivyohifadhiwa humo zikiwemo pesa za Zanzibar iliyoandikwa haafidh-hullah''

Hata hivyo henry Morton Stanley alipopita hapo alikaribishwa kama alivyokaribishwa huyo Dr livingstone, hakufanya khiyana, yeye akaziandika habari zake katika kitabu 
(How I found Livingstone)

Tabora ilikuwa ni kituo cha makaazi ya Waarabu kuenea AFRICA ya kati toka kapo tabora ilikuwa imekusanya zaidi ya maekfu ya tembe ambazo zilikuwa ndani ya nyumba moja (tembe ikulu ndogo) inaweza kuwaweka watu salama tena hata wakiwa kundi kubwa la watu wa kiarabu waungwana saana na wakaazi mpaka wakafika watu elfu tano.

kati ya tabora na Mji mwingine wa kwihara kulikuwa na miinuko vilima viwili ambayo inatofautisha Mji hiyo miwili ukiwa juu ya milima ya tabora unaweza kuuona Mji wa kwihara hakuna eneo lilikubalika zaidi kuliko Kazehili

Usiache ku follow Ukurasa Wetu kujifunza zaidi

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post