Je Unajua Kwanini Unakosa Hedhi Kwa Muda Mrefu Au Hedhi Yako Inavurugika???
Zijue sababu 8 kwanini unakosa hedhi au hedhi kuvurugika
*Jinsi Mzunguko Wa Hedhi Unavyofanya Kazi*
Kikawaida kila mwezi mwanamke hutoa yai moja ili lirutubishwe kutengeneza kichanga. Pale yai lisipotolewa kwenye kikonyo chake tunaita unovulation.
Moja ya dalili kwamba mayai yako yanapevuka lakini hayatolewi ni kukosa kabisa au kuvurugika kwa hedhi.Kwa wanawake wasio na ujauzito wenye umri wa kuzaa kuanzia miaka 15 mpaka 40 na hawapati hedhi, hiki ndio kisababishi cha kushindwa kushika mimba kwa karibu 30%.
Mpangilio wa hedhi unaratibiwa na vichocheo au homoni za mwanamke hasa estrogeni. Homoni za estrogeni husaidia kujenga ukuta na mazingira mazuri kwa ajili ya ukuaji wa kiumbe kinachozalishwa.
Mwanamke akishakoma hedhi uzalishaji wa estrogeni hupungua sana na ndio maana unaanza kukosa siku zako.
Kwa wanawake walio kwenye umri wa kuzaa, kuwa na kiwango kidogo sana cha estrogeni husababisha kukosa hedhi na kuvurugika kwa mpangilio wa hedhi... Bonyeza hapa Kuendelea na Makala hii
Tags
AFYA