TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

DUDU LA KIENYEJI (sehemu ya 01)

*DUDU LA KIENYEJI*
SEHEMU YA KWANZA.
Katika jitihada zangu za kutafuta kazi baada ya kuhitimu chuo kikuu nilijikuta nikipata tabu sana bila mafanikio nilibaki nikiwashuhudia classmates ( nilioslma nao darasa moja) wakipata kazi nzuri na kuyamudu vyema maisha yao lakini kwangu ilikuwa tofauti mpaka nikajuta kwanini nilisoma. Niliomba kazi sehemu nyingi tofauti lakini sikupata bahati ya ajira. Hapo ndipo nilipojikuta nashawishiwa kwenda kwa mganga fulani wa kienyeji na mmoja kati ya rafiki zangu wa karibu, aitwaye Irene. nikiamini kwamba huenda labda nitafanikiwa.
Shoga yangu huyo alimnadi mganga wake kuwa ndiye aliyefanya yeye akapata kazi nzuri katika kampuni fulani ya michezo ya kubahatisha. Alisema kuwa mambo yake mengi yalimnyookea kwa sababu ya yule mtaalamu. Alinisihi sana nikubali anipeleke. Hakupenda kuona shoga yake nikiwa sina kazi.
Hata hivyo haikuwa rahisi kunishawishi kwa kuwa sikuwa nimewahi hata kufikiria kwamba siku moja ningeenda kwa mganga wa kienyeji. Huwa siamini mambo hayo na pia mimi ni muoga wa mambo ya kishirikina. Lakini nikajikuta nimefika kwa mganga.

Mganga huyo alikuwa anaishi nje kidogo ya mji ambapo pia alikuwa anafanyia shughuli zake. Kwa muonekano wake nadhani ana miaka kama 40 na kidogo hivi. Tulipofika pale nikaeleza shida yangu ya hitaji la kazi baada ya salamu huku Irene akinisaidia kujieleza maana ndiye aliyekuwa mwenyeji wangu.

"Sawa. Nimekuelewa binti. Tutajaribu kufanya vitu vyetu ili Mungu akusaidie upate kazi. Unaitwa nani?"

Akaniuliza huku akichukua karatasi moja nyeupe kutoka kwenye moja ya karatasi zilizokuwa pembeni yake. Alikuwa amekaa kwenye mkeka huku mimi nikiwa kwenye kigoda pembeni ya Irene ambaye alikuwa amekalia kigoda kingine.

"Naitwa Elizabeth."

"Na jina la mama ni nani?"

Akauliza na jina la mama angu huku akianza kuandika vitu vyake kwenye karatasi nyeupe kwa kutumia wino mwekundu. Nikamtaji jina la mama. Akaendelea kuandika vitu alivyovijua mwenyewe. Alinyamaza kimya kwa dakika chache akiendelea kuandika.

"Sasa mwili wako inaonekana una nuksi. Inabidi uoge maji ya kuondoa nuksi na mikosi."

Yalikuwa maneno ya mganga yule aliyekuwa mrefu na mweusi. Alikuwa na sura ya kutisha kidogo. Nashindwa kutamka neno 'sura mbaya'. Akaniambia kuwa nirudi peke yangu usiku majira ya saa moja siku iliyofuata ili aniogeshe kuondoa mikosi kwenye mwili wangu kabla ya kufanya dawa zake kwa ajili ya mvuto wa kazi. Nikajibu "Sawa". Kisha tukamuaga na kutoa pesa kidogo kama malipo ya awali. Tukaondoka.

Lakini swala la kuogeshwa na mganga, tena kuogeshwa usiku, kwangu ulikuwa mtihani. Ilibidi nimuulize shoga yangu iwapo na yeye alifanyiwa hivyo. Niliishi labda pengine kuna kitu mganga alikuwa anataka kutoka kwangu maana kiukweli nimejaaliwa.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post