TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

INAWEZA KUWA NI TIBA KWAKO

INAWEZA KUWA TIBA.
_____________________________________
Juu ya kuumizwa ipo tiba.
Juu ya kuumizwa ipo faraja.
Juu ya kuumizwa yupo mtu atakufuta machozi.
Juu ya kuumizwa ipo unaweza kuwa mpya.

Jambo lililojificha sana.
Kutendwa,kuumizwa kila mtu anapata maumivu.
Isipokuwa tofauti ya maumivu ni kushindwa kuhimili maumivu na kufikiri kuvembeleza kwako ndio dawa,kutafuta huruma yake ndio kupona kwako,kujishusha ndiyo dawa.,hapana.

Hali ya mapenzi kupishana kutendana ni kama ushindani na anayejiona yupo top ndiye kiongozi wa kuvimba,kujikweza hana muda wa kujishusha,furaha yake ni kukuona unsjipendekeza,kuona vile unavyolia lia kutaka suruhu.
Nilichojifunza na ni tiba itakayokuponya na kukuweka huru,kujipa thamani.

Ni ushindani,usishindane nae.
Vile unavyoangaika kwake akuhurumie ni wazi ataongeza kukuumiza.
Kitu kitakachokuwa tiba kwako ficha maumivu yako,achana na huruma yake jihurumie mwenyewe ujitibu mwenyewe.
Kama ni jeuri ifanye jeuri kwa kumpotezea,usitumie muda mwingi kutaka suruhu ili hali ni yeye kila mara anakuvimbia.

Ukikuwa na tabia ya kumtext kumbeleleza acha.
Ulikuwa na kawaida kila dk,kila saa kila siku punguza,cancel.
Atakuambia una jeuri mpuuze,atakuambia umempata mtu puuza,atakuambia umpendi ni sahihi kama upendo ulishauonyesha sana matokeo anakuburuza.

Katika mahusiano kuburuzana sio mapenzi ni kutaka utukufu,ni kukufanya uwe mtumwa.
Usikubali kuwa mtumwa,msimamo wako ndiyo tiba ya kuteswa kwako,ukisimamia msimamo,penzi lako litapona na utaishi kwa furaha na amani.
Vyovyote atakavyokuhisi pokea na ushukuru sababu wewe ndio unaujua ukweli wako.
Usishangae akageuka kuwa mtumwa baaada ya wewe kupona.

Kubali apotee kuliko kuendelea kukumbatia utumwa.
Kubali kuanza upya ili kujenga utu wako na thamani yako.
Akienda ni wazi umejifingua nyororo za utumwa wa mapenzi,ndio usalama wako.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post