KUGAWANYIKA MARA MBILI KWA BARA LA AFRICA
Bara la Afrika litagawanyika mara mbili. Afrika Mashariki tutakuwa bara letu wenyewe. Taarifa iliyotolewa kwenye Jarida la Geophysical Research Letters inaeleza kwamba ufa uliotokea huko Ethiopia utaigawa misingi ya dunia(tectonic plates). Ufa huo unaendelea kuongezeka na hatimaye utasababisha bahari mpya kuzaliwa itakayofanya nchi za Afrika Mashariki kuwa bara lake lenyewe. Ufa huo ulioibuka huko Ethiopia mwaka 2005 una urefu wa kilomita 56 uko katika sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Kwa sasa ndio sehemu pekee duniani ambako wataalam wa Jiografia wanasema unaweza kushuhudia kuzaliwa kwa bahari mpya. Inadaiwa baada ya mchakato huo kukamilika nchi ambazo hazina fukwe za bahari kama Uganda na Zambia watakuwa na bahari zake wenyewe. Wataalam wanakadiria kwamba mchakato huo wa Bara la Afrika kugawanyika unatarajiwa kukamilika baada ya miaka milioni 5 hadi milioni 10 ijayo.
Tags
Duniani