USIPOTEZE SHABAHA
Mtu anayechimba madini anakumbana na jua kali anapoitafuta dhahabu,jasho linavuja lakini kwasababu shabaha yake ni kupata madini hapotezi focus yake.
Anakumbana na miamba lakinj anachohitaji ye ni kuvunja miamba na siyo kwamba ana maguvu sana bali ni mpango wa ndoto yake lazima avunje ili aendelee kutafuta madini.Anatumia kila nyenzo anayoiona inaweza kumsaidia kuvunja miamba,anakumbana na vumbi la kumkatisha tamaa lakini hajali.
Anakutana na stori za kumkatisha tamaa anapoambiwa kwamba,"Ebwana hilo shimo la pembeni kuna watu walikufa waliangukiwa na mwamba" Lakini yeye harudi nyuma anachohitaji ni kufanya kazi kwa tahadhari,yaani ni watu ambao hawahitaji kukaa chini na kuhesabu vikwazo.
Kama leo wamekosa wanalala hoi lakini kesho wakiamka wanaamka na imani wanaingia tena shimoni wanaoga michanga wanaendelea kuitafuta dhahabu.Hawapotezi shabaha.
Ndivyo ilivyo katika kila ndoto,utakumbana na vikwazo lakini usikubali kupoteza shabaha,wakati mwingine unaweza kukata tamaa kumbe mafanikio hayako mbali.
Ni nature ya kila aina ya ndoto lazima utapitia shida,vikwazo ndipo ukutane na kile unachokitaka.
Usianze kusema,"Oh!Mimi sina bahati......"Na nani amekwambia huna bahati.Pambana!
Usipoteze shabaha,tafuta mbinu za kutatua shida zinazokupata ukiwa unaielekea ndoto yako,kumbuka mnaweza mkawa na ndoto moja lakini kila mtu akakumbana na vikwazo tofauti na vyako.Usihesabu sana vkwazo unapoteza muda,utakata tamaa.
Tags
saikolojia