WIVU USIYO NA TIJA NI KUJITESA.
_______________________________________
Tunasoma kwenye machapisho ya MaPHD wabobezi ya kwamba wivu ni upendo,wivu ni dalili ya kukuweka moyoni,wivu ni afya ya mahusiano yenu,yes nakubaliana kabisa kabisa.
Kwa sababu ukiumbwa na moyo wa nyama kibinadamu na una mapenzi kitu fulani kama unakipenda na ukaona kinaenda tofauti ni wazi lazma moyo uumie,unapenda na upendi ushare na mwingine.
Shida ni kwamba,tunauweka wivu kwa hasara na inagharimu maisha yetu,inagharimu mahusiano yetu,inaondoa amani kwa wenza wetu na wanaotuzunguka.
Hatua ya kila mara kila wakati kumuhisi vibaya mwenza wako pasipo na sababu bila uhakika na ushahidi ni mbaya sana.
Hatufikiri chanya,unapokuwa mbali na simu,upo busy na kazi,mwenzio anawaza hasi uenda upo na mtu una jambo unafanya
Umetoka umechelewa kurudi,mawazo yake ulikuwa na mtu sehemu mna jambo lenu.
Umechelewa kurudi kazini,mawazo uenda kuna mtu umechelewa nae sehemu.
Hapana hii ni mbaya sana haina afya.
Haina afya kwa sababu ninachokiamini mimi mapenzi hayajifichi,mchepukaji ana njia anaweza kufanya lakini ni lazma kuna siku utagundua,vuta subra.
Sababu aonyeshi anachepuka usianze kumuhisi vibaya.
Wivu unapunguza upendo.
Kitendo cha kumfuatilia sana kana kwamba umuamini,wakati mwingine akikuambia alipo uamini mpaka mpigiane video call.
Unafanya nini,ukielezwa unawaza tofauti.
Usijitanue moyo kwa kuwaza mambo uenda hata hayapo,kama yapo subiri yataonekana tu
Unapomtuhumu kila wakati na uenda hana mpango wa kuwa hivyo kuna wakati inachosha na inamuondolea amani moyoni,kuna muda atafanya kweli.
Akiaga anaenda kazini weka akilini yupo kazini.
Kokote unajua anaenda weka akilini yupo huko
Ikitokea wazi wazi anaonyesha anafanya ni wewe sasa kuchukua hatua na nisingependa kukupa imani ya kuendelea kuvumilia ili uishi kwa amani,kwa furaha epukana nae.
MWISHO
Mnapoamua kuchepuka uenda ni ngumu kuacha lakini embu tengenezeni ulinzi kwa wenza wenu.
Sio jambo linalofanyika hadharani,ni siri basi muifanye iwe siri.
Mkirudi nyumbani muishi na wenza wenu kwa furaha na amani.
Ifike wakati asikushuku kwa chochote kama una mtu,asijue lini umemcheet kini ujamcheet,ukirudi nyumbani upunguzi kitu.
Ni kitu cha ajabu unamcheet bado unaonyesha,bado unampa uhuru mwizi wake awe busy na wewe ukiwa nyumbani.
Sometime hata hudumu kwa familia inamezwa na mwizi wake,watoto wanateseka kisa tu umchepuko amekumiliki.
Na niwashauri sana sana,ukiona mchepuko unaingilia mambo yako ya familia yako piga chini,huyu sio mtu nzuri hana nia njema.
Mchepuko ambao una moyo wa dhati kwako ni ule kwanza unakemea wewe kutowajibika kwako,kutokujali familia,yaani anang'ata na kupuliza,una adabu na heshima kwa anayemuibia.
Hawezi kukubali yeye awe sababu ya wewe kuitesa familia,kinyume na hapo ni shida achana nae
Tags
saikolojia