ACHA KUJICHANGANYA CHANGANYA, ELEWEKA WATU WAKUJUE.
Kwa bahati mbaya tunaishi kwenye dunia ambayo watu hawajikubali walivyo, hawakubaliani na uumbaji wa Mungu na matokeo yake wanaamua kujibadirisha wawe kama wanavyotaka, matokeo yake ni watu kujichubua, kuongeza na kupunguza shepu za viungo vyao. Hii ni mbaya sana lakini imeenda mpaka imezoeleka na inaonekana ni kitu cha kawaida.
Sasa kuna hii tabia ya watu kuto kueleweka, kuna mtu ametoka Kigoma akiwa na jina lake la Janeth, akija Dar es salaam anajiita Ashura, akienda Mwanza anajiita Amina, yani haeleweki hata akipata shida ni ngumu kumtambua na kiufupi anajiweka pabaya.
Kuna mtu mwingine leo ni Mkristo kesho ni Muialamu keshokutwa tena anarudi kwenye Ukristo, yani haeleweki hajulikani yupo upande gani hata akifariki anawaacha watu na maswali wamzike upande wa dini gani.
Kuna watu leo hii asubuhi wapo Kanisani usiku unawakuta Disco, Gesti wanafanya uzinzi, kuna mwanamke leo hii mchana kwenye macho ya watu anajistiri vizuri, ukikutana naye usiku yupo uchi, yani watu hawamuelewi wamuweke kwenye kundi gani, mume upo kwenye ndoa lakini umemficha mke wako kama una mwanamke mwingine ulizaa naye, mkeo hajui ila marafiki zako wanajua.
Sasa kwanini unajitesa? kwanini unajinyanyasa? kaa upande mmoja watu wakujue wewe ni wa upande gani, hakikisha kazini kwako bosi wako anajua dini yako na mahali unaposali, weka wazi kabila lako, weka wazi miaka yako, weka wazi jina la ukoo wako, mtamulishe mke wako kazini kwako watu wamjue, watambulishe wazazi wako watu wako wa karibu wajulikane, acha kuficha ficha mambo unajiweka gizani.
Muweke wazi mke wako wa ndoa, muweke wazi mume wako wa ndoa, waweke wazi watoto wako, weka wazi jina lako unaficha nini? jikubali ishi maishi yako, huyo ndiyo wewe huko unakofosi unajitesa, unapingana na Mungu... ukijikubali ni rahisi kujirekebisha lakini ukijidanganya ni rahisi kuanguka kiuchumi na hata kifikra, acha kujidanganya.
Tags
saikolojia