TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

BINTI MSAHAULIFU 01

SIMULIZI: BINTI MSAHAULIFU.                                                   SEHEMU: 01
ANZA NAYO.

Katika Jumba kubwa pembezoni na mji mkubwa uliokuwa umezungukwa na kisiwa, kulionekana kuna majadiliano kati ya pande mbili huku wakizidi kuvutana huku na kule.

Mama mmoja wa makamo alikuwa akimfokea mumewe huku akimulaumu sana.
"Baba Ndalu!! Kwanini umeamua kumsaidia huyu binti!! Unajua familia yake anakotokea!! Ni bora ungemuacha akasaidiwa na wengine isije ikawa ni Jini umelisogeza ndani!!!"

Muda huo huo akiwa anaendelea kuongea, kuna vijana watatu walifika wakimuulizia binti huyo!! Walitoa picha na kuwapatia kama watakuwa wanamjua huyo Binti.

Mama huyu alimtizama mumewe baada ya kuona anasita kuongea ilibidi amuulize.
"Baba Ndalu!! Mbona husemi kitu!!?"

Baadae Mumewe aliamua kuzungumza.
"Vijana wangu huyo mtu mnaemtafuta naona hatumfahamu, labda mjaribu kuulizia sehemu nyingine!! Kwani Binti Huyo kafanyaje!?"

"Tungempata ndio tungewaambia kwanini tunamtafuta kwa juhudi!!"

Wale vijana waliondoka na kuwaacha mke na mume wakiendelea kujadili.
"Kwanini unamficha Binti huyu!! Si ungewaambia tu, kuwa tupo nae?? Ayaa kamhudumie mpaka azinduke mimi simo kwenye kesi za kujitakia!!"

"Mke wangu acha kuwa na roho mbaya kiasi hicho!! Naona Binti huyu anahitaji msaada kwanza!! Acha apone halafu tutamhoji ujio wake huku!!'

Baba Ndalu aliingia ndani kumuangalia Binti yule!! Alinyanyua simu yake nakupiga kwa Doctor mmoja akihitaji msaada. Baadae Doctor alifika na kumcheki afya yake aligundua kuna kitu kizito alipigwa kichwani ndio kikamfanya azimie.

Alitumia jitihada zake kunusuru Maisha ya Binti huyo, baadae alimuita Baba Ndalu huku akionekana kuwa na huzuni Sana.
"Baba Ndalu!! Naona hali ya mgonjwa sio Nzuri!! Inatakiwa apelekwe hospital kwa uchunguzi zaidi naona kuna damu imegandamia kwenye ubongo hivyo inatakiwa akafanyiwe upasuaji!!

Jitihada zikaendelea wakawa wamefanikiwa kumpeleka hospital! Alienda kuwekwa moja kwa moja kwenye chuma cha ICU kwa uchunguzi zaidi.

Huku nyumbani kwa Mama Ndalu!! Aliingia kwenye chumba kimoja katika nyumba yake! Kilikuwa ni chumba cha siri, kulionekana ni Chumba cha muhimu Sana, Chumba hiki kilikuwa kimejaa nguo za mtoto wa kike mwenye umri kama wa miaka ishirini. Mama huyu alisogea ukutani kisha alichukua picha kubwa iliyokuwa mezani kisha alianza kuitizama huku akibubujikwa na Machozi.

"I'm sorry my Son!! Naimani huku uliko Bado wanikumbuka vizuri mimi mama yako!! Bado nakupenda sana japo ni miaka nane sijakuona kwenye mboni ya macho yangu ila naamini upo salama!!"

Wakati akiendelea kulia alisikia Sauti ya mume wake akifokea.
"Mama Ndalu!! Nishakwambia Hupaswi kuingia kwenye Chumba hiki!! Muda wote umekuwa ukimkumbuka huyu mtoto tayari ameshatangulia mbele za haki, Hupaswi kulia tenaa!!"

"Hapana!! Najua Mwanangu Bado anaishi!! Kama amekufa kwanini hutaki nichome nguo zake!! Hivi Ni wapi ulimpeleka Mwanangu!!!?" Mama alizidi kufoka Huku akimlalamikia mumewe.

Huku hospital Juhudi ziliiendelea kunusuru Maisha ya Binti, Baadae alitolewa na kupelekwa kwenye Chumba Cha kawaida, fahamu zilianza kurejea taratibu, baadae alifungua macho yake Huku akiangaza Huku na kule.

Kuna Dokta alifika pale kumtizama Baada ya Kumuona alishituka Sana, alitoka nje kumuita mganga mkuu wakawa wamekuja moja kwa moja Kumuona Mgonjwa. Daktari alimchukua kipimo Tena baadae Aliona hali yake inaendelea vizuri Ilibidi akae chini kwanza angalau azungumze nae kwanzaa alimuuliza;

"Vipi waendeleaje!!!?! Kichwa hakiumi teenaa!!? Na Vipi waitwa Nani jina lako!!?"

Binti alibaki kaduwaa Huku akizidi kumtizama Dokta, Lakini kwa Dokta aliona Bado hali yake haipo sawa aliamua kumuacha kwanza Kisha alimpatia dawa za maumivu Huku akimuachia maelekezo Nurse aliyekuwa ameingia zamu.

"Naomba muangalie mgonjwa huyu kwa umakini Sana!! Chochote kile kitatokea Naomba uniambie!!"

Baadae Aliondoka na kupiga simu moja kwa moja kwa Baba Ndalu,
"Hello mheshimiwa!! Naona mgonjwa wetu anaendelea vizuri kwasasa anajitambua ila hawezi kuongea!!"

"Sawaa!! Vizuri Sana Naomba endelea kumhudumia, hakikisha anazidi kuimarika halafu akiongea kitu chochote niambie!! Tumia njia yoyote Ili mradi aongee!! Ukihisi hawezi kuongea hebu jaribu kumpatia daftari na kalamu halafu muulize maswali huenda anaweza kukujibu kwa njia ya kuandika."

"Sawaa mheshimiwa nitafanya hivyoo!!!"

Majira ya Mchana Dokta alirudi Tena Wodini Kisha alimchukua Binti na kumpeleka Kwenye Chumba Cha Siri Huku Akiwa amembebea chakula!! Alifika na kumpatia chakula Huku akijaribu kumlisha, baada ya kuona kashiba alianzisha stori za Hapa na pale mpaka zikamfanya Binti huyo atabasamu, baadae alimpatia Daftari na kalamu Huku akimuuliza maswali.

"Wewe Ni Binti mzuri Sana ila Sasa sijakufahamu Majina yako!! Waweza niandikia Majina yako kamili!!?"

Binti alichukua kalamu Huku Akimtizama kwa makini Daktari baadae aliandika Majina yake kwenye Daftari, muda huo Daktari alikuwa akifatisha kila herusi ya jina linaloandikwa baadae Alirudia kwa kulisoma "TINNAH"

"Kwahiyo Wewe Ni Tinnah!!?"

Aliitikia kwa kichwa Ishara ya kukubali!!"

Baadae Doctor alimuuliza Tena!!
"Kwani Nyumbani kwenu Ni wapi!!? Au kuna kitu chochote wakumbuka Huko Nyuma!! Yaani ulikuwa ukiishi wapi na kwanini upo Hapa."

Binti Alitikisa kichwa Ishara ya kwamba hakumbuki chochote, isipokuwa anachokumbuka Ni jina lake TU.

Doctor alitoka nje kupiga simu kwa Baba Ndalu kumpatia information mpya, majibu yalitoka kwa Baba Ndalu.
"Okay!! Hakikisha asiwe anakutania!! Kama hakumbuki Basi iwe kweli!!"

Majira ya usiku Tinnah alikuwa kapumnzika lakini alianza kupata njonzi za kutisha zilimpelekea kichwa kuuma Sana baadae alianza kulia mpaka kukawafanya wale wagonjwa wengine washituke na kubaki wakimuangalia jinsi anavyoweweseka usingizini.

Mgonjwa mmoja alionekana kuwa na unafuu ilibidi ashuke kwenda kumuita Doctor wa zamu baadae Alikuja Kumuona.
"Vipi Tinnah!! Cha mno Nini!!?

Tinnah alibaki akishikilia kichwa chake Huku akizidi kuugulia maumivu. Doctor alibaki Akimtizama kwa hali aliyokuwa nayo Aliondoka Huku akiongea pekee.
"Hii serious case!!"

Alichukua file la mgonjwa Nakuanza kulipitia angalau ajue chanzo Cha ugonjwa kwanza. "Mgonjwa anaitwa Tinnah!! Alifanyiwa upasuaji.. inaonekana alipigwa kichwani na kitu kizito kilichosababisha damu kuganda kichwani ikabidi afanyiwe upasuaji... Mchana alifanyiwa checkup inaonekana hana uwezo wa kuzungumza ila anaweza kuandika na hii imesababishwa na shida ya upasuaji uliofanyika ikampelekea kushidwa kuzungumza.... Uwezo wake wa kuzungumza utakuwa unarudi taratibu endapo ataweza kukumbuka Kumbukumbu za Nyuma!!!"

Doctor baada ya kumaliza kusoma file la mgonjwa tayari alikuwa amepata majibu. "Inaonekana tatizo linalomsumbua Ni Kumbukumbu zinazokuja na kupotea Ndio zinamfanya apate maumivu makali." Alichukua Dawa ya maumivu na kwenda kumchoma baadae alitulia.

Ilikuwa Ni majira ya Asubuhi Huku Nyumbani kwa Mama Ndalu, alikuwa ameamka Huku akifanya usafi wa nguo, baadae mumewe alipita akitoka ndani kuelekea Nje, Mama Ndalu ilibidi asitishe kufua kwanza nakubaki akimwangalia mumewe, baadae alimuuliza.

"Lakini Baba Ndalu!! Maisha haya tutaishi mpaka lini!!? Tazama tuna kila kitu ila Nyumba yetu haina furaha!! Muda wote twaishi Mimi na Wewe kwenye jengo kubwa namna hii!! Hakuna hata mtu wakuongea nae nikuombe basi niletee hata mdada wa kazi angalau niwe naishi nae!! Au kachukue Basi mtoto kwenye kituo Cha kulelea Watoto yatima angalau azibe pengo la Ndalu."

Mumewe aliishia kumtizama baadae Alimjibu Huku akiondoka.
"Una uhakika utapata furaha ukipata mtu wa kuishi nae!? Okay nitalifikiria." Kisha alipanda gari na kuondoka.

   ******

Yapata wiki mbili kupita leo Tinnah alikuwa akihamishwa hospital na kupelekwa kwenye Nyumba iliyokuwa mbali kidogo na mji, Wakati maandalizi yakiendelea kulionekana kuna mtu mmoja alikuwa akifatilia kila hatua iliyokuwa ikiendelea pale, muda wote alikuwa na laptop yake ilimsaidia kunote kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Baadae Utaratibu mzima ulikamilika wa Tinnah kuondolewa pale, ilikuwa Ni majira ya Usiku Ndio ratiba ilipagwa ifanyike vile.

Yule mtu alizidi kufatilia mpaka akajua majira ya kuondoka pale!! Aliamua kufatilia utaratibu wa usafiri watakaotumia aliona Kuna gari ilikuwa imepakiwa Nje!! Alifanya utaratibu wa kutafuta ufunguo Kuna kazi alitaka aifanye.

Aliangaza Huku na kule baadae Aliona gari hiyo imeegeshwa vibaya!! Alitafuta Mlinzi mmoja aliyekuwa akilinda pale!! Alipiga stori nae baadae alimwomba apumzike kwanza kwa kudai ana mgonjwa pale muda mrefu wamekuwa wakifukuzwa na kulala Nje hivyo muda huo Kama atautumia kupumzika itakuwa Ni vizuri.

Mlinzi alimuamini Sana ilibidi amkabizi funguo baadae yeye aliendelea kuzunguka zunguka akiimarisha Ulinzi. Kijana Yule baada ya kuingia Ndani alichukua sare za walinzi zilizokuwa humo Kisha alivaa na kutoka Nje. Alichoamua Ni kumfata moja kwa moja Doctor aliyekuwa akihusika kumhudumia Tinnah.

"Doctor kwema Lakini!!!! Naona Gari yako umepaki vibaya!! Waweza irekebisha ukaipaki vizuri!!!?"

Muda huo Doctor alikuwa Busy Sana!! Ilibidi ampatie funguo ya Gari huku akimuelekeza aipaki vizuri.

Kijana Yule alichukua funguo Kisha Alielekea kwenye gari, Alichofanya Ni kufungua nakuingia kwenye gari Kisha alitegesha Camera vizuri, sehemu iliyokuwa imejificha kwa kutizama haraka huwezi kuiona!! Alimaliza kufunga Camera Kisha alipaki gari vizuri na kurudisha ufunguo.

Baadae Alibadilisha mavazi na kuvaa nguo zake huku akiwa amebeba begi lake mgongoni, ile anatoka nje alikutana na mabinti wawili walipishana nao Huku Akiwa busy na Mambo yake.

Mabinti wale walibaki wakimtizama mpaka anaishilia, baadae walianza kumujadili.
"Huyu Mkaka inaonekana Ni mgeni hapa naona hii itakuwa ni siku ya tatu Kumuona!! Ila naona yupo busy Kweli na laptop yake!!! Ila anajifanya yupo serious Sana!! Mpaka anachukiza japo Ni HB Kweli!!"

"Umeanza mambo yako Rose ya kuchunguza chunguza kila wakaka wageni wanaokuja!! Halafu kwani yupo word namba Ngapi au Ni Daktari bigwa yupo kwenye jengo lao!!?"

"Sijui Bhana!!! Kesho tutamfatilia angalau tumjue Zaidi."

   .... Itaendeleaa....

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post