TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

BINTI MSAHAULIFU 02

SIMULIZI: BINTI MSAHAULIFU.                                                   SEHEMU: 02
ILIPOISHIA....... 

"Umeanza mambo yako Rose ya kuchunguza chunguza kila wakaka wageni wanaokuja!! Halafu kwani yupo word namba Ngapi au Ni Daktari bingwa yupo kwenye jengo lao!!?"

"Sijui Bhana!!! Kesho tutamfatilia angalau tumjue Zaidi."

ENDELEA NAYO...... 

Huku kwa Tinnah alifikishwa kwenye jumba kubwa lililokuwa limezungushiwa fence kubwa pia kulikuwa na Ulinzi mkubwa!! 

Baadae Doctor Alikuwa akimuelekeza mazingira ya pale, Mara kidogo walitokea watoto watatu wenye umri wa miaka saba, walikuja pale kumsalimia Tinnah. Mtoto mmoja alimuita Doctor.
"Doctor!! Na huyu ndie Dada yetu ulikuwa unamsema atakuja!!?"

"Yaaah!! Ndio Dada yenu ambae mtakuwa mkiishi nae kwa sasa!!"

"Mbona haongei Sasa!!?""

"Anaumwa ila ataongea TU!!"

"Ila atakuwa Ni Dada mzuri!!"

Doctor alisogea karibu kisha alimshika kichwani Tinnah huku akiongea nae.
"Naamini utakuwa sawa hii ni familia yako kwasasa nimekukabizi jisikie uko huru muda wote!!"

Tinnah aliitikia kwa ishara ya kichwa, baadae Doctor alimpatia kaunta mbili na kalamu kisha alimkabizi huku akimuomba Kama atakuwa na shida yoyote ile anaweza kuandika nakuwapatia wanzake.

Baadae aliwaita watoto waliokuwa pale, muda huo  Tinnah aliitwa na yeye ili aweze kuungana nao alibaki akisikiliza maelezo yaliyotolewa pale make alikuwa akisikiliza.

Baadae Tinnah aliamua kuondoka pale na kwenda kwenye bustani iliyokuwa sehemu hiyo, alikaa huku akitizama mazingira yale moyoni alikuwa na Mambo mengi sana akijiuliza.
"Mbona kama sikumbuki kitu!! Hawa watoto ni wa Nani!?"

Muda kidogo alikuja Binti mmoja mwenye umri sawa na wake, muda huo alikuwa amepatiwa information zote kuhusu Tinnah, alifika na kumuuliza Tinnah huku akimpatia kibegi kilichokuwa na kaunta pamoja na kalamu.
"Waweza tumia begi pamoja na vitu vilivyomo ili kurahisisha mawasiliano."

Tinnah alifungua Begi kisha alichukua kalamu na kumuandikia kwenye karatasi maandishi yaliyosomeka hivi.
"Kwanini mnafanya haya kwangu!!? Kuna umuhimu wa Mimi kuandika!!?"

"Nafanya kwaajili yako!! Naona umpweke kweli natamani tushare furaha kwa pamoja!! Niite Naomi kwanzaa!!" Halafu Wewe Ndio Tinnah!!?"

"Sawaa!! Una kitu wataka tuzungumze na Mimi?" Tinnah alimjibu kwa kuandika maana alikuwa akisikiliza vizuri maongezi ya Naomi!!

"Natamani kuzungumza mambo mengi sana kuhusu Wewe!! Ila nikubalie kwanza umekubali niwe rafiki yako wa karibu!!?"

"Nimekubali.."

Naomi alimchukua Tinnah huku akiendelea kumzungusha mazingira ya pale. Baadae alistushwa na wale watoto wawili walikuja huku wakikimbizana.
"Dada!!! Dada!!!' Dada yule mwingine anaumwa ndanii!!"

Ilibidi watoke haraka kwenda kumuona ndani!! Kwavile lile jengo lilikuwa kubwa basi walitumia kama robo saa kufika kwenye kile chumba, kipindi wamefikia kile chumba Naomi alimgeukia Tinnah kisha alimwambia  amsubirie nje kwanza, baadae wale watoto waliondoka na wao huku wakiongozana na Tinnah.

Naomi aliingia kwenye kile chumba kilionekana kuwa na giza sana, alichukua torch huku akimurika ili apate nuru. Alifika hadi kitandani na kukaa huku akimtizama vizuri baadae alimuita.
"Ndalu!!! Unaumwa Nini tena!!! Nimeambiwa unalia!!?"

Ndalu aliinuka kisha alimshika mkono Naomi Huku akimuuliza.
"Ni lini nitatoka kwenye chumba hiki!! Nifungulie leo nitoke Hapa!! Tazama imekuwa ni miaka nane nipo hapa ni lini nitatoka!!?"

Naomi alimshika mkono huku akijaribu kumtia Moyo.
"Kwasasa muda wote utakuwa huru!! Naona kuna Binti kaja!! Ila nahisi kuna kitu ndani yake japo kwasasa simuelewi vizuri!!""

"Kwani ana nini anacho huyo Binti umeona!! Anaweza kunisaidia Mimi!!?"

"Sijajua vizuri ila yeye ni Binti msahaulifu!! Hakumbuki chochote na hawezi kuzungumza kwa njia ya mdomo ila anaelewa kila kitu utakachomuuliza lakini anajibu kwa kuandika."

"Sawaa!! Mfatilie vizuri utakuwa unaniambia!! Tatizo muda mwingi hauji kuniona kwa wakati!! Ndio maana nimewatumia wale watoto baada ya kuona wanapitapita huku!! Walisogea Hadi mlangoni wakawa wameniuliza wewe ni nani nikawaambia Dada!!" Nikawaomba waje kukwambia kuwa naumwa!!;"

"Sasa umeanza kuzingua huoni hawa watoto watamwambia Doctor kuwa wamekuona huku!! Kipi tunaenda kukifanya kwa Sasa!!?"

"Kawaonye wale watoto wasije kusema!! Watishie vikali sana naamini hawawezi kusema!!!"

Naomi alitoka kwenye Chumba kile kisha alielekea kwa wale watoto aliwakuta wapo wakila. Alitazama kwa pembeni alimuona Tinnah kasimama huku akiwa na Daftari lake kuna Picha alikuwa akichora.

Naomi alimsogelea Tinnah kisha alibaki akimtazama, ni kitu gani anakifanya baadae alichukua Daftari na kulisogeza karibu huku akizidi kuitazama picha baadae alimuuliza.
"Hii picha ni ya Nani umechora!??"

Tinnah alibakia kutabasamu tu, huku akimtizama Naomi baadae aliamua kumjibu kwa kuandika.
"Ndicho ninachokumbuka kwa Sasa!! Ila simkumbuki vizuri naona ni mtu aliyekuwa upande wangu muda mwingi!!"

"Ni Kaka yako!?" Mara ya mwisho ulimuona wapi!?"

"Hospitali!! Kuna Siku moja nilimuona kaja kuniona!! Ndio kumbukumbu zangu ninavyoziona!!"

"Sawaa!! Basi endelea kukumbuka Vizuri!! Ila njoo kwanza tupate chakula!!"

Tinnah aliwahi kumshika mkono Naomi baadae alimuandikia kikaratasi Kisha alimpatia, Naomi alikichukua Kisha alikisoma.
"Kwenye kile Chumba!! Ni Nani aliyekuwa mle akihitaji msaada wako!!?"

Naomi alishituka kidogo, aliamua kumjibu.
"Usijali siku nyingine nitakueleza, ila sio wakati huu."

"Wakati gani utanieleza.. kwanini isiwe Sasa!!!??"

Naomi alifanya kumkaushia kisha alimshika mkono na kwenda nae sitting room. Waliendelea kupata chakula lakini Tinnah alikuwa bado ni mtu mwenye mawazo sana alichukua karatasi tena kisha alimwandikia Naomi.
"Njia gani naweza itumia ili kumbukumbu zangu zikarudi tena kama awali!!?"

"Ruhusu ufahamu wako uwe wazi kila ukijaribu kukumbuka achilia fikra zako zote ziwe hewani!!"

°°°°°°°°°°°°°°°°

Majira ya usiku Tinnah alikuwa kasinzia huku akikumbuka maneno ya Naomi yakijirudia mara mbilimbili, ruhusu ufahamu wako wa akili uwe wazi!! Alijaribu kuvuta Kumbukumbu huku akifunga macho kama ataweza kumbuka lakini aliona giza lenye nyota nyota zikiwaka kwa kubadilika kila aina ya rangi, baadae alifungua macho na kubaki akicheka mwenyewe "hapa nafanya ujinga juu ya ujinga, Anyway Sitaki tena kukumbuka."

Huku nje kidogo na mji ule, katika Chumba kimoja alionekana kuna kijana alizidi kuchezea computer yake huku akizidi kuangalia location na ile Camera, baadae Alizima Computer nakubaki akizunguka huku na kule kana kwamba kuna kitu ameshidwa kukikamilisha.

Aliwasha tena Computer huku akizidi kuchezea computer yake lakini alibaki akiongea pekee.
"Lazima nitafanya kwaajili yako ili uwe salama!!"

Muda kidogo alikuja kijana mmoja aliingia ndani kisha alimuuliza jamaa yake.
"Ni kweli Aniseth.. umekosa mwanya wakumsaidia Tinnah!!?"

"Nahisi wametushtukia, ile Camera niliyotegesha kwenye gari!! Naona hainasi tena matukio!! Nahisi itakuwa imetolewa!!"

"Sasa tunafanyaje!! Ila nakuamini wewe kwenye maswala ya Network upo vizuri!! Kama utashidwa wewe tayari Tinnah utampoteza..!! Au tusitishe Jambo hili."

"Acha utani Leonard!!! Mambo ya serious usichukulie utani!!! Kumpata kwetu Tinnah mambo yetu yatafanikiwa!! Hapa kesho naomba twende moja kwa moja tukafatilie tukiwa huko..."

"Hebu sogea kidogo kwenye computer, hivi unaona Ulinzi uliopo hapa, walinzi wapo wakutosha unataka tukafie huko?"

"Haaaaa!!! Ama kweli hapa inatakiwa akili ifanye kazi, muda wote tucheze na mtandao vizuri tujue tunamsaidiaje Tinnah!!"

Siku iliyofuata Aniseth na Leonard walikuwa wakielekea kwenye Jengo alilokuwa Tinnah, uchunguzi uliendelea kufanyika muda kidogo waliona gari ikipaki pale, alionekana ni Baba Ndalu pamoja na Doctor wakishuka.

Aniseth aliamua kutafuta upenyo baada ya kuona walinzi wakizubaa aliingia taratibu akijificha kwenye gari, baadae alifanikiwa kuingia kwenye jumba hilo kazi aliyoifanya nikuzima camera zote ili zisimurike, kisha alichukua simu yake nakumpigia Leonard huku akimpatia information ya mambo yote alimsihi awashe Computer yake kisha aliunganisha mawasiliano yote yatakayoendelea pale.

Alitafuta sehemu nakukaa huku akizidi kuchunguza vizuri, baadae Alimuona Tinnah akiwa anapita sehemu yake, aliamua kumnyatia taratibu kisha alimvuta na kumziba mdomo huku akibaki kumtizama baadae alimuuliza.
 "Unanikumbuka!!!?"

Tinnah alibakia akimtizama TU, ishara ya kuwa hamkumbuki, Aniseth Alirudia Tena kumuuliza.
 'Tinnah!! Unanikumbuka?? Mbona huongei!!!!?"

Ilibidi Tinnah Amuandikie Chini. "Sikukumbuki kwani wewe Nani!!?"

Aniseth alisoma maandishi yale kisha alimtizama Tinnah usoni, kisha alinyanyua mkono wake na kumshika Tinnah lip's za mdomo huku akiwa haamini kwanza alimuuliza.
'Ni kweli huwezi kuzungumza tenaa!?"

Tinnah aliitikia kwa ishara ya kichwa kuwa hawezi zungumza.

Aniseth ilibidi amuachie kisha alimruhusu aende ila alimsihi asimwambie mtu yeyote kama kamuona mtu ila alimsihi kumsaidia. 

Baadae Aniseth alizidi kupandisha juu huku akiwa bado anawaza mambo mengi Sana.
"Tinnah... Hivi ni kweli haongei tenaaa!!? Nini kimemkuta Binti huyu!!?"

Kutokana na Stress za hapa na pale aliparamia ua lilokuwa limetengenezwa kwa Shaba likawa limeanguka chini na kupasuka, kelele ziliwashtua walinzi wakawa wamekimbia moja kwa moja kuangalia kitu gani kimeanguka. Mlinzi mmoja alitoa Sauti akisema huyo huyo mkamateni, juku wakizidi kumuandama Aniseth kwenye jumba Hilo.

Aniseth Alizidi kukimbia huku akijaribu kutetea maisha yake, bahati nzuri kuna mtu alitokea chap akawa amemvuta na kumuingiza Chumbani.

Walinzi walizidi kumtafuta lakini hawakufanikiwa baadae walirudisha majibu kwa Doctor kuwa wamemkosa!! Aliwaamuru watumie Camera kumpata lakini walipotizama waligundua Camera zilikuwa hazinasi matukio muda ule ilibidi wakae chini wakijadili kwa kina.

Upande wa Doctor alikuwa amekaa na Baba Ndalu ilibidi kila mtu afikirie kwa makini ilikuwaje mtu aweze kuingia na kuzima Camera itakuwa ni mtu mwenye uwezo sana wa kutumia Mtandao lakini Baba Ndalu alitoa hoja.
"Inaonekana mtu huyu anatufahamu vizuri huenda kila kitu kilichokuwa kikiendelea hapo nyuma anafahamu!! Ila sijajua kwanini alikuwa anafanya hivi kipi anachohitaji kwetu!!!"

"Ooh!! Umewaza vizuri sana hapa inabididi tuanze kufatilia pindi Tinnah akiwa hospital wording,' ngoja nimcheki Doctor Isaac atuangalizie kwenye Camera.

Doctor alipiga simu kwa Doctor Isaac kisha alimpa maelekezo baadae aliingia kwenye Computer huku akifatilia location ya Chumba kimoja ndipo wanagundua. 

Baada ya siku tatu Tinnah kufikishwa hospital kuna mtu aliingia akiwa amefunika uso wake na muda huo aliingia kama Doctor huku akiwa amevaa sare ya kidokta, mtu huyu alionekana kuingia huku akijaribu kukwepa Camera japo Camera ilifanikiwa kumnasa, alifika Kitandani kwa Tinnah nakuchukua dawa fulani akawa amepaka mikono ili kuondoa ushahidi.

Kisha alimshika usoni Tinnah lakini alionekana Ni mtu mwenye huzuni sana baada ya kumuona Tinnah kafugwa Bandage kichwa kizima baadae aliondoka.

Baba Ndalu alimkatisha kwa kumuuliza.
"Ngoja kwanza nikuulize"!! Muda huo kaenda kumtizama Tinnah, Je Alikuwa akijitambua!! Au hakuweza Kumuona yeye huyo mtu!!?".

"Ngoja nivute sura yake kwanza!! Inaonekana Tinnah alikuwa amelala na muda huo hakuwa na fahamu kwahiyo hakumfahamu!!!"

"Sawaa!! Ahsante kwa Ushirikiano Doctor!!"

Baadae walibaki tena wamekaa wakijadili. Inawezekana mtu huyu Ni mtu wa karibu sana na Tinnah!! Hapa inabidi tumuulize yeye mwenyewe atupatie majibu.

           .... Itaendelea....
Usikose Sehemu ya 03.

Nini kipo Nyuma ya pazia. Kwanini Tinnah anafatiliwa sana, na kwanini wanamuwekea ulinzi mkubwa, na vipi kuhusu Ndalu kipi kinaendelea kati yake na Baba yake!!? Aniseth nae amevutwa na nani huko chumbani? 
Masuala ni mengi ila tuendelee kuwa pamoja kwenye simulizi yetu ya Binti Msahaulifu (Tinnah)

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post