SIMULIZI: BINTI MSAHAULIFU. SEHEMU: 03
ILIPOISHIA.......
"Sawaa!! Ahsante kwa Ushirikiano Doctor!!"
Baadae walibaki tena wamekaa wakijadili. Inawezekana mtu huyu Ni mtu wa karibu sana na Tinnah!! Hapa inabidi tumuulize yeye mwenyewe atupatie majibu.
ENDELEA NAYO.......
Muda kidogo alifika Naomi huku akiwa amebeba vinywaji, aliweka mezani huku akitaka kuondoka lakini Doctor alimuuliza.
"Vipi!! Hakuna kitu chochote kilichotokea kwa Tinnah!!?"
"Aaa!! Labda kuna Picha alikuwa akiichora!! Naona ndio kitu kipya!!!"
"Waweza ifata...!!?"
Naomi aliileta ile picha kisha alimpatia.
Walianza kuifanyia kazi. " Inaonekana ni picha ya kijana wa kiume!! Inaonekana Ni kijana ambae atakuwa chini ya miaka thelathini!! Inaonekana kuwa Ndio mtu ambae ni wa karibu na Tinnah na mtu huyu huyu alikuja pale hospital!! Na kama amekuja hapa inaonekana kaja kumchukua Tinnah!! Na kijana huyu sizani kama atakuwa ametoka kwenye Jumba hili nahisi atakuwa amebana sehemu!! Na hapa lazima tutampata tu kikubwa ulinzi uimarike getini maana hamna njia nyingine atakayotumia kutokea, akiruka fence lazima atapigwa short ya umeme hapa tukasisitize ulinzi tu.
Walimaliza majadiliano Yao wakawa wameondoka.
Huku kwa Aniseth alikuwa kwenye Chumba cha giza kilichokuwa kikimpatia hofu sana lakini kila akimtizama mtu aliyemsaidia hakumuona vizuri!! Ilibidi ammurike kwa kutumia simu yake. Baadae aligundua kuwa Ni Binti aliyemsaidia ilibidi amuulize.
"Wewe ni Nani!!? Kwanini unakaa kwenye Chumba kilicho na Giza muda wote? Na kwanini Wewe hapo umenisaidia mimi!!?"
"Una maswali mengi!!! Najua umekuja kumsaidia yule Binti msahaulifu, naomba kabla hujamsaidia yule Binti!! Nisaidie kwanza Mimi!! Huyo Binti utamsaidia baadae!!" Ndio maana Mimi nimekusaidia Wewe kwanza kabla hujamsaidia yule Binti!! Kwahiyo fanya kunitoa hapa angalau univushe pale getini nipite kisha uniache na mimi nitajua pa kwenda!!"
Aniseth alibaki akimtizama Binti huyo, Kisha aliamua kumjibu.
"Ni sawa!! Umefanya vizuri kunisaidia ila kwasasa sijui kwanini upo hapa!! Sijui ulipatwa na Nini katika maisha yako!! Ila utanisamehe siwezi kukusaidia kwasasa labda mpaka nitoke hapa nikafanye upelelezi ndio nitarudi kukusaidia Wewe!!! Naomba unikutanishe na Tinnah kwanza nimchukue ila nitarudi kulipa fadhila kwa kile ulichonitendea!!!"
"Ndio wamaanisha Kweli huwezi nisaidia!! Ila kama utafanikiwa kurudi naomba usisahau kurudi kwaajili yangu!! Ila kwa Majina yangu naitwa 'Ndalu' hata ukienda nenda ukifanya Upelelezi kuhusu Ndalu!!"
"Sawa Nakuahidi!! Nitafanya hivyo!!!" Njia gani nitapita maana jengo hili Ni kubwa!!"
"Subiri kwanza!! Leo usiku naimani Binti msahaulifu atakuja kupeleleza kuhusu Chumba hiki naona anamashaka na hiki Chumba basi akifika ndio utaongozana nae!! Ila najua kwasasa kutakuwa kumuwekwa usalama wa kutosha kwahiyo kuwa makini!!"
Mnamo majira ya usiku kama walivyotabili Tinnah alikuwa Chumbani kwake muda huo alikuwa kashikilia touch huku akifikiria cha kufanya.
"Lazima niende kwenye kile Chumba nikajue kipi kinaendelea!"
Alisimama Nakuanza kutembea Mdogo Mdogo Hadi kwenye mlango, alisogea na kusikilizia lakini kulikuwa kimya maana muda huo walikuwa tayari wamesikia vishindo, ikabidi wakae kimya kusikilizia.
Tinnah alikuwa akifikiria kitu gani atumie kuingia kwenye Chumba jicho lakini akili ilimtuma atumie sauti ya Naomi ili aingie kwenye Chumba hicho ndipo anagundua Tena hawezi kuongea. Alishtushwa na sauti ya Naomi akimuita na muda huo alikuwa kafika pale.
"Tinnah!! Kipi unakifanya hapa!! Naomba tuondoke Haraka!" Alimchukua na kuondoka nae.
Huku kwa Aniseth Alibaki akimtizama Ndalu baadae alimuuliza.
"Kipi tunaenda kukifanya!!?' Nani aliyemchukua Tinnah tenaa!!?"
"Kaa kimya!! Muda huu atarudi, na akirudi naomba ukakae kwenye koridoo hakikisha asistukie kama uko Hapa!! Mimi nitakueleza jadi kwenye Chumba Cha Tinnah ukamsaidie!!"
Muda huo huo Naomi aliingia kisha alikaa kitandani ili aongee na Ndalu.
"Huyu Binti msahaulifu sijui anafanya Upelelezi ganii!! Nimemkuta yupo mlangoni anataka kuingia Huku!! Halafu kuna kijana kaingia hapa na yupo kwenye jengo hili inaonekana kaja kumtafuta huyu Binti.""
"Hawezi kukamatwa Kweli!!? Maana Baba si mtu wa mchezo mchezo!!"
"Daaah!! Namuonea Huruma!! Akikamatwa hapa sizani kama atatoka salama!! Na inaonekana bado yupo ndani ya Jengo hili!!"
"Kwahiyo akipatikana itakuwaje!!?"
"Hata akitaka kuondoka itakuwa hatari maana kila sehemu Camera zimetegeshwa ili kumpata mtu huyu!! Kwa umakini alioutumia labda ajaribu tena!!"
"Kwahiyo Vipi Tinnah!! Tunamsaidiaje kwasasa!! Upo radhi kumuacha aondoke na mtu huyo!!?"
"Hapana!! Tinnah nimewaza Kuna namna nataka tumtumie katika jengo hili hivyo bora azidi kubakia kwanza!! Mpaka kufikia atoke hapa!! Kuna vitu atakuwa ametutengenezea'' Wao wamtumie na sisi tutamtumia kivyovyote vile!!"
"Utanishirikisha sasa!! Kila hatua Lakini Ni kheri!!?"
"Kikubwa usalama wa maisha yako!! Wewe ukitoka salama!! Tinnah atakuwa na faida gani kwako? Okay uwe na usiku mwemaaa!!"
Naomi aliondoka huku akimuacha Ndalu akifikiria maneno yake lakini asielewe Ni mbinu gani anataka kuitumia. Upande wa Aniseth na yeye alisikia yote ilibidi asogee nakumkaba Ndalu.
"Kumbe nyie Ni wauaji!!? Ni kitu gani mnaplan mwataka kumuangamiza Binti wa Watu!! Nasema niache nikamsaidie Tinnah kwasasa!!"
Aniseth alitoka pale nakuanza kutafuta Chumba ambacho atakuwepo Tinnah, Ila aliamua kutembea kwa Tahadhari ili Camera zisimnase aliamua kutafuta Setting nzima ilipo Huku akizidi kufatilia Nyaya zote zinapoelekea baadae zilimfikisha kwenye Chumba kimoja aliona Ni Mlango uliokuwa umefungwa kwa kufuli ilibidi atafute namna yoyote ili aweze kufungua mlango huo!!
Bahati nzuri alibahatika kupata Chuma baadae alirudi kuvunja kufuli akawa ameingia Ndanii, alikuta kuna Aina ya kila mitambo ilibidi atazame switch ya kuzima Camera kwanza!! Baadae Alizima na kuchukua mkanda uliokuwa ukinasa matukio Hadi Nje!! Kisha alichukua simu yake na kumpigia Leonard ili amshirikishe mipango iliyoendelea wakawa wamekubaliana kuwa atamsubiri nje na usafiri ili akitoka tu Safari ianze. Baada ya hapo aliamua kutoka kwenye Chumba hicho huku akitafuta Chumba Cha Tinnah.
Kwa bahati nzuri alimuona Tinnah kakaa kwa nje huku akiwa na Daftari lake na kalamu, ilibidi asogee taratibu pasipo yeye kujua kisha alianza kumtizama kipi anaandika. Muda huo Tinnah alikuwa akichora ramani ya Jengo Zima huenda na yeye alikuwa na plan yakutoroka pale.
Lakini Aniseth alifikiria kitu, Kama ramani ya Jengo Zima Tinnah analo kwake atakuwa Ni msaada tosha wakutoka kwenye jengo hilo!! Aliweka plan endapo taa zitazima Walinzi wote watatoka getini Nakuja kutafuta chanzo Cha kuwa na Giza wao Ndio wataitumia njia hiyo kutoka.
Ilibidi amsogelee Tinnah kisha alimziba mdomo!! Baadae alimuachia na kumruhusu amtamtazame.
"Tinnah nishajua kitu unachoplan ila nataka tutoke hapa mapema ninachoomba ni saport yako maana hapa nitaenda kuzima taa zote!! Kwakuwa wewe ushakuwa mwenyeji hapa naamini utakuwa ukiongoza Njia!!
Tinnah aliitikia kwa ishara' kuwa yupo tayari!!
Aniseth alirudi hadi kwenye kile chumba kilichokuwa na Network kisha alifanya kuzima baadae alirudi hadi alipomucha Tinnah. Plan yake ilienda sawa walinzi wote walikimbilia ndani wakawa Wameacha geti wazi wakawa wamefanikiwa kutoka nje kiulaini.
Muda huo walimkuta Leonard akiwa mlangoni kawasubiri na usafiri wake ilibidi wapande na kuondoka sehemu hiyo.
Walifika hadi kwenye jengo lililokuwa pembezoni mwa mji kisha waliweka makazi yao lakini muda huo Tinnah alibaki kimya juku akiangaza mazingira ya hapa na pale huku wakiwa wamekaa Sebuleni, baadae alimgeukia Aniseth kisha alimwandikia kikaratasi.
"Wewe ndio Aniseth!!?"
"Ndio!!! Umenikumbuka!!?"
Alitikisa kichwa ishara hamkumbuki, baadae alimuandikia tena. "Si ulikuwa kwenye lile jumba la kina Naomi!!?"
"Ndio!! Hujakosea!!!"
Baadae walimuandalia sehemu ya kulala, kisha walibakia Sebuleni wao kama wao wakijadili.
"Inamaana kwamba kweli Tinnah hakumbuki!!?' Kipi tunaenda kukifanya kwasasa ilimradi Kumbukumbu zake zikarudi tena!!?" Aniseth alihoji.
"Daaah!! Labda tumrudishe kwao!!! Huenda atakumbuka!!" Halafu kwanini lakini Aniseth unafanya haya yote kwaajili ya Tinnah."
"Kwaajili ya Kaka yangu tu! Ndio maana nafanya hivi!! Haijalishi Kaka yangu alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha ila aliniambia nimlindie huyu mwanamke!!"
"Hivi unazani Tinnah!' fahamu zake zikimrudia huoni wewe itakuwa ngumu kumuelewesha!!"
"Nitamuelewesha!! Najua atanielewa TU."
Asubuhi kulipambazuka Tinnah aliamka Huku akisaidiana na wafanyakazi waliokuwa pale baadae alimuona Aniseth alikuwa akipita pita ilibidi amfuate. Aniseth na yeye alimgeukia Tinnah huku akimuuliza.
"Vipi unataka kuongea na Mimi?"
Aliitikia kwa ishara' ya kichwa.
"Sawaa lakini baadae nimalizie kazi moja nataka niifanye Kwanza!!"
Huku kwenye jumba la Doctor muda wote kulikuwa na msako wa hapa na pale kumtafuta Tinnah pamoja na Aniseth.
Upande wa hospital waliendelea kumtafuta Aniseth kwenye CCTV camera, baadae alifika Rose kwa Doctor aliyekuwa akishirikiana na Baba Ndalu.
"Samahani Dr. Najua wewe ndio umetoa time table ya kuingia zamu!! Kuna mkaka mmoja tulimuona ile siku nilikuwa mimi na Jamila kwa bahati mbaya aliangusha picha!! Maana nimemtafuta kweli nataka nimrudishie picha yake sijui yupo word namba ngapi!!?''
Doctor aliichukua ile picha kisha aliiangalia lakini aliona ni picha ya muda kidogo, wapo watu watatu yaani Tinnah na kaka wawili waliofanana sana!! Baadae aliiweka ile picha kisha alimuuliza Rose.
"Kijana huyo yukoje kwanii!!?"
"Ni mrefu mwembamba!! Alikuwa kavaa gwanda jeupe la udokta, mkononi alishikilia laptop, sura yake aliificha kwa proova nyeusi pia alivaa miwani.
"Sawaa waweza iacha ataikuta Ofsini!!"
Rose aliondoka pale huku akimuacha Doctor kwenye tafakuri nzito sana. Alinyanyua simu yake akawa amempigia simu Baba Ndalu kumpatia information alizozipata kwa Rose!! Baada ya mawasiliano yao kuisha walipeana maelekezo sehemu ya kukutana wazungumze.
Huku kwa Tinnah jioni alitoka na Aniseth angalau wazungumze. Walikaa sehemu kisha waliagiza juisi Huku stori ziliiendelea. Muda huo Tinnah alikuwa kaandaa daftari lake huku akihitaji kujua vitu vingi kwa Aniseth.
Aniseth muda huo alikuwa na maswali mengi ya kujiuliza kila akizidi mtizama Tinnah' inaonekana kuna mambo mengi sana alikuwa kamficha baadae alimuuliza.
"Vipi Tinnah!! Kuna kitu unataka kuniuliza maana naona upo serious Sana!! Okay uliza!!?"
Tinnah Alichukua kalamu yake na daftari lake kisha alimwandikia.
"Wewe ndio Albert au ndie Aniseth!!?"
Aniseth Alishtuka kwanza kisha alichukua juice na kumimina kwenye glass kisha alikunywa, muda wote Tinnah alikuwa akimtizama alichana karatasi ndogo kisha alimpatia tena Aniseth juku akiwa ameandika. "Wewe ndie Albert!!?"
Aniseth ilibidi akae vizuri kisha alimtizama Tinnah uso kwa uso kisha alimjibu.
"Kumbukumbu zako zimerejea!!?"
"Sikumbuki hataa!! Ila kwenye ufahamu wangu nakuwa naona sura yako ipo mara mbili mbili halafu kuna jina jingine linakuja Albert!! Nilitaka unifafanulie vizuri Aniseth na Albert Ndio kina Nani!!?" Alimaliza kuandika kisha alimpatia.
"Hapana huenda kuna kumbukumbu zinakujia ila Albert Ndio Aniseth!!" Naona kwasasa unawaza mbali sana.. endelea kukumbuka hivyo hivyo naimani muda si mrefu ufahamu wako utarudi!!"
"Nina Swali Tena."
"Niandikie...!!"
"Lini utaenda kumtoa Ndalu kwenye Jumba lile? Maisha yake yapo hatarini kwa Sasa!! Fanya kitu kumuondoa pale!!"
"Sawaa nakuahidi nitafanya hivyo!! Ila Na wewe niahidi siku tukipotezana hakikisha utarudi kuniulizia kwenye jumba hili maana kwasasa maisha yetu yapo hatarini sana!!"
"Sawaa muokoe kwanza Ndalu!!"
Maongezi yao yaliendelea baadae Aniseth alimrudisha Tinnah Nyumbani. Majira ya Jioni Aniseth na Leonard walichukua usafiri kurudi kwenye Jumba lile kwa lengo la kumkomboa Ndalu.
Wakati wamefika karibu na jengo hilo waliona kuna gari inatoka pale, Ilibidi waanze kuifatilia taratibu!! Iliwafikisha hadi kwenye jengo kubwa lilionekana kuna Ulinzi wa kutosha Ilibidi wakae sehemu Ili kutizama kitu kinachoendelea.
Walizidi kuangalia kwa makini Ghafla waliona kuna mtu alikuwa amebebwa huku kafunikwa nguo nyeupe, Mwishoni kabisa alionekana Naomi akishuka kwenye gari huku akilia, Sauti ya Mwisho iliyosikika Ni Ndalu umeniacha mapema mnooo!! Huku ikifatiwa na kilio kikubwa.
Mlinzi mmoja alikuja kumchukua Naomi huku akijaribu kumnyamazisha!! Kilio hicho kilipelekea hata Aniseth na Leonard washituke Sana!!
"Daaah!! Tayari Ndalu katangulia.... Maskini nitamwambia Nini Tinnah?"
Leonard alimshika mkono rafiki yake kisha alimuomba watoke sehemu hiyoo..
"Tuondoke hapa!! Tupo hatarini sana, tutaenda kuongea mbele ya Safari!!"
Aniseth alisimama kwa unyonge sana, walielekea kwenye gari huku kila mtu akiwa haamini kitu kilichotokea.
.... Itaendelea....
Like kama kawaida pamoja na comment za private ikiwa unazo.
Tags
simulizi