TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

FAHAMU SABABU AMBAZO HUATHIRI MAAMUZI TUYAFANYAYO MAISHANI MWETU.

FAHAMU SABABU AMBAZO HUATHIRI MAAMUZI TUYAFANYAYO MAISHANI MWETU...
________________________
Hivi unafahamu kwamba asilimia kubwa ya maamuzi yafanywayo karibu na kila binadamu huishia kumletea matokeo mabaya?

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika zimeonesha kwamba, kila binadamu hufanya maamuzi...

Na, hakuna ambaye hajawahi kufanya maamuzi kwani hata kutokuamua pia ni kuamua!

Niliposoma ripoti mbalimbali kuhusu tafiti zilizofanyika kuhusu matokeo yanayopatikana mara baada ya maamuzi kuchukuliwa nilipata sikitiko kubwa sana...

Killichonisikitisha zaidi kwenye ripoti za tafiti hizo, ni kile kilichooneshwa, kwani asilimia kubwa ya matokeo yanayopatikana mara baada ya maamuzi  kufanywa, huwa ni mabaya na mengine huenda kinyume kabisa na matarajio ya aliyechukua maamuzi hayo..

Kutokana na ukweli huo, ninawiwa kukufahamisha hivi, unatakiwa ufahamu kwamba kufanya maamuzi ni kitu kingine, na kupata matokeo kutokana na maamuzi utakayoyafanya ni kitu kingine...

Hata wewe hapo huenda ukawa umefanya maamuzi mbalimbali mara kwa mara maishani mwako, lakini hakuna matokeo ya maana uliyoyapata, hasa ukihusisha na maamuzi uliyoyafanya!

Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba, uhalisia wa leo yako umetokana na maamuzi yako ya jana. 

Vilevile uhalisia wa maisha yako ya kesho, utategemeana na maamuzi utakayofanya leo!

Hii inamaanisha kwamba, Unaweza ukatengeneza kesho nzuri kwa kufanya maamuzi sahihi Leo!

My friend unatakiwa kujua kwamba, kesho yako inatengenezwa na maamuzi yako!

Hii inamaanisha kwamba hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako mwenyewe, hivyo basi wewe kama mjenzi wa Kesho yako unashauriwa kufanya maamuzi sahihi leo ili kesho yako ije ikushukuru kwa kile ulichokiamua leo...

Hata hivyo, ili kufanya maamuzi sahihi, ni muhimu kujua sababu zifuatazo ambazo Huathiri Maamuzi Tuyafanyayo Maishani Mwetu...

Je ni sababu zipi Ambazo Huathiri Maamuzi Tuyafanyayo Katika Maisha Yetu? 

Usijalii, muda siyo mfupi unaenda kubadili maisha yako, mara baada ya kuzjiua sababu hizo....

Zifuatazo ni sababu hizo:
___________________________

1. Kutokumshirikisha Mungu Wakati Wa Kuamua Kwetu!

Hivi unafahamu kwamba Mungu ndiye aujuaye mwanzo wako na mwisho wako?

Kwanza kabisa sote tumeumbwa na Mungu, kwa mantiki hiyo Mungu wetu anatujua sisi kuliko hata sisi wenyewe tunavyojijua!

Hivyo basi, ikiwa Mwenyezi Mungu ndiye aujuaye mwanzo wako na mwisho wako, unatakiwa kujua kwamba endapo utamuacha katika kufanya maamuzi ni rahisi kwenda kinyume na mipango yake aliyoiweka kwako!

Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba kuna sababu iliyomfanya Mungu aweze kukuumba!

Yaani kama vile mtu aliyetengeneza simu, alivyokuwa ana sababu ya kutengeneza kifaa hicho, vivyo hivyo hata Mungu alikuwa na sababu iliyomfanya akuumbe!

Unatakiwa kujua kwamba kuna kusudi lililomfanya Mungu akuumbe!

Na, endapo utafanya maamuzi bila kumshirikisha, unaweza ukaamua kinyume na kusudi lake ukaishia kuharibu na kujibebesha msalaba mkubwa sana!

Huenda ukawa tayari umeshaamua kuingia kwenye ndoa!
Huenda tayari ukawa umeshaamua kuingia kwenye mahusiano!
Huenda tayari ukawa umeshaamua kuingia kwenye biashara fulani!
Pamoja na maamuzi mengi ambayo huenda tayari umeshaamua!

Swali ninalotaka ujiulize ni hili, je katika kufanya hayo maamuzi umemshikirikisha Mungu?

Au unategemea kuongozwa kwa kutumia njia na akili zako zilizo na ukomo?

Mpenzi msomaji unatakiwa kufahamu kwamba, njia zake na mawazo yake Mungu siyo kama njia zako na mawazo yako. 

Kwani, njia zake ni za juu!  Hii inamaanisha kwamba ukimshirikisha Mungu katika maamuzi yako utabaki kuwa juu mawinguni, na utafanikiwa Kwa kila jambo utakalolipanga na kuliamua!

Kumbuka ukimshikisha Mungu yeye ni BWANA wa haki, atakuongoza, atakufundisha ili uweze kupata faida! 
Kwani Yeye ndiye BWANA Mungu akufundishaye, akuongozaye ili upate faida!

Nimalize kwa kusema kwamba, iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti!

Kama ulishafanya uamuzi ukamsahau Mungu, nipo hapa kukusihi urudi kwenye chanzo chako! Katu usisahau ulikotoka!
Kumbuka hata mtu ambao haujui chanzo chake utakauka muda wowote ule!

2. Mazingira Yanayotuzunguka...
Hakuna maamuzi ambayo utafanya yatakayoenda mbali zaidi ya mazingira uliyopo!
Hii inamaanisha kwamba mazingira yanayokuzunguka yatakupa ukomo fulani kwenye maamuzi utakayoyafanya!
 
Unatakiwa kujua kwamba mazingira ni nguvu isiyoonekana ambayo humtawala binadamu kifikra, kimawazo, kitabia, kimienendo pamoja na kimtizamo!

Jaribu kufikiri umezungukwa na mazingira yaliyojaa uhaba na ukomo je utapata wapi msukumo wa kufanya maamuzi ya kupambana na umaskini?

Au jaribu kufikiri umezungukwa na mazingira ambayo hayana support kwenye ndoto Yako, je utapata wapi hamasa ya kuamua ili utimize ndoto Yako? 

Mwanadamu hujiwekea Ukomo kutegemeana na mazingira aliyopo! 
Je linapokuja suala la kuamua mazingira yamekuathiri kwa Kiasi gani?

Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba huwezi ukachagua sehemu ya Kuzaliwa, hayo mazingira uliyokutana nayo huenda hukupanga ukutane nayo. Ila umekutana nayo kwa sababu ulizaliwa hapo! 
Ninachokushauri ni kwamba usiwe mtumwa wa mazingira. Unatakiwa utoke kwa kwenda mazingira mengine yatakayokupa hamasa ya kufanya maamuzi!

3. Marafiki wanaokuzunguka!
Kisaikolojia inamaaminika kwamba akili yako inajua jinsi ya kuendana na wengine!
Kutokana na ukweli huo unatakiwa kujua kwamba marafiki ulionao wamechangia katika kukufanya ufanye maamuzi fulani!
Endapo utashinda na marafiki chanya utafanya maamuzi sahihi. 

Hata hivyo endapo utashinda na marafiki hasi utaishia kufanya maamuzi mabaya ambayo yatakuathiri!
Je ni nani unayeshinda naye kila siku?
Je ni nani anayekushawishi sana katika kuishi Kwako?
Usijidanganye mwenyewe, kumbuka huwezi ukashinda na watu hasi halafu ukafanya maamuzi sahihi!
Badili aina ya marafiki ili ufanye maamuzi sahihi!

4. Kujiona Bado Wadogo...

Mbali na ukweli kwamba, "kadri siku zinavyozidi kwenda mbele kila mtu anakua kuwa mtu mzima, na hakuna mtu anayekua kuelekea utotoni"

 Lakini nimeshangazwa sana pale ninapomkuta mtu akisema bado yu mdogo, na kujiona kama hastahili bado katika kufanya maamuzi. Ila ukimuangalia unamkuta tayari yupo nyuma ya muda...

Hivi unaposhindwa kufanya maamuzi kwa kudai bado u mdogo unataka kumaanisha utabaki kuwa mtoto maisha yako yote?

Nakumbuka marehemu Charles Kanumba katika moja ya filamu zake aliwahi kusema kwamba, mtu mzima ni mtoto aliyekua, ilihali mtoto ni mtu mzima anayekua!

Rafiki yangu uko nyuma ya wakati tayari! Nipo hapa kukusihi kwamba suala la kuamua ni juu yako na huwezi kubaki kuwa mdogo milele...

Unatakiwa kujua kwamba muda muafaka wa kufanya jambo fulani ukifika, lifanye acha kuweka kisingizio cha kudai kwamba bado u mdogo!

Kumbuka kisingizio huwa hakitekelezi jambo.

Vilevile katika kufanya maamuzi usiamue kwa kufuata akili za kitoto, kwani utu uzima siyo suala la umri, bali ni suala la majukumu unayopambana nayo!

5. Namna ulivyoseti fikra zako na Fahamu zako...

Kuna baadhi ya watu linapokuja suala la kufanya maamuzi huwa ni kama wamejizila vile!

Jaribu kufikiri mtu anafanya uamuzi, huku akisema liwalo na liwe...
Au mtu anafanya uamuzi huku akisema maisha yenyewe ni mafupi..
Au mtu anafanya maamuzi huku akisema wengi wape..
Au unafanya maamuzi huku ukiamini kwamba maisha halisi huanzia miaka arobaini. N.k

Je kwa mtindo huo wa kufikiri unahisi mtu huyo atafanya maamuzi sahihi na yenye tija?

Hoja inayotengenezwa hapa ni kwamba mtindo wako wa kufikiri una athari sana linapokuja suala la kufanya maamuzi!
Hivyo basi endapo utafanya maamuzi Kwa kutumia Fikra hasi lazima utapata matokeo mabaya!

Ni sayansi ya ulimwengu mzima kwamba maji hutiririka kufuata mkondo pamoja na aina ya mwamba uliopo, vivyo hivyo na maamuzi yako yatategemea mtindo wako wa kufikiri ulivyo!

Hivyo basi ili Kuamua vyema huna budi kubadili mtindo wako wa kufikiri!

6. Kiwango chako cha uzoefu kimaisha...

Sisi sote ni mazao ya uzoefu tuliokutana nao katika kuishi kwetu!
Kwamba endapo utakuwa na uzoefu wa mambo mengi ni rahisi kufanya maamuzi..

Sasa kama hujawahi kukutana na mikikimikiki ya hapa na pale manake utakuwa ni mzito sana katika kufanya maamuzi!
Mwisho wa siku utajikuta haufanyi uamuzi kabisa!

Vilevile kuna baadhi ya watu ambao katika kuishi kwao wameweza kupitia manyanyaso pamoja na magumu mbalimbali, watu hawa huwa wanakuwa wamekubuhu Kiasi kwamba huona maisha katika namna hasi tu!

Watu hawa huvurunda hata katika kufanya maamuzi kwani huyaona maisha katika namna hasi kuliko namna chanya...
Hivyo basi historia ya maisha yako pamoja na uzoefu wako Huathiri aina ya Maamuzi unayoweza kuyafanya!

Sababu zingine ni:
7. Aina ya washauri ulionao.
8. Kiwango chako cha elimu.
9. Athari za malezi.
10. Mudi uliyonayo wakati wa kuamua.
11. Exposure uliyonayo.

Huo ndiyo wa somo la leo!

Kesho nitakueleza kuhusu, mambo ya Kuzingatia Wakati Wa kufanya maamuzi!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwalimu, mwandishi, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329

Au tembealea blog yangu kwa kutumia link ifuatayo: https://ekingunge.blogspot.com/2023/04/je-ni-namna-gani-ninaweza-kutawala.html

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post