TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

FAHAMU SABABU ZINAZOPELEKEA GARI KUWAKA MOTO

FAHAMU SABABU ZINAZOPELEKEA GARI KUWAKA MOTO
  Kuna sababu nyingi zinazopelekea gari kuwaka moto/kuungua na hii inatokana na mifumo ya gari kuchoka au kuwa sio sahihi (feki).

  Hapa nitazitaja sababu kuu tatu (3) ila kuna moja itakuwa kama nyongeza kwani watu wengi wanaifanya pasipo kujua madhara yake.

SHUKA NAYO

1. HITILAFU YA MIFUMO YA UMEME
Hitilafu ya mifumo ya umeme au shoti inaweza kuwa kisababisha cha gari kuwaka moto hasa hasa kinapotokea karibu na mirija ya mafuta ya gari. 

2. KUVUJA KWA TANK AU MIRIJA YA MAFUTA
Tanki kuvujisha mafuta au mirija ni kisababishi kingine cha gari kuwaka moto hasa ukipita au kupaki karibu na chanzo cha moto au shoti ikiwa karibu na njia ya mafuta.

3. MFUMO WA BREKI
Pia mfumo wa breki hupelekea gari kuwaka moto hii inatokana na mifumo hiyo kuisha au kutumia mifumo isiyo sahihi (feki) ambayo inashindwa kuhimili msuguano (friction) kwa muda mrefu. 

4. NYONGEZA
Kuna hii kitu ya kupimp gari kwa kufunga taa zenye mwanga mkali bila kuzingatia mahitaji ya current ambayo yanatakiwa kupitishwa kwenye waya mpaka kufika kwenye taa.
  Hii kitu ipo hivi unakuta gari inabeba taa ya walt 600 beam na walt 800 full ,sasa unapoenda kwa fundi kumwambia apimp gari yako manake inamlazimu atoe zile taa za asili na kuweka hizi ambazo unazihitaji hapa sasa unakuta fundi anafunga kwa mfano walt 800 beam na full anaweka walt 1000 bila kubadili wiring ya mfumo wa taa na hii inapelekea waya kuzidiwa na mzigo wa current unaopelekwa kwenye taa na lenzi kuzidiwa nguvu na mwanga unaozalishwa na kupelekea kushika zaidi moto na kusababisha gari kuwaka moto.

ZINGATIO: Muhimu kukagua vyombo vyetu vya moto kila siku ili kuepuka na athari zisizo za lazima.

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post