Kwanini Huwa Unapata Kinyume Na Kile Unachokiomba...
__________________
Hivi unafahamu kwamba zaidi ya asilimia 90 ya sala zinazoombwa na watu wengi huishia kuwaletea matokeo yaliyo kinyume na matarajio yao?
Kwa mujibu wa tafiti binafsi nilizofanya nimebaini kwamba, hili limekuwa ni tatizo linalowakumba watu wengi sana!
Huenda hata wewe umekuwa ukikumbana na tatizo hili, usijisikie mpweke kwani wapo watu wengi sana wanaokumbwa na changamoto kama yako!
Habari njema ni kwamba makala hii inaenda kutatua kabisa tatizo hili ambalo huenda limekutesa kwa muda mrefu, na huenda umekuwa ukijiuliza maswali mengi pasipo kupata majibu muafaka!
Kwa mfano huenda ukawa umemuomba Mungu akujaalie utele katika jambo fulani, halafu ukaishia kupata ukomo!
Na kinachokuvunja Moyo zaidi ni pale unapotambua fika kabisa kwamba, Mungu wetu ni tajiri na vitu vyote ni mali yake!
Sasa inakuwaje Wewe unakuwa siyo sehemu ya utajiri huo?
Je ni kweli kwamba Mungu anakuwa amekutenga?
Je ni kweli kwamba Mungu anakuwa hakujali?
Je ni kweli kwamba Mungu anakuwa hakusikilizi?
Jibu ni hapana, kwani kwa upendo Mungu alikuumba kwa thamani kubwa sana ukilinganisha viumbe vyote alivyoviumba!
Wewe hapo ndiyo humsikilizi Mungu, humjali na umejitenga mbali naye...
Najua unajiuliza nimejitenga naye kivipi mbona kila saa nasali?
Huenda ukawa unasali, lakini changamoto ikawa dhambi!
Yes boss, unatakiwa kujua kwamba dhambi ndizo hututenga mbali na Mungu!
Neno la Mungu linasema kwa uwazi kabisa pasipo kigugumizi 👉 "maombi ya mwenye dhambi ni kelele mbele za mwenyezi Mungu"
Hivyo basi Kabla hujaanza kuomba, unatakiwa ujitakase, ujioshe na utubu kwanza.
Unachopaswa kujua ni kwamba Mungu ni mtakatifu anayeishi patakatifu pa patakatifu, hivyo basi kama hutakuwa msafi hawezi kukusikiliza kwani utakuwa ni sawa na unampigia kelele!
Sasa nikupeleke moja kwa moja kwenye lengo la makala hii!
Swali lilikuwa je, ni kwanini huwa unapata kinyume cha Sala zako?
Kabla sijajibu swali hili naomba uchukuee bilblia Yako, then ufungue Mathayo 18:19
Neno la Mungu linasema "Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni"
Kwanza kuna wawili, hao wawili ni akina nani labda? Je ni mimi na wewe? Jibu ni hapana!
Je ni kina nani hao sasa?
Okay wala usijalii, soon utapata jibu...
Hao wawili siyo watu wawili tofauti bali ni nafsi moja ya mtu.
Unatakiwa kujua kwamba, unapoomba kuna vitu viwili:
Cha kwanza ni lile ombi la kile kitu unachokiomba! (your desire)
Na cha pili ni ile picha unayoitengeneza juu ya kile Unachokiomba (your imagination)
Sasa basi endapo itatokea picha unayoitengeneza juu ya jambo unaloliomba (your imagination) ikawa ipo kinyume na kile Unachokiomba (your desire), basi hao wawili kati yako watakuwa hawajapatana katika jambo hilo, hivyo basi Baba yetu wa mbinguni hatakufanyia chochote kile juu hilo!
Unachopaswa kujua ni kwamba kile unachokiona wakati unaomba ndicho utakachokipata!
Kwa mfano tufanye unaomba Mungu abadilishe hali yako ya kiuchumi halafu wakati unaomba, unazidi kuona hali ngumu na umaskini zaidi!
Ndugu unatakiwa kujua kwamba hicho unachokiona ndicho utakachokipata katika maisha yako!
Yamkini utakuwa umefunga hadi kufunga, lakini umeishia kuambulia patupu! Usijue kwamba umeambulia patupu kwa sababu sababu wakati wa kuomba kwako uliona hivyo!
My friend zingatia Sharti hili! Wawili kati yenu lazima wapatane!
Kwa maana isiyo rasmi manake kile unachokiona ni kipatane na kile unachokiomba!
Kwa mfano kama unaomba ongezeko la mauzo kwenye biashara yako, jione ukiwa unawahudumia wateja nyomi kwenye biashara yako!
Unachopaswa kuondoka nacho hapa ni hiki; endapo Wawili kati yenu watapatana, basi Baba yenu aliye mbinguni atafanya jambo fulani juu ya ombi hilo!
Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba, inahitaji imani kubwa sana ili uweze kuuona mwisho mwema wa kile unachokiona wakati unasali!
Kwa tafsiri iliyotukuka imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
Mbali na hilo hautakiwi kuishia tu kuwa na imani bali unatakiwa uamini imani yako juu ya jambo hilo!
My friend unatakiwa kuamini katika kuamini!
Yaani uamini mwisho ule uliouona nao utakuja kutokea vivyo hivyo!
Kwa ujumla unatakiwa uenende kwa imani na siyo kwa kuona! Amini katika kuamini! Kumbuka yoyote Yale myoambayo aminini kuwa mnayapokea nayo yatakuwa yenu!
Ziba jicho la nyama, fungua jicho la kiroho! Ama hakika utabadili maisha yako!
Endapo unachokiomba na unachokiona vitapatana basi utapata kama ulivyotarajia!
Jiamini, amini katika kuamini! Jione katika viwango vya juu!
Kumbuka, kile unachokipata kwenye maisha ni uakisi wa kile unachokiona akilini mwako!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, mwandishi,, mwalimu, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329
Tags
Elimu