*HATUACHANI!!*❤️
*SEHEMU YA 01
"...mamy mmwaaaaah!!" Yvonne alimbusu mama yake kwenye paji la uso wakati akimuaga akiwa anatoka, amebeba mkoba (handbag) begani
"Uwahi kurudi, si unamjua baba yako alivyo mtata, lawama zote ataniangushia mimi!"
"Sawa mama usijali, siwezi kusababisha baba akulaumu na kukusema, leo narudi mapema tu!"
"Basi vizuri, umependeza sana Yvone binti yangu mrembo"
"Ooooh leo makubwa mpaka wewe mama umenisifia basi nimependeza kweli haswa"
"Sasa kwahiyo umezoea kusifiwa na vijana wa kiume huko, wakikusifia hao ndo unajua kweli ila mimi mama yako unaniona kama mnafiki eti?"
"Hamna mama siyo nakuona kama mnafiki no, ni kwamba...."
"Hebu toka hapa nendaga huko usinitie usiku"
"Jamani mama ndo umenuna?"
"Ninunie nini?"
"Haya mamy bye!" Yvonne alimwambia mama yake na kutoka taratibu kwenda sebuleni mpaka nje huku simu yake ya mkononi ikiita muda wote akapokea na kuiweka sikioni
"Babe?" sauti ya kiume ilisikika upande wa pili wa simu
"Abee baba"
"Mbona hutoki tu umeniacha hapa nje kama sanamu la nguo?"
"Nakuja my Boo si unajua tena lazima nitokelezee?"
"Fanya chap chap basi si unajua mambo ni mengi?"
"Am coming my Love" Yvonne alijibu kwa kudeka na simu ikakatwa akatoka mpaka nje ya geti lao na kwenda nje kukiwa na gari dogo aina ya Toyota Harrier likimsubiri nje mita kadhaa kutoka kwenye nyumba yao ilipo, akalifuata gari hilo lenye vioo vyeusi (tinted) visivyoonesha kinachoendelea ndani, kioo cha dereva kikashushwa taratibu na kijana mwenye miwani myeusi (tinted) alionekana, akiwa amevalia tshirt nyeupe na kofia kichwani, shingoni akiwa na mikufu ya madini, inayong'aa
"Unataka kunikera sasa Yvonne" aliongea
"Hamna babe si nimekuja jamani usinune mmwaaah" alimbusu shingoni
"Panda kwenye gari" jamaa huyo aliyeonekana kukasirika alimwambia,
"Jamani baby ndo umenikasirikia?"
"Yvonne panda kwenye gari twende!" aliambiwa kwa mara ya pili akaingia kwenye gari hilo zuri, Toyota Harrier jeupe, New Model, wengi wakiliita Harrier mayai au macho ya paka kutokana na muundo wake, alikaa pembeni mwa kijana huyo mpenzi (boyfriend) wake, akamshika begani
"Tunaenda hotel gani babe?"
"Tutajua hapo hapo"
"Usinikasirikie bwana jamani Gerald, si nimechelewa kidogo tu eti?" Yvonne alimwambia mpenziwe huyo na kumshika kidevu akamgeuza uso taratibu wakatazamana machoni (usoni) kisha taratibu wakasogezeana midomo (lips) na kuanza kunyonyana mat** (denda) taratibu, Gerald akamdaka shingo mwanadada huyo asije akathubutu kutoa midomo yake wakizidi kunyonyana mat** (denda) huku akikipandisha taratibu kioo cha dirisha, Yvonne akajitoa kwenye midomo ya Gerald
"Nipe Yvonne, nipe!" Gerald aliongea kwa sauti ya chini akionekana kunogewa na mat** (denda) akitaka tena
"Twende bwana G jamani nitakupa yote hotelini bwana hapa njiani mama asije akatoka ndani bure"
"Nimepandisha kioo hawezi kutuona" aliongea jamaa huyo huku akiyatazama mapaja ya Yvonne kwa uchu, mwanadada huyo akiwa amevalia sketi fupi iliyoacha mapaja yake wazi, mkono wa Gerald ukapita na kuanza kuyapapasa papasa taratibu, Yvonne akautoa na kumtazama Gerald kwa macho makali,
"Nimekwambia twende hotelini, kwani una haraka gani jamani?"
"Oky sawa!" Gerald alimuacha na kuwasha gari akiliondoa kwa kasi
"Ndomana nampendaga binti yangu Yvonne, hajuagi kuchagua wanaume magarasa magarasa wasio na kitu, anachagua mali safi zinazojiweza, huyu ndiye mkwe sasa ninayemtaka, yaani binti yangu hajarithi tu mwili wa mama yake ila karithi mpaka akili zangu mama yake!" mama Yvonne, mwanamama Kezia aliongea mwenyewe akiwa dirishani amesimama, sebuleni akitazama nje binti yake alivyoingia kwenye gari la mwanaume mpaka walivyoondoka
"Shangazi...!" aliitwa nyuma akageuka
"Unasemaje?"
"Shikamoo!"
"Zungumza unachotaka kuzungumza Anna" alimwambia msichana huyo ambae alivaa gauni refu kuu kuu la mtumba akiwa ameshika kisu na kitunguu mkononi ametokea jikoni, akitazama chini kiuwoga uwoga
"Nilikuwa nasema vipi kuhusu suala la kwenda shule shangazi kama ulivyoniahidi?"
"Shule, shule gani na utu uzima huo Anna?"
"Si QT, ulisema nikija kukaa huku kwako utanisomesha sasa naona miezi mitatu sasa hakuna chochote shangazi"
"Oooh shida yako kusoma tu?"
"Ndiyo shangazi"
"Basi subiri mwakani kuna hela yangu naisubiri nitakulipia ada, nitakununulia uniform, soksi, blauzi, sketi mpaka chupi utaenda kusoma tu usijali!"
"Lakini shangazi mpaka mwakani tena mbona mbali, kwani si ulisema ni mwaka hu...."
"Kelele, unanifundisha kazi na cha kufanya, unanipangia?!!" Mwanamama Kezia alimkaripia msichana huyo mpaka akashtuka
"Hapana shangazi sikupang..."
"Huli, hunywi, huvai hapa ndani, haunyi chooni?"
"Hapana shangazi sijamaanisha kuwa..."
"Pumbavu na ungeendelea kukaa kijijini uzidi kupauka mshenzi wewe, kila siku kusoma kusoma, shule shule, shule unaenda bure, niharibu pesa zangu mimi kukupeleka shule, fanya kazi utafute za kwako uende shule, binadamu gani wewe usiyeridhika eeh?"
"Samahani shangazi..."
"Hebu kapike, nitokee hapa nisije nikakuzaba makofi bure!" alimwambia, msichana Anna akageuka na kuanza kuondoka taratibu kuelekea jikoni alipokuwa anapika huku machozi yakimlenga lenga machoni, alipofika jikoni machozi yalizidi na kuanza kuchuruzika mpaka mashavuni huku akijifuta futa, alikuja mjini kwa shangazi yake huyo kwa makubaliano ya kusomeshwa, kupelekwa kwenye Elimu ya sekondari ya watu wazima (QT) lakini badala yake akajikuta anaishia kuwa dada wa kazi (housegirl)
Anna alishindwa kujizuia na kujikuta akilia kama mtoto lakini kwa kwikwi, gauni lake akalitumia kujifuta futa machozi yaliyoambatana na kamasi,
"Mimi nataka kusoma lakini..."
"Lakini nini?" alikatishwa alipokuwa akiongea mwenyewe na akageuka na kukutana na shangazi yake, mwanamama Kezia akiwa amesimama kwenye mlango wa jikoni akimtazama huku amejishika kiuno,
"Hamna kitu shangazi" alijifuta machozi kwa gauni lake haraka haraka
"Badala ya kupika chakula watu tule tuna njaa umekaa unajiliza liza hapo, umefiwa au?"
"Hamna shangazi sijafiwa, wala sikuwa ninalia"
"Kwahiyo mimi muongo, hiyo michozi na mimacho yako myekundu imetoka wapi?"
"Nilikiwa nina..."
"Mpuuzi wewe kachukue mimaji michafu ile nje pale kamwage nje, unafua nguo mimaji yako michafu unamwachia nani?"
"Sijafua mimi shangazi, ni Yvonne ndiye aliyefua, mimi leo sijafua"
"Sasa kama Yvonne kafua ndo unashindwa kutoa, ulitaka atoe yeye, wewe una kazi gani humu ndani hebu kayamwage!" alikaripiwa,
"Sawa shangazi naenda kuyamwaga, Anna alijibu na kumpita shangazi yake huyo mlangoni kwa wasiwasi mkubwa akihofia kupigwa, shangazi yake akamsindikiza kwa macho makali
"Kama kichawi, kione vile!" mwanamama Kezia akamsonya na kwenda kuitazama mboga jikoni, Anna alipofika uwani alipunguza maji kwenye beseni kwa sababu yalikuwa mengi na kubeba mpaka getini akayarusha maji nje kuyamwaga lakini akajikuta akimmwagia mwanaume aliyesimama getini ambae hakumwona akiwa amevaa vizuri akiwa na shati na suruali na viatu huku mikononi akiwa na maua ameyashika maalumu kama zawadi kwa mtu, Anna akabaki ametoa macho baada ya kummwagia mwanaume maji machafu mwilini na kumloweshea nguo zake.....
*SEHEMU YA 02*❤️
Anna alibaki ametoa macho akiwa na beseni lake mikononi baada ya kummwagia maji machafu kijana huyo mtanashati aliyekuwa amependeza akiwa na ua lake kubwa mikononi ambalo kwa bahati nzuri aliliwahi na kulikwepesha pembeni lisije likalowa akajikuta akilowa mwili na nguo tu, ua hilo kubwa jekundu likiwa salama salimini halijaguswa na maji hayo machafu yaliyotoka kufuliwa, kijana huyo akabaki anajitazama huku akisikitika mwenyewe akijaribu kujifuta futa maji kwa mkono na Anna akalitupa beseni chini na kujiziba mdomo kwa mikono
"Uuuwiiii jamani pole kaka yangu sikukuona ni bahati mbaya"
"Usijali hata mimi sikukuona ningejua kama unataka kumwaga maji ningekukwepa"
"Ngoja nikufute" alimkimbilia mwanaume huyo na kulishika gauni lake la mtumba akitaka kumfuta maji
"Wala usijali haina haja nitajifuta mwenyewe, nitakwenda kubadilisha nyumbani cha msingi ni kitu muhimu nilichokibeba hakijalowana maji"
"Kipi hicho?"
"Hili ua!"
"Mh jamani, yaani ua ndo la muhimu kuliko nguo zako kaka?"
"Yeah ni kwa sababu nimelileta kwa mtu maalumu"
"Angalau basi nikufute usoni maji" Anna alimwambia akimshika kichwa kijana huyo ambae aligoma kuinama lakini akamlazimisha na kumfuta futa maji usoni kwa gauni lake refu alilolishika upande akifanya kama kitambaa
"Oooh asante imetosha usijali, nipo sawa kabisa nitabadili nyumbani nguo"
"Sawa, pole tena sikukusudia!" Anna alijibu kiunyonge na kuokota beseni lake chini kisha akageuka kutaka kurudi ndani akiwa amejaa masikitiko
"Oooh samahani dada unaitwa nani?" yule mwanaume alimwuliza
"Naitwa Anna"
"Oooh Anna, samahani tena kwa maswali yangu mengi ila hili litakuwa swali langu la mwisho, hivi unaishi humu ndani?"
"Ndiyo naishi humu kwanini?"
"Ni housegirl eeh, I mean ni dada wa kazi?"
"Mh kwani unanionaje kaka, nimekaa kidada dada wa kazi?"
"Hamna sijamaanisha hivyo, samahani kama nimekukwaza, namaanisha una mahusiano gani na wenye nyumba humu ndo maana yangu"
"Mahusiano yangu na wenye nyumba yana umuhimu gani kwako kuyajua kaka yangu, sikuelewi"
"Tafadhali usinielewe vibaya kuna kitu nakitafuta ndo maana nakuuliza uliza, ngoja niende kwenye pointi ya msingi, naitwa Peter...aamh!"
"Oooh sawa karibu"
"Aaamh nilikuwa naulizia hivi Yvonne yupo ndani, hapa si ndiyo kwao?"
"Mh Yvonne, kwanini unamwulizia wewe ni nani mbona sikujui maana hapa ni mjini mambo mengi"
"Aaam mimi ni boyfriend wake, I mean mchumba wake"
"Mchumba wake...unamaanisha wewe ni...?"
"Yap mchumba wake, Peter!"
"Oooh kumbe shemeji, samahani jamani sikufahamu ndomaana nikadhani mtu tu mpita njia"
"Usijali, Yvonne yupo ndani?"
"Hapana hayupo ametoka, samahani sana shem, mimi ni Anna, Yvonne ni binamu yangu, hapa ni kwa shangazi yangu, mama yake Yvone" Anna ilibidi ajichekeshe chekeshe na kumchangamkia kijana huyo baada ya kugundua kuwa aliyekuwa anamjibu majibu ya mkato ni mpenzi wa Yvonne
"Oooh kumbe, nashukuru kukufahamu Anna!"
"Karibu ndani shem"
"Hapana Anna ndani siingii nataka tu uniitie Yvonne hapa nje nataka kuzungumza nae dakika mbili tatu, ila tu mama yake asijue chochote kama kuna ugeni hapa nje"
"Mh shem nasikitika kukuambia kuwa Yvonne wala hayupo, ameondoka muda si mrefu kutoka sasa, yaani ni dakika chache tu ni kama mmepishana vile!"
"Ameondoka?"
"Ndiyo"
"Wapi?"
"Sijajua, mara nyingi hanishirikishagi safari zake"
"Mh!?" Peter aliguna na kushusha pumzi akionekana kunyong'onyezwa na taarifa hiyo ya kutokuwepo kwa Yvonne
"Mbona umekuwa mnyonge ghafla shem?"
"Nikwambie kitu Anna, Yvonne nimemsapraizi tu hapa sijamwambia kama nakuja kwao na hata hapa kwao hajawahi kunileta, nimemfuatilia tu kimya kimya na kichini chini bila yeye kujua mpaka nikapafahamu sasa unadhani ni mpenzi gani anakubali kuwa kwenye mahusiano na mwenzake bila hata kupafahamu kwao kwanza, ndomaana nikaamua kufanya utafiti mimi mwenyewe mpaka nikapafahamu maana kila nilipomuomba anilete tu hata nje ya geti nipafahamu akawa ananikwepa kwepa na kunipa vijisababu vingi vingi visivyo na mkia wala miguu sasa nikamwuliza leo kwenye simu kiujanja ujanja kama atakuwepo nyumbani au atatoka, akaniambia kuwa leo yupo ana ratiba tu za kujisomea somea nyumbani hatotoka, sikumwambia kama nakuja kwao kwa sababu hajui kama ninapafahamu nikaamua kuja kumsapraizi lakini nashangaa unaniambia ametoka na wala hajaniaga kama leo anatoka, au amekupanga kuwa mgeni akija umwambie hayupo?"
"Sasa shem ushasema hajui kama unapajua hapa nyumbani sasa atanipangaje?"
"Oooh sorry Anna, ni kuvurugwa tu ila ni sawa, naomba uupokee mzigo huu kwa niaba yake, akija umpe na usimwambie umetoka wapi mwambie tu mtu wako maalumu sana amekuletea, yeye mwenyewe ataelewa nani kampa" Peter alimpa Anna ua hilo kubwa na zuri la bei, jekundu
"Sawa shem mzigo umefika"
"Asante sana Anna"
"Karibu tena shem na....!"
"Kuna nini kinachoendelea hapa nje?" kabla Anna hajamaliza sentensi yake ilisikika sauti nyuma alipogeuka uso kwa uso akakumbana na shangazi yake, mama wa Yvonne, Peter akajikuna kichwa na kujiweka sawa
"Oooh mama shikamoo" alimsalimia akitegemea salamu yake kuitikiwa na mwanamama huyo ambae alimtazama Peter kwa kumpandisha kutoka chini mpaka juu na kumshusha tangu juu mpaka chini na hakuitikia salamu wala kumjibu chochote akamgeukia Anna akilitazama ua alilolishika mwanadada huyo mikononi
"Yaani Anna umeacha mapishi jikoni umekuja nje kutongozwa tongozwa na wanaume mpaka mnacheza na kumwagiana maji machafu kama watoto?"
"Hapana shangazi sijaja kucheza ni..."
"Kelele, mpumbavu wewe, msichana gani usiyejiheshimu hata kidogo, kazi kujichekesha chekesha kwa wanaume?"
"Hamna mama Anna alikuwa ana...."
"Kelele na wewe kijana muhuni kabisa, kwenye mageti ya watu mchana mchana kutongoza tongoza wasichana hauna kazi za kufanya, kasombe hata vinyesi vyooni mwa watu mbona kazi zipo nyingi sana mjini hapa siyo kuzurura tu na kujifanya shababi kwenye nyumba za watu mstcheeeewwwwww!!" mwanamama Kezia alimkatisha Peter ambae alitaka kumtetea Anna, kijana huyo akabaki kimya baada ya kuporomoshewa maneno makali ya fedheha (aibu) akikosa cha kujibu
"Peter bye!!" Anna alimuaga kijana huyo haraka haraka akataka kuingia getini lakini akadakwa mkono na shangazi yake kabla hajaingia
"Unaenda wapi na hiyo takataka, ndani ya nyumba hii yangu?"
"Hamna shangazi hili ni ua, siyo langu ni la....." kabla hajamaliza sentensi yake alinyang'anywa ua hilo kubwa na shangazi yake ambae alilikunja kunja mara kadhaa kama uchafu kisha akalitupa chini likiangukia miguuni mwa kijana Peter aliyelinunua na kwa gharama, akainama taratibu na kiunyonge akiliokota ua hilo likiwa limechafuka na maji machafu chini kisha akainua uso wake na kutazamana na mwanadada Anna ambae alikuwa nae amegeuka akimwonea huruma kijana huyo kwa kitendo alichofanyiwa na shangazi yake, macho yao yakigongana.....
*SEHEMU YA 03*❤️
Peter alibaki amelishika ua hilo kubwa mikononi alilokusudia kumpa Yvonne, likiwa limechafuka na kukunjwa kunjwa, likiwa halitamaniki tena, yaani halivutii, wakati huo mwanadada Anna akiishia getini na shangazi yake na geti likafungwa kwa kubamizwa kwa nguvu, kijana huyo akashusha pumzi na kugeuka akitembea kwa mwendo wa taratibu, miguu akiiona mizito sana kama amebeba mapipa ya maji, akijiona kama siyo yeye vile, akitamani kukaa chini lakini hapakuwa na mahali pa kukaa
"Kwanini umenidanganya Yvonne, umesema kuwa upo nyumbani na kumbe umetoka kimya kimya na wala hukutaka kuniaga?" aliongea mwenyewe na mara akasikia kicheko kikali kutoka kwa watoto wadogo akageuka na kuwaona wakiwa wawili, mmoja wa kiume na mwingine wa kike, walipoona amewatazama wakanyamaza kimya kwa hofu
"Shikamoo!"
"Shikamoo!" walimsalimia walipoona amewakazia macho, akawasogelea na kuinama akiwatazama vizuri
"Watoto wazuri mnaweza kuniambia kinachowachekesha ni nini, je nina mapembe au nina mkia wa punda nyuma?"
"Hamna huyu hapa alikuwa ananiambia eti wewe hapo kaka umebeba ua chafu ndo maana uliyempelekea akalikataa" wa kike alijitetea akimwonyesha kidole mwenzake wa kiume
"Hamna mimi sijasema hivyo unanisingizia tu" wa kiume alibisha
"Haya msigombane nendeni nyumbani" aliwaambia watoto hao waliovalia sare za shule (uniform) wakakimbia mbio mbio, kisha yeye akasogea mpaka kwenye mtaro na kuliweka ua hilo chini pembezoni mwa barabara hiyo ya vumbi, akatabasamu tu na kuondoka kuendelea na safari yake, akachukua simu yake na kumpigia mwanadada Yvonne, mpenziwe na alipogeuka nyuma akawaona wale watoto wakiwa wamerudi na kuokota ua hilo ambalo kumbe walikuwa wanalitaka kisha wakakimbia, Peter akatikisa kichwa wakati huo simu aliyompigia Yvonne ikiita bila kupokelewa na mwishowe ikakatwa, akapiga mara ya pili ikaita tena bila majibu mwishowe akajibiwa na mwanamke.... 'NDUGU MTEJA NAMBA UNAYOPIGA HAIPATIKANI KWA SASA TAFADHALI JARIBU TENA BAADAE' hiyo ni baada ya kupiga mara tano bila kupokelewa
"Umepatwa na nini Yvonne mbona hupokei simu na sasa haipatikani kabisa, kuna kitu nimekukosea?" alijiuliza mwenyewe bila majibu akitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa,
"Piiiipiiiiiii!!" mara alipigiwa honi kali ya pikipiki akatazama na kukutana na piki piki hiyo 'boda boda' ikiwa tayari imefika miguuni mwake kwa sababu akili na mwili vilikuwa mbali alijikuta akitembea kwenye barabara hiyo ya vumbi (kokoto) bila uangalifu wowote, akashindwa kufanya maamuzi ya haraka haraka ndani ya sekunde hizo chache na kujikuta akigongwa, mita chache tu kutoka ilipokuwa nyumba ya wazazi wa Yvonne.....
"Nani huyo anayekupigia saa hizi, mbona umemkatia?" Yvonne aliulizwa na mpenziwe, Gerald wakati wakiwa kwenye gari
"Mjinga mjinga mmoja hivi ananisumbua sumbua sana" alizuga
"Si ungepokea tumsikie huyo mjinga mjinga anasemaje, mbona umemkatia simu?"
"Haina haja babe, mbona unakuwa na wasiwasi hivyo"
"Wasiwasi ndo akili" jamaa huyo aliguna huku akiendesha gari kwa mwendo wa taratibu,
"Yaani Gerald wewe una mawivu ya ajabu ajabu mh" Yvonne aliongea akimuegemea mwanaume huyo begani ambae alisimamisha gari kisha akamtazama
"Kwahiyo wewe Yvonne hauna wivu juu yangu?"
"Ninao ila G wewe umezidi maana mh" Yvonne alimjibu mwanaume huyo ambae alimgeukia na kumtazama na kutikisa kichwa chake na kutabasamu huku macho ya jamaa huyo yakiangalia kifuani mwa Yvonne, mwanadada mrembo aliyejaaliwa kifua kilichobeba matit** ya kuvutia ambayo yalikuwa yamachungulia kwenye blauzi aliyovaa, Yvonne akarembua macho yake akimtazama Gerald kwa aibu huku akijifanya kugeukia pembeni, kidevu chake kikadakwa na kurudishwa tena watazamane
"I love you Yvonne na wewe unajua"
"Nakupenda pia G my Love" Yvonne alitabasamu na kilichofuata ni midomo (lips) yao kusogeleana, wakaanza kubadilishana mat** taratibu huku mkono wa Yvonne ukiteremka mpaka kwenye zipu ya suruali ya Gerald na kuanza kumpapasa papasa taratibu Jogoo' wa mpenzi (boyfriend) wake huyo ambae alikuwa amesimama ndani ya suruali na hakuishia hapo akafungua zipu kabisa na kumtoa nje akimshika shika na kumpapasa papasa kwa mikono yake yenye kucha ndefu bandia za kubandika huku mikono ya Gerald ikiwa kifuani mwa mwanadada huyo akimpapasa papasa kwenye matit** yake na Gerald akakifyatua kiti chake yeye mwenyewe kikalala kidogo kilichofuata Yvonne akaishusha sketi yake na kuivua kabisa akiitupia kwenye viti vya nyuma, hakuishia hapo akavua mpaka chup** na kuining'iniza kwenye usukani wa gari, Gerald akaishusha suruali yake nusu usawa wa mapaja pamoja na boksa yake kisha mwanadada huyo akaja na kumpandia kwa juu yake huku midomo (lips) yao ikiwa haijaachana, imeng'ang'aniana bado.....
Upande wa pili mwanadada Anna alikuwa jikoni akimalizia mapishi lakini akiwa amejawa masikitiko mengi kufuatia kilichotokea getini kwa yule kijana mpenzi wa Yvonne aliyejitambulisha kwa jina la Peter ambae alimletea Yvonne ua lakini mama wa Yvonne akalitupa ua hilo na kumtolea maneno machafu akijua ni Anna aliyeletewa
"Masikini kaka wa watu jamani, hivi ni kweli shangazi hamjui mpenzi wa Yvonne au hamtaki tu sasa mbona amemfanyia vile?" Anna alijiuliza mwenyewe huku akitikisa kichwa
"Wewe mjinga mjinga" aliitwa akashtuka
"Abee aunty?"
"Mimi natoka naenda kwenye kikao cha wanawake sasa ole wako uanze kutoka toka na kuzurura, kaa humu ndani, fanya usafi na kila kazi, nisikute vyombo vichafu wala usafi wowote ule"
"Sawa aunty"
"Mwanangu Jimmy amerudi chuoni mwandalie chakula"
"Haya shangazi" alijibu, mwanamama Kezia akaondoka na kumwacha mwanadada huyo ambae alimaliza kupika na kwenda kuandaa chakula kwenye meza maalumu ya chakula (mess) kama ilivyo kawaida, wakati akimalizia kuandaa kijana Jimmy kaka wa Yvonne alikuwa nyuma yake akimtazama kwa uchu msichana huyo akimwangalia kwa kumshusha tangu juu kichwani mpaka chini miguuni na kumpandisha tangu chini miguuni mpaka juu kichwani kisha akajiramba midomo kwa ulimi, Anna akageuka na kumwona
"Ooh kaka umerudi?"
"Yap Anna nimerudi, niletee chakula chumbani" Jimmy aliongea maneno machache akiwa kifua wazi amevaa bukta tu na kuondoka taratibu kurejea chumbani kwake alipokuwa amelala, Anna akiwa anaimba nyimbo akabeba chakula na kuelekea chumbani kwa kijana huyo akagonga mlango ukafunguliwa
"Chakula hiki hapa kaka"
"Pita tu uniwekee"
"Hapana kaka chukua tu, ukimaliza utaniambia nivifuate vyombo" Anna aligoma kuingia chumbani kwa kijana huyo ikiwa siyo utamaduni aliouzoea kuingia chumbani kwa mwanaume
"Anna kwani una wasiwasi gani, pita tu si unaniwekea kisha unatoka, mpaka kaka yako unaniogopa, usiwe hivyo bwana, haya niwekee pale" alimfungulia mlango zaidi, Anna akiwa na wasiwasi na mashaka akashusha pumzi kwanza na kuingia taratibu kwenye chumba cha kijana huyo akamwekea chakula chake kwenye stuli na kugeuka akamkuta Jimmy akifunga mlango kwa ufunguo kwa ndani
"Kaka Jimmy mbona unafunga mlango?"
"Wewe mkubwa bwana umeshaelewa" alimfuata
"Hapana nifungulie"
"Nipe kidogo Anna mimi nakupenda" alimshika mabegani
"Niache Jimmy niache" alimsukuma kwa nguvu
"Oooh kumbe demokrasia haina kazi eeh, sasa tutajua mimi na wewe nani mwanamke na nani mwanaume!" Jimmy alimshika msichana huyo kwa nguvu akimbana kwa mikono yake na kumsogeza mpaka kitandani
"Niache Jimmy sitaki, niachee!" Anna alipiga mayowe akijitahidi kutaka kujinasua kwenye mikono ya mwanaume huyo lakini haikuwa rahisi, alidhibitiwa ipasavyo....
*SEHEMU YA 04*❤️
"Niache Jimmy niache unaniumiza!!" Anna alilalamika akijitahidi kufurukuta mikononi mwa kijana huyo mwenye nguvu bila mafanikio
"Kidogo tu Anna kidogo tu nawewe, acha uchoyo bwana, utakufa nacho hicho" Jimmy hakutaka kumsikiliza ndiyo kwanza alimbana kwa goti huku akiishika mikono yake kumdhibiti asije akajaribu kufurukuta furukuta huku gauni lake refu likipandishwa juu kwa mkono mmoja wa kijana huyo, kaka wa Yvonne
"Jimmy mbona unakuwa hivyo!" Anna alizidi kupingana na kitendo hicho cha kutanga kuingiliwa kimapenzi kinguvu na hakukubali akauotea mkono wa Jimmy na kuungata kwa nguvu
"Annaaa!!" Jimmy alipiga makelele na kumwachia mwanadada huyo, akasukumwa kwa nguvu na kuanguka kutoka kwenye kitanda juu mpaka chini sakafuni akiwa anaugulia maumivu ya kung'atwa meno, Anna akaukimbilia ufunguo wa mlango wa chumba hicho
"Mbona una tabia za kishenzi shenzi, ulitaka kunifanya nini, unibake ili, mimi sikutaki na nilishakwambia nimekuja hapa kwa ajili ya kusoma na siyo mengine yoyote, halafu wewe si ndugu yangu?"
"Wa kusoma utakuwa wewe Anna, dah umeniumiza mkono aashh!"
"Ili usirudie tena, nitasoma tu Mungu yupo" alimjibu na kumsonya akafungua mlango kutaka kutoka
"Anna!" akaitwa na kugeuka
"Unadhani una cha kuniambia tena nikakusikiliza?"
"Usimwambie mama wala mtu yeyote tafadhali sana" Jimmy aliongea,
"Sijakutegemea!" mwanadada huyo alitikisa kichwa kusikitika kisha akatoka na kuubamiza mlango wa chumba hicho akimuacha Jimmy anainuka pale chini sakafuni na kukaa kitandani
"Yaani wewe wa kunishinda mimi Anna, sijawahi kumpenda msichana akanikataa, lazima nitakufunza adabu na nitakupata tu" Jimmy aliapa kwa hasira za jambo lake kutokufanikiwa, Anna akaenda na kukaa kwenye kochi (sofa) kwa hasira huku akitikisa tikisa mguu wake wa kulia kama ilivyo kawaida yake pindi anapokasirika, akashusha pumzi ndefu ya kupunguza hasira kisha akachukua hela jikoni kwa ajili ya kwenda kununua kitu dukani, akatoka mpaka nje ya geti na kuanza kutembea mita kadhaa kuelekea dukani
Peter alikuwa chini amekaa kitako baada ya kusukumwa na pikipiki ambayo ilitaka kumgonga lakini kwa bahati nzuri aliwahi kuiona ikamsukuma kudogo, dereva wa pikipiki hiyo na abiria wake aliyempakiza (wote wanaume) akasimama mita kadhaa mbele
"Wakati mwingine acha kuwaza mapenzi barabarani mpaka unataka kutuletea usiku hapa saa hizi mse(...) wewe" Peter alitukanwa na dereva huyo
"Samahani kaka!" aliwajibu wakaondoka kwa kasi
"Peter!!" akasikia akiitwa na sauti ya kike alipogeuka akamwona Anna akija mbio mbio mpaka pale alipo
"Anna"
"Umepatwa na nini tena jamani mbona upo chini, ile pikipiki imekugonga?" Anna alijawa wasiwasi akimshika kijana huyo na kumwinua
"Hapana haijanigonga imenisukuma tu kidogo"
"Hujaumia jamani?"
"Sijaumia Anna usijali"
"Wale.madereva jamani wa boda boda sijui wapoje wanaendesha kama walevi"
"Wala siyo kosa lao, ni kosa langu sikuwa natembea kwa uangalifu nilikuwa nawaza mbali"
"Usiwaze sana kaka inuka" alimshika mkono kumsaidia kunyanyuka
"Usijali naweza kuinuka mwenyewe" alikataa na kusimama mwenyewe
"Umeumia" Anna alimwambia akimtazama mguuni, Peter akiwa hajajiona bado akajitazama na kugundua kuwa damu zinamchuruzika kwenye mguu wa kushoto kutokana na mchubuko alioupata, na ndipo alipomshuhudia mwanadada huyo akichana upande wa gauni lake hilo refu na kisha akakichana tena kipande mara mbili, na kuchuchumaa
"Unafanya nini Anna?" alimwuliza
"Sitaki maswali shem" Anna alimjibu na kumfuta damu hizo mguuni kwa kipande kimoja cha nguo yake alichokitoa kwenye gauni lake mwenyewe kisha kipande kingine akamfunga jeraha hilo, Peter akibaki anamtazama tu mwanadada huyo akiwa hajaamini kilichotokea, Anna alipomaliza kumfunga jeraha akasimama na kujikung'uta kung'uta mikono
"Asante sana Anna lakini hukupaswa ku..."
"Eeh shem, mbona hivyo, jambo dogo tu unataka kulikuza, haya uwahi nyumbani salama mimi nawahi dukani" Anna aliondoka mbio mbio na gauni lake lililochanika chini likining'inia, Peter akabaki anamtazama akimsindikiza kwa macho
"Mwanamke wa aina gani huyu?" alijiuliza mwenyewe na kujikuna kichwa kisha akaanza kuondoka taratibu huku akichechemea, safari kurejea stendi ya daladala ili apande gari na kurudi kwake na ndipo alipoliona gari likinesa nesa pembeni mwa barabara likiwa pembezoni mwa barabara akasimama na kulitazama, likiwa na vioo vyeusi (tinted) aina ya Toyota Harrier New Model, vijana wakiliita Harrier Mayai' au macho ya paka'
"Unashangaa nini kaka watu wanafanya yao humo" mpita njia mmoja ambae alielewa kinachoendelea ndani ya gari alimwambia Peter ambae alitikisa kichwa kusikitika tu na kuendelea na safari yake huku akichechemea baada ya kushtuliwa na mpita njia huyo,
Ndani ya gari hilo shughuli ilikuwa inaendelea, mwanadada Yvonne alikuwa amevua nguo za chini yaani sketi na chup** amemkalia Gerald kiunoni, akimpa penzi mpenzi (boyfriend) wake huyo ndani ya gari
"G jamani uuwiii basi twende hotelini basi kwanza aaasssh!" alilalamika,
"Tutaenda tu kwanza nitoe gundu hapahapa si unajua ni wiki sasa sijaonja tamu yako oooosh!" Gerald aliguna akiwa amekishika kiuno cha mwanadada huyo mrembo huku akiwa ameshusha suruali na boksa usawa wa magoti akiwa amekaliwa kwa juu na kiti amekilaza kidogo kwa nyuma, macho ya mwanadada Yvonne yalitazama dirishani akashtuka alipomwona mpenziwe, Peter akiwa anakatiza nje
"Peter?!" alijikuta akiropoka
"Peter ndo nani?" Gerald aliuliza baada ya kusikia jina la mwanaume mwenzake linatajwa katikati ya mchezo, wakati akimaliza kazi yake ya dakika takribani sita na kushusha mzigo kwenye kisima' cha mwanadada huyo
"Hamna sijasema Peter nimesema tu ni..." Kabla Yvonne hajazungumza, Gerald akamsukuma na kumtoa juu yake, mwanadada huyo akajikuta akikalishwa kinguvu kwenye kiti chake, mwanaume huyo akachukua kitambaa (leso) na kujifuta futa mtalimbo🍆wake baada ya kumaliza kazi
"Yaani unamtaja Peter masikioni mwangu nasikia halafu unanikatalia, ina maana mimi sisikii vizuri?"
"G mpenzi wangu jamani kuna mtu tu nimemwona nimamfananisha nje ame..."
"Shuka kwenye gari yangu Yvonne!"
"Jamani babe kwani si tunaenda hotelini mbona tunagombana kwa mambo madogo tu?"
"Kwako mambo madogo siyo, chukulia picha mimi ndiye ningetaja jina la mtoto wa kike mfano Angel, Jenipher au Rose au yeyote yule katikati ya tendo wewe ungechukuliaje, ungefurahi siyo?"
"Hamna babe please nisamehe usichukulie kitu seriously jama..."
"Get out of my car please!!" Gerald aliongea kwa msisitizo na kwa ukali akimtaka mwanadada huyo atoke kwenye gari huku akivaa suruali yake,
"Yaani kisa mambo madogo ndo unanigeukia namna hiyo Gerald"
"Out!"
"Oky naenda, usinitafute tena" Yvonne alijibu kwa hasira na kuvaa nguo zake haraka haraka akaufungua mlango na kutoka kwenye gari hilo Peter akauvuta mlango na kuubamiza kisha akaliondoa gari kwa kasi
"Gerald kwanini unanifanyia hivi?" Yvonne alimpigia makelele akilikimbiza gari bila mafanikio, Peter aliyekuwa mita kadhaa mbele akageuka na kuona gari hilo aliloliacha nyuma likimpita kwa kasi na kumwona mwanadada mita kadhaa akiwa ameinama amejishika magoti anamwita dereva wa kwenye gari hilo, akasimama na kumtazama vizuri mwanadada huyo ajue kilichomsibu....
*SEHEMU YA 05*❤️
Peter akiwa amesimama mita kadhaa aliliona tukio hilo la mwanadada kuachwa na gari akasimama kumtazama msichana huyo kwa mbali mita kadhaa akiwa hajamwona vizuri akaamua kugeuka kurudi kwenda kumtuliza
"Gerald I hate you, I hate you (nakuchukia, nakuchukia)" Yvonne msichana msomi ambae kwenye maneno yake matano basi moja lazima liwe la Kiingereza aliongea kwa hasira huku akiwa analia, mikono kichwani baada ya kuachwa na mpenzi (boyfriend) wake huyo, na ndipo alipomwona Peter mita kadhaa mbele akija ambae nae pia ni mpenziwe, haraka haraka Yvonne akageuka na kutazama nyuma kabla hajaonwa vizuri na boda boda ilipopita akaisimamisha na kupanda akaondoka haraka haraka na Peter aliyekuwa anamfuata ikabidi asimame baada ya kumwona muhusika amepanda boda boda anaondoka
"Mbona kama namfahamu yule dada ila sijamwona vizuri, ningemsogelea ningemwona" Peter aliguna na kugeuka kurudi kuendelea na safari yake,
Anna alikuwa tayari ameshamaliza kupika amekaa mezani anakula peke yake huku akiwa anatafakari mengi yanayozunguka kwenye kichwa chake, kubwa likiwa ni Elimu au shule aliyoahidiwa na shangazi yake lakini mpaka sasa alikuwa hana matumaini na haoni uelekeo na ndipo Jimmy kaka wa Yvonne nae akaja sebuleni na sahani yake ya chakula akiwa hajakigusa akakiweka mezani huku akimtazama Anna, bado akiwa na hasira na mwanadada huyo baada ya lengo lake la kumtaka kimapenzi kilazima kushindikana, Anna akamtazama kijana huyo bila kumsemesha chochote, Jimmy akaichukua sahani na kuiweka chini sakafuni kisha akamwita paka kwa mruzi, akaja na kuanza chakula hicho kwenye sahani, Anna akamtazama kijana huyo kwa mshangao kwa jinsi anavyokifanya chakula hicho alichoandaliwa, yeye anampa paka
"Jimmy ndo unafanya nini sasa, chakula cha kwako halafu unampa paka?"
"Kwani paka hatakiwi kula Anna?"
"Paka si nimeshampelekea chakula chake tayari, vichwa vya samaki nje kwenye chombo chake?"
"Kwani chakula si umeniandalia mimi mbona kama unanipangia matumizi yake, ni mimi niliyeamua kumpa paka sasa wewe kinachokuuma nini?"
"Lakini huo ni uharibifu wa chakula Jimmy"
"Hata kama, kwani wewe umetoa shilingi tano kwenye chakula mbona inaonekana kinakuuma sana kama vile umechangia kitu?"
"Siyo kuchangia kitu, hata kama lakini kuna watu wanalala njaa kwa kukosa chakula halafu we unachezea namna hiyo hata siyo vizuri mpaka Mungu mwenyewe hapendi"
"Sijisikii kula chakula chako kwanza licha ya hivyo usijifanye mcha Mungu sana kujifanya una huruma na masikini sijui wanalala njaa sijui nini, kalale nao njaa kama unawapenda sana sasa mbona upo kwenye nyumba za watu unawabana bana?" Jimmy alimwambia Anna ambae aliishiwa maneno ya kuzungumza kutokana na majibu ya kijana huyo, akatingisha kichws tu kusikitika na wakati huo huo mlango wa sebuleni ukafunguliwa akaingia Yvonne kwa mwendo mkali bila kumsemesha mtu yeyote akiwa amejawa hasira akapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake, Anna na Jimmy wakabaki wanatazamana tu
"Yvonne amepatwa na nini tena jamani?" Anna alijiuliza
"Fuatilia yanayokuhusu, ya watu achana nayo" Jimmy alimjibu na kuondoka taratibu akimwacha mwanadada huyo peke yake mezani, Anna akashindwa kuvumilia, akatamani kujua kilichomsibu ndugu (binamu) yake huyo akainuka na kuelekea chumbani kwa Yvonne na kumkuta amejitupa kitandani huku amejikunja ameukumbatia mto
"Yvonne, una tatizo lolote?"
"Sihitaji kelele wala kuongea na mtu yeyote kwa sasa waweza kwenda"
"Lakini nilitaka kujua tu labda naweza kukusaidia kiushau..."
"Anna nimesema sihitaji usumbufu wa aina yoyote na sihitaji ushauri wa aina yoyote ile kutoka kwako ama kwa mtu yeyote yule" Yvonne alimgeukia na kumtazama Anna kwa macho yake mekundu kutokana na kulia, Anna akatikisa kichwa na kugeuka kutaka kuondoka lakini akasimama tena na kugeuka
"Aaaam samahani nimesahau kitu, Peter alikuja kukuona muda mfupi tu baada ya wewe kuondoka akasema nikufikishie ujumbe huu kuwa anakusalimia"
"Asante kwa taarifa waweza kutoka sasa"
"Sawa!" Anna alijibu kiunyonge na kutoka chumbani kwa Yvonne ambae alijinyoosha na kuendelea kulala akipunguza hasira alizonazo moyoni kutokana na kutimuliwa kwenye gari la mpenzi (boyfriend) wake, Gerald, na safari yao ya kwenda hotelini ikiishia hapo hapo, safari ambayo aliipania kwelikweli, simu yake ya mkononi ikaita, akatazama namba ilikuwa ni ya rafiki yake mkubwa na wa karibu aitwae Rahma, akapokea na kuiweka sikioni
"Yvonne nakupigia simu muda mrefu hupokei"
"Nilikuwa nimelala, vipi?"
"Eeh umelala tena, kwani safari ya kwenda hotelini na babe imekufa"
"Hamna kuna mambo tu yameingiliana ingiliana"
"Oooh makubwa, mimi nikadhani upo hotelini sasa hivi unakula bata kumbe upo nyumbani, au kaku..."
"Rahma hayakuhusu, ongea kingine kilichokufanya unipigie"
"Hamna nilikuwa nakusalimia tu mwenzangu..." Rahma aliongea na vikasikika vicheko vya wasichana wengine wakionekana wapo nae wanasikiliza umbea, Yvonne akakasirika na kumkatia simu baada ya kujua anachekwa na marafiki zake hao....
Upande wa pili Gerald alikuwa bado yupo kwenye gari anarejea nyumbani kwao, simu yake ya mkononi ikaita akapokea na kuiweka sikioni
"Naam naam damu yangu" aliongea kwa mbwembwe
"Vipi mtoto Yvonne mmeshamalizana hotelini?" rafiki yake huyo alimwuliza
"Hotelini wapi, mimi nina hela hiyo ya kumpeleka demu hotelini, nimemla kwenye gari kwisha habari sasa hivi narudi zangu home mwepesi, hotelini ilikuwa gia tu ya kumnasa ndege kwenye mtego aingie mazima"
"Duh siyo poa mzee, sasa kaka yangu ameshaanza kuliulizia gari lake harakisha Gerald ulirudishe gari hilo kabla hajagundua kuwa nimekuazima, usiniponze damu yangu"
"Usijali kaka nakuja na gari la bro wako, mishe yangu nimeshamaliza ya kumla mtoto anayependa watu wenye maisha mazuri, Yvonne, gari tu limeshamchanganya mpaka sasa anajua ni la kwangu hahaha!" Gerald alucheka kwa furaha huku akiwa amefungulia muziki mkubwa kwenye gari na ndipo macho yake yalipomwona mwanadada mrembo anatembea kando kando ya barabara, Gerald akatoa macho akiwa na simu sikioni
"Oya G mbona kimya?" rafiki yake aliita upande wa pili wa simu
"Ngoja mwanangu kuna pisi kali nimeiona hapa" alimjibu na kumkatia simu akakunja kona haraka kutaka kulitoa gari barabarani na ndipo piki piki iliyokuwa pembeni kwenye mwendo ambayo hakuiona ikampigia honi na kuja kujibamiza ubavuni mwa gari hilo, Gerald akafunga breki na kusimamisha gari baada ya kusababisha ajali, haraka haraka akashuka kwenye gari na kuangalia ubavuni akikuta gari limebonyea,
"Dah huu msala nimeshaharibu gari la watu nitamweleza nini rafiki yangu?" alijishika kichwa akisikitika mwenyewe huku askari akija na watu wengine kutazama madhara ya ajali hiyo ya barabarani.....
ITAENDELEA.......
Tags
simulizi