SIRI YA NDOA YANGU
Queen Lizzie
*SEHEMU YA KWANZA*
Anaonekana mwanamke mmoja akitembea pembezoni mwa barabara iliyoko pembezoni mwa msitu wa shinyanga,akiwa peku tena amevalia nguo zilizochakaa Sana,alikua na makadirio ya miaka 30 mpaka 32..
Ni barabara iliyokimya sana,na ni mara chache sana kuona watembea kwa miguu wakipita kwenye barabara hio kwani ni barabara inayotisha sana kutokana na ukimya wake.
Lakini mwanamke huyo hakuonesha kuogopa wala kujali yliotawala katika barabara hio.
Alikua anaonekana mwenye mawazo sana na akilia kilio cha kimya kimya...
Ghafla ikapita gari aina ya macdez benz,Ilimpita na kufika mbele kidogo kisha ikarudi nyuma mpaka alipokuwepo mwanamke yule na kusimama.
Akashuka mwanaume mrefu mwenye weusi wa wastani na kusema"angel ni wewe"
Mwanamke yule hakujibu vhochote aliendelea kutembea bila kujali kama anasemeshwa.
Kijana yule alionesha kumfahamu yule mwanamke na kumuomba apande kwenye gari amueleze amepatwa na nini.
Mwanamke yule hakujibu chochote akaendelea kutembea huku akiwa anajifuta machozi.
Kijana yule aliamua kutumia nguvu i ilikumuingiza yule mwanamke aliemtambua kwa jina la Angel kwenye gari lake.
Ila mwanamke yule hakutaka kuingia kwenye gari na kuanza kuleta vurugu kana kwamba anataka aachwe pale alipokutwa lakin hakuweza kushindana na mwanaume hivyo kijana yule alifanikiwa kumuingiza kwenye gari lake na mwanamke yule alietambulika kwa jina la Angel akaendelea kulia.
Ukimya ulitawala ndani ya gari huku kikisikika kilio cha chini chini kutoka kwa mwanadada Angel.
Kijana yule aliendesha gari lake mpaka nyumban kwake maeneo ya buzuruga Mwanza na kumkaribisha Angel kwenye chumba cha wageni ili walau ajifanyie usafi,na yeye kuandaa chakula kwa ajili ya mgeni wake.
Yule kijana alimaliza kuandaa chakula na kutoka kwenda dukani kununua vinywaji..
Aliporudi alitegemea kumkuta Angel ameshamaliza kuoga lakin haikuwa Kama anavyofikiria.
Alikaa ukumbini kumsubiri Angel atoke Ila hakutoka na hali hio ilianza kumpa wasiwasi kijana yule na kuamua kwenda chumba alichomkaribisha kuangalia anatatizo gani..
Alifika na kugonga hodi kwenye chumba alichomkaribisha mgeni wake lakin hakuitikiwa ikabidi ajaribu kunyonga kitasa cha mlango na bahati nzuri mlango ulikuwa wazi.
Alipoingia alikutana na karatasi mlangon.
Mwanzo alitaka kuipuuzia lakin akili yake ikamtuma aokote na kutizama.
Alikutana na ujumbe unaosema"Alphonce nashukuru kwa kunisaidia ila mimi sistahili kuishi maana maisha yangu ni aibu kubwa kwenye jamii,ungeniacha kule uliponikuta,bora ungeniacha niliwe na wanyama wa kali au nigongwe na gari kuliko kuendelea kuishi maana naweza Kuleta laana kwenye maisha yako..
Mara ghafla akasikia mtu anakoroma kutoka bafuni,Ikabidi akaangalie kuna nini.
Alipofika kwenye mlango wa bafu alipokelewa na alama za damu zilizotapakaa kwenye bafu zima na Angel alikua kazimia kwa kunikata mshipa mkuu wa mkononi mwake.
*SEHEMU YA PILI*
Alipofika kwenye mlango wa bafu alipokelewa na alama za damu zilizotapakaa kwenye bafu zima na Angel alikua kazimia kwa kunikata mshipa mkuu wa mkononi mwake....
Songa nayo...................
Alphonce alumuwaisha hospitali Angel na kwa bahat mbaya hawakutaka kumpokea bila kibali kutoka polisi maana ilionekana ni kesi ya kutaka kujiua.
Alphonce aliwaomba sana madaktar walau wampatie huduma ya kwanza,Walikataa kata kata ikabidi atoe pesa kidogo kama rushwa kwa madaktari ili wampatie huduma ya kwanza Angel yeye akiaendelea kufuatilia pf3..
Alphonce alitoka hospital mara baada ya Angel kupokelewa na kwenda kufuatilia kibali kutoka polis I.
Aliporud alikuta Angel kashapewa huduma ya kwanza ingawa hakuwa amepata fahamu.
Angel alikaa hospitali kwa siku nne bila kufungua macho.
Siku moja mchana Alphonce alienda kuangalia hali ya Angel,alipewa ruhusa ya kwenda kumuona na kumkuta anaweweseka na akiongea kwa sauti ya chini sana ambayo Alphonce hakuisikia.
Ikabidi Alphonce amsogelee Angel na kumsikiliza anaongea nini,alisikia akisema"usiniue..usiniue ...nitafanya utakavyo naomba usiniue mume wangu,Alafu akafungua macho huku akiwa anahema kwa kasi sana kana kwamba ametoka mbio ndefu.
Alphonce alikimbia na kutoka nje kuwaita wauguzi na kuwaambia mgonjwa amegungua macho waje wamuangalie.
Wauguzi walipofika chumba alichokua Angel wakamuomba Alphonce atoke ili waendelee na matibabu.
Baada ya dakika kadhaa Daktar alitoka na kumuomba Alphonce aende ofisini kwake.
Baada ya Alphonce kufika offisin kwa Daktar mazungumzo yao yakaanza.
Mgonjwa wako anaonesha anamsongo mkubwa wa mawazo na presha yake iko juu sana hivyo tunakuomba usije ukamkumbusha jambo lolote lililopita katika maisha yake,alisema Daktari.
sawa Docta nitafanya kama ulivyoniagiza,akajibu Alphonce.
Na zaidi usimpe vyakula vyenye mafuta,wala vyenye chumvi nyingi anaweza kupata strock,akaendelea kusema Daktari.
Sawa nitajitahid akajibu Alphonce.
Baada ya siku kadhaa Angel aliruhusiwa kurudi nyumban maana hali yake ilitengamaa kwa kiasi fulani.
Alphonce alimchukua na kurudi nae nyumban kwake.
Walipofika walimkuta binti wa kama miaka 24 akifanya usafi.
Alphonce alimkaribisha Angel na kuanza utambulisho.
Angel huyu ni mtu wangu wa karibu Sana anaitwa Glory.
Glory huyu ndie yule mgonjwa niliekuambia anaitwa Angel.
Glory akasimama kwenda kumpa mkono Angel lakin cha ajabu Angel akasimama na kwenda kwenye chumba Alichokaribishwa mara ya kwanza na kuwaacha wenyeji wake kwwnye mshangao.
Akaingia na kujifungia kwa ndani.
*SEHEMU YA TATU*
Glory akasimama kwenda kumpa mkono Angel lakin cha ajabu Angel akasimama na kwenda kwenye chumba Alichokaribishwa mara ya kwanza na kuwaacha wenyeji wake kwwnye mshangao.
Akaingia na kujifungia kwa ndani......................
Songa nayo...................
Mbona kama anahasira,aliuliza glory kumuuliza Alphonce.
Au ndo umeniletea mke mwenzangu akaendelea kulalamika Glory kwa sauti ya kiwivu kidogo.
Alphonce akamsogelea Glory na kumshika kiuno kisha akasema"Sijawah kumpenda mwanamke kama ninavyokupenda ww Glory wangu,acha wivu basi unanihuzunisha".
OK Mr A wangu twende tukale Ila nataman sana kujua kuhusu huyu mwanamke,akasema Glory.
Anaitwa Angel,ni mwanamke ambae tulikuwa pamoja kwa maana tyliishi mtaa mmoja na kusoma shule moja,alisema Alphonce mara baada ya kumaliza kula.
Alikuwa rafiki yangu sana,tulitengana kipindi tunaenda Advance.
Mm nilibaki hapahapa mwanza yeye akachaguliwa kujiunga na shule ya Bagamoyo mkoani pwani.
Ila pia urafiki wetu haukuisha,akaendelea kusimulia Alphonce.
Kwa bahati nzuri tukachaguliwa chuo kimoja cha Mzumbe yeye alikua anasomea sheria mimi nilikuwa pharmacy.
Urafiki wetu uliendelea kukua na alikua mtu wangu wa karibu sana,na kwa kipindi kile alikua binti mrembo sana ambae wanaume wengi walimtaman na kunishangaa mimi na kuwaje na ukaribu na mwanamke mzuri halafu sina mahusiano nae.
Ukweli nilishaanza kumtaman ila kutokana na namna tulivyokuwa tukiheshimiana niliogopa kuongelea swala la mapenzi na yeye maana niliogopa asije akanichukia,akaendelea kusema Alphonce.
Kwa hio bado unampenda akauliza Glory kwa sauti ya wivu kidogo.
Acha basi mrembo wangu,nitampendaje wakati nipo na ww malaika wangu,akasema Alphonce kwa sauti ya kubembeleza kidogo.
Siku moja alikuja akanambia anataka kuacha chuo maana amepata mchumba wa kimoroko ambae anampa kila anachokitaka na anamimba yake,nilimsihi sana asiache chuo kwa maana alikua yupo mwaka wa Mwisho Ila hakuonesha kunielewa na mwezi mmoja baadae akasafiri na huyo mpenzi wake na sijawah kumuona tena wala kupata taarifa zake mpka siku ile niliyomuokota,akaendelea kusema Alphonce.
Nakupenda sana naomba usije ukampenda mtu mwingine zaid yangu,alisema Glory wakati ameenda kujipakatisha kwenye mapaja ya Alphonce huku akiwa anachezea ndevu zake.
Wakaanza michezo ya kimahaba pale pale kwenye kochi mpka walipoamua kukokotana mpka chumban ambako wangepeana burudani kwa kujiachia.
Angel alienda kukaa pale walipotoka Glory na Alphonce na kuanza kulia huku akisema"kwa nn hukuniambia kama unanipenda Alphonce huenda leo nisingeishi ndoa ya mateso,ndoa iliyotawaliwa na siri nyingi,Alphonce...Alphonce rudi tena kwangu nataman niishi maisha ya ndoa yenye furaha".
*SEHEMU YA NNE*
Wakaanza michezo ya kimahaba pale pale kwenye kochi mpka walipoamua kukokotana mpka chumban ambako wangepeana burudani kwa kujiachia.
Angel alienda kukaa pale walipotoka Glory na Alphonce na kuanza kulia huku akisema"kwa nn hukuniambia kama unanipenda Alphonce huenda leo nisingeishi ndoa ya mateso,ndoa iliyotawaliwa na siri nyingi,Alphonce...Alphonce rudi tena kwangu nataman niishi maisha ya ndoa yenye furaha".
Songa nayo.................
Siku hio ilipita hatimae pakapambazuka,Glory hakuwa mke wa Alphonce Ila walikuwa wachumba tu na alikua kaaga kwao kuwa amekuja kutafuta kazi mkoan Mwanza kwani alimaliza chuo mwaka mmoja nyuma na kuondoka kwao mkoan Dar es salam.
Glory aliamka wa kwanza na kuanza kumuandalia Alphonce kifungua kinywa ili awahi kazin.
Alimkuta Angel akiwa nje amekaa.
Ilikua asubuhi sana,alishangaa kwa nn ameamka mapema kias kile na kumsogelea walau amsalimie lakin Angel hakuoneshwa kufurahi kusalimiana na Glory akainuka na kuelekea chumban.
Glory alishangaa ila hakutaka kuuliza.
Alimuandaa Alphonce na kuanza kumsindikiza kuelekea kwenye gari.
Lakin kabla hawajatoka mlangon.
Angel alitoka chumban kwake na kumfata Alphonce na kumkumbatia kisha akaanza kumtengenezea shati lake vizur na kusema"usichelewe Kurud mpenzi nataman kuongea mengi na ww"Alphonce na Glory walibaki wakimshangaa maana n kama hakutegemea.
Glory alijiskia vibaya na kuwaacha Alphonce na Angel wakiwa wanatazamana na kukimbilia chumban kwao na kuanza kulia kwa kuhisi Alphonce amemleta Mke mwwnzake na kusingizia anamsaidia.
Unafanya nn ww,Alifoka Alphonce kumuambia Angel.
Kwan nimefanya kosa,siulikua unanipenda?akajibu Angel kwa sauti ya kujidekeza.
Alphonce aliachia msonyo na kuelekea chumban kumuangalia Glory.Glory alikua akilia,na kuanza kumbembeleza na kumueleza kuwa hakuwa na mahusiano yoyote na Angel.
Alimbembeleza sana,Mwisho Glory alimuelewa na Alphonce kumuacha kuelekea kazin.
Visa vilizidi kwa Angel kumfanyia Glory.
Glory hakuwa na aman kabisa ila aliamua kumvumilia na kumchukulia kama mgeni tu.
Siku zilienda na visa vya Angel vilizidi kiasi cha kumtaka Glory aondoke kwenye nyumba ya Alphonce akidai Alphonce n mpenzi wake na hataki Glory aharibu mahusiano yake na Alphonce.kumbe siku hio Alphonce aliwah kurudi hivyo aliyasikia matambo ya Angel.
Akaingia ndani Angel akamkimbilia na kumuambia"pole na kazi mume wangu"Alphonce alimtoa mwilin mwake na kumsukuma pemben ambapo Angel alijifanya kazimia.
Hakumjali sana maana alishachoshwa na vitimbi vyake na kumfuata Glory.
Angel alipoona hafatilizwi akaamka na kwenda chumbani kwake kwa hasira.
Siku hio ilipita hatimae kukapambazuka.
Glory aliamka mapema kama kawaida yake lakin siku hio hakumuona Angel akahisi labda kalala akaanda kifungua kinywa na kumuandaa Alphonce.
Alphonce alipomaliza kujiandaa hakumuona Angel 'na hakutaka kuuliza na kuhisi kalala.
Hakutaka kumuamsha ilikukwepa kero zake.
Alienda kazin na mida ya saa nne asubuhi alipigiwa simu na mtu aliejitambulisha kama polisi na kumtuhumu kwa kesi ya mauwaji yeye pamoja na mpenzi wake.
Alphonce alishangaa sana.
Ikabidi aombe ruhusa arudi nyumban kwake kuangalia hali upoje.
Alikutana na Askari wamezingira nyumba yake na mpenzi wake Glory katiwa pingu.
Aliingia nyumban kwake na kuwakuta maaskari kama wakikusanya ushahidi.
Askari mmoja akasema kuwa alipigiwa simu na mwanamke asiye mfahamu na kumuambia kuwa yeye Alphonce pamoja na mpenzi wake wanataka kumuuwa kwa kumtoa kafara ili apandishwe cheo.
Alphonce akashangaa sana.
Akaingia chumban kwa Angel na kukta damu imetapakaa chumba kizima.
Askari hawakutaka kusikiliza maelezo yoyote ya Alphonce na kumkamata ili kuelekea kituoni.
Muda wote Glory alikua akilia tu.
*SEHEMU YA TANO*
Askari hawakutaka kusikiliza maelezo yoyote ya Alphonce na kumkamata ili kuelekea kituoni.
Muda wote Glory alikua akilia tu.
Songa nayo......................
Walifikishwa mahabusu,kesi ilienda haraka haraka sana,maana hta wakili wa Alphonce hakupewa nafasi ya kutosha kumtetea Alphonce na Glory.
Miezi mitatu baadae walihukumiwa k8fungo cha maisha jela.
Wazaz wa glory walilia sana,wakataman binti yao angefanya mambo yaliyompeleka mwanza na sio kuishia kwenye mapenzi Ila ndo hivyo hawakuwa na namna nyingine ya kumnusuru binti yao.
Siku zilienda maisha ya magereza yalianza kati ya Alphonce na Glory,hawakuweza kuonana hata kidogo Kutokana na sheria za gereza.
Walipokelewa na wababe wa gereza kama ilivyokawaida kwa mgeni yoyote anayeingia magereza.
Yalikua n maisha ya mateso sana ambayo sio Alphonce wala Angel aliyazoea.
Siku moja ilkuwa n siku ya kutembelea wafungwa alikuja mwanamama mmoja na kuomba Kuonana na Alphonce.
Alphonce alifika na kukutana na yule mwanamama.
Hakuwa anamfahamu ila hakutaka kuuliza sana maana alijua fika kuna sababu ya yeye kutaka kumuona.
Ujambo kijana,alianza kusalimia mwanamama yule kumsalimia Alphonce.
Sijambo shikamoo,akaitikia Alphonce kwa heshima.
Mwanamama yule akaangalia kushoto na kulia kama kuna mtu anawatazama na kumpitishumia kijibomba kidogo Alphonce kwenye nyavu za gereza na kumuambia lazima utoke huku.
Alphonce alishangaa na kutaka kuuliza maswali zaidi ila yule mwanamama alishaondoka.
Alphonce alirud kwenye chumba ambacho anaishi na wafungwa wenzake na kuanza kukikagua kile kibomba ndipo alipokutana na karatasi dogo ndani ya lile bomba.
Akakitoa na kuanza kukisoma kiliandikwa hivi"Nisamehe Alphonce najua ww n mtu mwema ila nimefanya hivi kwa ajili ya wanangu,Angel"Alphonce alitaman kutoa tusi maana alijua kuwa kweli Angel kafariki kumbe kuna mchezo ulikua unachezwa.
Hakujua Kama anauadui na mtu yoyote katika maisha yake.
Hakujua n kwanini Angel kamfanyia vile na nani yupo nyuma yake,alijiuliza maswali mengi bila kupata majibu.
Mara ghafla mpango wa sero aliyekuwepo kuafunguliwa na kuingia Askari mmoja aliekuja kumuita Alphonce.
Alphonce alitoka na kuongozana nae.
Walitoka mpaka kwenye nyumba za askari magereza na kuingia ndani.
Alimkuta Daktar mkuu wake wa hospital aliyekuwa anafanyia kazi.
Alishangaa kidogo lakin alijua amekuja kumsalimia tu.
Najua unashangazwa na ujio Wangu ila tule kwanza.
Vikaletwa vyakula vya aina mbalimbali,wakala.
Mpenzi wako ameshatoka Ila kukutoa ww kuna kazi kidogo,alianza kusema yule daktar.
Huu n mchezo na alie ucheza namjua maana ulikua unatakiwa kupandishwa cheo mwezi huu,cheo kikubwa sana kutokana na utendaji wako ila kunabaadhi ya watu wakahisi wanastahili wao zaidi kuliko ww,hivyo ni lazima utoke ukazungumze na mwenye hospitali kisha tutajua tunakusaidiaje maana alikuwa anakuamin Sana na Mara baada ya wewe kuhukumiwa iman yake kwako imepotea kabisa,Hivyo lazima utoke maana yeye pekee ndio wakukusaidia,alisema Daktar.
Nitatokaje,akauliza Alphonce.
Daktar akamsogelea na kumnong'oneza jambo.
Alphonce alionesha kushtuka kidogo kisha akaonesha kukubaliana na daktar aliekuja kumtembelea.
Full ni 1000
Wasiliana Nami kupitia Whatsapp
Ama Andika nahitaji kwenye comment hapo chini
Tags
simulizi