TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

JE Ni NAMNA GANI NINAWEZA KUTAWALA VEMA MATUMIZI YA MUDA WANGU

JE Ni NAMNA GANI NINAWEZA KUTAWALA VEMA MATUMIZI YA MUDA WANGU
________________________

Sote tumekuwa na muda wa kutosha kabisa wa kutuwezesha tuishi maisha yenye mafanikio! Cha ajabu na kinachosikitisha zaidi wengi wetu tumeshindwa kuyafikia mafanikio hayo kutokana na kushindwa kuutumia vyema muda wetu!  
Ukifanya upembuzi yakinifu utagundua kwamba wengi wetu tupo nyuma ya muda!

Kwa mfano kwa siku ya leo sote tumepewa muda sawa, ambayo ni masaa 24, lakini kila mtu alivyotumia masaa hayo anajua yeye!
Ukija kwangu mimi nimetumia baadhi ya muda kwenye hayo masaa 24, kukuandikia wewe ujumbe kuhusu namna ya kutumia muda wako kwa usahihi!

Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba, unahitaji kujitawala mwenyewe ili uweze kutumia muda wako kwa ufasaha!
Zifuatazo ni mbinu zitakazokusaidia ili uweze kutumia muda wako kwa ufasaha: 

1. Anza na Mungu kwanza: (Labda uwe huamini katika Mungu, na ninakupa pole sana Kama huamini katika Mungu!)

Njia nzuri ya kwako wewe kutumia muda wako ni kupitia kuanza na Mungu kwanza!
Tenga muda wa kusali 
ukimuomba Mungu kibali cha kukuongoza kwa siku nzima!

Sasa kama haunzi na Mungu unaanza na nani?
Na kama hautaki Mungu akuongoze unataka kumaanisha ni nani atakayekulinda na kukuongoza kwa siku nzima?

Au unataka kumaanisha kwamba unatumaini kuongozwa na akili pamoja na njia zako mwenyewe zilizo na ukomo?

Ndugu mpe Mungu nafasi katika maisha yako ndipo utajikuta ukitumia muda wako vema!

Yaani hakikisha: kila siku unaanza na Mungu, kila mwezi unaanza na Mungu, kila mwaka unaanza na Mungu!

Anza siku Yako kwa kusali, kusoma biblia pamoja na kujikabidhi kwa Mungu ili aongoze hatua zako!
Kumbuka ukianza na Mungu atakuangazia roho wake, hivyo kwa muda wote utajikuta ukifanya mambo yenye tija tu hali itakayokufanya utumie muda wako vizuri!
Ndugu Tenga angalau saa moja kwa siku kwa ajili ya kuongea na Muumba!

2. Kuwa na orodha ya vipaumbele unavyotaka kuvitekeleza!

Ili kutumia muda vizuri ni lazima uwe na orodha kamili juu ya masuala yote ambayo unataka uyatekeleze kwa kipindi fulani cha muda!
Pia, unatakiwa uweke bayana juu ya jambo lipi linatakiwa lianze kutekelezwa likifuatiwa na jambo!
Unatakiwa kujua kwamba ukiweza kuweka bayana masuala yanayohitaji utekelezwaji, utajikuta ukizingatia muda wako automatiki! 
Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba ukiwa na vipaumbele vya kutekeleza hutokuwa mtu wa kufanya kila jambo litakaloibuka mbele ya safari ambalo linaweza kukupotezea muda!
Kumbuka ukiwa hauna utaratibu wa kuweka bayana vipaumbele vyako, utakuwa ni mtu wa kufanya kila jambo litakaloibuka hata kama hukulipanga kabisa hali itakayokufanya upoteze muda wako!

3. Tumia kanuni ya 24 kwa tatu:
Hii imekaaje? Ok usijalii fanya hivi!
Chukua 24 gawanya Kwa tatu, bila shaka utapata masaa nane yaliyopo kwenye makundi matatu!

Kundi la kwanza la masaa nane ni muda maalumu wa kulala!

Unatakiwa kujua kwamba ni muhimu kulala kwani, kisaikolojia kulala ni hitaji la msingi la kila mtu! Hata hivyo sote huwa tunalala ili Mungu awasiliane na sisi, kumbuka Mungu huwasiliana nasi usiku tukiwa tumelala!

Kundi pili la masaa nane ni muda maalumu wa kwenda kazini! 
 Hapa ndipo wale wafanyakazi wa ofisini huenda kazini, wanafunzi nao huenda shuleni, watu wengine huenda kwenye shughuli zao za hapa na pale hata hivyo wafanyabiashara nao hutumia muda huu, kufanya biashara zao.

Kundi la tatu la masaa nane,
Ni muda maalumu ambao hutumika kiupotevu!

Huenda hayo makundi mawili ya massa nane yamekubana sana mpaka umekosa muda wa kujiandaa!

Basi tutoe masaa mawali kwenye kundi la tatu la masaa nane! 

Bila shaka utapata masaa sita! Je huwa unafanya nini ha haya masaa sita!
Nakualika tena huw unatumia haya masaa sita kufanyia nini?
Utashangaa mtu anakwabia hana muda kumbe ana muda wa kutosha tu,  na mwingine unabaki hadi kubaki.
Asijue kuwa tatizo siyo muda, bali tatizo ni yeye kwani hajui jinsi ya kupangilia muda wako!
Unatakiwa kujua kwamba muda upo wa kutosha tu! Ukitaka kutumia vyema muda wako nakualika utumie kanuni hii! 

4. Epuka tabia ya kughairisha mambo:
Kughairisha mambo ni mwizi hatarii sana wa muda!

Utamsikia mtu akisema, hili jambo nitalifanya kesho!
Ndugu kwani unasubiri kesho ipi? Kwani leo si ndiyo ile kesho uliyoisema jana, au kuna kesho ipi Tena unayoisubiri?

Mpendwa kwanini ulisukumie leo suala unalotakiwa kulifanya leo?

Au, unataka kumaanisha wahenga waliosema "linalowezekana leo lisingoje kesho" walikuwa ni wapumbavu?

Kwanza unaposema jambo fulani utafanya kesho, ni nani aliyekwambia hiyo kesho utaifikia? 
Vipi kama kesho itakuja na lake? 
Na vipi kama hiyo kesho itasogezwa na kuwa kesho nyingine tena?

Mpenzi msomaji epuka kuwa mr tomorrow and Mrs tomorrow!

Unatakiwa ufanye leo linalopaswa lifanywe Leo!
Leo ndiyo leo asemaye kesho ni muongo!

Unatakiwa kujua kwamba tofauti iliyopo kati ya waliofanikiwa na wasiofanikiwa haipo kwenye maarifa, ujuzi au kiwango cha elimu, bali ipo kwenye namna ya kujua afanye kipi na lini! Pasipo kughairisha!

5. Epuka wezi wa muda wako:

Kuna watu wengine huwa wanakuja kukupotezea muda mara baada ya wao kumaliza majukumu yao, waepuke watu hao kama ukoma!
Unakuta mtu anakuja ofisini kwako, akiwa hana shida iliyomleta hapo. Mwisho wa siku ataishia  kuanza kukupigisha stori ambazo hazihusiani na masuala ya kiofisi!  Huyo ni mwizi wa Muda wako mwepuke.

Hata hivyo wezi wengine wa muda wako wanaweza kuwa:
✔️Vikao visivyokuwa kuwa na kichwa wala mkia!
✔️Kuchati muda wa kazi!
Simu zisizohusiana na masuala ya kiofisi!
✔️Kuangalia sana TV
kulala sana pamoja na kukaa tu pasipo kujishughulisha na chochote kile!

Ndugu unatakiwa uwe macho, usikubali Tena mtu akuubie muda wako wa thamani uliopewa na Muumba!

Kumbuka unahitaji kujitawala mwenyewe ili uweze kutumia muda wako vyema!
Jifunze kukomboa wakati!

Na, huo ndiyo mwisho wa somo la leo!
Kesho nitakuja na mbinu nyingine Zitakazokusaidia ili uweze kutumia muda wako vizuri!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwalimu, mwandishi muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!

Unaweza ukawasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post