KISA CHA KUSISIMUA HUSNA 01.
Ilikuwa asubuhi nikiwa ndani nikiwa nimekaa chumbani ambako nilikuwa nikilala pamoja na dada yangu binamu mtoto wa shangazi yangu aitwaye Neema.
Tulikuwa tunakaa nyumba ya familia upande wa baba hivyo Shangazi yangu mkubwa na baba ndio watu wenye mamlaka ndani ya nyumba hiyo mama yangu hakuwa chochote maana hakuna aliyekuwa anamsikiliza hata kama ataongea point ni lazima atapingwa tu.. Hali hiyo ilikuwa inaniumiza sana nilijikuta namchukia shangazi na baba kupita maelezo maana licha ya kutokuwa kitu kwao pia walikuwa wanamtegemea yeye kuhusu kula alikuwa anaangaika usiku na mchana alishe familia nzima.
"Weeeee... Husna ebu njoo mara moja. Ilikuwa ni sauti ya baba ikifoka nje nilitoka haraka kumfata alipo nilipiga magoti mbele yake kama ilivyo kawaida yangu tabia hii nimeipata kutoka kwa mama yangu mara nyingi hufanya hivyo pindi aitwapo na baba au shangazi mkubwa..
"Ebu taja namba yako ya mtihani majibu yameshatoka.. Sasa hapa ndio nitajua kama ulikuwa unasoma au umalaya ndio uliokupeleka shule.. Alisema baba maneno makali yaliyozidisha hofu niliyoyanayo maana sikuwa na uhakika wa kufaulu kabisa licha ya kuwa nilikuwa nikijitahidi kusoma kwa mda mchache ninaoupata baada ya kumaliza kazi za nyumbani..
"Ina maana hunisikii au ndio kiburi kama mama yako.. Yalikuwa ni maneno yaliyonikurupua kwenye dimbwi la mawazo na kutaja namba zangu za Necta.
Baada ya sekunde kadhaa baba sijui alikuwa ameshayaona matokeo yangu au laa maana nilishtukia nimepokea kibao cha uso kilichofanya nianguke chini kama mzigo..
"Nilijua tu haya ndio matokeo yake... Unaweza kunambia ulikuwa unaenda kufanya nini shule.. Alisema baba huku akininyanyua pale chini kwa kunikuda hakuniacha hivyo hivyo alinipa tena kibao kingine nilishindwa kujizuia tena vilibao viliniingia balabala na kufanya nianze kulia kilio cha kwikwi..
"Sio hivyo baba mitihani ilikuwa migumu.. Mazingira pia yamechangia mimi kufeli... Nilijitetea kwa kutumia ukweli.
"Yaani utalipa gharama zangu zote nilizotumia.. Mtoto mpuuzi kweli ona watoto wa mzee Mneka walivyo na akili lakini sio wewe... Alilalamika baba ambaye hakuwa anahusika na chochote tangu naanza shule mpaka namaliza Mama yangu ndio alikuwa akijinyima ili nipate kusoma pia hata kuhusu kula ilikuwa hivyo hivyo mama ndio uangaika kuilisha familia.
Baba aliondoka bila kunambia matokeo yangu na kuniacha peke yangu maana hata Mama na Shangazi hawakuwepo kwa wakati huo..
Mda wa jioni mama alirudi na kunikuta nikilia alinikimbilia nishindwa kujizuia niliongeza kilio mara dufu na kusema kwa kwikwi..
"Mama naomba nionyeshe baba yangu... Huyu sio baba yangu... Huyu sio.
Bado nilikuwa nikilia mda wote mama alikuwa akinibembeleza baada ya mda nilitulia maana niliona mama akiwa na huzuni kuliko kawaida nilijiona mkosaji..
"Nisamehe Mama.. Usiwaze sana Mama yangu.. Nilisema kwa upole huku nikiwa mapajani kwake nilipoa kwasababu mama anamatatizo ya presha hivyo akiwa mawazo huwa anazimia na hiyo hali umtokeaga mara kwa mara..
Tukiwa pale chini kabla mama hajasema chochote tulisikia makofi yakipigwa sote tuligeuka kuangalia alikuwa ni shangazi mkubwa Batuli..
"Vizuri sana naona unampongeza mwanao... Mwanamke huna akili wewe yaani mtoto kafeli kwasababu ya umalaya harafu unajifanya umemkumbata mapajani..
Mama alijinyanyua pale chini na kusema huku akimtazama shangazi "Husna wangu hawezi kufeli na hajawahi kufeli huwa anatembea na baraka zangu popote aendapo.. Alisema mama kwa ujasiri niliinamia chini kwa aibu maneno ya mama yalifanya nijione mkosefu amenipambania sana na ana imani na mimi kuliko kawaida harafu nije kumpa taarifa nimefeli atalipokeaje..
"Husna Mama eti matokeo yametoka!?.. Umepata wastani gani mama.. Aliuliza mama mfululizo tena kama mtu aliyechanganyikiwa sikumjibu machozi yalishatawala usoni mwangu..
"Atakujibu nini huyo.. Ni amefeli na humu ndani sitaki kumuona na kama utamuonea huruma muondoke wote nisiwaone kabisa................
HUSNA 02.
Atakujibu nini huyo.. Ni amefeli na humu ndani sitaki kumuona na kama utamuonea huruma muondoke wote nisiwaone kabisa..
Alisema shangazi huku akiingia chumbani napolala alitoa furushi langu la nguo na kulitupia sebreni kisha akasogea tulipo na kusema.
"Aya wee mtu mzima ovyo utabaki au utaongozana na hilo toi lako!?..
Alimuuliza mama huku akiwa ameshikilia kiuno chake sikusubiri mama ajibu nilinyanyuka hadi chumbani kwa Mama nilitoa begi lake la nguo na kutoka nalo sebreni nilikuwa nikimtazama shangazi kwa hasira mno.
"Mama tuondoke nimeshindwa kuvumilia aya manyanyaso.
Mama alinitazama kwa huruma kisha akasema "Hatuwezi kwenda popote wewe na mimi tutabaki hapa siku zote za uhai wetu.
Nilishtuka hata shangazi hakufurahishwa na hiyo kauli alisogea alipo Mama na kuanza kufoka.. "Wewe mwanga tumeshakuchoka hakuna hata anayekutaka humu ndani.. Nifanye nini mpaka ujue kama nakuchukia nikuwekee sumu eh.
Nilisogea karibu ya shangazi na kusema "Usimwambie maneno makali mama yangu kama uona kutuwekea sumu ndio suluhisho anza na mimi.
Alinisukumiza na kufanya nianguke chini "Umeota mbawa wewe mtoto wa kahaba.. umekuja nakuona umenyorodoka tumekulea umeshaanza kuwajua wanaume unaanza kujibishana na mimi.
Nilibaki pale chini nikijiwazia mengi sikuwa na nguvu ya kufanya chochote hadi nilikuwa natamani nife uenda nitaenda kupumzika na haya manyanyaso ya waziwazi nilijivuta alipo Mama.
"Mama embu tuondoke.. Si unaona shangazi hatutaki, ametufukuza tuondoke.
Niliona Mama akinyanyuka aliokota begi lake nilijua amekubali tuondoke lakini haikuwa hivyo alilibuluza na kuingia nalo chumbani kwake nililia sana tena zaidi ya sana
Nilishikwa na uchungu kwanini sasa Mama anang'ang'ania kubaki ndani ya nyumba yenye manyanyaso kila siku nilishindwa nifanye nini binti mdogo mimi nisingeweza kuondoka na kumuacha Mama yangu nilipaza sauti na kusema kwa hasira.
"Nambie basi kuhusu baba yangu mzazi.. Huyu siye, hakuwahi kunipenda hata kwa sekunde..
Mama hakunijibu aliingia ndani kwake nilibaki na Shangazi pale sebreni alikuwa akinitazama kwa jicho la chuki nilikamata mafurushi yangu niliyaingiza ndani lakini shangazi alinifata.
"Kateke maji kisimani mwanangu atarudi shule sasa hivi aje kuoga..
Nitoka mule ndani bila kumsemesha nilienda kuchota maji kisimani nikiwa huko nilikutana na Somoe ni rafiki yangu tulikuwa tunasoma dalasa moja nilitamani kujificha maana nilijua fika yeye atakuwa amefaulu.
Nilishangaa ananipa hongera, ni ya nini nilimuuliza huku nikiwa makini kumsikiliza.
"Umejitahidi sana kwani hujaenda kuangalia matokeo. Niliacha ndoo langu pale chini na kukimbilia shule sikutaka kuendelea kumsikiliza zaidi nilifika shuleni wanafunzi walikuwa wengi sana wakitazama matokeo tena mengine yalishaanza kuchanwa niliangalia namba yangu nilitabasamu nilipata division two nilirudi nyumbani nikiwa nafuraha nilisahau hata kwenda kufata ndoo yangu kisimani nilipokelewa na macho ya Shangazi akiwa amesimama mlangoni..
"Naona ndio unarudi sasa hivi kiboss na ndoo ukaiacha hukohuko.
Alisema huku akijiandaa kunikamata anivute masikio yangu nilimpiga tobwe aligeuka mzima mzima kutaka kunikamata bahati haikuwa upande wake maana alipiga mwereka na kuanguka chini.. Moja kwa moja nilikimbilia chumbani kwa mama nilimkuta ameshika kitu kama picha baada ya kuniona alishtuka sana kisha aliificha, alikificha alichokuwa anatazama nilishangaa.
"Uko sawa mama!?.. Nilimuuliza huku nikikaa pembeni yake aliitikia kwa kutikisa kichwa lengo la kumfata chumbani kwake ilikuwa ni kumwambia kwamba nimefaulu lakini bado hatujapangiwa shule nilimwambia hadi tukio la baba kunipiga akidai nimefeli..
"Pole mwanangu utasoma tu... Nitapambana kwajiri yako usijaribu kuondoka ukaniacha yataisha tu.
Tuliongea sana mda wa jioni nilipika tulikula na mama wengine tukawaekea kwenye Hotpot kama kawaida yao..
Usiku tulienda kulala nikiwa nipo katikati ya usingizi nilishtuka kutokana na kelele zikizosikika nje alikuwa ni Baba..
"Haiwezekani huyu mtoto ampige dada yangu.. Husna toka nje sasa hivi..
"Mtoto hana adabu huyu.. Ndio maana siku zote huwa nakwambia Kayombo hapa umebambikiwa kwenye ukoo wetu hatuna watoto wenye laana.. Aliongeza chumvi shangazi..
Nilianza kutetemeka maana namjua baba vizuri atanichezeshea kipigo cha Mbwa mwitu basi nilijikausha mule ndani..
"Wewe kahaba wa kike hunisikii... Toka nje kabla sijaja kukutoa mwenyewe..
Alisema Baba huku akigonga gonga mlango wa chumbani kwetu mara nilisikia Mama akitoka nje..
"Husna hajafanya chochote mshazoea kumuonea mwanangu... Wifi embu muogope Mungu Husna kakupiga saa ngapi!?...
Alinitetea Mama lakini Baba hakutaka kuelewa shangazi ndio kwanza alikuwa ananikandia kwa Kaka yake nilivyoona baba anamfokea Mama kwa mambo yanayonihusu mimi niliona bora nitoke nje..
"Wala sitakupiga leo... Kuanzia leo huyu asitoke hata nje namtafutia mume hawezi nipa hasara mara mbili..
Alisema Baba ili nilishindwa kuvumilia "Mbona nimefaulu Baba hukuangalia vizuri matokeo... Niamini nimefaulu nilienda kuangalia shule nimefaulu baba..
Kwani hata alinielewa alikazania kuwa lazima niolewe yaani hakuwa na sababu ya msingi nilimkimbilia na kumsogelea kwa mara nyingine.
"Baba hukuangalia vizuri nimefaulu.. Mimi sitaki kuolewa nataka kusoma..
Nilisema huku nikipiga magoti mbele ya baba lakini alinisukumiza na teke zito lililofanya nianguke na nianze kukohoa............
HUSNA 03
Baba hukuangalia vizuri nimefaulu.. Mimi sitaki kuolewa nataka kusoma..
Nilisema huku nikipiga magoti mbele ya baba lakini alinisukumiza na teke zito lililofanya nianguke na nianze kukohoa mfululizo
Mama aliniwahi kunikimbilia pale chini "Vipi Husna uko salama mama angu!?..
Aliniuliza Mama nilijibu kwa kutikisa kichwa kua niko sawa nilivumilia maumivu niliyoyapata na kubaki nikimtazama baba aliyekuwa anaishia chumbani kwake..
Nilitamani kumuuliza kitu mama ila niliogopa nitamtia simanzi ila tu akilini mwangu iliniwekea picha kamili kuwa huyu sio baba yangu mzazii..
"Usiwazeee....usiwazee sana yatakwisha tu husna wangu..
Alisema Mama huku akifuta machozi yaliyoanza kutiririka usoni mwake shangazi mda wote alikuwa akitabasamu maana kwamba kilichokuwa kinaendelea pale kilikuwa kinamfurahisha nilibaki nikimtazama tu...
****
Ilipita wiki nilikuwa nikifungiwa ndani tu ila mama alikuwa akinipa moyo kuwa lazima nisome kivyovyote atanipambania tu..
Jioni hiyo tukiwa tumekaa sebreni Baba alifika na mgeni alikuwa ni Baba wa makamo tu..
"Karibu... Jisikie uko nyumbani mshenga.
Alimkaribisha huku akimuonyeshea sehemu ya kukaa "Ahsanteee sana..
Baada ya salamu nzito mgeni alikabidhi bahasha kwa baba kisha aliondoka kwa wakati huo wala sikuwa nawaza chochote...
"Husna njoo hapa.. Aliita Baba nilinyanyuka na kwenda kupiga magoti mbele yake.
"Hizo heshima unazojifanya kuziekti hapa na ukazionyeshe hadi ukweni kwako... Nimekuita kukwambia kuwa nimepokea barua ya posa hivyo ujiandae na harusi mda wowote kuanzia sasa utaondoka kwako...
"Sitaki kuolewa nimefaulu mimi nahitaji kusoma... Nilisema huku nikinyanyuka kwani nilifika mbali sasa yaani hata sikujua baba alinyanyuka saa ngapi pale kwenye kiti maana nilikula mtama ndani ya sekunde sifuri akili zote zilihama.
"Ole wako uje unitie aibu siku ya siku maana nitakuchezeshea mbele ya wageni na sitajari chochote... Umesikia wewe Malaya..
Alisema Baba kwa jaziba huku akiendelea kunichezeshea makofi..
"Utakuja kuniulia mwanangu siku moja.. Hivi hujui uchungu wa mtoto wewe!?..
Alisema Mama huku akiingilia kati lakini hakuweza kuzuia chochote sababu hata yeye aliambulia makofi..
"Baba muache mama.. Nipige mimi ndio niliyekukosea.
Nilisema huku nikimkingia mama... Baba aliondoka tulibaki peke yetu niliingia chumbani ambako huwa nalala na binamu yangu nilikusanya mafurushi yangu na kutoka nayo nje..
"Mama nakupendaa sana... Nakupenda sana mama yangu ila siwezi kuendelea kubaki hapa nitarudi tu kwajiri yako...
Kumbe baba hakwenda mbali alikuwa amejibanza mlangoni maana aliingia ndani speed na kunipeleka chumbani kwetu kisha akafunga mlango kwa nje..
*****
Nilikuwa nakaa ndani tu sikuruhusiwa kutoka walikuwa wanakuja wabibi wa kila aina kunifunda Shangazi ndio alikuwa mpambe lakini Mama yangu hakuwa anafurahia kabisa..
"Mwanangu nimeshindwa kukupigania mama... Naomba uende tu mimi naimani huko ndipo ilipo ridhiki yako mungu atakupambania..
Alisema Mama akiwa amekaa pembeni yangu nilikubaliana na matokeo ndoto zangu zilishayeyushwa ..
" Ndoa ni kesho mwanangu.. Nashindwa niseme nini ila naomba tu ukawe mke mwema mungu anamakusudio yake na imani atakuvusha katika hili............
HUSNA 04
" Ndoa ni kesho mwanangu.. Nashindwa niseme nini ila naomba tu ukawe mke mwema mungu anamakusudio yake naimani atakuvusha katika hili.
Nilikuwa tu kimya nikitamani iwe ndoto labda niwe naota lakini haikuwa hivyo yaani kesho ndio niikuwa nakwenda kuolewa tena na mtu nisiyemfahamu wala sikujua mahali yangu ilikuwa kiasi gani...
****
Kulikucha asubuhi Shangazi na Baba walikuwa na Shamra shamra mfano hakuna niliandaliwa vizuri nilipambwa kawaida tu niliveshwa shera zuri ambalo lilikodiwa nilipendeza na vile nilikuwa na damu ya nguo basi ilikuwa poa japo sura yangu haikuwa na furaha kabisa...
Mda uliwadia nje tulisikia vigere gere ishara kuwa wakiumeni wamefika mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio mfano hakuna..
Basi nilikuja kuulizwa mda niko ndani "Husna Ally umekubali kuolewa na Ibrahimu Othmani kwa mahari mliyokubaliana..
Nilikubali kinyonge baada ya ndoa kupita waliingia wamama baadhi pamoja na wazee wachache..
Mmh mbona hakuna kijana ina maana ndio nimeozeshwa na mzee Maskin nimekubali kuolewa pasi na kumjua anayenioa..
Walianza kupiga vigeregere huku wakiimba nyimbo za kikwao nilikosa nguvu kabisa..
"Usihofu Mkwe wangu.. Mumeo hayupo alipata safari ya ghafla lakini ndani ya wiki anarudi hivyo lazima mtafanya sherehe upya..
Alisema mama huyo huku akiweka vizuri mtandio wangu huku akinifuta machozi sikuelewa kama alikua anajua kuwa sikuwa naitaka hii ndoa kabisa..
Mama aliingia ndani walisalimiana Mama wa Babu harusi (Mkwe wangu)..
Baada ya hapo nilikabidhiwa nguo zangu ambazo nilikuwa nimenunuliwa na Mama kisha tuliondoka nikiwa na huzuni sana machozi hayakukauka usoni mwangu Make up yote niliivuruga ..
****
"Karibu wifi.. Karibu aliiiiliilii.. Ilikuwa nisauti ya mdada aliyetupokea ndani ya nyumba kubwa tuliyofikia.
Alinishika mkono na kunipeleka chumbani moja kwa moja kulikuwa kumerembwa ajabu chumba kilikuwa kikubwa kizurii hakina makorokoro..
"Hapa ndio chumbani kwako kuwa na amani..
Alisema wifi huyo huku akinikalisha kwenye kitanda kikubwa cha kifahari kilichopo chumbani humo maana hata jina sikuwa namjua kwa wakati huo..
"Sasa Mimi nakuacha ngoja nikuandalie msosi..
Alisema huku akitoka nje baada ya mda alirudi na chakula kwa kuwa nilikuwa na njaa nilikula bila kusita baada ya Mda alikuja mama Mkwe alinikabidhi dera nzuri pamoja na khanga za kuvaa asubuhi na kunitakia usiku mwema..
Nilibaki peke yangu nikiwaza kuhusu hii ndoa isiyoeleweka.
Nilipitiwa na usingizi nilishtuka kukiwa kumeshakucha niliingia bafuni nilioga na kuvaa dera kisha nilitoka nje..
"Shikamoo Mama.. Nilimsalimia yule Mama baada ya kumuona sebreni..
"Marhaba mwanangu vipi umeamka salama... Pole na uchovu wa safari..
"Asante.. Nilimjibu huku nikisogea alipo kumsaidia kazi lakini alinizuia..
"A aah.. Acha usijali mwanangu wewe pumzika usifanye kazi yoyote ile mpaka kuwe na ulazima.
Nilirudi chumbani kukaa niliwaza sana itakuaje huyo mwanaume kama mbabu ebu ngoja nipekue pekue uenda nitakuta hata picha yake..
Nilisogelea droo lililopembeni ya kitanda nilifungua kulikuwa na vikolokolo kibao nililifunga na kurudi kukaa nikiwa naangaza angaza macho ukutani nilikutana na picha nilishtuka sana..
"Mungu wangu...
Ilikuwa ni picha ya mbaba mtu mzima tu nilianza kulia yaani nilivyo mdogo hivi niolewe na babu kweli ghafla mlango uligongwa nilifuta machozi na kujiweka sawa...
"Karibu..
Alikuwa ni mschana tu nadhani tulikuwa tunalingana kiumri "Wifi mama anakuita tukanywe chai..
Kwani hata nilikuwa na hamu ya kula basi nilikuwa nakiwaza iko kibaba nilijikaza na kutoka nje................
HUSNA. 05
Alikuwa ni mschana tu nadhani tulikuwa tunalingana kiumri "Wifi mama anakuita tukanywe chai..
Kwani hata nilikuwa na hamu ya kula basi nilikuwa nakiwaza iko kibaba nilijikaza na kutoka nje.
"Wiki ijayo kaka yako anarudi
Alisema mama tukiwa mezani na kufanya yule mschana aliyekuja kuniita apaliwe yaani mbona ameshtuka kusikia kaka yake narudi nilizidisha hofu mara dufu hata chai yenyewe sikuitamani...
"Shangazi mimi kesho kutwa naondoka kwangu mume wangu ameshanitumia nauli.. Alisema yule mkubwa ndipo nilipogundua kuwa yeye ameolewa alikuja kwasababu ya shughuli ya kaka yake Binamu basi Baada ya kula yule Mama alinikabidhi zawadi ya nguo zilikuwa nguo nyingi tena nzuri akanipa na bahasha ndani yake ilikuwa na pesa nilimshukuru.
Zilipita siku mbili nilikuwa nimeshaanza kuzoea mazingira nilimkumbuka sana mama yangu nilitamani hata kusikia sauti yake nikiwa nipo chumbani nawaza mlango uligongwa nilinyanyuka na kwenda kufungua alikuwa ni wifi yangu tunayelingana Aisha yule Mkubwa alishaondoka kwa mumewe.
"Wifi kuna mgeni wako...
Mgeni wangu gani tena nilijiuliza huku nikifuata wifi nje nilikutana na dereva wa boda boda ambaye mara nyingi huwa anambebaga baba alinisalimia alikuja kuchukua gauni la harusi la watu maana lilikuwa la kukodi nilirudi chumbani kwangu kumfatia,
"Vipi ulionana na mama!?.. Nilimuuliza huku nikimpatia gauni nililolihifadhi kwenye mfuko.
"Ndio anakusalimu sana... Alisema yule kijana nilitabasamu kusikia kuwa ajambo nilimpa bahasha ndani yake kulikuwa na pesa 50000 akampe Mama na amwambie kuwa sijambo nitaenda kumtembelea..
Si kwamba nilikuwa na pesa za kutosha hapana ila niliyajua vizuri maisha ya pale nyumbani na nilitaka kumtoa hofu pia ajue tu kuwa niko mahali salama..
***
Nilirudi ndani nikiwa na furaha kuwa Mama akipata salamu zangu atafurahi pia kama nilivyofurahi mimi sikurudi tena chumbani nilimfata wifi Aisha..
"Kaka anarudi alhamisi yaani.. Alinung'unika Aisha.
Nilivuta pumzi nzito kiukweli sikutamani hata arudi huko alipo nilikuwa mnyonge ghafla furaha yote ilitoweka maana zilibaki siku nne tu ifike hiyo Alhamis..
"Baadae kuna part ya rafiki yangu wifi... Ni vizuri tungeenda wote umepoa sana.
Alisema Aisha nilitamani pia kutoka nikaangaze angaze macho "Mama atakubali!?...
Nilimuuliza Aisha alinambia atamalizana nae basi nilifurahi kuona tunatoka niliandaa dera langu mwenyewe nywele zangu vile zilikuwa ndefu nilipanga kubana tu.
Ilifika jioni Aisha alienda salon kuset akavaa gauni yake fupi ya kubana alipendeza sana.
"Mbona hujajiandaa wifi!?... Aliniuliza baada ya kuniona nipo na dera langu.
"Nijiandaaje nishavaa kama uko teyari tuondoke...
Aliangua kicheko mpaka nilijihisi vibaya "Wifi hii ni party utaonekana wa ajabu sana atleast ungevaa gauni.. Ebu ngoja nikuletee gauni ujaribu. Alisema huku akielekea chumbani kwake baada ya mda alirudi akiw ameshikilia nguo mkononi.
"Kajaribu hii hapo.. Alisema Aisha huku akinikabidhi kile kigauni..
***
Niliijaribu ilinipendeza kweli tatizo ilikuwa fupi tu nilichukua upande wa khanga nikajifunga kisha nilimfuata Aisha aliyekuwa na hekaheka teyari alishamaliza kujiandaa basi tulitoka.
Kwenye part watu walikuwa wengi kiasi tena walipendeza sana tulikaribishwa na rafiki ake Aisha ndie mwenye part yake.
Tulitafuta sehemu nzuri tukaketi niliagiza juisi na kuanza kunywa taratibu Aisha yeye aliagiza bia tena alikuwa anainywa Kama maji kiufupi alikuwa mzoefu..
Nilikuwa namzuia asinywe sana ili asilewe sababu yeye ndio mwenyeji mimi sipajui..
"We tulia Yaani leo ndio nafurahi Mara ya mwisho mwisho akirudi huyo Ibra amri ni moja tu.
Kwakuwa alikuwa akataziki nilimuacha anywe atakavyo basi mda ulienda sana matukio ya muhimu yalishaisha watu walikuwa wanacheza mziki tu.
Mda ulikuwa umeenda sana nilizidi kuwa na hofu..
"Aisha mda umeenda sana turudi mama atakuwa na wasiwasi..........
Kwa mwendelezo Wasiliana Na MWANDISHI
Queen Lizzie
06839443333
Tags
simulizi