MISS TRINNIE
SEHEMU YA NNE
Mwandishi - Queen Lizzie
_______________________________________
nilijikalisha kwenye kiti huku nikiitazama ile simu macho yakiwa yamenitoka huku nikihema.😨😨
"Jack..Jack ni nan..na nani kaisevu namba yake kwenye hii simu"
Nilijiuliza lakini ghafla simu yangu iliita yaani ile 'Samsung J7' ambayo Sophia aliita ya kimasikini.
Niliinuka na kuifata pale kitandani ambapo nilikuwa nimeiweka.
'SOFIA' 📱 ndiye ambaye alikuwa anapiga.
"Heloooo...📲"
"Wewe Binti una matatizo gani, mbona nakupigia unakata...😬"
"Oooh sorry mamy hivi ni wewe ambaye ulikuwa umepiga jina likaja Jack"
"Yeah ni mimi "
"Oooh sorry nilikuwa naogopa maana simu imeita ikaja na jina kabisa pia halijaja Sofia..."
Nilijielezea lakini nilikatishwa.
'Sofia' alihitaji zaidi kutawala mazungumzo na alihitaji niwe msikilizaji, nilipoa.
"Kwanzia sasa sitaki unifahamu kama Sofia, nitambue kama Jack na hiyo namba ambayo nimekupigia katika hiyo Iphone ndiyo ambayo tutaitumia kwenye mawasiliano ,sawa 😎"
"Ooooohpppps"
Nilihema..
"Sawa..."
"Halafu kingine katika kazi hii utatumia jina bandia kila kitu kuhusu wewe kitakuwa bandia taarifa zako zote zitakuwa fekiii, jina lako litakuwa MISS TRINNIE ,mahali unapotokea patakuwa Arusha.."
Sofia alisema.
"Sawa mamy"
"Keshokutwa ndio siku ambayo mume wangu atatoka Dar es Salaam ataelekea Morogoro na atafikia katika hotel ya Morena, kashafanya Booking chumba namba 14, ila na wewe tayari nishakufanyia Booking chumba namba 12 vyumba vyenu vitakuwa karibu karibu, please binti fanya kazi yako kwa kufanya usivuke mipakaa 😬 narudia tena hizi gharama zote ninazozitumia ukithubutu kutoka nje ya maelekezo hata kwa hatua nne, utazitapika ukiwa umesimama wimaaa 😬"
Sofia alisema.
🤦♀️Daah sikuwa na jibu la kumpa zaidi ya kuitikia 'ndio'.
"Ok nakutakia kazi njema usisahau kujiandaa jiweke vizuri, muonekano wa kihela hela yaani classic..mume wangu anapenda wanawake wenyewe mionekano nadhifu "
"Sawa mama..."
Niliitikia lakini kichwani bado nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza na pia moyoni kama nilikuwa na donge flani hivi na hili ilo donge litoke basi Sofia alihitaji kunijuza jambo.
"Lakiniiii..."
Nilisema kwa kusita sita.
"Yes.."
"Samahani kwa kuuliza swali ambalo si sehemu ya kazi , ila nilikuwa nahitaji kujua mamy, why unafanya haya yote kwa mumeo tena wa ndoa ambaye umezaa naye kabisaa..."
"Fanya kazi binti, maswali yako hayahusiani na kazi hii"
Sofia alisema kisha akakata simu na kuniacha nimepigwa na butwaa🤦♀️
Nilirudi kitandani nikajilaza chalii huku nikiendelea kumfikiria Sofia mwanamke wa ajabu.
Ni kipi hasa kilikuwa nyuma ya panzia ambacho kilimfanya afanye yote haya 🤷🏻♀️
Majibu nilikosa.
Ilikuwa ni kazi nzuri yenye hela nyingi lakini ilikuwa imejaa ukungu wa kila aina na iliniumiza kichwa mnooo...
Niligeukia upande wa pili niliitazama ile picha ya mume wa Sofia, ambaye ndiye alikuwa mlengwa namba moja 🤦♀️.
Daah alikuwa 'Handsome' wa maana, alikuwa na sura, kimo pia hata mwili wake ulikuwa ule wa kuvutia haswaa🥰
Pia hata umri wake haukuwa mkubwa ukilinganisha na wa Sofia, Sofia alikuwa mkubwa sana kwa mumewe.
Niliitazama ile picha kwa zaidi ya nusu saa kisha mwisho niliikumbatia kifuani , usingizi ukanipitia 🛏️
**********************
Siku iliyofata ilikuwa siku ya ijumaa na kwa maelezo ya Sophia ni kwamba siku inayofata ndiyo itakuwa siku rasmi ya kazi.
Hivyo siku hii mimi na rafiki yangu Irene tulihangaika kariakoo katika maduka ya nguo kutafuta nguo nzuri za gharama, pesa ilikuwepo ya kutosha maana Sofia alinipa laki tano hiyo kwa ajili ya nguo tu.
"Unajua Irene mimi bado huyu mwanamke simuelewi na simuamini pia japo hela naitaka🤦♀️"
"Kivipi shogaaa..😳"
"Unajua mpaka sasa hivi kashateketeza zaidi ya milioni mbili kasoro, kanipa hela 'Iphone' mpyaa, kanipa hela na tayari kashanifanyia Booking ya hotel 🤦♀️, pia kaniambia gharama zote kwa kipindi hiki atakuwa anasimamia yeye...huoni kama kuna kitu anakitaka kutoka kwangu🤦♀️, sio mtego huuu ?, mimi naogopa mwenzio"
Yalikuwa mazungumzo kati yangu na Irene ambaye ndiye alinikutanisha na yule mwanamke maana mimi sikuwa namjua kabla.
"Mmh shoga mbona una hofu hivyo, hivi utauweza utajiri wewe ambao siku zote unauimba...hahahaha😂😂"
Irene, alisema kwa mzaha lakini kama angejua namna ambavyo nilikuwa najisikia moyoni, daah asingethubutu kuleta mzaha vile.😬😬
"Acha utoto basi..kuwa 'serious' "
"Ok wewe wasiwasi wako upo wapi hapo 🤷🏻♀️"
"Anatumia gharama nyingi sana katika kitu ambacho kinatia walakini, hivi wewe Irene unaweza kumlipa mwanamke hela ili achepuke na mumeo ?🤷🏻♀️"
"Mmhh...mimi binafsi siwezi ila unajua ndoa inakuwaga na mambo mengi..."
Irene, alisema lakini kabla hata hajamaliza nilimkata.
"Ninahisi jambo..."
"Lipi..!"
"Mke wake Mudrik yupo nyuma ya hili na ila huyu mwanamke anatumika tu kama chambo ili kunipoteza maboya na kuna lao ambalo wamelipanga...🤦♀️"
"Hapana sio kweli..."
"Ok niambie ukweli Irene maana wewe sio rafiki tu kwangu wewe ni ndugu..🤦♀️"
"Ukweli gani huo"
"Ni kweli huyu mwanamke umekutana naye mtandaoni kama ulivyoniambia au kuna ambalo unanificha unataka kuniuza rafiki yako 🤦♀️🤦♀️"
Nilimuuliza Irene swali ambalo hata yeye mwenyewe lilimuacha mdomo wazi yaani hakulifikiria hata kidogo.
Macho yalimtoka 😳😳 lakini sikujali kitu pekee ambacho nilikuwa nahitaji kukijua ni ukweli tuu basi.
Maana Irene ndiye aliniunganisha naye.
Mwanzoni aliniambia kwamba mwanamke huyu alikutana naye tu mtandaoni akamuelezea shida yake lakini yeye hakujiona kama ana vigezo hivyo akaamua kunisukumia mimi mpira. Lakini kwa upande wangu nilihisi kuna zaidi ya hayo, ila Irene ananificha.
Nilijikuta nakosa kumuamini rafiki yangu mwenyewe ambaye urafiki wetu ulidumu zaidi ya miaka 15 Tangu tukiwa shule ya msingi.
ITAENDELEA........
Tags
simulizi