TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

MISS TRINNIE 03

MISS TRINNIE 
SEHEMU YA TATU
Mwandishi - Queen Lizzie 
_______________________________________
Nilirudi nyumbani kwetu nikiwa naruka ruka shangwe nyingiiiii👌💃 kwani nilikuwa na pesa pia nilikuwa na simu aina ya Iphone 13 ambayo kiukweli nilikuwa sijawahi kuiwaza hata siku moja kama nitakuwa mmliki wa Iphone tena 'Iphone 13' ambayo ilikuwa on trend🙈🙈
Nilimkuta mama anapika pika lakini kiukweli sikuwa hata na njaa zaidi ya furaha nilipitiliza chumbani kwangu moja kwa moja.
Zile pesa ambazo nilipewa na yule mwanamke sasa nilipata wasaa wa kuzihesabu.
Woow zilikuwa ni laki 5 🥰😁 
Simu, pesa na ile picha ya yule mwanaume yaani mume wa sophia, nilisambaza pale kitandani na mimi nikalalia upande wa pili , ndani ya dakika tatu tu usingizi ulinichukua 🛏️🥱.

*********************
Majira ya saa tatu usiku nilikuja kuamka na kilichoniamsha kilikuwa ni mlio wa simu📲📲, ile 'Iphone 13' ambayo nilipewa mchana na Sofia na wala sio kile kisamsung changu 🙈
Haraka niliikamata simu lakini cha ajabu nilipoangalia kwenye kioo nilikuta jina na wala si namba. 'JACK' ndilo jina ambalo lilisemeka pale kwenye kioo. 
"Jack..😳"
Nilistuka maana sikuwa namjua huyo Jack pia simu ilikuwa mpya pia laini ilikuwa mpyaa na kwa masharti ambayo Sophia alinipa ni kwamba simu hiyo inahitajika kuwa na namba moja ya kwanza ni ya kwake mwenyewe Sofia na ya pili basi iwe ya mumewe 🤦‍♀️
Lakini cha ajabu simu iliita na jina ambalo lilijitokeza kwenye kioo lilikuwa Jack. 
Na nilipoweka kumbukumbu zangu vyema nilikumbuka kwamba sikusevu namba ya mtu yeyote katika simu hiyo tangu nilipopewa, 🤦‍♀️
"Jack...Jack...Jack ni nani...? na kwanini namba yake iseviwe humu"
Lilikuwa ni swali ambalo nilijiuliza lakini sikupata majibu.
Nlijishauri kwamba nipokee au niipotezee lakini mwishoni nilifanya maamuzi, nilipokea huku simu ikiwa mbali na sikio. 
"Ha..haa..halooo"
Nilisema baada ya kupokea lakini sauti moja kali ilipenya masikioni mwangu ikitokea upande wa pili wa simu. 
"Wewe Sarah....😬"
Nilitetemeka haraka nilikata simu 😳🙈
Maana yule mtu alilitaja jina langu kama lilivyo na nisijue kalijuaje.
Nilitetemeka 😭😫

ITAENDELEA......

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post