MISS TRINNIE
SEHEMU YA TANO
Mwandishi - Queen Lizzie
_____________________________
"Nooh Sarah siwezi nikakuuza rafiki yangu sio kwa pesa sio kwa dhahabu wala si kwa gharama yoyote ile, ila nilikuunganisha na huyu mwanamke kwa nia ya kukusaidia tu na nina uhakika kama utaifanya kazi yake vizuri basi utabadilisha maisha yako kwa asilimia kadhaa.. una ndoto ya kufungua duka la vipodozi.. hii ndio itakuwa njia moja wapo ya kuikamilisha ndoto hiyo"
"Aaaah...Irene lakini ni kweli kabisa hajakwambia kwanini anayafanya haya🙆♀️"
"Hapana hajaniambia...ila fanya kazi mimi nipo nyuma yako🥰"
Irene alisema kisha tukakumbatiana 🫂🫂.
nilijikuta nairudisha tena imani yangu juu yake.
***********************
Siku iliyofata ilikuwa ni jumamosi na ndio siku yenyewe ya kazi. Bado nilikuwa na hofu ila Irene alijitahidi sana kuniweka sawa🤦♀️
Sofia naye aliniambia kwamba mumewe atawasili morogoro majira ya saa nane ila mimi natakiwa kufika morogoro kabla ya saa saba. Yaani mumewe afike anikute mimi.
Mapema sana kama kwenye saa 4 asubuhi nililetewa dereva, dereva huyu ndiye ambaye angetumika kunisafirisha mpaka morogoro, hakutaka nipande basi za abiria.
Huku akinisisitiza kwamba taarifa zangu zote zinatakiwa kuwa bandia.
Tukiwa njiani dereva hakuacha kunipiga maswali ambayo yalizidi kunipasua moyo.
"Umejuana na Sofia kwa muda gani"
"Miezi sita 😒"
"Mmmhh Kweliii ? 🤔"
"Enhee ni ukweli.."😒
"Nakuonea huruma sana..🙂."
Yule dereva alisema macho yalinitoka.
"What..why..how ( nini..kwaniii...kivipi)😳😳"
"Unaitwa nani ?"
Alibadilisha mada haraka hakutaka kunipa majibu ya swali langu.
"Unaitwa nani.."
"Sarah...ooh noo sio Sarah ni... Trinnie..Miss Trinnie , ndio jina langu🤦♀️"
Mwenzenu nilitatarika zaidi ya bisi kikaangoni 😭 sikuwa na asili ya uwongo pia nilikuwa siwezagi kutunga uwongo. Hivyo nilijikuta najikanyaga kanyaga.
"Aaah sawa 😁"
Yule dereva aliitikia kisha tokea hapo hukujibu lolote ambalo nilimuuliza wala hakusema lolote lile alibaki kimya 🤐. hata kuniangalia hakuniangalia🤷🏻♀️
Safari iliende kibubububu japo nilijitahidi sana kujiongelesha lakini nilionekana kama napiga kelele tu.🤦♀️
Mwisho niliamua kufunga mdomo 🤐
*******************
Majira ya saa saa saba na nusu tulifika morogoro.
Yule dereva aliniacha kwenye lango la hotel ya 'Morena' ambapo ndipo mahali ambapo kazi yangu itafanyika kisha yeye akatokomea zake.
Lakini muda wote huu nilikuwa nikiwasiliana na Sofia na maelezo ambayo alinipa ni kwamba.
nisiende kuchukua funguo ya chumba changu mpaka mumewe atakapowasili 🤦♀️
Na aliniambia mumewe atakuwa hapo ndani ya nusu saa tu. Niliyafatisha maelekezo yake 🙆♀️
Nilijikalisha mapokezi huku nikusubiria mumewe Sofia afike.
Kwa jinsi nilivyovaa nilikuwa sina tofauti na mwanamitindo 'Flaviana Matata' ama muigizaji wa kitanzania wema Sepetu 😘
Nilipendeza sana pia mwili wangu ulichangia jamani 👌😂
Nilivaa Gauni jekundu aina ya 'evening gown' ambalo lilikuwa refu mpaka miguuni kisha mpasuo mmoja ukapita kwanzia kwenye paja mpaka chini. Kama ungeniona basi labdda ungedhani ni supastaa anaenda kwenye zuria jekunu (Redcarpet) kumbe nilikuwa naenda kuchepuka na mwanaume wa mtu 🙈 lakini hata hivyo nilikuwa kazini 😁.
Wanaume ambao walikuwa katika eneo lile hawakuacha kunikodolea mimacho ya uchu😳 na wengine walifika mbali zaidi na kuanza kunikonyeza 😉.
🤦♀️ niliwapotezea.
"Nadhani tayari kashawasili "
Ujumbe uliingia katika simu yangu ukitoka kwa Sofia ambaye kwa sasa alitaka nimfahamu kwa jina la Jack.
Nilijiweka sawa baada ya kupokea ujumbe huo lakini hazikupita dakika tano. Kweli nilimuona mume wake kaingia akiwa na begi moja kubwa mkononi 😳
Sikupata shida kumtambua maana nilikaa na picha yake kwa takribani siku mbili, hivyo nilipomuona tu nikagundua kwamba ni yeye.
Alivaa suti moja nyeusi, ambayo ilimkaa vyema ikimbanabana maeneo ya mikononi na kifuani, pia suruali yake haikuvuka vifundo vya miguu na chini alimalizia raba , ule uhandsome ambao niliuona kwenye picha sasa uliongezeka mara dufu🥰.
Alikuwa ni muonekano wa kisanii sanii hivi.
"Woooow...he is very handsome 😘😘"
Nilijisemea lakini ghafla nilisikia sauti ikitoka ndani yangu 😫
"Acha tamaa upo kazini😜"
Nilizifuta hisia za tamaa ambazo nilikuwa nazo kisha nikauvaa uso wa kazi.
Nilimtazama alienda mapokezi akaongea ongea na yule muhudumu pale mapokezi.
Sikutaka kulaza damu haraka na mimi niliinuka na kuanza kuelekea pale pale kwa muhudumu alipo.
Lakini hata hivyo nilipiga hatua tano tu.
Ghafla msauti mbaya ulipenya katika masikio yangu.
"Sarah...Sarah...Sarah "
Nilistuka mapigo yangu ya moyo yalipiga paah!😫
Niligeuza shingo yangu nyuma ili nimtazame huyo aliyeniita kwa jina langu katika eneo lile wakati jina langu lilitakiwa liwe Misa Trinnie.
Oooh sikuamini macho yangu kwa kile nilichokiona baada ya kuigeuza shingo yangu 😨😳
ITAENDELEA......
Sehemu zinazo fuata Wasiliana Na MWANDISHI katika Whatsapp
Tags
simulizi