( 6——10 )
🔞
🔞MKE WA MGANGA 06
Tulipoishia
Nilipofika ndani, upepo wa nguvu uliingia ukifuatiwa na kelele za kutosha halafu kama zimwi niliona mganga ametokea mbele yangu akiwa amefura hasira usoni
“Haaha….unataka kwenda wapi kijana” Mganga aliniambia mimi sikuweza kujibu chochote nikabaki namtazama huku nikitetemeka na kurudi nyumba mpaka wenye kitanda nikaketi bila taarifa
ENDELEA
“Nimekuja kwako leo, nimeshaona mmekolea sana katika mapenzi, samahani sana, mapenzi yanauma kuliko kitu chochote, hivyo unapoendelea kutembea na mke wangu roho inaniuma hivyo nimekuja kwako kukupa onyo kwamba uachane na Zuhura yule ni mke wangu….. na ejapo ukiendelea naye magumu yatakukuta kijana…” alisema mganga na kupotea katika mazingira ya kutatanisha nikajiuliza hii inakuwa ni nini mbona kutishiana amani katika mapenzi jamani
Nilibaki na uoga wangu, yaani muda ule ule nilipanga kwamba sitaki mazoea tena na Zuhura, yaani aniache tu na maisha yangu kwa sababu nilikuwa sitaki kufa kabla ya siku zangu
Raha ilikuwa ni kitu kimoja ni kwamba mimi nilikuwa sina namba ya Zuhura, naye pia alikuwa hana namba yangu ya simu hivyo ngoma ikawa ni droo, niliamua kwamba nitamkwepa kwa njia yoyote kuanzia siku ile
**
Siku mbili baadaye nilikuwa nimeamka asubuhi na kunyesha mboga zangu, na kwa bahati yule fundi bomba alinitafuta kwenye simu akawa anataka tuende naye jobu, hivyo niliamua kuvaa nguo zangu vizuri na kuondoka nikaenda hadi maeneo ambayo aliniambia nitamkuta.
“kaka vipi za asubuhi” nilimuambia Ba Fetina
“Kwema umeamkaje?” aliniuliza
“Sikiliza, mimi kuna vifaa ninaenda kuchukua katika mtaa wa pili hapo kwa ajili ya kufanya huu ufundi, hivyo wewe nisubiri, endelea kukata kata hivi vitu hapa” aliniambia, hiku akinipa vifaa fulani vidogo vidogo nivikate ili akirudi kazi iwe nyepesi
“poa poa broo” niliongea na kuchukua kamsemeno fulani hivi ka kishikwambi halafu nikaketi chini kwenye udongo nikawa ninakata vifaa vile huku nikiimba kawimbo ka tenzi za rohoni maana nilikuwa nimeshaamua kumrudia Mungu
Yaani popote Mungu anapoajaribu kukuweka salama, shetani naye anatafuta njia zote zile ili aweze kukutoa katika mstari, hivyo basi, wakati niko pale nakata kata vile vifaa, nilishuhudia msichana wangu wa kwanza kabisa, akiwa amerudi kutoka shule maana alikuwa akisoma boarding
Msichana yule alikuwa amebeba Begi kubwa la nguo na mgongoni akavaa lingine, kichwani alikuwa amesuka mabutu, na alikuwa ndo anazidi kupendeza
Hakuna kitu kibaya kama umuone EX wako amependeza, unajihisi wewe ndo ulikuwa nuksi, sikuthutu hata kumsalimia, lakini nilishuhudia mwenyewe amenichangamkia kama vile bado ninaishi moyoni mwake
“mmmh kaka Festo” alinisalimia kwa furaha mpaka nikajikuta nimetabasamu na kuinuka kumsogelea
“Giva” nilimuita kwa furaha na kuinuka pale nilipokuwa nimeketi, nikamsogelea njiani kidogo halafu nikamkumbatia nikaona kajileta mwenyewe kifuani
“Shikamoo” alinisalimia
“mmmmmh…..hiyo shikamoo hiyo” nilisema na kumnyooshea kidole huku nikiona anatafuta gia ya kuninyima utamu
“Ahahahaaa hutaki nkusalimie?” aliniambia kwa furaha
“wee, nope, sitaki……vipi lakini shule?” nilimuuliza na kumshika mkono kama vile ninamsalimia halafu nikawa namtekenya tekenya mpaka akaanza kutabasamu huku akiwa ameulegeza ule mkono, nikajua lazima niirudishe ndani siku sio nyingi
“Shule bwana ni safi tu, nimekuja likizo fupi hapa nimepamiss”
“ohohooo na sisi tumekumiss hasa mimi nimemiss vingi kutoka kwako”
“mmmmmh” aliguna na kuniangalia kwa jicho fulani hivi lililoonyesha kwamba nilichokimiss lazima nikipate, ile ghafla niliona kundi la wanawake wanne likija kutoka upande wa mbele yetu.
Nilipowatazama vizuri sikuwajua wote lakini mmoja alikuwa ni Zuhura, ambaye nilikuwa nishapiga kama mara mbili tatu hivi ila nikawa nimeamua kumpotezea
Alinikuta bado nikitekenya mkono wa mtoto yule wa kike na nilpomuona Zuhura anakuja na wenzake, ilibdi nionyeshe manjonjo zaidi ili anichukie na kuniacha na maisha yangu
Zuhura na wenzake, walifika pale mbele yetu, kiukweli hakuweza kuvumilia, aliamua kunifuata kwa ukaribu na kutusalimia kinafiki
“Mambo zenu” alisema akijizungusha zungusha kinafiki
“Safi vipi?” niliitikia ile salamu
“Shikamoo?” Giva naye alimsalimia Zuhura
“Marahaba, ninawaona” alisema kaiwa anamuangalia kuanzia juu mpaka chini kikuda na alitaka tu kujua kwamba tunafanya nini
“Tupo kwani vipi?” nilimuuliza kwa jeuri mimi
“Hamna wala, nilisema niwasalimie tu” alituambia na kuniangalia vibaya halafu akaanza kutembea kuondoka na kwenda kuwafuta wenzake mimi akaniacha na Giva tukiwa tunaongea pale
Baada ya dakika moja, Giva aliondoka akaendelea na safari yake kuelekea nyumbani, mimi bado nilibaki kazini kwangu
“Yessss, hapo sawa nimemkomesha nina imani hatokuja kwangu tena” nilisema kwa furaha na kuketi tena halafu nikaanza kukata kata vitu nilivyokuwa nimeambia na Ba Fetina
Baadaye Ba Fetina alikiwa na vitu alivyoleta, na tulianza kupiga kazi ambayo tuliimaliza baada ya masaa kadhaa na kunilipa 8000 yangu nikaondoka kwenda nyumbani,
Siku hiyo nilikuwa sina shida sana ya chakula kwani bado vile vitu alivyokuwa ameniletea Zuhura vilikuwepo na nilienda dukani kununua mchele nusu tu, na mafuta, halafu nikarudi nyumbani kwa ajili ya kufanya mapishi, halafu nikala na kulala mpaka asubuhi
*
Ilipofika asubuhi na mapema niliamka na kupiga mswaki kisha nikanyesha mboga, mimi sikuwa na mpango wa kunywa chai kwa mama ntilie tena, mambo yalikuwa kidogo yanaenda barabara, hivyo nilijipikia chai yangu, nikala na kiporo cha wali halafu nikaketi sebuleni huku nikisikiliza karedio kangu, tena ilikuwa ni redio One nilikuwa nasikiliza
Nikiwa nazidi kula uhondo wa habari pale ndani, nilisikia kasauti kwa nje
“Hodiii?” ilikuwa sauti ya kike ikabidi nipozi kwanza ili aite tena “Hodiii” aliita kwa mara ya pili ndipo nikaitika hodi yake “Shikamoo kaka” huyo mtu alisema
“Marahaba” nilisema na kuinuka nikatoka moja kwa moja na kwenda nje kwa ajili ya kushuhudia ni nani alikuwa ananiita asubuhi asubuhi, nilipofika nje nilikutana na sura ya Mwanafunzi Giva
“mmmh umelala hadi sa hizi?”aliniuliza
“hamna….” Niliongea nikitazama kushoto kulia kwa mshangao, ili tu nimfurahishe “samahani” nilimuambia
“nini?”
“wewe ndo umeniambia shikamoo?” nilimuuliza kwa macho makali mpaka mwenyewe akacheka
“ndio…..kwanini unaniuliza”
“mmh jana nilikuambiaje?” nilimuuliza
“hahaaa, jana uliniambia kwamba Shule inasemaje” alinitajia hicho yaani mimi mwenyewe nilicheka maana nilijua kabisa kwamba anaelewa kwamba nilimuambia kwamba asinipe shikamoo
“hahaha sio hicho bana, mimi nilikuambia kwamba usiniambie shikamoo maana nishajua kuna kitu unataka kuninyima”
“hahahaa” alicheka na kuinama, halafu nikajisogeza ndani ya nyumba, “karibu ndani” nilisema na kuingia ndani huku nikiwa ninataka naye aingie ili tuweze hata kuongea zaidi, na kama pia ikitokea bahati, akanipa utamu, basi nipate raha
Bila ubishi Giva aliingia ndani na kuketi kwenye kochi, halafu na mimi nikaenda nikaketi kwenye kochi lililokuwa likitazamana na hilo kochi lake hivyo tukawa tunatazamana usoni kwa aibu
“unajua ulivyoenda shule umezidi kupendeza, unasoma kweli au kujiremba?”
“mmmh bhan, Festo”
“nini sasa” nilisema na kuinuka nikaenda kuketi pale alipokuwa naye ameketi, hivyo tukakaa karibu “Shule mnafungua lini?” nilimuuliza
“Wiki mbili tu tumefunga”
“ooh kafupi sana, lakini ndani ya hizi wiki mbili ninajua nitainjoy sana” nilijaribu kumtania nione atanichukuliaje kwa kauli hiyo
“mmmh uinjoy kisa?” aliniuliza na kunitazama kwa jicho la wizi”
“mmmmmh naniliu” nilisema na kumvuta kwa nguvu mabegani, mpaka akainuka na kunisogelea karibu kabisa uso ukawa umenikaribia, ambapo ilinifanya mimi niombe denda, denda inavyoombwaga ni kumsogezea mwenzako mdomo tu, akiupokea ina maana umekubaliwa, akisogeza uso pembeni basi ujue umekataliwa, hivyo basi niliona ameupokea akawa ameniruhusu
Mkono wake ulimlegea ukawa umeanguka juu ya suruali yangu na ulikuwa ukipapasa mashine yangu, nikawa nimeanza kudindisha, hivyo nikamsogezea mkono kwenye sketi yake fupi na kuanza kumpapasa mpaka mikono nikawa nimeizamisha ndani ya sketi yake na kuishika chupi nikawa nimeisogeza pembeni na kumtekenya kwa kidole
Niliona haitoshi nikamnyanyua na kuishika chupi akanyanyuka kidogo na mimi nikaishusha “Kaka bhana mimi sitaki hivyo” alisema kwa maneno tu lakini matendo yalionesha kwamba anataka hivyo kunifanya niendelee kumpapasa na chupi nikaishusha mpaka chini na kuitoa miguuni.
Niliona sio mbaya, nikainuka ili nikafunge mlango kwa ajili ya usalama zaidi, lakini nilichungulia nje hivi, nilimuona mke wa mganga anakuja kwa speed ya ajabu kabisa, alikuwa anawahi sana
“Wait wait wewe usifunge mlango” aliniambia nikaona Giva ameshtuka na kuinuka na kukimbilia chumbani pa kulala maana aliogopa akikutwa pale na mtu itakuwa keshi kubwa
“Nini sasa” Nilimuuliza Zuhura kwa mshtuko maana alikuwa ananiharibia riziki
Yeye alikuja mpaka mlangoni, nikaona anaangalia kwenye suruali yangu, niliyokuwa nimedindisha vibaya sana, halafu akanitazama usoni
“Unafunga mlango wa nini, unataka upige punyeto au kuna mwanamke ndani?” aliniuliza kwa hasira mi kabla sijajibu aliusukuma mlango na kuingia ndani, cha kwanza kukiona ni chupi ya Giva iliyokuwa sakafuni pale pale sebuleni kudadededeki
“Ni nini hiki????” aliniuliza kwa hasira huku akiinyooshea kidole ile kofuli ya Giva, nilishindwa kujibu kwa kweli…….ITAENDELEA🔞MKE WA MGANGA 07
Tulipoishia
“Unafunga mlango wa nini, unataka upige punyeto au kuna mwanamke ndani?” aliniuliza kwa hasira mi kabla sijajibu aliusukuma mlango na kuingia ndani, cha kwanza kukiona ni chupi ya Giva iliyokuwa sakafuni pale pale sebuleni kudadededeki
“Ni nini hiki????” aliniuliza kwa hasira huku akiinyooshea kidole ile kofuli ya Giva, nilishindwa kujibu kwa kweli…….
Endelea
Niliona Zuhura ameondoka pale kwa kasi ya ajabu halafu akaenda moja kwa moja hadi chumbani, nikaweka mikono kichwani huku nikiwaza itakuwaje akimkuta mtoto wa kike kule ndani, nilikaa kama sekunde kumi nikisubiri matokeo lakini sikusikia hata kofi kutoka kwake lakini alitoka akiwa ameikunja sura kwa hasira
“Jamani F” alinita kwa kifupi “nimekukosea nini lakini mbona unanisaliti jamani tena kirahisi kiasi hiki?” aliniuliza “au kisa mimi ni mke wa mtu? Umeshanitumia halafu unafanya hivi kweli?” aliniuliza tena mimi nikabaki nimeduwa maana nilikosa jibu la kumpa
“Zuhura, wewe ni mke wa mtu mbaya, juzi tu amenitokea na kunipa onyo kali kwamba nisiendelee na wewe, teana ameniambia kwamba nikiendelea na wewe ni makubwa yatanitokea” aliniambia
Haikupita sekunde nyingi Giva alitoka kule chumbani, akatoka nje akikimbia sijui aliogopa nini kiasi kile, hata chupi yake hakuiokota pale ilipokuwa imedondoka chini,
“Samahani Zuhura mimi sitaweza kudeti na wewe tena” nilimuambia kwa kiburi halafu nikaona Zuhura amepiga magoti chini na kuniomba msamaha
“Nisamehe, ninajua kwamba alikutokea maana amenipiga sana juzi, lakini kiukweli Festo mimi mpaka muda huu, nimeshanogewa na penzi lako, yaani naomba tu tuendelee, hata ikiwezekana nitaachana naye tutatoroka tuende zetu karatu, kule kuna mashamba ya kutosha tutalima karanga halafu tutasambaza tupate hela” aliniambia mtoto Zuhura kidogo yale maneno yakanilegeza
“Inuka basi jamani” nlimuambia na kumshika misulini nikamnyanyua
“Umeshanisamehe na kunielewa?” aliniuliza
“Nimekuelewa, ninaomba unielewe pia wewe, kwamba mimi sitaki kuishi kwa mawazo Zuu
“Hautaishi kwa mawazo nakuambia, ni kwamba mimi ninataka tutoroke wote maana mimi nimeshamchoka”
“Ok sikiliza, mimi ulivyokuja ulinikuta nakaribia kula mzigo, nataka basi unipe ili niamini” nilimuambia kwa kujiamini
“Jamani, sitaweza kukupa leo, maana nipo kwenye siku zangu, subiri baada ya siku mbili nitakupa maana niliingia mwezini juzi”
“Doooh” niliguna baada ya kujua kwamba nakosa utamu kwa siku ile, hakika aliniharibia kabisa
“Umekasirika?” aliniuliza
“Nope siwezi kasirika vitu vidogo hivyo bana ah”
“Ok powa mi naondoka asije kunifuata hapa”
“Haya poa, byee” nilimuambia nikaona ametoka nje lakini hakufika mbali nikamuita “Samahani Zuhura”
“Niambie”
“Naomba namba yako basi”
“Oh 0674838383” alinitajia nikaisevu halafu akaondoka.
Nilirudi ndani nikaichukua ile kofuli ya mage na kuiweka sehemu nzuri na kuketi kitandani nikasikia voooop mtu katua mbele yangu, ikabidi nimtazame na kukuta ni yule mganga amenitokea tena, nilishtuka nikaogopa
“kijana, nimekuja kwako mara ya pili na ya mwisho, ninaomba uachane na mke wa mganga Kamulenga, utakuja kupata matatizo magumu hautaamini” mganga alinitamkia maneno yale ya kishujaa kisha akatoweka zake.
Nilijikuta kama hali ile ya kutokewa na mganga ninaizoea kwa sababu alikuwa ananitishia tu na hamna action yoyote inayochukua nafasi, hivyo mimi sikujali nikajua kwamba kwa sababu mke wake ameishi naye kwa muda mrefu hivyo basi ataweza kunisaidia mimi wakati nikipata matatizo.
Nilimtumia message “Umefika?”
“Hapana ndo ninakaribia” alinijibu
“Ok but Mzee kanitokea tena, nimeogopa sana na ameniambia kwamba ni onyo ya mwisho hivyo yatakayonikuta nisimlaumu”
“mmh, embu subiri nakupigia” aliniamba Zuhura
“Poa” nilimjibu na kutulia kimya nikisubiri nipigiwe, lakini ilichukua muda mrefu kama dakika kumi hivi ndipo niliona amenipigia simu na mimi nikapokea
“Hallo……hallooow” niliita lakini sikusikia akijibu, ikabidi niweke sauti kubwa ili nimsikie lakini kiukweli hakuniongelesha bali alikuwa amenipigia makusudi ili nisikie anayotaka kuyafanya kwa mumewe
Zuhura: We mzee (Allimuita mumewe)
Mganga: Unaniita mimi mzee
Zuhura: Unadhani, nani si tupo wawili tu hapa, au unamuona mzee mwingine hapa?
Mganga: Zuhura, acha kunidharau
Zuhura: Lazima nikudharau, wewe umeamua kunioa mimi ili nije niwe mkeo, maana ya mke ni nini? Ni kuja kufanya hizi kazi zako za kitumwa za kutumikishwa katika uchawi? Ee sawa ulilipa mahari, mahari ya nini sasa wakati hakuna hata mapenzi tunayofanya, ndoa gani haina tendo lake? Au unafikiri mimi ninaweza kuvumilia, mbaya zaidi ni kwama unaenda eti kwa mtu wangu unamtishia tishia, ole wako apate tatizo lolote
Mganga: Hivi Zuhura mimi ndiye unaniongelesha hivyo?
Zuhura: Wewe hujielewi mzee, kwanza ninataka niondoke kwetu nikakae na wazazi wangu mimi sitaki tena kuishi na wewe
Mganga: Hahahaa, ukisema unafanya hivyo, wazazi wako wote watakufa
Zuhura: Usinitishe
Mganga: Sikutishi wewe ni mtoto mdogo, nakuambia hivi, hautakiwi kufanya tendo na yule mtoto mdogo sasa ukifanya naye mbona wote mtajuta
Hizo zilikuwa sauti kutoka kwenye simu ilibidi nikate kwa uoga maana sikuwa na njia ya kufanya nilikuwa nimeshapata uoga sana
Nilibaki nikitafakari nifanyeje ili kupata uhuru wa mahaba na msichana mzuri kama yule, lakini niliogopa nisije nikauawa au nikafanywa kichaa duniani wakati sina hata mtoto wala kitu chochote cha kukumbukwa nacho kama nyumba au gari
Ilionekana kwamba mwanamke yule alinipenda kweli ndo maana amekuwa tayari kumwambia maneno magumu kiasi hicho mke lakini sikuwa na budi kuzidi kumkwepa. Nikiwa nawaza hayo yote, mara message iliingia kwenye simu yangu “Hallo umesikia nilivyokuwa namchana et?” aliniambia lakini mimi sikujibu nikatulia huku nikiwaza na kuwazua
Niliondoka moja kwa moja na kwenda hadi nyumbani kwa Ba Fetina, nia yangu ilikuwa ni kumuomba ushauri kuhusu mke wa mganga lakini kwa bahati mbaya sikumkuta nikaondoka na kwenda mpaka kwa mangi ndipo nilipomuomba anishauri
“Kaka nimepata taabu sana siku hizi” nilimuambia baada ya kufika pale kwake
“Tabu gani kijana wangu”
“broo unamfahamu Zuhura?”
“yule mke wa mkuu?”
“ndio”
“amefanyaje?”
“Daah, yaani ananisumbua kila mara anataka nitoke naye, mganga kila siku ananitokea akinipa onyo yaani naogopa sana kaka” nilimuambia kwa wasiwasi
“ahahaaha” mangi alicheka sana “si ushakula lakini?” aliniuliza nikashindwa kujibu lakini aliponitazama usoni tu najua alipata jibu kwamba nimekula ile kitu “sawa nimeshajua kwamba ushapita, sasa sikiliza, yule mganga hana lolote wewe piga tu, atakutishia tu lakini hawezi kufanya chochote, mimi mwenyewe mke wake wa pili ndo nakulaga” alinitia moyo
“Kweli?” niliuliza
“Ndio bosi, usiwe na wasiwasi kabisa”
Basi baada ya dakika kadhaa niliamua kuondoka na kwenda nyumbani kwangu, kichwani nilipata nafuu ya maumivu yale ya kitu nilichokuwa nimeambiwa na mangi kwamba niitafune ile kitu ndipo nikapata jibu kwamba kumbe hata nikila sitapata shida kama na yeye alikuwa anakula mke wa pili wa mganga basi mambo ni safi
Kwa sababu nilikuwa nimeshakolea na penzi la binti yule nilijipata namuandikia sms muda huo huo “Baby nina ny…. Balaa” nilimuambia
“mmmmmh, wait siku mbili tu, nitakupa utamu kwanza ninakuandalia uinjoy ninaifukiza na majani ya kutosha” alinijibu nikapata munkari
“mmmh haya bana ila angalia nisife”
“usiogope hamna chochote kitakachotokea
***
Siku iliyofuata nilienda kazini na Ba Fetina halafu nikarudi jioni na kuandaa mazingira kwa ajili ya kesho yake asubuhi, nilimaliza nikampigia simu na kumuambia awahi asubuhi ili tukulane kwa raha, kichwani sikuwa na wasiwasi sana maana mangi alikuwa ameshanitia moyo tayari kwamba hata kama ni mke wa mganga hiyo haina shida
Nilipika cha jioni nikala na kulala.
Asubuhi saa kumi na mbili mlango uligongwa “Nani?” niliuliza baada ya kutoka usingizini
“Zuu Baby” nilisikia sauti ya mtoto
“Ooooh baby” niliamka nikiwa tayari nimeshapata steam za kutosha kwanini litamani sana siku ifike ile, nilishuka kitandani, nikaenda kufungua mlango, binti aliponiona tu hivi akanikumbatia
“Subiri nikakojoe kwanza basi mamy” nilimuambia maana mkojo ule wa asubuhi ulikuwa umenibana hasa
Zuhura hakutaka kuniachia, alizidi kunikumbatia na kunitekenya, huku akicheka cheka na kunipa ulimi nikajikuta nalegea kwa raha kutoka kwake, alinisukuma mdogo mdogo mpaka kitandani nikaenda nikajilza nae akafuata juu yang “Baby si nikakojoe kwanza?” nilimuuliza lakini hakujibu aliendelea tu kunichezea mwilini
Alianza kupapasa hadi akafika katika usawa wa bukta yangu na kupapasa nikashangaa ameduwaa kidogo huku akizidi kupapasa, niliinua usoni na kutazama lakini alikuwa ameshangaa
“Vipi” nilimuuliza nikashangaa ameshusha bukta yangu na kutazama ndani ndo akashangaa zaidi “mbona umeshangaa sana?” nilimuuliza
“Haipo” aliniambia kwa mshangao, ndipo nikashtuka na kuinuka kutazama
“Haipo nini?” nilimuuliza na kujaribu kujishika katika sehemu zangu nyeti, kiukweli nilishangaa pako flat yaani hakuna kitu, lakini mkojo ulikuwa umenibana, yaani niliogopa kwa kweli “We acha masihara” nilisema huku nikianza kutetemeka halafu nikainuka na kushusha bukta vizuri nikashangaa kweli haipo nikaogopa zaidi baada ya kuthibitisha kwamba haipo kweli…...ITAENDELEA🔞MKE WA MGANGA 08
Tulipoishia
“Haipo” aliniambia kwa mshangao, ndipo nikashtuka na kuinuka kutazama
“Haipo nini?” nilimuuliza na kujaribu kujishika katika sehemu zangu nyeti, kiukweli nilishangaa pako flat yaani hakuna kitu, lakini mkojo ulikuwa umenibana, yaani niliogopa kwa kweli “We acha masihara” nilisema huku nikianza kutetemeka halafu nikainuka na kushusha bukta vizuri nikashangaa kweli haipo nikaogopa zaidi baada ya kuthibitisha kwamba haipo kweli
Endelea
“Festo” Aliniita Zuhura na kunishika mimi nikawa naanza kulia machozi maana ni mateso nilikuwa ninaanza kuyapata “Relax, jilaze kitandani niirudishe kichawi” Aliniambia
“Unaweza kweli?” niliongea naye kwa wasiwasi mkubwa
“Usijali we lala chali”
Ilibidi nifuatie maelekezo aliyokuwa amenipa hivyo nikajilaza chali na kusubiri anifanyie mchakato wa kurudisha “daaaah ikirudi hakika sitarudia tena” niliwaza kichwani mwangu na machozi yalikuwa yananitiririka hasa
Zuhura aliegesha mkono wa kushoto juu ya eneo la sehemu zangu nyeti, lakini msomaji/msikilizaji kumbuka palikuwa kweupe yaani hamna kitu, mkono mwingine aliunyosha juu na kuanza kutamka maneno ya ajabu ajabu ambayo sikuweza kuyashika kabisa kwani yalikuwa ni maneno ya kichawi wakati mimi mwenye nilikuwa sio mchawi
Alitamka maneno hayo kwa muda mrefu kama dakika tano hivi, macho yake alikuwa amefumba na alipokuja kufungua na kutazama pale bado kitu kilikuwa ni empty, nikaona amenitazama usoni na kukimbia kwa uoga kuelekea nje na hakurudi tena
“We Zuu, vipi tena?” niliita kwa mshtuko na mimi nikainuka kwenda moja kwa moja hadi njekumtazama, kwanza sikumuona nikajua ameshindwa ndo maana ameamua kukimbia baada hakuwa na uwezo wa kurudisha ile kitu
Nilirudi ndani nikiwa nalia, kichwa changu kilikuwa kizito, mikono niliiweka kwenye maeneo hata kama itatokea nifurahi tena lakini ndo hivyo siku na uwezo kabisa, nilikata tama
Kilichokuwa kinaniuma zaidi ni kwamba nilikuwa nina bonge la mkojo katika kibofu changu, lakini namna ya kulitoa hilo kojo nilikuwa sina, hivyo basi niliamua kujilaza kitandani huku nikiwa na mawazo sana
“Mzee kamulengaaa” niliongea kwa wasiwasi huku nikilia sana, kichwani nilikuwa nawaza itakuwaje na nitaishi vile kwa muda gani “Naomba unisamehe baba yangu, ni ulimbukeni tu sitarudia tena” nilijikuta nikiomba msaada kwa mtu ambaye hata nilikuwa simuoni lakini nilihisi huko alipo angesikia kwa sababu alikuwa ni mchawi.
Niliendelea kulala mwisho kausingizi kakanipitia kabisa nikasinzia, nilikuja shtuka kama baada ya saa zima hivi, nilikuta uso wangu umeloa maji mengi halafu mimi ule mkojo niliokuwa nao ulikuwa hamna tena, ikabidi nijishike kwenye sehemu nikashangaa kwamba sehemu bado hazijarejea
Nilianza kufuta maji usoni, lakini nilipofuta hivi, nilishtuka kwamba kuna kitu kiko usoni ambacho sio cha kawaida, nikaguna na kukishika vizuri ili nijue nini nini
Nilipojaribu kukishika vizuri niligundua kuwa kilikuwa ni uume umehamia katika paji langu la uson, nilishtuka na kuinuka kitandani nikatoka chapu na kuchukua kioo nikajitazama usoni
Simanzi ilizidi pale nilipokuta sehemu zangu za siri zimehamia katika uso wangu na zimening’inia na korodani zake kabisa, “mamaaaa” nilijikuta ninalia kwa uchungu huku nikilegea na kuketi chini bila kutarajia halafu, nikajishika shika usoni na kujipapasa bila kujua nifanye nini
Akili yangu ilikuwa imeshaganda, machozi yalikuwa yananitoka, ndipo nikagundua vitu vitatu kwamba kumbe mangi alinidanganya, halafu cha pili kumbe ndo sababu ya yule binti kunitazama usoni halafu akakimbia baada ya kuona kitu kiko usoni mwangu na cha tatu, yale maji yaliyokuwa usoni baada ya mimi kushtuka kumbe yalikuwa sio jasho wala maji, bali ulikuwa ni mkojo niliojikojolea kwa dudu iliyoko usoni
Hakika niliishiwa nguvu
Nilianza kumlaumu Mungu kwa kuniachilia mateso kama yale, hata hivyo nilipata wazo kwamba nimpigie mangi, ndiye anayeweza kunisaidia katika tukio lile linitoke, hivyo niliinuka na kwenda moja kwa moja hadi chumbani nikachukua simu yangu na kumtumia ujumbe mangi
“Kaka naomba ufike nyumbani sasa hivi nimepata tukio gumu sana, naomba tafadhali” nilimtumia ujumbe lakin yeye hakujibu, nilibaki nikilia maana sikuwa na dakika za kumpigia mangi ili aje kunisaidia muda ule
Nilikaa kama dakika ishirini hivi, nikasikia mlio wa pikipiki nje ya nyumba, hivyo niliinuka taratibu na kusogea dirishani nikachungulia nje
Nilipochungulia nje, niliona kumbe ni mangi ametii wito wangu, alikuwa amekuja na pikipiki yake akapaki halafu akasogea nyumbani na kuanza kuita “Hodiii hodi” aliita
“Karibu kaka” niliitika na kusogea mlango nikafungua halafu nikachukua shuka nikajifunikia asije akaona tukio lile lililokuwa limetendeka katika uso wangu “Broo ingia ndani” niliongea kwa sauti yenye kukata tama nikaona mangi ameingia ndani
“Vipi asee kuna shida gani mbona umeniita harihari sana” aliniuliza, mimi nikatoka chumbani na kwenda sebuleni, na shuka langu hivyo hivyo., machozi yalikuwa yananitoka maana sikuwa na tumaini hata chembe la kuwa mzima, nilijua lazima tu nitadhalilika
Nilishindwa kumuelezea maana nilikuwa nimechanganyikiwa, nilibaki nalia tu “Nini sasa bwashee mbona unalia tu, nikueleweje” Aliniuliza nikamtazama usoni “Halafu hayo mashuka ya nini kichwani”
“Broo….” Niliita kwa huzuni “brooo” nilijaribu kuongea lakini bado nilishindwa, nikaona amesogea karibu yangu na kulishika lile shuka akalivuta na kuacha kitu nyeti iliyokuwa usoni ikionekana
“Oh oh ohoh oh oh” aliguna kwa mshangao kwa kweli nafikiri hakuamini kilichonitokea “Hii imekuwaje tena ndugu yangu?” aliniuliza mimi nikaendelea kulia tu
“N yule mke……..hihihiiii” nilishindwa kumalizia sentesi nikabaki ninalia tu lakini aliniaelewa nikaona amenifunika kwa ile shuka
“Nenda kavae nguo tukalimalize ili tatizo haraka, usije ukaaibika hapa mjini” aliniambia
“Kweli broo?” nilichangamka kidogo baada ya kusikia maneno yale
“Wee nenda kavae vizuri atakuwa ni Kamulenga huyu aliyefanya hivi nakuambia”
Hata hivyo niliona kwamba sio mbaya ngoja nikaingia chumbani haraka, nikavaa nguo zangu na kutoka huku nikiwa bado nimefunika paji la uso wangu watu wasijeona lile tukio
Haikuchukua muda, tulitoka nje, mangi akanisaidia kufunga mlango wangu wa nje halafu tukaenda kwenye pikipiki tukapanda na safari ikaanza
“Itakuwa yule mganga hajapenda kitendo cha wewe kukata masharti ndo maana anakuonea” aliniambia “Unajua yule yeye hafanyi chochote na wanawake wake, hivyo basi huwaacha tunawala sisi, sasa nashangaa huyu yeye kakufanyia hivi kwanini” aliniambia mangi
“Daaah naogopa sana” niliongea kwa busara na nidhamu huku nikitikisa kichwa changu kwa huzuni,
Hata hivyo japo palikuwa mbali sana kule tulipokuwa tunaelekea, lakini pikipiki ilitusaidia tukafika baada ya dakika kama 30 hivi, ilikuwa ni katikati ya barabara iliyozungukwa na misitu kila kona japo ilikuwa barabara ya lami, ilikuwa inaitwa misitu ya miombo ambayo ilikuwa ikitisha sana mitaa ile.
Kwanza tukiwa pale tulishangaa limekua kundi la nyuki wengi halafu wakanivamia mimi, na kumuacha mangi salama, nilipiga yowe maana waliniuma sana, lakini sikuishiwa nguvu, nilikuwa nataka msaada, ikabidi tuanze sasa kuingia ndani ya msitu, ghafla nikasikia kama masizi yananidodokea nikatazama juu hivi, moshi umetanda, yaani panatisha
“Kaka ndo nini hiki?” nilimuuliza mangi maana mimi nilikuwa siamini
Mangi alianza kushangaa naye, tukawa tunashangaa wote kinachoendelea
Sasa tukiwa tunashangaa pale, ghafla moto ulituzunguka pembeni yetu, ukawa unachoma kwa kasi yaa ajabu sana ,tukijaribu kukimbilia kushoto moto, kulia moto, nyuma moto, mbele moto, nikabaki nimeduwaa na nimekata tama
“MUNGU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOWAHI KUKUKOSEA KWA KUWAZA KWA KUNENA NA KWA KUTENDA, MAANA NAJUA HUU NDO MWISHO WA MAISHA YANGU, NINAOMBA NIJE NIURITHI UFALME WAKO… AMEN” hiyo ilikuwa ni sala yangu niliyohisi itakuwa ya mwisho maana sikuwa na pa kukimbilia kutokana na moto kutuzunguka pande zote………ITAENDELEA🔞MKE WA MGANGA 09
Tulipoishia
Sasa tukiwa tunashangaa pale, ghafla moto ulituzunguka pembeni yetu, ukawa unachoma kwa kasi yaa ajabu sana ,tukijaribu kukimbilia kushoto moto, kulia moto, nyuma moto, mbele moto, nikabaki nimeduwaa na nimekata tama
“MUNGU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NILIZOWAHI KUKUKOSEA KWA KUWAZA KWA KUNENA NA KWA KUTENDA, MAANA NAJUA HUU NDO MWISHO WA MAISHA YANGU, NINAOMBA NIJE NIURITHI UFALME WAKO… AMEN” hiyo ilikuwa ni sala yangu niliyohisi itakuwa ya mwisho maana sikuwa na pa kukimbilia kutokana na moto kutuzunguka pande zote
Endelea
Baada ya kuomba pale moto ulitufikia nikapiga kelele lakini ghafla ni kama vile nilivutwa na kitu fulani, nikapotea katika ulimwengu wa kawaida, halafu nikawa sina fahamu kamili
Nilikuja kuzinduka nikiwa nimezunguka na mganga yule na wake zake watatu, pembeni yangu alilaza Zuhura na nilipomtazama alikuwa usoni naye kabandikwa kidubwana chake nikachanganyikiwa
“Niko wapi?” niliongea kwa mshangao maana sikuamini kwamba nimeweza kuwa salama kutoka katika moto ule
“Hahahaaa” mganga alicheka “Hapa panaitwa Katikati ya Miombo, nimeamua kukuleta sasa na kukuonyesha kwamba nina nguvu za ajabu sio wa kunidharau
Ilibidi niinuke na kupiga magoti “Baba” nilianza kumuita jina baba
“Aaah, usiniite baba, mimi sio baba yako, ninaomba tuheshimiane, wewe ni mume mdogo kwa mke wangu, sasa nimewawekea sehemu za siri usoni fanyeni mlichokuwa mnataka kufanya pale nyumbani basi” alisema kwa hasira
“hana mkuu wangu, naomba unisamehe, nisaidie niweze kuwa salama, nakuahidi hivi mimi sitorudia tena” aliniambia
Zuhura alikuwa amekata moto pale chini, na niliona amezinduka kutoka kwenye kupoteza fahamu halafu akanitazama usoni “nono nono usiogope Festo, niko hapa” aliniambia na kuinuka pale alipokuwa amelazwa akanishika mkono na kumgeukia mumewe
“Sikiliza Mzee kamulenga, mimi sikupendi, na sasa ninaomba talaka yangu, hizi zilizoko usoni hazina shida tutaendelea kufanya kama kawaida” aliongea ikabidi nimshangae maana kwa hali zile tulizokuwa nazo mimi sikuamini kama angeongea shiti kwa mumewe kiasi kile
“unaongea nini Zuhura?” nilimuuliza kwa mshtuko maana sikuamini kama ni sahihi yeye kuongea vile
“Acha nimpe talaka yake nione ataenda kufanyeje huko mbele” alisema mzee na kuingia kibandani halafu akatoka na kikaratasi kilichoandikwa talaka tena zikiwa ni tatu kabisa
“Hapana mzee kama ukimpa talaka wewe mpe, lakini mimi ninakuomba msamaha, naomba uniponye niweze kuwa mzima nifuate maisha yangu mwenyewe”
“Hongera kijana, una nidhamu, hili limwanamke ni likahaba, acha akaendelee kuiuza hiyo hapo usoni” alisema na kumkabidhi yule mwanamke talaka halafu Zuhura alinivuta tuondoke wote lakini mimi niligoma kuondoka naye
Alipoona nina msimamo wa kutoondoka naye, basi aliamua kuondoka akiwa na hasira kali na kupotelea msituni
Mimi nilizidi kumpigia magoti mkuu mganga huku nikimuomba msamaha, hata sikuelewa kwanini Zuhura ameamua kunipenda mimi kabisa yaani, nilichanganyikiwa nikamuona kama vile hana akili
“Mzee nisaidie niweze kutoka katika hali hii”
“hahahaa, sawa kijana, lakini unapoambiwa uwaheshimu wazee wa Ujiji kigoma, Basi inabidi uwe makini sana” Aliniambia mzee mimi nikatikisa kichwa ishara ya kumkubalia
Wale wake watatu waliobaki, walinishika na kunilaza chali halafu wakanivua nguo zangu zote nikabaki kama nilivyozaliwa, hata sikuona aibu maana nilikuwa na stress za hatari na nilikuwa ninahitaji msaada hivyo sikuwa mbishi
Mke mmoja kati yao alichukua Kibuyu chenye damu halafu akaanza kunizunguka na kuimba nyimbo za ajabu ajabu huku akimimina ile damu juu paji langu, na maeneo ya chini ya kitovu.
Niliona mganga amekuja na panga lililokuwa limeng’aa vizuri halafu akanitazama usoni “Fumba macho” Aliniambia na mimi nikamtii
Baada ya kufumba macho nilimsikia ameanza kunena kilugha, sio kilugha kiarabu sio kiarabu nikabaki nimetulia kimya kama dakika tatu hivi halafu nilisika paaaah amenishushia upande wa panga kwenye sehemu za chini ya kitovu changu.
Nilipiga kelele kwa maumivu makali mpaka nikafungua macho, ile nafungua macho hivi nilishangaa sipo tena eneo lile yaani nilijikuta niko eneo la barabarani, tena nimesimama na Mangi tunashangaana, nikahisi nilikuwa naota
“Vipi kijana” mangi aliniuliza
“mh sio kitu” nilisema na kujipapasa usoni, nikashangaa ile kitu haipo, nikashtuka na kujigusa katika sehemu zangu za siri nikakuta kitu imerudi pale kwenye sehemu yake sikuamini “Broo….imerudi” nilisema kwa furaha maana nilikuwa siamini
“Twende nyumbani sasa” aliniambia na kuisogelea pikipiki akapanda na kupiga stata, tusepe
“No broo hii imekuwaje, huyu mganga anaishi wapi sasa mbona kila nikija nakutana na mauza uza tu nahisi kama ninaota” nilimuuliza
“Hahaha, achana na mke wa mganga, utateseka sana hapa mjini, anampenda yule mwanamke” aliniambia Mangi
“Mbona uliniambia, kwamba hana shida?” nilimuuliza na kupanda pikipiki safari ikaanza kurejea mtaani
“Hahaha, nilikuambia vile ili mwenyewe uamini, yaani kama ningekuambia uachane naye, basi wewe ungehisi labda ninamtaka kumbe hata simtaki mimi”
“Ok ila mke wa pili ni wewe unakula?”
“hapana nilikudanganya”
“Dooh haya bwana”
Unajua nilivyokuwa nimepitia mambo magumu, mimi sikutamani tena kumuona Zuhura, kwani yeye ndo alikuwa chanzo cha matatizo hayo, kichwani mwangu kwanza sikuamini kwamba nitakuwa nadindisha tena, hivyo basi nilipofika nyumbani tu hivi, nilienda bafuni nikaoga huku nikitafuta stim ya hisia angalau niweze kuthibitisha kama imerudi ikiwa nzima
Nilivuta hisia za yule mwanafunzi lakini haikusimama, nikavuta hisia za madem zangu wa nyuma kibao yaani lakini bado haikusimama, nikahisi bado haijakaa mkao, hivyo bado uoga ulizidi kuniandama.
Nilianza kuvuta picha za video za ngono nilizokuwa nimezitazama siku za nyuma yaani lakini kamwe kitu hakikusimama, nikawa nimeshapata stress upya lakini nilipojaribu tu kumvuta Zuhura kwenye akili yangu, haikuchukua hata sekunde kumi, nikaanza kusikia utamu na ub…ukasimama dede
Nilishangaa sana, na niligundua kuwa nina hisia kali sana na Zuhura, yaani nilipokumbuka body yake tu hivi, nilijikuta nimeshaanza kujichua kwa mkono wa kushoto taratiiibu na kufmba macho halafu sikuweza kuacha kujichua mpaka nikakojoa mule bafuni
Baada ya tendo lile nilijidharau nikaona kama vile nimezingua sana kwa kweli, hii ni kwa sababu nyeto haikuwa kitu cha maana kabisa na hata hivyo nilijilaumu, lakini nilijiuliza “Mh kwani Zuhura ana nini mbona ni mtamu kiasi hicho jamani”, hata hivyo nilijikuta nimemaliza kuoga na kutoka nje.
Nilienda chumbani nikiwa ninajiamini kwamba na mimi ni mzima kabisa kwa nilikuwa nimedindisha kiukweli lakini nilidindisha baada ya kumkumbuka Zuhura.
Baadaye ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni, niliondoka na kwenda kwa mama ntilie nikale maana nilikuwa naona uvivu wa kupika kichizi yaani, hapo nilijikuta nimeshaishiwa pozi kwa sababu ya tukio lililonitokea asubuhi yake
Nilipofika kwa mama ntilie niliketi pembeni ya mwadada mmoja aliyekuwa amejifunikia hijabu, na alikuwa anakula viepe, halafu alikuwa anaitazama simu yake
“Za saa hizi” nilimsalimia
“Poa” nilishangaa sauti ya Zuhura imetokea nikashtuka kwanza na kumtazama
Yule mwanamke aliinua uso akanitazama, alikuwa ni Zuhura kweli, uso aliufunika kwa hijab yakabaki macho tu, nikaamini ni yeye na alikuwa amefunika ili ile naniliu isionekane.
“Zuhura” Nilimuita kwa mshanga halafu akatabasamu na kuzidi kunitazama
“Hahahaaaa ni mimi ndio”
“Daah, basi kwa heri” niliinuka na kutaka kuondoka lakini alinivuta nikajikuta nimeketi tena kwenye kiti nikamtazama kwa hasira, lakini alishika pini za hijabu zake akafungua na na kuacha uso wake wazi, nilipomtazama hivi kile kidude kilichokuwa usoni kilikuwa hakipo tena, sijui alikitolea wapi
“Hee umekitoaje kile?” niliuliza
“haha, hakuna nisiloliweza, si nilikuambia unifuate ukakataa?” aliniambia
“Dooooh” nilibak nikimshangaaa……ITAENDELEA🔞MKE WA MGANGA 10
Ilibidi niahirishe tu kula, nikaondoka pale na kuenda kwa mama lishe mwingine, nikiwa njiani nilikuwa nawaza sana kwamba haya mambo yanaendaje “hivi ni kweli au naota?” nilikuwa nikijiuliza peke yangu “au karudi kule kwa mumewe kufanya mpango wa kuwekwa sawa?”
Nilijiuliza maswali mengi sana maana nilikuwa siamini kwamba yule binti aliweza kujitoa kidude chake kilichokuwa kimehamishiwa usoni kwa uchawi halafu akitoe bila kwenda kwa mchawi aliyemuwekea, hakika nilipata mawazo
“usikute ni trick wananichezea, sasa kwa taarifa yao hawanipati kirahisi” nilijisemea kwa roho shupavu na muda huo nilikuwa njiani nikielekea kwa mama ntilie mwingine nikale
Nilifika kwa mama lishe huyo nikaagiza ugali mkubwa na samaki, halafu nikala kwa furaha na na kumaliza fasta kisa tu nilikuwa na njaa sana siku ile
Nilitoa shilingi 5000 mfukoni nikamkabidhi akakata hapo buku mbili na kunirudishia chenji nikaondoka zangu, njiani nilikuwa sijiamini kabisa lakini nikiwa nazidi kutembea nilikutana na kijana mmoja ambaye alikuwa amevalia suruali ya kitambaa akaifungia maiyeno halafu na shati jeupe aina ya taxido huku kwenye shingo akiwa amenyonga katai kale ka kipepeo
Mkononi alishikia biblia na kitabu cha tenzi halafu alikuwa anaimba zake nyimbo za tenzi peke yake. Nikapata wazo la kumsalimia ili wote tuongozane njia moja
“Habari kaka” nilimsalimia kwa nidhamu maana salama za hawa waliokoka zinatakiwa kidogo zisiwe za kidunia
“Salama Ndugu, bwana Asifiwe” aliniambia sasa hiyo ilikuwa salamu ya kilokole na mimi nilikuwa ni mkatoliki nikajichanganya
“Milele amina” nilimjibu halafu tukaendelea na safari yetu taratiibu lakini tulikuwa wote mabubu ndani ya dakika tano hatukuzungumza
Tukiwa tunazidi kutembea nilisikia simu imeita mfukoni, na muito wa simu yangu ulikuwa ni ule wa Kuku Kapanda Baiskeli wa Mr Nice. Niliitoa simu mfukoni na kutazama nikakuta ni Zuhura ananipigia, hasira ilinishika nikakata na kuweka mfukoni halafu nikatulia
Nilitulia kama sekunde 20 hivi akapiga tena sasa nilikasirika nikakata na kutaka kuzima lakini kabla sijazima nikasikia yule kijana wa kanisani ameniita “Mdogo wangu” aliniita kwa nidhamu
“Nambie broo” nilisema na kurudisha simu mfukoni halafu message ikaingia na wimbo wa Alikiba – Usiniseme, nikaona broo yule ametabasamu
“Sasa ni nyimbo gani hizo unazoweka kwenye simu bwana wewe” aliniongelesha nikatulia sikumjibu mimi nikachukua simu na kusoma ujumbe ule nikakuta ni wa Zuhura
“Sikiliza wewe mwanaume hata kama umeamua kukata simu lakini sikiliza, ninaamini kwamba unajua kabisa kwamba mimi nimeachika, na kuachika nimeachika kwa sababu yako, lakini kamwe sitokubali uniache tafuta njia sahihi ili nifurahie talaka yangu” alinitumia sms iliyoniopa hasira kali mpaka nikatulia kimya tu na kutukana kwa sauti ndogo huku nikiwa nimesahau kwamba nimefuatana na mlokole
“EH eh EH….umeniitaje?” Alisema yule broo mimi nikashtuka na kumtazama
“Mh sio wewe bwana samahani kuna mtu ananiboa kwenye messages, yani ni mke wa mganga mmoja hivi anaitwa kamulenga kama unamfahamu”
“Kamulenga?” yule jamaa aliniuliza kwa mshtuko “Mke yupi Hamisa, Pili, Tatu au Zuhura?”
“Zuhura, yaani naona kama ananiganga wakati mwenyewe namuogopa mume wake”
“Hahaha…..ndugu yangu hilo ni liroho linakusumbua ninawajua vizuri watu wale” aliniambia
“Uliwajulia wapi?”
“Ndugu nimepelekwa pale kutafuta pesa, lakini yaliyonikuta sio mema, nimetoka na mke wa Tatu wa mganga, kilichonikuta sitokisahau, hakika ninatamani nisikumbuke”
“Acha utani kaka”
“Kweli ndugu, yaani usinione nimebeba biblia hivi, yule mganga ndio alinifanya nikaingia kanisani, yaani sitaki kukumbuka
“Ilikuwaje kaka?” niliuliza
“Yaani nilitoka na Tatu, nikashangaa nimegeuza makalio yakakaa mbele, na huku mbele kukawa nyuma, hakika nilidhalilika”
“wacha”
“Ndio, lakini, nilipata uponyaji kwa Yesu, kwa kweli Yesu amenisaidia sitomuacha, nimeshapata amani kwake kabisa na ninamshukuru na nitamtumikia milele Haleluya” alisema mtu yule akinyoosha mkono wa kulia juu uliokunjwa ngumi kwa ishara ya ushindi, hapo hapo nikapata wazo
“Kaka, nisaidie kwa kweli nimeteseka sasa wiki hizi mbili hapa naomba unisaidie”
“Ohohoho,,, pole sana, sikiliza ndugu, mimi ninaitwa Yusufu Mwakisambwe, wewe je?”
“Ninaitwa Festo Dodo” nilimpa jina
“Hongera sana, ninafikiri nimefika nyumbani, maana ni hapa, lakini ninachoomba unisaidie namba yako ya simu, halafu nitakuunganisha na mchungaji wangu Benard Francis halafu atakusaidia kuwa salama” alisema na kutoa simu kali mfukoni nikaguna sana maana nilikuwa na goroka mwenzake
“Mh”
“Mbona unaguna”
“Hamna, naona una msimu wa maana, aisee” nilisema huku nikiichukua ile simu na kuitazama vizuri
“Hahaha, hivi vyote vinapatikana kwa Yesu nakuambia”
“Ok broo andika namba mwenyewe mi hizi simu hapana aisee” nilisema
Yule broo alipokea simu na kuandika namba yangu kisha akaondoka zake kuelekea nyumbani halafu mimi nikanyoosha mpaka nyumbani hata hapakuwa mbali kivile
Nilipofika nyumbani nilifungua mlango wangu na kujilaza kitandani “Naomba Mungu uhakikishe ninaepuka haya matatizo yanayoniandama.
Mara nilisikia mlangoni mtu anagonga, nikamuuliza nani lakini hakujibu akaendelea kugonga
Haikuchukua sekunde nyingi nikajikuta nimeshasepa moja kwa moja na kwenda moja kwa moja hadi mlangoni kufungu, ile nafungua mlango hivi, nkakuta ni binti alikuwa emesmima mlangoni mwangu huku akitabasamu na kunyonya lol pop
“Zuhura” nilimuita kwa mshangao halafu akanifuata na kunikumbatia
“Siitwi Zuhura, mi naitwa Matrida bwana” aliniambia nikashangaa jina gani kama hilo la matrida sasa
Nilimuachia na kumtazama usoni kwa makini nikagundua ni yeye, akili yangu ikaniambia, labda jina kwa mwanzo alinidanganya
“Festo, nimekaa nyumbani, nimepanga chumba changu, nasikia nawashwa halafu wanaume wote naona kama vile wanatania tu, tangu nije Tabora ni wewe tu uliyeweza kunitekenya nikatekenyeka, nataka unisugue unikune mpaka nikuambie basi” alisema kwa hisia na kunisukuma nikadondoka kwenye kochi chali, nikawa nataka kuinuka nimzuie asinifanye hivyo lakini nilishindwa kujiinua pale nilipokwa nimejilaza sijui hata ni nini kilinizuia
Hata hivyo nilizidi kujaribu kujiinua lakini nilishindwa kabisa yaani utafikiri nilikuwa nimepigwa kwa misumari pale kwenye kochi
Niliona Zuhura amevua kanga yake na kuitupa chini halafu akabaki uchi wa mnyama, “Zuhura mimi nitoe hapa”
“MMMMH si nimekuambia naitwa Matrida lakini?”aliniuliza na kunisogelea yani hata mkoni nilikuwa siwezi kunyanyua, nikaona amechuchuma na kunikoboa bukta yangu na boxer nikabaki kama nilivyozalia nay eye akiwa kama alivyozaliwa.
Nilimtazama sana “Sasa unataka mganga aniue?” nilimuuliza lakini hakujibu chochote nikaona amesogea karibu yangu na kuna kupiga magoti halafu akaanza kuichezea koni yangu kwa mikono na kuiingiza mdomoni,
Haikuchukua sekunde hata kumi, nilishuhudia imeinuka na kufoka kwani tayari ilitaka kitumbua, nikaona ametabasamu kwa furaha na kuibusu kichwani
“Naipenda hii, na nataka nikupe utamu wewe Festo” alizid kunitamanisha halafu akainyonya huku akinipapasa katika korodani zangu, nikawa nazidi kupagawa
Aliporizika kuinyonya, niliona ameinuka na kujigeuza halafu makalio yake malaini akiniachia niyaone vizuri,
Zuhura alirudi nyuma taratibu, na kufika pale nilipokuwa nimeketi, halafu akainama na kusogeza miguu halafu akijipanua na kuishika koni akailengeshe kwenye kitumbua chake ambacho nilikuwa nakiona kwa nyuma, kwa kweli nilipagawa hasa nilivyokuwa natazama ikiingia mpaka mwisho
Niliona ameanza kuhangaika nayo kushoto kulia mdogo mdogo huku akitoa miguno iliyokuwa inanipa utamu, nikaanza kunogewa
Nilijaribu kunyanyua mikono ikagoma tena “Zuu achia basi hata mikono yangu basi nishikilie kiuno” nilisema kwa hisia maana utamu ulinoga kila nilipotazama kalio lake akilishusha na kulirudisha juu, yaani hamna raha kama kufanya huku ukimtazama mwanamke kila inapoingia na kutoka…..yaani unajihisi upo peponi
“Nyanyua mikono nishainenea tayari” alisema Zuhura na mimi nilijaribu kunyanyua mikono ikanyanyukaa halafu nikashika kiuno chake huku binti akiwa bado anahangaia nayo
“Ash asssssh oooh baby…..tamu” Zuhura alisema kwa utamu huku akizugusha kiuno tukawa tunasuguana
Nilisikia utamu mpaka nikasikia mbegu zinakuja kwa kasi “Aaaaaagh” nilipiga kelele na kuvuta vizuri kile kiuno nikamwagia ndani, ndipo niliposhtuka kumbe nilikuwa naota usingizini daaah
Boxer yote ilikuwa imechafuka bao nililopiga kwenye ndoto ikabidi nishuke kitandani niende moja kwa moja mpaka bafuni kwa ajili ya kujisafisha, yaani nikiwa bafuni nawaza tu “Daaah mbona kila saa namuwaza huyu mwanamke, ana nini lakini?”……ITAENDELEA
Tags
Simulizi 🔞