TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

NIVYOPATA DANGA USIKU WA MANANE KUMBE NI JINI 1-3

1-3

NIVYOPATA DANGA USIKU WA MANANE KUMBE JINI😳😳😳🗣️🙌
EP 001..
Ilikuwa ni majira ya saa nne usiku, mida hiyo kwangu ndio kulikuwa kunakucha. Nilikuwa tayari nishavalia kitopu changu ambacho kiliacha tumbo langu dogo wazi na chini nilivalia kimini ambacho kiliacha mapaja yangu yote nje.

Mwilini nilijipulizia manukato ya kunyegesha pindi mwanaume yoyote ayasikiapo basi anapata hisia kali za mapenzi. Kiunoni nilining'iniza pochi yangu ya kuwekea pesa na mguuni nilipigilia Raba kali nyeupe ambayo ilikuwa ikionekana hata gizani kwani ilikuwa na mistari ya reflector,kisha nikatoka nje na kuwafungia mlango watoto wangu wawili ambao nilikuwa nikiwalea kwa kudanga ili mradi siku ziende.

Niliamia mtaani kwenda kutafuta noti au chambi chambi ili niweze kusukuma hili gurudumu la maisha.

Nikifika kijiweni ambapo ndipo tunapojipanga usiku huo kwa ajili ya kuwasubiri wateja wetu ambao hawaridhishwi vizuri na wake zao ili tuwatimizie haja zao, lakini wengine ni wale ambao hawana wapenzi basi haja zao walikuwa wanamalizia kwetu.

Pale kijiweni kwetu palikuwa na msikitini ambao ulikuwa haujaisha hivyo baadhi yetu tulipenda kulitumia jengo lile kwa ajili ya kuwaridhisha wateja wetu ili zile gharama za gesti ambazo wangetoa tuchukue sisi.

Wakati tumesimama pale kijiweni, akatokea kaka mmoja mrefu na mwenye asili ya kiarabu, kila mmoja wetu akaanza kumpapatikia lakini kaka yule alinifuata mimi. "Ooh jamani mie nimempenda huyu, leo nataka mwenye makalio makubwa"Alisema kaka yule huku akibinya binya makalio yangu mithili ya mtu anayechagua parachichi lililoiva. "Mrembo mzigo huu shi ngapi?" Aliuliza yule kaka. 

" Elfu tano tu Fasta" Nilimwambia.  "Aah mbona bei hivyo wakati hapo bado sijachukua chumba gesti" Aliuliza yule kaka. "Usijali tuzunguke hapo nyuma kuna jengo la msikiti hapo tukamalizane hapo" Nilimwambia huku nikimshika mteja wangu huyo mkono na kumpeleka kwenye jengo la msikiti ambalo tunamalizia haja zetu.

Tulipofika sikuwa na haja ya kuvua nguo nilipandisha tu kimini changu juu kwani hata kufuli sikuvaa kwasababu nilikuwa kazini!.

Ajabu nilipogeuka nyuma ili nimruhisu kaka yule aanze kazi, nilishangaa kumuona sio yeye kasimama nyuma yangu bali mtu aliyevalia baibui refu lililofunika mpaka miguu yake, uso wa mtu huyo ulikuwa hauonekani bali ni giza tupu! Nilitaka kukimbia uchi lakini kabla sijanyanyua hatua moja ghafla .....

NINI KILITOKEA? WANGAPI MPO TAYARI KWA SEHEMU IJAYO! NIWAJUE WAFUASI SASA

NILIVYOPATA DANGA USIKU WA MANANE KUMBE NI JINI😳😳😭🗣️

EP 02.
Tulipofika na yule kaka wa kiarabu kwenye lile jengo la msikiti ambalo lilikuwa halijaisha, nilipandisha kimini changu juu, sikuwa nimevaa hata kufuli kwani bado nilikuwa kazini nikitafuta pesa ya kulea wanangu. Kaka yule alikuwa nyuma yangu akinitizama tu jinsi ninavyojitega mbele yake. Nilipoona nimejitega lakini hafanyi chochote ikabidi nigeuze shingo yangu nyuma ili nimruhusu aanze kazi.

Ajabu nilipogeuza shingo nilishangaa kuona mtu wa ajabu akiwa amesimama nyuma, alivalia babuibui refu sana lililofunika miguu yake,  uso wake ulikuwa hauonekani bali ni giza tupu, nilipiga kelele na kutaka kukimbia lakini ghafla nilijikwaa na kuanguka mbele yake, niliamka haraka na na kuanza kukimbia mbio huku mtu yule wa ajabu akinikimbiza. 

"Pumbavu simama mwanaharamu mkubwa wewe! Unayethubutu kulitia najsi jengo linalotarajiwa kufanyia ibada!" Alisema mtu yule wa ajabu huku akinifukuza kwa speed sana. Hata hivyo sikutaka kusimama, kwani kila nilipogeuza shingo yangu nyuma nilimuona akija spidi sana.

Nilidondosha kimini changu, na wala sikutaka kusimama na kukiokota bali nilikimbia uchi wa mnyama juu nikiwa nimevaa kitopu tu. Kwa bahati nzuri usiku huo mtaani hakukuwa na watu wengi bali kulikuwa na wahuni tu wamejikusanya wakivuta bangi zao. 

Nilipita mbele yao mbio na kuwaacha wakicheka tu huku wakisema "kahaba huyoooo leo kafumaniwa!" Walizomea vijana wale, lakini mimi sijali maneno yao, langu kichwani lilikuwa moja tu. Kujiokoa dhidi ya mtu yule wa ajabu ambaye bado alikuwa ananikimbiza lakini wale vijana nahisi walikuwa hawamuoni.

Nilikunja kona mbili tatu nikapoteana na mtu yule wa ajabu, hapo nikaomgeza mbio na kwenda kufunga breki kali nje ya mlango wa chumba changu ambapo nilikuta taa inawaka kwa ndani, huku kufuli ambalo niliwafungua wanangu likiwa halipo. "Heee kufuli limeenda wapi na nani kawasha taa ndani, au ni watoto wamewasha?" Nilijiuliza mwenyewe huku nikiwa nimepigwa na butwaa mara ghafla nikashangaa.......

JE NINI KILIENDELEA? HAKIKISHA UKISOMA UNALIKE NA KUKOMENT ILI UWEZE KUONA SEHEMU INGINE KWA HARAKA!!!!!
🗣️🗣️🗣️🗣️

NILIVYOPATA DANGA USIKU WA MANANE KUMBE JINI😳😆 03

Nilikimbia ajabu mithili ya swala anayeyanusuru maisha yake dhidi ya swala mwenye njaa kali ajabu😆nilikimbia nikiwa mtup kama nilivyozaliwa lakini sikujali kwani ilikuwa ni usiku tena wa manane na hapakuwa na mtu mtaani, basi, nikakunja🏃‍♀️kona mbili tatu na kupotezana na yule mtu wa ajabu, nilienda kufunga  breki kali nje kwangu😳 baada ya kuona mlango ambao nilikuwa nimewafungia watoto wangu na kufuli usiku ule walale ulikuwa wazi na isitoshe taa ya ndani ilikuwa inawaka.

😳"Mungu wangu sijui kama watoto wangu wapo salama kweli" nilijisemea mwenyewe huku nikipiga hatua taratibu kweli kuusogelea mlango ili nichungulie ndani kwani nilichowaza kama nwanamke ni usalama wa wanangu ambao nadanga kila kukicha ili niwakuze.

Nilipoukaribia mlango nikachungulia ndani 😳 kupitia mwanya mdogo wa mlango, ajabu sikuwaona watoto wangu bali yule mtu wa ajabu mwenye sura ya kutisha ndiye aliyekuwa amekaa kitandani. 

"Heee! Au kawala wanangu! "  Niliwaza huku mapigo ya moyo yakinidunda sana, "aaaah bora tu anile na mimi kama kawala wanangu, sioni faida ya kuishi bila wanangu ambao nimehangaika sana kuwakuza mpaka walipofikia acha niingie ndani na mimi niliwe" nilijisemea mwenyewe moyoni kwa ujasiri sana. Kisha nikafungua mlango.

Ghafla😳 yule mtu wa ajabu akabadilika na kurudi kwenye ule muonekano wake wa kibinadamu na kuwa kijana mzuri wa kiarabu.
"Nimeamua nitangulie mimi maana unajifanya una mbio sana, nilikutega tu nijue kama unaweza kukukubali kufanya mapenzi kwenye jengo la ibada, kumbe ndio kazi yako eee?" Yule kijana wa kiarabu aliniambia na kunifanya nitetemeke sana kwani macho yake yaliwasha taa ambayo ilikuwa inabadilika badilika rangi. 

"Tafadhali nisamehe na unionyesje wanangu walipo?" Niliongea huku nikitetemeka sana. "Sawa nitakusamehe na nitakupeleka sehemu watoto wako walipo lakini ukubali kufanya mapenzi na mimi nikiwa kwenye umbo la jini" alisema nikaogopa sana lakini nikaamua kujikaza iwapo nitaweza ili nisiuliwe na kuwaacha watoto wangu duniani ambao bado walikuwa ni wadogo.

"Sawa nimekubali kwa ajili ya wanangu" nilijibu. 

😳 Ghafla kijana yule wa kiarabu akageuka na kuwa jitu la ajabu sana, alikuwa mrefu mpaka kichwa chake kiigonga kwenye bati,  mwili wake ulifunikwa na koti refu, jeusi, ambalo alianza kulivua,  nilipotupia jicho uuume wake khaaaa😳 nilijukuta......

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post