Muda hutufundisha thamani ya maisha...
______________________
Usipotumia muda wako katika kufanya mambo ya msingi, basi mambo yasiyo ya msingi ndiyo yatatawala matumizi ya muda wako!
Uelewa kuhusu muda bado upo katika kiwango cha chini sana miongoni mwa watu wengi, na hii ndiyo sababu kubwa watu wengi hutumia sehemu kubwa ya muda wao kufanya vitu visivyokuwa na thamani kabisa au vyenye thamani ndogo!
Je muda wako wote wa thamani ulionao huwa unatumia kufanya nini?
Kumbuka, ili jambo fulani liweze kutokea ni lazima lifungamane na kipindi fulani cha muda!
Hii inamaanisha pasipo uwepo wa muda hakuna chochote kile kitakachotokea!
Hivyo basi endapo utakuwa hauna chochote cha maana unachokifanya kwenye matumizi ya muda wako, hakuna matokeo ya maana utakakayoyapata maishani mwako!
Unatakiwa kujua kwamba wengi wetu huwa tunaishia kuwa watu wa kawaida, pamoja na kupata matokeo ya wastani kutokana na namna tunavyotumia muda wetu!
Weka suala hili akilini mwako, daima muda huwa ndiyo kizuizi cha mwisho, kwani hauwezi kurudishwa nyuma, kusimamishwa, kusogezwa mbele wala kupunguzwa...
Mpenzi msomaji unatakiwa kujua kwamba kuna muda ndani ya muda!
Hivyo basi unaalikwa kuanza kuhesabu muda wako kuanzia sekunde moja hadi nyingine, kwani kupitia sekunde dakika hupatikana, kupitia dakika saa hupatikana, kupitia saa siku hupatikana kupitia siku wiki hupatikana, kupitia wiki miezi hupatikana, kupitia miezi mwaka, hupatikana kupitia mwaka miaka hupatikana. N.k
Hii inamaanisha kwamba kuna muda ndani ya muda hivyo basi ukipoteza hata sekunde moja tu umepoteza kitu kikubwa sana...
Hakuna aliyependelewa muda, bali sote tuna muda sawa, ila tunaishia kupata matokeo tofauti kutokana na namna tunavyotumia muda wetu!
Usipochunga matumizi ya muda wako, hakuna atakayechunga!
Jifunze kukomboa wakati, ili upate matokeo makubwa maishani mwako!
Kumbuka kwa kila jambo Kuna majira yake.
Hata hivyo hauwezi kuotea muda bali unaweza kuotea kufanya jambo fulani kutokana na muda uliopo!
Kesho nitakusogezea mambo matano Kuhusu Muda!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e mwalimu mwandishi muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi life coach and consultant!
Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no+255744284329
Tags
Elimu
Good work bro
ReplyDeleteAppreciate it
ReplyDeleteSee you at the top 😊