Huwezi Kufanikiwa Kimaisha Kama Hutojijua Wewe Ni Nani...
______________________
Katika maisha usipojijua wewe ni nani na unaweza ukafanya nini, basi mtu mwingine atautumia huo udhaifu wako ili ajinufaishe zaidi...
Moja ya kitu cha msingi sana unachopaswa kujua ni kwamba, utaanza kuishi Maisha yako halisi siku utakayojijua wewe ni nani!
Vilevile unatakiwa kujua kwamba, kama mpaka leo hii bado hujajijua wewe ni nani, basi bado hujaanza kuishi maisha yako halisi!
Sijajua labda kama nimekuchanganya, lakini niko hapa kukuletea habari njema kwamba, utaanza kuishi Maisha yako halisi siku siku utakayojijua wewe ni nani, unaweza ukafanya nini na uliumbwa kwa kusudi gani...
kwa muda mrefu nimekuwa nikichunguza jamii yangu pamoja na wanajamii wake! Kwa harakaharaka naweza kusema nimebaini tatizo kubwa sana! Tatizo lenyewe ni kwamba wanajamii wengi hatujijui sisi ni akina nani na tunaweza tukafanya nini!
Kutokana na suala hilo nikaona leo nikuandalie makala kidogo kuhusu elimu ya kujitambua, ili tujijue sisi ni akina nani, na tukishajijua basi itakuwa ni rahisi sasa kuweza kujisimamia, kujiongoza pamoja na kujitawala...
Pia tutajua nini tunakitaka katika maisha yetu, pamoja na kujua tujifanyie nini sisi na maisha yetu!
Nini Maana Ya Kujitambua?...
Kwa tafsiri nyepesi kujitambua ni ile hali ya mtu kujifahamu kiundani kuhusu hisia, ubora, udhaifu, mahitaji yake pamoja na vitu vinavyoendesha mfumo wa maisha yake...
Au kujitambua ni ile hali ya mtu kujifahamu yeye na utu wake...
je wewe unautambua vyema utu wako kweli?
Hata hivyo kwa mujibu wa tafiti za kisaikolojia zilizowahi kufanyika zimeonesha kwamba watu wengi ni wajinga kuhusu sisi wenyewe yaani hatujijui kuanzia:
Mimi ni nani....
Ninamiliki nini ndani yangu....
Ninaweza nikafanya nini...
Nidhibiti nini katika maisha yangu pamoja na kutokujua ubora na udhaifu wetu...
Ukiachilia mbali suala hilo kuna watu ambao hudhani kujitambua ni kuwa na umri mkubwa, kuna watu hudhani kujitambua ni kujua jinsia zao, kuna watu hudhani kujitambua ni kuwa na kiwango kikubwa cha elimu, kuna watu hudhani kujitambua aidha ni kuoa au kuolewa, kuna watu hudhani kujitambua ni kuwa na cheo kikubwa pamoja na kuwa na kazi nzuri...
Kitu unachopaswa kujua ni kwamba hizo zote ni dhana potofu kuhusu tafsiri ya neno kujitambua...
Mpendwa kujitambua kunakozungumziwa hapa ni ile hali ya wewe kujijua vizuri hasa wewe ni nani, umetoka wapi, uko wapi na unakwenda wapi?
Kwa ufupi niseme kujitambua ni uwezo wa kutambua kusudi la kuumbwa kwako...
Je mpaka hapa ni kweli unajitambua?
Na Kama unajitambua je wewe ni nani?
Kwanini upo hivyo ulivyo?
Unataka nini katika maisha yako?
Ubora wako ni upi?
Na je unaweza ukafanya nini kitakachokufanya wewe uwe Wewe?
Mpenzi msomaji unahitaji maarifa ya kutosha ili ujijue wewe ni nani!
Wengi wetu tumeshindwa kuwa akina sisi halisi, kwa Sababu maarifa yetu tuliyonayo yameshindwa kututambulisha sisi ni akina nani!
Nakutakia tafakari njema!
Tafadhari chukua hatua, unatakiwa kujua kwamba hakuna atakayebadili maisha yako pasipo uhusika wako!
Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwalimu, mwandishi, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!
Unaweza kuwasaliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329
Tags
Elimu