TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

MWANAMKE ANAOMBA RUHUSA ILA MWANAMME ANATOA TAARIFA TU

CHUKUA HII ITAKUSAIDIA
 Sikupangii ila kama unaingia kwenye ndoa beba hiki kitu “Mwanamke anaomba ruhusa ila Mwanaume anatoa taarifa! Tu.
Hakuna usawa katika ndoa bali kuna wajibu katika ndoa, ndiyo maana Mwanaume asipohudumia familia mwanamke analalamika lakini hujawahi sikia mwanamke kapelekwa ustawi wa jamii kisha hatoi matumizi!

Achana na kelele za mtaani eti kwakua una kazi yako mwanaume hawezi kukupangia kitu!

Hapana dada ni mume wako anaweza kukupangia kila kitu. Haimaanishi kwamba ni lazima ukubali kila kitu lakini pima kwanza kabla ya kubisha!

Mwisho jiulize, hivi nikimbishia hiki kitu nitapata faida gani? Au hivi nikikifanya hiki kitu nitapata hasara gani?

Kwa mfano, ukimuambia mume wako “Naomba kwenda saluni…” nihasara gani unapata mpaka uende saluni aje kusikia kwa watoto!

Kwa mlioko kwneye ndoa najua labda mna utaratibu wenu mshajuana ndoa zenu zishakomaa mshajuana hata hakuna haja ya kuomba ruhusa!

Mume ashakujua ni taarifa ila kwa mnapoingia penda kutumia neno “NAOMBA”

Sio tu wanapangiwa mpaka nguo za kuvaa, lakini hata kwenda kwao kusalimia wanapangiwa!

Kuna wengine wana miaka 7 kwenye ndoa hawajui kwao kukoje ila kwenye Comment wanadai “Mwanaume hawezi kunipangia!”

 ndoa iheshimiwe

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post