TAHADHARI ⚠️ KATIKA TOVUTI /APP HII HAKUNA SEHEMU YA KULIPIA ONLINE UKIHITAJI MWENDELEZO WA SIMULIZI BONYEZA HIYO BUTTON YA WHATSAPP AMA ANGALIA NAMBA YA MTUNZI WA SIMULIZI HUSIKA KATIKA SIMULIZI HIYO

NILIVYOMPENDA MLINZI WA GETINI KWETU BILA KUJUA NI BILIONEA ANAYETAFUTA MKE

*(NILIVYOMPENDA MLINZI WA GETINI KWETU BILA KUJUA NI BILIONEA ANAYETAFUTA MKE💕💕💕🗣️*
*SEHEMU YA KWANZA*

"Norah, we Norah samahani kidogo" Alisema Prosper baada ya kufungua geti ili Norah mtoto bosi aingize gari ndani. Norah alishika Breki na kutoa kichwa nje ya kiyoocha gari. "Unasemaje wewe!" Aliuliza Norah kwa sauti kali.

"Mbona mkali hivyo? Haya vipi sasa kuhusu lile jibu langu?" aliuliza Prosper. Ilibidi Norah atoke nje ya gari. "Hivi wewe Prosper una matatizo ya akili eeh" aliuliza Norah huku akiwa  ameshika kiuno. 

"Inawezekana kwasababu matatizo yangu ya akili yanasababishwa na kukipenda wewe, nikubalie Norah" Alisema Prosper."Nahisi umevurugwa wewe sio bure yani mimi ndio wa kuwa mtu kama wewe, kazi yenyewe kufunga na kufungua geti" aliongea Norah huku akimsogelea Prosper na kumtemea mate usoni. 

Belinda mdogo wake Norah ambaye alikuwa kabaki ndani ya gari, aliamua kutoka garini na kumtuliza dada yake. "We Norah nawe kwani Prosper kakutukana mpaka umtemee mate? Kila mtu ana haki ya kueleza hisia zake haijalishi atakataliwa au atakubaliwa lakini hivi ulivyomfanyia Prosper sio uungwana" Aliongea Belinda. 

"Huyu kazidi huyu, kila siku ananiuliza jibu langu vipi, yani akiniangalia nina hadhi ya kuwa naye au hata kutembea naye barabarani? Wewe mbwa! Niheshimu mimi ni mtoto wa bosi wako?" alisema Norah kisha akaingia kwenye gari na kwenda kulipaki kwenye maegesho yake.

Pale getini alibaki Norah na Belinda. "Yani dada yangu sijui anachoringia ni nini haswa,  hajui maisha yanabadilika haelewi hilo mh shauri yake, usijali Mwaya kaka Prosper ila kesho nilitaka nikutoe out kidogo, twende sehemu tuongee unielewe maisha yako, mimi nitakusaidia hata mtaji ukafanyanye biashara ndogondogo inaniuma sana jinsi unavyotumikishwa hapa nyumbani, juzi nilichukia sana. Norah kakojolea kwenye kopo ndani anakuita mlinzi ukamwage mkojo yani!

Alisema Belinda!

JE NINI KITAENDELEA? ITAKUWAJE KAMA BELINDA AKIJUA KUWA MTU ANAYETAKA KUMSADIA NI BILIONEA ALIYEKUJA NYUMBANI KWAO NA KUJIFANYA MLINZI WA GETINI KUMBE LEO LAKE ANATAFUTA MKE???? ITAKUWAJE SASA.. NIJEEEE AU ???!
NILIVYOMPENDA MLINZI WA GETINI KWETU BILA KUJUA NI BILIONEA ANAYETAFUTA MKE💕💕💕💕🗣️


*SEHEMU YA PILI*

Siku iliyofuata Belinda aliamua kumtoa out Prosper Mlinzi wao. Walitoka asubuhi  kusudi wawahi kurudi ili Prosper aendelee na lindo lake. Kazi kubwa ya Prosper ilikuwa ni usiku lakini mchana, mara nyingi alikuwa anatumia mda huo kulala kusudi usiku asisinzie akiwa kwenye lindo lake. 

Basi cha kwanza Belinda alimpitisha Prosper kwenye duka la nguo za thamani kwani prosper hakuwa na nguo nzuri za mtoko. Alimnunulia full wearing, yani suti ya nidhamu, kiatu cha bei mbaya na uzuri duka waliloingia ukitaka kuvalishwa unavalishwa hapohapo.

Prosper alionyeshwa bafu akaoga vizuri kisha baadae alipotoka bafuni alitinga suti yake kali na kiatu cha thamani alichonunuliwa na Belinda. Kwa upande prosper kuvaa vile halikuwa jambo geni hata kidogo, ila alipoenda kuomba kazi ya ulinzi kwa mara ya kwanza  kwao Belinda alienda na mavazi ya kifukara kusudi aonewe huruma na kupewa kazi lakini lengo lake halikuwa kupata kazi, bali alikuwa anatafuta mke mwenye upendo wa dhati. Na katika nyumba hiyo aliyoomba kazi aliwaona mabinti wawili, wazuri kupindukia Belinda na Norah "

Basi Prosper alipomaliza kuvalishwa alitoka nje yani sehemu ya mapokezi alipo Belinda. Ile tu Belinda anamuona haraka alimkumbatia "Waooo your looking soo. Mwaaa! " Alisema Belinda akimbusu Prosper kwenye paji la uso.walishikana  mikono na kutoka nje lilipo gari lao wakapakia garini, Belinda aliendesha gari mpaka UTULIVU HOTEL hapo walishuka garini na kwenda kuketi eneo la garden. Waliagiza vinywaji wakawa wanakunywa polepole huku wakiongea.

"Prosper unajua kila mtu ana vitu ambayo anavipenda, mi napenda mwanaume wa kawaida tu mpole yani kiufupi nimevutiwa na jinsi ulivyo licha ya kuwa huna. Ki...." Kabla Belinda hajamalizia kauli yake Ghafla alishtukia akipigwa risasi eneo la bega alidondoka chini akigaragara huku damu nyingi zikimvuja, hata Prosper mwenyewe alishindwa kuelewa ile risasi ilitoka wapi kwani aliangaza macho kila kona mpigaji hakuonekana!

JE NINI KILIENDELEA? UNAHISI NI NANI ALIYEMPIGA RISASI BELINDA? KUMBUKA KWAO BELINDA WAPO WAWILI TU NORAH NA BELINDA, NORAH NDIO MKUBWA LAKINI BELINDA NDIO KIPENZI CHA WAZAZI WAKE? JE UNADHANI PROSPER ATAELEWEKA! HAKIKA USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA....
NILIVYOMPENDA MLINZI WA GETINI KWETU BILA KUJUA NINI BILIONEA ANAYETAFUTA MKE💕💕💕💕🗣️

*SEHEMU YA TATU*

Prosper na Belinda wakiwa wamekaa eneo la garden pale UTULIVU HOTEL mara ghafla Belinda akashtukia amepigwa na risasi ya bega, alidondoka chini huku akipiga kelele na kugaragara kama mbuzi aliyeponyoka kwenye kisu cha mchinjaji, damu nyingi zilimtoka. Prosper alitazama kila kona ya hoteli ile lakini hakufanikiwa kumuona aliyempiga Belinda risasi. 

Haraka alimchukua Belinda na kumpakiza garini, mbio alimuwahisha hospitali. Wauguzi walimpokea, na haraka wakamuingiza Belinda kwenye chumba cha huduma ya dharura wakati huo Prosper akiwa nje. Aliwaza sana akaona atoe taarifa kwa ndugu na wazazi wa Belinda kusudi nao wajue kilichotokea. Alianza kumpigia simu baba yake  Belinda, akamuelezea kila kitu.

"Prosper! Nadhani hunijui vizuri na hata huna aibu ya kuniambia ulitoka na binti yangu kipenzi out. Hivi unaakili wewe? Yani kijakazi wa getini unatoka out na binti yangu na unaniambia kabisa upuuzi huo?" Alifoka sana baba yake Belinda, "Mzee Nisamehe na wala sikujua kama yatatokea haya" Prosper alijitetea.

"Nisubiri tu hapo hospitali yani usiondoke! Nakuambia leo ndio utajua kuwa watoto wa matajiri hawachezewi kijinga namna hiyo" Alisema baba yake Belinda kisha akakata simu na kumuacha Prosper akiwa amezubaa tu. 

😭😭

Baba Belinda alimpigia simu Norah mwanaye ambaye hakuwa nyumbani wakati huo, akampa taarifa na kumwambia wakutane, walikutana na kisha wakaanza safari ya kwenda hospitalini. Walipofika hospitalini walimkuta Prosper amekaa sehemu ya mapokezi, kaulamba suti safi na iliyoonekana ni mpya kabisa. "Baba huyu mlinzi sio bure huyu ndiye kamloga Linda huoni hata nguo inaonekana kanunuliwa na Linda, yani vijana wanaotoka kwenye familia za kimaskini wanapenda sana kutumia uchawi na madawa kwenye mapenzi na tusipokuwa makini atatuloga nyumba nzima" Norah akamwambia baba yake.

"Hebu subiri kwanza! " Alijibu baba yake Belinda na kwenda pembeni kidogo kupiga simu. Punde lilifika gari jeusi, lenye vioo vya Tinted walishuka wanaume wawili waliojazia mbavu, wakamtwaa Prosper na kumtia gari kisha wakaondoka naye na kumuacha baba yake Belinda na Norah pale hospitalini.

"Hawa vijana nimewaambia wakamuulie mbali huyu fukara, nimewaambia wakimaliza kazi waje wachukue milioni moja, acha akafilie mbali hiyo ndio dawa ya mafukara wanaojipendeleza kwa watoto wa matajiri. "Alisema baba yake Belinda. 

JE NINI KILIENDELEA? PROSPER ATAUWAWA AU ITAKUWAJE? HAKIKA USIKOSE SEHEMU IJAYO UTASISIMKA SANA.
NILIVYOMPENDA MLINZI WA GETINI KWETU BILA KUJUA NI BILIONEA ANAYETAFUTA MKE💕💕💕💕🍎

*SEHEMU YA NNE*


"Jamani hebu simamisheni gari tuongee kidogo ni kwa faida yenu lakini" Prosper aliwaambia wale watu waliopewa kazi na baba Belinda ya kumuua. "Max hebu park gari pembeni tumsikilize huyu shoga kwamba anasemaje na ole wake atuambie vitu ambayo havina impact kwetu" Roja Alimuambia dereva Max.

Max akapack gari kando ya barabara"Haya ongea we mjinga" Roja alimuamru Prosper. "Ni kweli yule mzee kuwatuma muniue sikatai kwasababu na nyie mnatafuta pesa, pia mzee yule ametoa amri hiyo akijua mimi ni masikini siwezi kumuoa mwanae, mimi nina pesa ya kumlisha mzee yule yeye na familia mpaka siku ya vifo vyao" Aliongea Prosper Roja akapiga kibao kikali cha macho. "Bwege wewe umechanganyikiwa naona leo ulivuta bangi sio bure na leo bangi zako utazijutia hebu Max washa gari tuendelee na safari.

"Hapana Roja hebu msikilize aongee amalize usimdharau usiyemjua" Alisema dereva Max. "Haya ongea" Roja alimwambia Prosper. "Nataka tu kusema kwamba pesa, magari, mali ni vitu vya kupita, na ni vya kutafuta hivyo mzee Raymond anaona kama pesa alizonazo, majumba na magari yatadumu milele kumbe hajui hivyo ni vitu vya kupita tu vinaweza kuyeyuka kama barafu Juani, duniani tunachotafuta ni amani, utulivu wa moyo na zaidi thawabu zitakazotuingiza kwenye ufalme wa mbinguni" Aliongea Prosper, Roja akampiga kofi lingine kali la macho, lilimuingia Prosper vilivyo hadi akatoa sauti ya kilio 😭😭 .

"Hatukuja kuhubiri hapa sema unachotaka kutuambia hii ni nafasi ya mwisho nakupa ukiongea utumbo hakuna rangi utaacha kuona" Roja alimwambia Prosper. "Nachotaka kuwaambia mmepewa shi ngapi ya kunitoa mimi uhai?" aliuliza Prosper.

"Max unaona maswali anayouliza huyu mwehu" Roja alimwambia dereva Max. "Hapana we mjibu tu kwasababu huyu ni marehemu mtarajiwa" Alijibu Max. "Haya tumepewa milioni kwani wewe unasemaje" Alijibu Roja huku akitoa sigara kubwa na kuwasha akaanza kuvuta. "Hahahahhaaaa yani milioni tu ndio iwasababishe mumtoe mtu roho?" Aliuliza Prosper huku akicheka sana. "Wewe sasa naona umeanza kutukashifu sio" Roja aliuliza huku akimpulizia Prosper moshi wa bangi machoni.

"Hapana maana naona hiyo pesa ni ndogo isitoshe mpo wanne inamaana mtagawana laki mbili na hamsini tu pesa ambayo naweza kuitumia kwa siku kula na yatima au wajane, basi naombeni simu yenu nimpigie mtu awaletee milioni hamsini pengine itawasaidia muache kazi hizi za kuua" Alisema Prosper ikabidi Roja acheke sana kwa kebehi.

"Roja mpe simu tuone halafu ole wake aite polisi, yani ukiongea na simu ongea kwa sauti sawa" Max alimwambia Prosper huku wakimpatia simu.

"Hallo Vicent" Alisema Prosper baada ya kupiga simu ikapolewa. "Naaam bosi" Sauti upande wa pili wa simu ilijibu na kuwafanya Roja na Max wabaki kinywa wazi baada ya kusikia Prosper akiitwa bosi, kidogo wakawa kama wanamwamini hivi.  

"Vicent nenda bank, utoe milioni 60 uniletee maeneo ya msitu wa Simba, utanikuta huku  sawa?" Prosper alisema kwa amri. "Sawa bosi nakuja sasa hivi" Alijibu Vicent kisha Prosper akakata simu . Bado Roja na Max walikuwa wamezubaa hawaamini wanachokisikia, waliona kama maigizo lakini dakika ishirini mbele wakashangaa......
JE NINI KILIENDELEA? HAKIKA USIKOSE SEHEMU IJAYO UTATETEMEKA SANA KAMA SIO KUSISIMKA
NILIVYOMPENDA MLINZI WA GETINI KWETU BILA KUJUA NI BILIONEA ANAYETAFUTA MKE💕💕💕👸🏻

*SEHEMU YA TANO*

Baada ya dakika 20 mbele  lilifika gari la kifahari eneo lile walipo Max, Roja na Prosper. Bado tu Roja na Max walikuwa hawaamini kabisa mambo wanayoyaona  mbele ya macho yao. Wakashangaa kumuona Vicent akishuka kwenye gari lile la kifahari akiwa ameshika Brifcase yenye pesa ndani mkononi. "Bosi mzigo wako huu hapa" Alisema Vicent huku akimkabidhi Prosper Brifcase ya pesa.

"Ahsante sana rudi kazini ukaendelee na majukumu yako" Alisema Prosper huku akipokea ile Brifcase ya pesa. Vicent alirudi kwenye gari lake na kuanza safari yake ya kurejea kazini. "Mzigo wenu huu hapa bado mna nia ya kuniua?" Prosper aliwakabidhi Max na Roja mzigo wao na kuwauliza swali hilo.

Roja aliifungua ile Brifcase, macho yake yakakaribishwa na noti noti nyekundu tupu "Mheshimiwa ahsante yani ndio maana nilikuwa namwambia Roja awe mtulivu akusikilize kwanza mpaka umalize kuongea nadhani hapo amejifunza kutomdharau asiyemjua" Alisema dereva Max.

"Msijali ndio maana nimeona niwape milioni 60 kabisa kusudi mgawane milioni 15 kila mtu, ahsante nanyi kwa kunisikiliza" Alisema Prosper huku akitengeneza suti yake vizuri.


"Hapana Roja hapa atapata milioni 1 ambayo ilikuwa tupewe na Raymond baba yake Belinda" alianza kusema Max. "Kwanini mimi nipewe milioni moja" Alisema Max kwa ukali.  "Kwasababu kwanza hukutaka kumsikiliza muheshimiwa mpaka tulipokushurutisha sisi, na pia  umempiga muheshimiwa vibao, kwahiyo halali yako ni milioni moja pesa ya mtu ambaye uliona ni wa maana sana kuliko wengine huyo baba Belinda" Alisema Max haraka Roja akachomoa bastola, Max naye akachomoa, wale wawili waliobakia nao wakachomoa na kunyoosheana. "Hiyo pesa isipogawa sawa kwa wote nasema tunatoana roho" alisema Roja.

"Hapa ukibisha hulambi kitu mwanaharamu wewe" alijibu Max. Roja akamfyatulia risasi na kwa ushapu wa hali ya juu Max akikwepa yani ikamkwaruza tu kidogo pembeni ya shingo, naye Max hakuzubaa akamfyatulia Roja risasi ya kichwa palepale Roja akapoteza maisha.

Max na wenzake watatu wakapakia kwenye gari na kutimka zao, Prosper  alianza kuondoka zake mdogo mdogo eneo lile akirudi Hospitali kusudi akamjulie hali Belinda kwani moyo wake bado ulikuwa unampenda. "Belinda ana upendo wa dhati sana acha nikamjulie hali Mwanamke aliyepigwa risasi kwa ajili yangu, yani hata baba yake akiamua kuniua aniue tu, ila nipo tayari nife kwa ajili ya Linda. "Aliongea Prosper peke yake huku akitembea. Alipakia daladala na kurudi hospitalini lakini alimkosa Belinda, madaktari walimuambia kuwa wazazi wa Belinda walikataa mwanao alazwe hivyo wamemtoa hospital wanaenda kumtibia nyumbani. "Any way Acha niende huko huko nyumbani kama ni kufa acha nikafe" alisema Prosper kimoyomoyo

🥱🥱🥱
Belinda hakulazwa hospitali siku ile alitibiwa na kupewa dawa za kwenda kutumia nyumbani. Baba Belinda akiwa nyumbani amepumzika na familia yake akiwemo Norah bintiye mara akapigwa simu na msimamizi wake wa kampuni kubwa inayomuweka baba Belinda mjini. Akapokea akijua ni taarifa nzuri ya michongo ya pesa lakini kumbe........
JENI NINI TENA KIMETOKEA KWENYE KAMPUNI YA BABA BELINDA? KUMBUKA PROSPER NAYE YUPO NJIANI ANAELEKEA KWAO BELINDA? ITAKUWAJE? HAKIKA USIKOSE.....

 Full shillingi 1000 😄
 Lipia katika namba hii hapa
Airtel - 0683 944 333
Jina - Hiwalis Hiwalis

kslprojects

kslprojectstz@gmail.com Entrepreneurship Power

Post a Comment

Previous Post Next Post